TRA kwanini Wamehamishia akaunti ya malipo KCB, siyo tena NMB? Ni ufisadi baada ya Magufuli?

Inawezekana Serikali ilichukua credit facility (Bank overdraft)kulipa madeni au wadai wake wa SGR au Nyerere dam Rufiji.Mara nyingi credit facility Kama hizi zinaenda na makubaliano ya kuwa unaweka(deposit) fedha kwenye benki hiyo kupungaza riba.
Nadhani Serikali itakuja na ufafanuzi,juu ya suala hili la kuweka fedha kwenye benki ya nje wakati tunazo benki za ndani,labda Kama TRA wanazo account kwenye benki zingine local.
Watanzania wengi wasofahamu haya masuala hawatachukulia maanani.

Magezeti kama Raia Mwema na mengine wakihoji wata.....

Ila fedha zote za kodi kwenye nchi yoyote ile inayojitambua huingizwa serikali kuu yaani hazina kupitia benki kuu.

Kwa wenzetu waloendelea manispaa na halmashauri za miji hutakiwa kujiwekea viwango vyao vya kodi lakini pia hupelekwa hazina kwanza kabla ya kurudi kwenye maeneo hayo.

Kwa kuwa mfumo wa kodi umevurugwa na hata hatufahamu kinachoendelea TRA ikiwa ni chombo cha serikali ni lazima kitakuwa kimepata baraka za hazina kufanya walofanya kimyakimya.

Ila masuala yote ya kodi, tozo na mengine, yalipaswa kupitishwa na bunge baada ya kujadiliwa badala ya bunge hilohilo kufukuzana na wabunge Jerry Slaa, Gwajima na Polepole.

Hayati Magufuli pamoja na mapungufu yake lakini aliwaambia tayari watanzania madhara ya serikali kufanya biashara na benki.

Jenerali Ulimwengu amesema tayari "Nchi hii ni ngumu".
 
TRA na BOT watajitetea kwa sababu zozote zile lakini sisi tunaolipa kodi ktk nchi hii, kwa kujua nani anamiliki KCB (Kenya Commercial Bank) hii ni chini ya kiwango cha uzalendo uliohubiliwa miaka mitano iliyopita. Nalinganisha malipo niliyofanya 2020 na mwaka huu, yakielekezwa benki tofauti kabisa!!

Tunafahamu ni Benki iliyosajiliwa hapa nchini lakini pesa ya kodi za serikali kupitia benki ya muwekezaji wa nje badala ya NMB ambako serikali ina hisa, ni ufisadi. TRA wanafidika nini kuitumia KCB? Imetokea nini baada ya kifo cha Magufuli? Je, KRA ya Kenya, kwa ubaguzi wao kibiashara, inaweza kupitishia pesa za kodi za serikali yao benki ya TZ, hata kama imesajiliwa nchini Kenya?

View attachment 1926663

View attachment 1926664
Mkuu, bado hujaelewa tu?

Wewe utakuwa ni kati ya watu wagumu wa kuelewa.

Nchi IMEFUNGULIWA HII!

Unajua maana ya hayo maneno?

Hii hapa unayolia nayo bado ni rasha rasha tu, subiri gharika litakalokuangukia ukibahatika kuishi kwenye nchi iliyofunguliwa.

Miaka michache iliyopita, enzi za Kikwete, mabenki haya yalineemeka sana sana kwa faida yaliyokuwa yakizoa hapa nchini. Tulikuwa tukipigana vibega na 'jamaa' toka huko kwao mabenki hayo wakibeba maburungutu kama vichaa!

Vuta subira kidogo mkuu, you ain't seen nothing yet! Tutayasemea sana haya, lakini ukweli ni kwamba tuna mapandikizi waliowekwa maksudi kwenye nafasi za uongozi kuihujumu nchi hii.
 
Hayati Magufuli pamoja na mapungufu yake lakini aliwaambia tayari watanzania madhara ya serikali kufanya biashara na benki.
Magufuli alikuwa na mapungufu makubwa sana, lakini kwa upande huu wa maslahi ya nchi alikoga nyoyo za wengi.
 
TRA na BOT watajitetea kwa sababu zozote zile lakini sisi tunaolipa kodi ktk nchi hii, kwa kujua nani anamiliki KCB (Kenya Commercial Bank) hii ni chini ya kiwango cha uzalendo uliohubiliwa miaka mitano iliyopita. Nalinganisha malipo niliyofanya 2020 na mwaka huu, yakielekezwa benki tofauti kabisa!!

Tunafahamu ni Benki iliyosajiliwa hapa nchini lakini pesa ya kodi za serikali kupitia benki ya muwekezaji wa nje badala ya NMB ambako serikali ina hisa, ni ufisadi. TRA wanafidika nini kuitumia KCB? Imetokea nini baada ya kifo cha Magufuli? Je, KRA ya Kenya, kwa ubaguzi wao kibiashara, inaweza kupitishia pesa za kodi za serikali yao benki ya TZ, hata kama imesajiliwa nchini Kenya?

View attachment 1926663

View attachment 1926664
Hio sio kweli. Ukiangalia vizuri hizo form utaona kwamba KCB na NMB ni benki ya anaefanya malipo (account holder). Na hela inalipwa kwenda kwa Commissioner for Customs and Excise (TRA) - Bank of Tanzania.
 
Pole sana ndugu, naomba nikueleweshe hiyo unayoiona hapo ni bank ya mlipa kodi (payer) na si bank ya mpokeaji (receiver) wakati wa kujaza return forms ili upate kiwango ambacho unatakiwa kulipa kama kodi, huwaga unaingiza na jina la bank yako na details za akaunti yako, hii inawezesha bank yako ku transfer hela kutoka kwenye akaunti yako na kwenda BOT moja kwa moja ambapo walipa kodi wote ndio tunapeleka huko. So worry out hakuna makusanyo ya kodi yanayokaa kwenye commercial bank. Kila unapolipa kodi iwe ni bank A, au bank B, mzigo wote unaenda BOT hapohapo!!!
 
Tuna safari ndefu sana. Mabenki ni wakusanyaji tu wa mapato ya TRA yanayopelekwa BoT. Huko kwenye taasis za kifedha zinapita

Sio kwamba zinapita tu!

Hiyo ni tenda au biashara kapewa Mkenya. Faida inayopatikana inaenda kwa mmiliki wa Kenya Commercial Bank huko Kenya!

Kwenye dunia ya ushindani au vita ya kiuchumi kwa nini usaidie kujenga taasisi za kibenki za nchi nyingine badala ya za kwako mwenyewe ????

Kwa nini hiyo tenda asipewe Tanzania Postal Bank, au CRDB au Benki ya Wanawake Tanzania??????!
 
TRA na BOT watajitetea kwa sababu zozote zile lakini sisi tunaolipa kodi ktk nchi hii, kwa kujua nani anamiliki KCB (Kenya Commercial Bank) hii ni chini ya kiwango cha uzalendo uliohubiliwa miaka mitano iliyopita. Nalinganisha malipo niliyofanya 2020 na mwaka huu, yakielekezwa benki tofauti kabisa!!

Tunafahamu ni Benki iliyosajiliwa hapa nchini lakini pesa ya kodi za serikali kupitia benki ya muwekezaji wa nje badala ya NMB ambako serikali ina hisa, ni ufisadi. TRA wanafidika nini kuitumia KCB? Imetokea nini baada ya kifo cha Magufuli? Je, KRA ya Kenya, kwa ubaguzi wao kibiashara, inaweza kupitishia pesa za kodi za serikali yao benki ya TZ, hata kama imesajiliwa nchini Kenya?

View attachment 1926663

View attachment 1926664
Ukiwa unatengeneza control namba system inakupa option ya kuchagua bank unayotaka kulipia, system inatoa list ya bank zote na mteja alichagua KCB ndo maana inaonekana apo
 
Kwa kujenga uwanja wa ndege Chato sio ? Na kukwapua Tri 1.5?
Mkuu 'Lord', sisahau mtu ninapojibishana naye humu ndani ya JF, na ninakumbuka sana nilishajibishana nawe na nakuelewa vyema ulivyo kutokana na michango yako ya ushabiki tu!
Sasa hivi umehamishia ushabiki wako kwa 'Maza Mizinguo', kwa hiyo bila shaka hukumbuki chochote ulichokwisha shabikia enzi hizo za Magufuli.

Sasa sijui upofu wa ushabiki wako kwa mama ndio unakufanya usahau , na kudhani kwamba nami nashabikia uwanja wa ndege wa Chato?
 
TRA na BOT watajitetea kwa sababu zozote zile lakini sisi tunaolipa kodi ktk nchi hii, kwa kujua nani anamiliki KCB (Kenya Commercial Bank) hii ni chini ya kiwango cha uzalendo uliohubiliwa miaka mitano iliyopita. Nalinganisha malipo niliyofanya 2020 na mwaka huu, yakielekezwa benki tofauti kabisa!!

Tunafahamu ni Benki iliyosajiliwa hapa nchini lakini pesa ya kodi za serikali kupitia benki ya muwekezaji wa nje badala ya NMB ambako serikali ina hisa, ni ufisadi. TRA wanafidika nini kuitumia KCB? Imetokea nini baada ya kifo cha Magufuli? Je, KRA ya Kenya, kwa ubaguzi wao kibiashara, inaweza kupitishia pesa za kodi za serikali yao benki ya TZ, hata kama imesajiliwa nchini Kenya?

View attachment 1926663

View attachment 1926664
TRA wanatakiwa kujibu hii hoja
 
Sikia ndugu, serikali ina hisa 100% kwenye benki ya serikali iliyoitwa TPB bank (Tanzania Postal Bank) au Bank ya Posta ambapo kwa sasa inajulikana kama TCB (Tanzania Commercial Bank), sasa swali la kizushi ni kwamba kwanini huduma nyingi za kiserikali hazipitii bank hii ya serikali mfano mishahara ya watumishi wa umma na malipo mengine kadha wa kadha?
Swali zuri sana
 
Sio kwamba zinapita tu!

Hiyo ni tenda au biashara kapewa Mkenya. Faida inayopatikana inaenda kwa mmiliki wa Kenya Commercial Bank huko Kenya!

Kwenye dunia ya ushindani au bita ya kiuchumi kwa nini usaidie kujenga taasisi za kibenki za nchi nyingine badala ya za kwako mwenyewe ????

Kwa nini hiyo tenda asipewe Tanzania Postal Bank, au CRDB au Benki ya Wanawake Tanzania??????!

Unauhakika na ulichokiandika?
Kwamba KCB peke yake ndio wanakusanya mapato ya TRA kwa control number?

Na hata kama ni kweli tenda ilitangazwa benki zingine wakashindwa kwa vigezo, ingekua nongwa?
 
Hio sio kweli. Ukiangalia vizuri hizo form utaona kwamba KCB na NMB ni benki ya anaefanya malipo (account holder). Na hela inalipwa kwenda kwa Commissioner for Customs and Excise (TRA) - Bank of Tanzania.
Alietoa mada ni mpotoshaji tuu hajui anachoongea au ana Nia ovu.
 
NMB kama inaogopa mteja wa diaspora kuwa na account ya U$ 10,000 wanaogopa siku ukitaka kutoa hela yako watayumba, je siku serikali inataka kutoa Tshs1,000,000,000,000 NMB inaweza kuyumba hivyo serikali imeamua kusambaza makusanyo yake ya trilion karibu 2 ktk Benki zaidi ya moja na kuwa na uhakika kuzipata wakitoa taarifa ya dharura / short notice .

NMB ukwasi wake haumpi mteja uhakika wa kupata fedha akiomba ghafla kiasi kikubwa kitoke kwa mara moja.

Tujiulize kwanini serikali haikopi mkopo wa kujengea miradi mikakati mikubwa toka CRDB Bank, NMB Tanzania, DTB n.k Benki za kitanzania? Kwanza hazina mtaji mkubwa kuhimili pesa ndefu kutoka mara moja pia hazina mtaji wa fedha za kigeni kama US$, Euro£ kuikopesha Serikali ya Tanzania kujenga reli, mabwawa ya umeme au hata barabara ya kilometa 100 !

Ni kama uende kwa agent wa M-Pesa uchochoroni ukasema unataka kutoa au kuhamisha Tshs. 20,000,000 muda huo huo, ajenti hataweza kutekeleza wala hatakubali ufanye naye biashara maana mtaji wake ni mdogo na ndivyo ilivyo kwa NMB Tanzania, KCB, CRDB Bank haiwezi kufanya miamala mikubwa na serikali ya trilioni kadhaa kwa mkupuo mmoja kama itahitajika kwa dharura ya haraka au mikopo mikubwa ya fedha za ndani au kigeni na ndiyo maana serikali za nchi masikini huenda kukopa benki kubwa za mabeberu wa ulaya, Marekani na Asia.
 
Unauhakika na ulichokiandika?
Kwamba KCB peke yake ndio wanakusanya mapato ya TRA kwa control number?

Na hata kama ni kweli tenda ilitangazwa benki zingine wakashindwa kwa vigezo, ingekua nongwa?

Tenda ilitangazwa wapi KCB wakashinda ???

Na hata kama kulikuwa na tenda, kwa nini mgeni aalikwe kwenye strategic tender such as this?

Benki ya kibongo inaweza kuachwa ishinde tenda ya kutunza hela ya kodi ya Kenya ???

Tusiwe vidampa mbele ya Wakenya jamani!

Hii dunia ni ya ushindani, Kenya is a regional competitor, mnampaje ashike hela ya kodi ya Mtanzania nyinyi TRA dunderheads ?

Fukuza kazi CEO wa TRA. Juzi kafanyisha written interview, vijana wamekwenda Dodoma from across the country halafu matokeo yamefutwa, kisa, TRA walivujisha majibu kabla ya interview.

Fire the dusche bag executives.
 
Back
Top Bottom