TRA kwanini Wamehamishia akaunti ya malipo KCB, siyo tena NMB? Ni ufisadi baada ya Magufuli?

Geza Ulole

JF-Expert Member
Oct 31, 2009
43,646
2,000
Tuna safari ndefu sana. Mabenki ni wakusanyaji tu wa mapato ya TRA yanayopelekwa BoT. Huko kwenye taasis za kifedha zinapita tu.

Hapo chini kwenye kiambatanishi inasoma malipo yanaenda kwa:-

Commissioner of customs and excise
TRA
BoT

Sasa hapo KCB analaumiwa kwa lipi?
Tukiambiwa malipo yote yafanyike kwa bank moja hizo foleni na ucheleweshwaji tutauvumilia?

Kama sijaelewa vizuri naomba kueleweshwa.
Hakuna kupitisha fedha za Watanzania KCB hata Mo ananibore kuweka account za simba KCB! Ni ushenzi!
 
The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
16,389
2,000
Hakuna kupitisha fedha za Watanzania KCB hata Mo ananibore kuweka account za simba KCB! Ni ushenzi!

Hiyo ni kwa mujib wa mtizamo wako.
Lakini uhalisia na hali ilivyo sasa ndio hiyo.

KCB ni benki hapa kwetu na wanatoa huduma kama benki zingine ikiwepo kutusaidia kukusanya mapato ya TRA.

Achilia mbali ajira waliyotoa kwa watanzania ndani na nje ya Tanzania.
 
Ndombwindo

JF-Expert Member
Nov 23, 2013
603
1,000
Tra unawalaumu bure ndg yangu, wa kuulizwa na kutoa majibu ya haya mazongozongo yote yanayoendelea ni Rais. Yeye anapinduapindua kila alichokikuta wima ni sharti akilaze ili mumuone naye wamo
Wapo wanaopinga juhudi kwa nguvu zote as if Magu hakufanya ya maana, wacha tu kazi iendelee.
 
emmanuel mruma

JF-Expert Member
Feb 14, 2017
1,576
2,000
Haha ila uelewa wamaswala ya finance kwa mtoa Mada ni mdogo Sana... TRA Ina clearence account karibia bank zote.. Inakua ni maamuz ya mteja anapendelea kulipa kupitia nini, hata kupitia mitandao ya simu unaweza Lipa Kodi... Mfan NMB shareholder makubwa ni mholanzi haina maana hizo hela zinaenda uholanzi... Kwene hizo commercial banks hela zinapita tu kwenda BOT, zinafaidika transaction fees tu ambazo serikali itakuja kufaidika Kodi as well kupitia hio miamala...
 
HORSE POWER

JF-Expert Member
Feb 22, 2015
1,827
2,000
Shughuli ya upigaji imerudi kwa kasi ya tsunami ndugu.Manyang'au na mapakashume yaliyokua yanararua na kutafuna pesa za umma,sasa yamefunguliwa.Walikua 'kifungoni' kwa miaka mitano maana ofisi kuu ilipata mwamba aliyejua mamlaka yake.
 
Geza Ulole

JF-Expert Member
Oct 31, 2009
43,646
2,000
Hiyo ni kwa mujib wa mtizamo wako.
Lakini uhalisia na hali ilivyo sasa ndio hiyo.

KCB ni benki hapa kwetu na wanatoa huduma kama benki zingine ikiwepo kutusaidia kukusanya mapato ya TRA.

Achilia mbali ajira waliyotoa kwa watanzania ndani na nje ya Tanzania.
KCB Bank Tanzania ipo zaidi ya miaka 15 lakini hawajatengeneza faida na kama wametengeneza basi ndo wameanza ina branch network ndogo! Huwezi kuitetea ati ikusanye mapato ya Tanzania! Taahira kama wewe ndo anaweza tetea huu ujinga!
 
Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
7,525
2,000
Viwanda vya uongo kumchafua Mama Samia vipi kazini.

TRA wana utaratibu wa kumpa mteja control no kwenye bank yeyote ambayo mteja atahitaji kutumia ili kufanya malipo yake.
Huu ulioleta hapa ni uongo wa mchana kweupe
 
The Wolf

JF-Expert Member
Sep 10, 2013
8,595
2,000
Kuna kitu bado hukijui vizuri, kuanzia July 2021, taasisi karibu zote za serikali inatakiwa iwe imekamilisha mfumo mpya wa malipo ya serikali uitwao MUSE.. Hii MUSE inarahisisha sana malipo ya mishahara na malipo mengine ya serikali moja kwa moja toka BOT, yaani mshahara wako na madai mengine yako yote yanalipwa toka BOT kwenye account yako, hivyo hata ukiwa na account bank yoyote sio tatizo, na hii inaharakisha malipo sanaa, within few hours unapata malipo moja kwa moja toka BOT kwenye personal account yako, hapa Serikali imefanya la maana sana, hii itaondoka ule mtindo wa zamani sijui mshahara upitie bank fulani toka BOT, alafu Bank hiyo ianze kuweka kwa individuals na ilitia hasara sana serikali kuwapa bank tender hiyo ya mishahara. Sasa hivi unalipwa direct to your account from BOT within few hours.

