TRA kwanini Wamehamishia akaunti ya malipo KCB, siyo tena NMB? Ni ufisadi baada ya Magufuli?

robinson crusoe

JF-Expert Member
Oct 22, 2020
740
1,214
TRA na BOT watajitetea kwa sababu zozote zile lakini sisi tunaolipa kodi ktk nchi hii, kwa kujua nani anamiliki KCB (Kenya Commercial Bank) hii ni chini ya kiwango cha uzalendo uliohubiliwa miaka mitano iliyopita. Nalinganisha malipo niliyofanya 2020 na mwaka huu, yakielekezwa benki tofauti kabisa!!

Tunafahamu ni Benki iliyosajiliwa hapa nchini lakini pesa ya kodi za serikali kupitia benki ya muwekezaji wa nje badala ya NMB ambako serikali ina hisa, ni ufisadi. TRA wanafidika nini kuitumia KCB? Imetokea nini baada ya kifo cha Magufuli? Je, KRA ya Kenya, kwa ubaguzi wao kibiashara, inaweza kupitishia pesa za kodi za serikali yao benki ya TZ, hata kama imesajiliwa nchini Kenya?

TRA2.png

tra.png
 
View attachment 1926663

View attachment 1926664
Inawezekana uko sawa lakini je hiyo bank ya wazalendo huduma zake zikoje ukilinganisha? Je bei na gharama kwa wateja?

kibiashara hakuna bank yeyote inatakiwa kuwa na uhakika wa soko uwekaji wa pesa ni kitu binafsi huwezi kulazimisha kama bank imebakia kutegemea serikali lakini huduma mbaya au tozo ni nyingi haina uhusiano na share za serikali inabidi kuwe na ushindani
 
Tuna safari ndefu sana. Mabenki ni wakusanyaji tu wa mapato ya TRA yanayopelekwa BoT. Huko kwenye taasis za kifedha zinapita tu.

Hapo chini kwenye kiambatanishi inasoma malipo yanaenda kwa:-

Commissioner of customs and excise
TRA
BoT

Sasa hapo KCB analaumiwa kwa lipi?
Tukiambiwa malipo yote yafanyike kwa bank moja hizo foleni na ucheleweshwaji tutauvumilia?

Kama sijaelewa vizuri naomba kueleweshwa.
 
Ww ndio hujui kitu, Tanzania Government ina NMB shares 31.8%. Next time kama hujui kitu, nyamaza

Sikia ndugu, serikali ina hisa 100% kwenye benki ya serikali iliyoitwa TPB bank (Tanzania Postal Bank) au Bank ya Posta ambapo kwa sasa inajulikana kama TCB (Tanzania Commercial Bank), sasa swali la kizushi ni kwamba kwanini huduma nyingi za kiserikali hazipitii bank hii ya serikali mfano mishahara ya watumishi wa umma na malipo mengine kadha wa kadha?
 
Back
Top Bottom