TRA kwanini Wamehamishia akaunti ya malipo KCB, siyo tena NMB? Ni ufisadi baada ya Magufuli?

The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
16,389
2,000
Tenda ilitangazwa wapi KCB wakashinda ???

Na hata kama kulikuwa na tenda, kwa nini mgeni aalikwe kwenye strategic tender such as this?

Benki ya kibongo inaweza kuachwa ishinde tenda ya kutunza hela ya kodi ya Kenya ???

Tusiwe vidampa mbele ya Wakenya jamani!

Hii dunia ni ya ushindani, Kenya is a regional competitor, mnampaje ashike hela ya kodi ya Mtanzania nyinyi TRA dunderheads ?

Fukuza kazi CEO wa TRA. Juzi kafanyisha written interview, vijana wamekwenda Dodoma from across the country halafu matokeo yamefutwa, kisa, TRA walivujisha majibu kabla ya interview.

Fire the dusche bag executives.

Sio kwamba zinapita tu!

Hiyo ni tenda au biashara kapewa Mkenya. Faida inayopatikana inaenda kwa mmiliki wa Kenya Commercial Bank huko Kenya!

Kwenye dunia ya ushindani au bita ya kiuchumi kwa nini usaidie kujenga taasisi za kibenki za nchi nyingine badala ya za kwako mwenyewe ????

Kwa nini hiyo tenda asipewe Tanzania Postal Bank, au CRDB au Benki ya Wanawake Tanzania??????!

Wewe si ndio ulisema tenda?
 

vtuko

Member
Jun 12, 2016
5
45
NMB kama inaogopa mteja wa diaspora kuwa na account ya U$ 10,000 wanaogopa siku ukitaka kutoa hela yako watayumba, je siku serikali inataka kutoa Tshs1,000,000,000,000 NMB inaweza kuyumba hivyo serikali imeamua kusambaza makusanyo yake ya trilion karibu 2 ktk Benki zaidi ya moja na kuwa na uhakika kuzipata wakitoa taarifa ya dharura / short notice .

NMB ukwasi wake haumpi mteja uhakika wa kupata fedha akiomba ghafla kiasi kikubwa kitoke kwa mara moja.

Tujiulize kwanini serikali haikopi mkopo wa kujengea miradi mikakati mikubwa toka CRDB Bank, NMB Tanzania, DTB n.k Benki za kitanzania? Kwanza hazina mtaji mkubwa kuhimili pesa ndefu kutoka mara moja pia hazina mtaji wa fedha za kigeni kama US$, Euro£ kuikopesha Serikali ya Tanzania kujenga reli, mabwawa ya umeme au hata barabara ya kilometa 100 !
Pesa ya serikali ikishakusanywa inakaa bank yoyote nadhan wiki 1 tu then inaenda BOT so bank yoyote haikai na pesa ya serikali zaidi ya wiki 1 pesa yote inaenda BOT then this is automatic transfer kwenda BOT.
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
13,555
2,000
Pesa ya serikali ikishakusanywa inakaa bank yoyote nadhan wiki 1 tu then inaenda BOT so bank yoyote haikai na pesa ya serikali zaidi ya wiki 1 pesa yote inaenda BOT then this is automatic transfer kwenda BOT.

Tunaongea lugha moja Benki ndogo za kiTanzania na kiAfrika hawana ubavu wa kutoa huduma kubwa kwa serikali na ndiyo maana wanaziona ni za moto wanahamishia BoT.

Benki kama NMB au KCB ni kama maajenti wa M-Pesa kimtaji hawawezi kukaa na pesa nyingi zitawayumbisha ki-operesheni na kushindwa kutuhudumia sisi wateja wadogo tulio wengi.
 

Mwamba 777

JF-Expert Member
Nov 23, 2020
742
1,000
TRA na BOT watajitetea kwa sababu zozote zile lakini sisi tunaolipa kodi ktk nchi hii, kwa kujua nani anamiliki KCB (Kenya Commercial Bank) hii ni chini ya kiwango cha uzalendo uliohubiliwa miaka mitano iliyopita. Nalinganisha malipo niliyofanya 2020 na mwaka huu, yakielekezwa benki tofauti kabisa!!

Tunafahamu ni Benki iliyosajiliwa hapa nchini lakini pesa ya kodi za serikali kupitia benki ya muwekezaji wa nje badala ya NMB ambako serikali ina hisa, ni ufisadi. TRA wanafidika nini kuitumia KCB? Imetokea nini baada ya kifo cha Magufuli? Je, KRA ya Kenya, kwa ubaguzi wao kibiashara, inaweza kupitishia pesa za kodi za serikali yao benki ya TZ, hata kama imesajiliwa nchini Kenya?