Ila hili la TRA kutumia KCB, hii mbaya sana, sana, sanaaaa, na hatari kabisa. Sielewi TRA nini kimewapata. This is unacceptable kabisa.

I hope, Waziri wa Fedha lazima atarekebisha hili. Hii ni kosa
Mkuu umeanzia mbali lakini inaonekana bado ni kilaza kwenye ufahamu wa hili jambo, huyu mleta mada analeta taharuki, kwenye kulipa kodi za TRA unaweza ku order transfer directly to BOT ama kupitia hizi commercial banks ambapo zipo almost bank hapa Tanzania, KCB ni bank iliyosajiliwa Tanzania kama zilivyo bank zote, sijui kwanini kachagua kuweka hiyo KCB na siyo equity ama FNB n.k
 
The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
16,389
2,000
KCB Bank Tanzania ipo zaidi ya miaka 15 lakini hawajatengeneza faida na kama wametengeneza basi ndo wameanza ina branch network ndogo! Huwezi kuitetea ati ikusanye mapato ya Tanzania! Taahira kama wewe ndo anaweza tetea huu ujinga!

Sawa mkuu, ila jua tu nimehudumu na hiyo bank kwa miaka zaidi ya mitano.

Kuhusu faida, fuatilia taarifa zao za kifedha zinazotolewa kwa umma kisha urudi kuandika kuhusu faida.

Mmejichanganya eneo dogo sana, mnaandika utafikiri ni KCB pekee ndio wameambiwa wakusanye pesa za TRA na taasisi zingine zikazuiliwa. Serikali wamefanya hivyo kuwarahisishia walipa kodi waweze kulipa mapato TRA kwa urahisi. Sijajua unaiona KCB haina huo uwezo wa kukusanya kwa vigezo vipi wakati wana mifumo bora kabisa ya kibenki na CRDB wataiga huo mfumo muda si mrefu?

Uzuri ni kwamba, hivi tunavyoongea, KCB wanaisaidia serikali kukusanya mapato. Unaweza kuwashauri wakasitisha ikiwa una sababu za kueleweka.
 
Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
5,469
2,000
Mkuu umeanzia mbali lakini inaonekana bado ni kilaza kwenye ufahamu wa hili jambo, huyu mleta mada analeta taharuki, kwenye kulipa kodi za TRA unaweza ku order transfer directly to BOT ama kupitia hizi commercial banks ambapo zipo almost bank hapa Tanzania, KCB ni bank iliyosajiliwa Tanzania kama zilivyo bank zote, sijui kwanini kachagua kuweka hiyo KCB na siyo equity ama FNB n.k
Nimewahi kulipa kwa mtindo huu. TRA wakiniambia kuna KCB katikati, lakini pesa niliingia NMB kwa maana nyingine ziliingia NMB to KCB to BOT! Kwa nini yote haya?

Kuhusu KCB na siyo benki zingine, tukubali ktk uchumi wa EAC hatujawahi kuwa ktk favour ya wa-Kenya kwa lolote! Hata tukiwazidi kwa mizigo bandarini kwao ni hasira. Benki zetu hapa TZ siyo kwamba hazina mitaji ya kuwekeza Kenya, bali wakenya hawako tayari kuweka pesa zao kwa Benki ya TZ kwa sababu ya chuki tu! Nakumbuka maelezo ya Rostam Aziz akiwa NRB ktk ziara ya rais. Kenya kuna hostile environment kwa bussiness za TZ. Kwa tabia hiyo, kwa nini TRA waweke pesa zao KCB. Kwa nini sasa? Ni kwa comfort ipi? Ni kwa kumfurahisha nani? Kamishna wa TRA? Labda!
 
Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
5,469
2,000
Viwanda vya uongo kumchafua Mama Samia vipi kazini.

TRA wana utaratibu wa kumpa mteja control no kwenye bank yeyote ambayo mteja atahitaji kutumia ili kufanya malipo yake.
Huu ulioleta hapa ni uongo wa mchana kweupe
Ukishapewa control number kama huo mfano, ujue iko linked na KCB. hata kama pesa utaingiza desk la NMB pesa itakwenda lakini kupitia KCB. Kila pesa itakayowekwa itakuwa na faida kwa KCB. Hawaiandiki KCB kukurahisishia kuweka pesa maana unaweza hata kulipa kwa m-Pesa, ni dhamana ya uhusiano wa KCB na TRA.
 
Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
7,525
2,000
Ukishapewa control number kama huo mfano, ujue iko linked na KCB. hata kama pesa utaingiza desk la NMB pesa itakwenda lakini kupitia KCB. Kila pesa itakayowekwa itakuwa na faida kwa KCB. Hawaiandiki KCB kukurahisishia kuweka pesa maana unaweza hata kulipa kwa m-Pesa, ni dhamana ya uhusiano wa KCB na TRA.
Hujaelewa nini?
Umeambiwa wana utaratibu wa kulipia kupitia bank karibu zote zinazo operate hapa nchini. Na Hii ni ili kurahisisha malipo
 
The Wolf

JF-Expert Member
Sep 10, 2013
8,595
2,000
Kuna jambo la kujifunza juu ya viongozi wetu na utendaji wao maofisini. Kwa mfumo huu wa control number, kuna sababu gani ya kuweka benki nyingine kati kati ya BoT na TRA? Nimewahi kulipa kwa mtindo huu. TRA wakiniambia kuna KCB katikati, lakini pesa niliingia NMB kwa maana nyingine ziliingia NMB to KCB to BOT! Kwa nini yote haya?

Kuhusu KCB na siyo benki zingine, tukubali ktk uchumi wa EAC hatujawahi kuwa ktk favour ya wa-Kenya kwa lolote! Hata tukiwazidi kwa mizigo bandarini kwao ni hasira. Benki zeru hapa TZ siyo kwamba hazina mitaji ya kuwekeza Kenya, bali wakenya hawako tayari kuweka pesa zao kwa Benki ya TZ kwa sababu ya chuki tu! Kwa tabia hiyo, kwa nini TRA waweke pesa zao KCB. Ni kwa comfort ipi? Ni kwa kumfurahisha nani? Kamishna wa TRA? Labda!

Ha ha acha propaganda mimi ninafanya hizi transactions every day, na katika utendaji wangu miaka yote sijawahi kukutana na hili jambo, katika procedure ya payment, utaweka details zako mlipa kodi ikiwemo account yako na bank yako(ambazo ameweka mtoa mada kwenye lawama kwamba ndio kcb anawekewa) value date, na details nyingine ni unalipa TZ mainland au zanzibar, kama tz itakuletea options kama 3 hivi, baada ya hapo ni swift to bot ama pay to other banks, sijawahi kuona unachokisema
20210907_191706.jpg
 
Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
2,020
2,000
Tra Wana account kwenye bank zote kilichotokea hapo ni wakati control number ina tegenezwa aliokuwa anajaza alijaza bank ya KCB hayo malipo yapitie

Ni Jambo la kawaida mwingine anaweza kwenda kulipoa equity, abbsa, crdb.
Hapana! Huo ni uongo. Kama angepewa Control number ya malipo ya BOT, kusingekuwa na sababu ya kumwambia apeleke KCB, hiyo ingekuwa lobbing. Kama wengi wanavyoeleza, hiyo control number lazima ina connection na KCB na hata kama utalipa kwa simu, bado pesa itapitia KCB. Control number ilipoanzishwa haikuwa na uhusiano na aina ya benki ya kibiashara. Huu ni ufisadi tu umeanzishwa kwa malengo fulani na wezi wazoefu wa TRA.

Ukiwauliza watu wa mabenki, utakuta kuna lobbing inafanyika pamoja na ahadi kibao! Kwa pesa kama za TRA, Kamishna anaweza hata kuahidiwa bilioni kadhaa za bure ili pesa ya kodi ipitie pale. Kumbuka makusanyo yetu ni karibu trioni 2 kwa mwezi!
 
Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
2,020
2,000
Ha ha acha propaganda mimi ninafanya hizi transactions every day, na katika utendaji wangu miaka yote sijawahi kukutana na hili jambo, katika procedure ya payment, utaweka details zako mlipa kodi ikiwemo account yako na bank yako(ambazo ameweka mtoa mada kwenye lawama kwamba ndio kcb anawekewa) value date, na details nyingine ni unalipa TZ mainland au zanzibar, kama tz itakuletea options kama 3 hivi, baada ya hapo ni swift to bot ama pay to other banks, sijawahi kuona unachokisema View attachment 1928347
Nahisi unaeleza unachokijua lakini hakina uhusiano na kinachojadiliwa hapa. Wewe na TRA kama taxation institution kuna tofauti kubwa sana.

Ninachoweza kuhisi ni kwamba makusanyo hayo yanakwenda benki tofauti kutegemea aina ya kodi. Lakini pamoja na hayo, kama mada iliyopo, why KCB today?
 
The Wolf

JF-Expert Member
Sep 10, 2013
8,595
2,000
Nahisi unaeleza unachokijua lakini hakina uhusiano na kinachojadiliwa hapa. Wewe na TRA kama taxation institution kuna tofauti kubwa sana.

Ninachoweza kuhisi ni kwamba makusanyo hayo yanakwenda benki tofauti kutegemea aina ya kodi. Lakini pamoja na hayo, kama mada iliyopo, why KCB today?
Wewe unahisi mimi ninafanya
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom