NMB yawaburuza CRDB na wenzake kifaida chini ya Mwanamama Ms Ruth Zaipuna, huenda Ukimwacha Rais Dkt Samia na Spika Dkt. Tulia mwingine ni huyu Mama

Financial Intelligence

Senior Member
Sep 29, 2023
114
246
IMG-20231106-WA0013.jpg

MS Ruth Zaipuna Mkurugenzi Mkuu NMB.

======
Wasalaam Jf team,

Waswahili tunasema " Mnyonge Mnyongeni lakini haki yake Mpeni "

Sote tunakumbuka baada ya NBC Bank kuvunjwa Mwaka 1997 na baadae kuanzishwa kwa Benki mpya ya Makabwera ya NMB na baadae Benki hiyo kubinafsishwa kwa Rabobank ya Uholanzi iliyomiliki hisa asilimia 49 na Rabo baadae kumuuzia baadhi ya Shea Arise,

Wakati wote NMB PLC imekuwa ikiongozwa na watu kutoka nje ya nchi tu isipokuwa huyu Mkurugenzi wa Sasa Bi Ruth Zaipuna aliyekabidhiwa nafasi hiyo ya Ukurugenzi Mkuu rasmi mwaka 2020.

Kumbukumbu zinaonesha wakati mama huyu anaingia madarakani NMB bank ilikuwa na matawi yapatayo 100 tu nchi nzima na ATMs zipatazo 500 nchi nzima.

Leo NMB bank imefikisha matawi zaidi ya 230 na ATMs zaidi ya ATMs 1,000 na mawakala zaidi 12,000 nchi nzima hii ni sawa na kusema mama huyu ameikuza bank hii ya Makabwera kwa zaidi ya marambili, yaani ukuaji wa 100% au kwa lugha rahisi ni sawa na kusema NMB bank PLC imefika katika Kila Jimbo la Uchaguzi la kiserikali haba bara.

Kutoka katika tovuti ya NMB taarifa zinaonesha NMB bank ilikuwa na wateja wasiozidi 600,000 miaka kumi iliyopita na wakati huu wa Ruth Zaipuna banki hii imefikia wateja zaidi ya 6M nchi nzima,karibu mara kumi zaidi.

Kuhusu Uzalendo & Uzawa Kunajambo la kujifunza kwa hawa wanawake watatu yaani Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan, Spika wa bunge la JMT na IPU Mhe Dkt Tulia Aksoni na Mkurugenzi Ruth Zaipuna kwa namna wanavyoleta mabadiliko ya kasi kwenye taasisi wanazoziongoza,

Hebu tazama orodha hii ya faida kwa mabenki kumi ya Tanzania yaliyofanya vizuri katika robo ya tatu tu ya mwaka huu wa 2023 ndio utaelewa vizuri nachosema kuhusu huyu Mkurugenzi.

1. NMB Bank: TZS 398 billion

2. CRDB Bank: TZS 280 billion

3. Stanbic Bank: TZS 95 billion

4. StanChart: TZS 64 billion

5. NBC Bank: TZS 62 billion

6. Citibank TZS 44 billion

7. PBZ TZS 41 billion

8. Exim Bank TZS 40 billion

9. Absa Bank TZS 37 billion

10. KCB Bank TZS 35 billion

Taarifa zinaonesha faida ya Jumla kwa mabenki yote Tanzania ni shilingi trilioni moja katika robo hii ya tatu, Hii ni sawa na kusema NMB PLC pekee anamiliki 40% ya faida yote huku ikimpiku kwa mbali mshindani wake wa karibu CRDB bank kwa zaidi ya TZS 118 BL sawa na 70% ya faida yake.

Wakati Ruth Zaipuna anakuwa Mkurugenzi Mkuu Benki hii ilikuwa na wastani wa faida ya TZS 200BL baada ya kodi wakati Leo faida imekuwa na kufikia wastani wa karibu TZS 400BL kwa mwaka yaani sawa na marambili zaidi.

Pia, taarifa zinaonesha Benki ya NMB inashika nafasi ya sita kwa Ukubwa katika nchi zote Kusini mwa jangwa la Sahara na ndio Benki pekee toka Tanzania inayoshindana kimataifa katika ukubwa wa Biashara.

Watanzania tuna la kujivunia toka kwa Mkurugenzi huyu mzawa akisaidiwa na management nzima ya NMB PLC pamoja na Bodi ya Wakurugenzi wa NMB PLC chini ya Dkt Edwin Mhede, Hakika Mmestahili Heshima.

Kwa msiofahamu Mwaka 2021, Benki ya NMB chini ya Ruth Zaipuna ilitambuliwa na kutunukiwa tuzo saba za kimataifa
ikiwemo tuzo ya Euromoney ya Ubora, ikiitambua benki ya NMB kama Benki
bora Tanzania (kwa miaka tisa mfululizo) na tuzo kutoka Jarida la Global
Finance ikiitambua benki ya NMB kama benki salama zaidi Tanzania.

Pia mwaka 2021, benki ya NMB ilitambuliwa na kupewa tuzo na Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) ikiitambua kama mlipa kodi mkubwa zaidi kwenye
sekta ya fedha na pia mlipa kodi mkubwa namba tatu kwa ujumla nchini hii ni chini ya Ruth Zaipuna.

Kwa matokeo haya, Huenda Ukimwacha Rais Dkt Samia na Spika Dkt Tulia mwingine ni huyu Ruth Zaipuna wa NMB PLC deserves better.
 
Leo NMB bank imefikisha matawi zaidi ya 200 na ATMs zaidi ya ATMs 1,000 nchi nzima hii ni sawa na kusema mama huyu ameikuza bank hii ya Makabwera kwa zaidi ya marambili, yaani ukuaji wa 100% au kwa lugha rahisi ni sawa na kusema NMB bank PLC imefika katika Kila Jimbo la Uchaguzi la kiserikali haba bara.
Ingekuwa analysis nzuri kama ungesema as compared to what? Maana banking industry yote ya Tanzania miamala ya ATM, mobile banking, branches zimekua zaidi ya mara mbili!! Yaani hata Maendeleo bank imekua zaidi ya Mara mbili ilihali ina assets ndogo zaidi.
Pia,taarifa zinaonesha Benki ya NMB inashika nafasi ya sita kwa Ukubwa katika nchi zote Kusini mwajangwa la Sahara na ndio Benki pekee toka Tanzania inayoshindana kimataifa,
Yes ilikuwa na assets nyingi miaka na miaka wala sio sababu ya
Wakati Ruth Zaipuna anakuwa Mkurugenzi Mkuu Benki hii ilikuwa na wastani wa faida ya TZS 200BL baada ya kodi wakati Leo faida imekuwa na kufikia wastani wa karibu TZS 400BL kwa mwaka yaani sawa na marambili zaidi
Analysis ya faida za kibenki hatupimi kwa billion hizi na hizi, maana obvious mtaji ukikua lazima faida ikue. So huwa wanapima kwa return on assets, au return on equity, sasa tukienda huko ndio ungetupa picha kamili kwamba kwa kila ongezeko la mtaji je kazalisha shingapi. ROA, ROE, au NIM.
Watanzania tunalakujivunia toka kwa Mkurugenzi huyu mzawa akisaidiwa na management nzima ya NMB PLC pamoja na Bodi ya Wakurugenzi wa NMB PLC chini ya Dkt Edwin Mhede, Hakika Mmestahili Heshima.
Yeah apewe pongezi kwa kumaintain ukubwa wa NMB lakini kama mnamfanyia branding ili ateuliwe na Mama samia kwenye siasa mtampoteza. She might be good sababu ya ukubwa wa taasisi ila mkimpeleka sijui wizara ya uchumi, au sijui biashara na viwanda she'll be exposed of her weaknesses na atapoteza status yake.

Waacheni wabaki kwenye corporate world wana mchango mkubwa huko ila kwenye siasa atakua kama Kimei au Muhongo
 
Kuna vichwa pale NMB ni balaa ukiacha ZAIPUNA Kuna kichwa kinaitwa MPONZI Jamaa mmoja hivi ana upara ni hatari. Kuna DONATUS Richard mkuu wao wa biashara yaani wapo creative balaa I wish hivi vichwa vije vimsaidie mama kwenye uchumi pia vipewe uhuru wa kufanya kazi aiseee tutatoboa
 
Back
Top Bottom