View attachment 1926663

View attachment 1926664
Wee inamaana hujui tangu Magufuli akiwa hai, Mwingereza mwenye hisa na NMB Bank alichukua hisa zake kalala mbele?

NMB ilikuwa share ya Serikali na Mwingereza. Baada ya mwingereza kujitoa yawezekana ishashindwa kujiendesha.

Wee huoni hata mandege (ATCL) ya Serikali wameshashindwa kujiendesha? ni hasara tupu.
 

LexPaulsen

JF-Expert Member
Jul 30, 2018
249
500
Mleta uzi hafahamu kwamba TRA inatumia mabenki karibia yote yaliyosajiliwa nchini kukusanya kodi kwa mfumo wa TaxBank. Hiyo payment order form uliyopost TRA wanakuprintia kulingana na wewe uko benki gani, ukitaka hata mwenyewe unajiprintia online.
 

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
2,020
2,000
Inawezekana uko sawa lakini je hiyo bank ya wazalendo huduma zake zikoje ukilinganisha? Je bei na gharama kwa wateja?

kibiashara hakuna bank yeyote inatakiwa kuwa na uhakika wa soko uwekaji wa pesa ni kitu binafsi huwezi kulazimisha kama bank imebakia kutegemea serikali lakini huduma mbaya au tozo ni nyingi haina uhusiano na share za serikali inabidi kuwe na ushindani
Inapokuja suala la taasisi kama TRA, siyo suala la huduma. TRA haendi benki hata siku moja kutafuta huduma kama wewe unavyokwenda na kujaza vikaratasi na kuulizia salio. Huui ni uhusiano wa taasisi ya serikali na benki ambayo serikali pia ina hisa ndani yake. Huduma zao wanawasiliana kwa ngazi ya juu, siyo dirishani.

Hata hivyo naamini hili ni suala pana zaidi. BOT wanahusika. Iwe kwa sababu yoyote ile, huu ndo unafiki na bei ndogo ya maafisa wa serikali. Imefikia hata taasisi zinafanyakazi kwa kushawishiwa na watu, tena kwa kupewa chochote.
 

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
2,020
2,000
Watanzania wengi wasofahamu haya masuala hawatachukulia maanani.

Magezeti kama Raia Mwema na mengine wakihoji wata.....

Ila fedha zote za kodi kwenye nchi yoyote ile inayojitambua huingizwa serikali kuu yaani hazina kupitia benki kuu.

Kwa wenzetu waloendelea manispaa na halmashauri za miji hutakiwa kujiwekea viwango vyao vya kodi lakini pia hupelekwa hazina kwanza kabla ya kurudi kwenye maeneo hayo.

Kwa kuwa mfumo wa kodi umevurugwa na hata hatufahamu kinachoendelea TRA ikiwa ni chombo cha serikali ni lazima kitakuwa kimepata baraka za hazina kufanya walofanya kimyakimya.

Ila masuala yote ya kodi, tozo na mengine, yalipaswa kupitishwa na bunge baada ya kujadiliwa badala ya bunge hilohilo kufukuzana na wabunge Jerry Slaa, Gwajima na Polepole.

Hayati Magufuli pamoja na mapungufu yake lakini aliwaambia tayari watanzania madhara ya serikali kufanya biashara na benki.

Jenerali Ulimwengu amesema tayari "Nchi hii ni ngumu".
Hii ndo ideal situation kwa serikali ambayo ni ideal. Huwezi kusanya kodi ya nchi kupitia benki binafsi tena ya nje! That is stupidity of highest order. Kwa uzoefu wangu sitegemei hata siku moja Benki ya TZ ipate wateja kwenye nchi ya Kenya. Hata CRDB wamefanikiwa hapo Rwanda tu na wakijaribu Nairobi, wanabaguliwa kwa sababu tu ni ya TZ. Sasa leo TRA inafungua akaunti KCB!

Kwa ujumla ninaamini viongozi wetu wanakuwa ni watu wa bei ya chini sana! Wanavutiwa hata na mambo ya kipuuzi. Ukiuliza hapo, unaweza jibiwa waliahidi mkopo kwa waziri ili ajenge hotel, basi!
 

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
2,020
2,000
Kama sijakosea TRA ina accounts kwenye mabenki kibao ambazo zinapokea malipo halali ya Shirika hilo.
Suala siyo uhalali wa akaunti, tunajiuliza ni kwa manufaa ya nani? Yaani sisi kama nchi tuko tayari kunufaisha KCB na siyo NMB, CRDB, NBC, etc. our very homegrown banks?
 

mzeewaSHY

Member
Aug 31, 2021
81
125
TRA na BOT watajitetea kwa sababu zozote zile lakini sisi tunaolipa kodi ktk nchi hii, kwa kujua nani anamiliki KCB (Kenya Commercial Bank) hii ni chini ya kiwango cha uzalendo uliohubiliwa miaka mitano iliyopita. Nalinganisha malipo niliyofanya 2020 na mwaka huu, yakielekezwa benki tofauti kabisa!!

Tunafahamu ni Benki iliyosajiliwa hapa nchini lakini pesa ya kodi za serikali kupitia benki ya muwekezaji wa nje badala ya NMB ambako serikali ina hisa, ni ufisadi. TRA wanafidika nini kuitumia KCB? Imetokea nini baada ya kifo cha Magufuli? Je, KRA ya Kenya, kwa ubaguzi wao kibiashara, inaweza kupitishia pesa za kodi za serikali yao benki ya TZ, hata kama imesajiliwa nchini Kenya?

View attachment 1926663

View attachment 1926664
Kazi Imeanza ?
 

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,232
2,000
TRA na BOT watajitetea kwa sababu zozote zile lakini sisi tunaolipa kodi ktk nchi hii, kwa kujua nani anamiliki KCB (Kenya Commercial Bank) hii ni chini ya kiwango cha uzalendo uliohubiliwa miaka mitano iliyopita. Nalinganisha malipo niliyofanya 2020 na mwaka huu, yakielekezwa benki tofauti kabisa!!

Tunafahamu ni Benki iliyosajiliwa hapa nchini lakini pesa ya kodi za serikali kupitia benki ya muwekezaji wa nje badala ya NMB ambako serikali ina hisa, ni ufisadi. TRA wanafidika nini kuitumia KCB? Imetokea nini baada ya kifo cha Magufuli? Je, KRA ya Kenya, kwa ubaguzi wao kibiashara, inaweza kupitishia pesa za kodi za serikali yao benki ya TZ, hata kama imesajiliwa nchini Kenya?

View attachment 1926663

View attachment 1926664
Ili uwekezaji kwenye sekta binafsi uimarike, shurti ifanye kazi na serekali.
Ninaamini move hii ni kwa ajili kuwavutia zaidi wawekezaji kutoka nje ambao Magufuli aliwapiga pini pakubwa.

Kwa hili kama ni kweli nasimama na TRA!
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
49,613
2,000
Tuna safari ndefu sana. Mabenki ni wakusanyaji tu wa mapato ya TRA yanayopelekwa BoT. Huko kwenye taasis za kifedha zinapita tu.

Hapo chini kwenye kiambatanishi inasoma malipo yanaenda kwa:-

Commissioner of customs and excise
TRA
BoT

Sasa hapo KCB analaumiwa kwa lipi?
Tukiambiwa malipo yote yafanyike kwa bank moja hizo foleni na ucheleweshwaji tutauvumilia?

Kama sijaelewa vizuri naomba kueleweshwa.
Sure
 

Wakabambee58

Member
Aug 14, 2020
61
125
Tra unawalaumu bure ndg yangu, wa kuulizwa na kutoa majibu ya haya mazongozongo yote yanayoendelea ni Rais. Yeye anapinduapindua kila alichokikuta wima ni sharti akilaze ili mumuone naye wamo
Waziri WA fedha kasema mini sababu ya kuanika mapato yeti nje ya nchi
 

casampeda

JF-Expert Member
Jul 28, 2012
2,828
1,500
We chizi! kwahiyo huku Tandahimba hamna KBC kwahiyo hatupati huduma!!!mimi nina akaunti ya NMB nalipia fresh tu.mukiambiwa muende Burundi munakasirika!nani alikuambia NMB yetu?benki ya Poster ndio yetu.
 

buchenza

Senior Member
Aug 24, 2012
185
225
Labda Ndugu yetu Mfumo wa Malipo TRA huujuwi Vizuri, ukiwa unafanya malipo kuna wengine wanaenda TRA anaomba control, wanamtengenezea na kumwekea bank atakayo kwenda kulipia, hapa sasa inategemea TRA kakchagulia Bank gani, hii ndiyo system wengi wanayo tumia. Wengine wamekuwa registered na TRA jkwenye mfumo wa kutoa control Numba upo hivi. unaenda kwenye web site ya TRA unabofaya Payment registration unaweka details zaoko jina la kampuni, TIN numba kuna mahali unafika panasema TAXPAYER BANK NAME hapa zinakuja BANK zote ambazo zipo approved na BOT kwa kukusanya Mapato ya Serekali. mimi naona karibu bank zote zinazo operate hapa Tanzania zote zipo. kulingana na milipaji account yake amefungulia wapi. kwaiyo hizi bank ni collector to wa Mapato ya TRA na ikifika Jioni lazima wawkilishe
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom