UZUSHI Tohara hupunguza ukubwa wa sehemu za siri za mwanamme

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Wataalamu wa afya huelezea umuhimu na faida za kufanyika kwa tendo hili kwa wanaume.

Baadhi ya sehemu wanaume huwa hawatahiriwi kabisa, na wengine wanaotahiri husubiri hadi mtoto afikishe walau miaka 12 ndipo afanyiwe tendo hilo kwa uoga wa kupunguza ukubwa wa viungo hivyo.

B9D7E489-4826-4743-A8E2-CB85C73E2EF3.jpeg

Madai haya yamekuwepo kwa muda mrefu, na majibu sahihi bado hayajatewa. Ni kweli kuwa tohara hupunguza ukubwa wa via vya uzazi vya mwanamme?
 
Tunachokijua
Ni upasuaji mdogo unaofanyika ili kuondoa ngozi ya mbele inayofunika sehemu za siri za mwanamme.

Asili ya utamaduni huu ni imani za kidini, ambazo baadae zilithibitishwa kuwa na faida kiafya. Leo, watu hutahiri kwa sababu za kiafya, au za kidini.

Tohara ifanyike Hospitalini
Mwanamme huzaliwa na ngozi inayofunika uume. Kupitia tohara, ngozi hii huondolewa kwa kufanya upasuaji mdogo usiotumia muda mrefu sana, kati ya dakika 15-30.

Kwa sababu za kiusalama, pamoja na kuhakikisha kuwa tendo hili linafanyika kwa ufanisi mkubwa, ni vizuri kama likifanywa hospitalini.

Tohara kupunguza ukubwa wa uume
Tofauti na jinsi ambavyo watu wengi huamini, tohara haiwezi kudumaza afya ya sehemu za siri za mwanamme hata kama itafanyika kwa mtoto mchanga.

Ukuaji wa viungo vyote vinavyounda mwili wa binadamu huongozwa na mifumo rasmi iliyoshikizwa kwenye vinasaba vya urithi pamoja homoni mbalimbali za mwili.

Msingi wa taarifa hizi hauwezi kuathiriwa kwa kukata ngozi ya mbele inayofunika sehemu hizo.

Kama ambavyo mtu huzaliwa akiwa na asili ya urefu, ufupi, macho makubwa au kipara na asiwe na uwezo wa kuibadili asili hii, vivyo hivyo kwa ukubwa au udogo wa maungo haya muhimu kabisa kwa afya ya uzazi wa mwanamme kwa sababu kinacho ondolewa ni ngozi tu, siyo kichwa wala nyama ya sehemu hizo.

Aidha, Dkt. Godfrey Chale ambaye ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi nchini Tanzania akizungumza na JamiiForums amesema kuwa madai haya hayana ukweli.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, miongozo ya Shirika la Afya Duniani (WHO) pamoja na Kituo cha Udhibiti na Kinga ya Magonjwa (CDC), tohara huwa na faida nyingi kwa afya ya mwanamme mwenyewe, pamoja na mwanamke ambaye atashiriki naye tendo la ndoa.
  1. Tohara hupunguza nafasi ya kupata maambukizi ya mara kwa mara kwenye mfumo wa mkojo hasa kwa watoto wadogo.
  2. Hupunguza nafasi ya kuugua Saratani ya uume pamoja na magonjwa mengine ya zinaa hasa VVU/UKIMWI
  3. Hupunguza uwezekano wa kuugua saratani ya mlango wa kizazi kwa wanawake. Hii ni kutokana na ukweli kuwa mwanamme asiye tahiriwa huwa na uwezekano mkubwa wa kubeba Virusi vya Human papilloma kuliko yule aliyetahiriwa.
  4. Tohara husaidia pia kurahisisha suala la usafi kwa mwanamme.
Tohara inaweza kufanyika muda wowote, kwa watoto wachanga pamoja na watu wazima, hata hivyo uponaji wa haraka huonekana kwa watoto kwa kuwa huwa bado hawajafikia umri wa kuonesha mwitikio wa hisia za kimapenzi hivyo kuufanya uume usimame mara kwa mara kama ilivyo kwa watu wazima.

Katika dini za Kiyahudi, tendo hili la kiimani hufanyika siku ya 8 tangu kuzaliwa kwa mtoto. Kwa ujumla wake, jamii mbalimbali huamua kwa kadri wao wanavyoona inafaa ni lini hasa tohara ifanyike kwa vinaja wao wa kiume.
Wataalamu wa afya huelezea umuhimu na faida za kufanyika kwa tendo hili kwa wanaume.

Baadhi ya sehemu wanaume huwa hawatahiriwi kabisa, na wengine wanaotahiri husubiri hadi mtoto afikishe walau miaka 12 ndipo afanyiwe tendo hilo kwa uoga wa kupunguza ukubwa wa viungo hivyo.

View attachment 2410644

Madai haya yamekuwepo kwa muda mrefu, na majibu sahihi bado hayajatewa. Ni kweli kuwa tohara hupunguza ukubwa wa via vya uzazi vya mwanamme?
Sio kweli mkuu ni maneno ya kukatishiana tamaa mbaki na magovi ambayo SI mazuri kiafya
 
Fungua hii link mkuu utapata madini. Does Circumcision Affect Penis Length?
Mkuu nimesoma lakini naona hakuna hoja nzito Sana juu ya swala Hilo

Kikubwa kama wanavyosema Ile ngozi ya juu ikiondolewa inapunguza urefu WA penis Hilo liko wazi kwakuwa kulikuwa na linyama la ziada,lkn si kwamba inapunguza urefu WA penis excactly

Wanasema kuna upungufu WA 3/8 inches hata kama ni kweli sio big ishu coz tofauti ni ndogo Sana kana kwamba hakuna tofauti

Lkn nimechoka zaidi kuona wenye utafiti wao kushindwa kuona athar za kiafya kama mtu akiwa hajataahiriwa, nimejiuliza hata kama ni sahihi kuamini watu kama hawa.

Lakini vile vile wamesema Hali hiyo pia husababishwa na mambo ya genetics,hormonal imbalances na matatizo mengine ambayo huwakumba watoto udogoni

Kwa upande wangu sikubaliani na utafiti wao naona hauna mashiko.
 
Ila ni kweli kabisa ikifanyika udogoni inapona mapema sana
ni kweli inapona mapema na pengine mtoto anakua anajiona yupo hivyo ni jambo jema ila kanakuwa kafupi, hakarefuki wa mpangilio ambao huwepo kiasili.
 
ni kweli inapona mapema na pengine mtoto anakua anajiona yupo hivyo ni jambo jema ila kanakuwa kafupi, hakarefuki wa mpangilio ambao huwepo kiasili.
Kuhusu kuwa kafupi si sahihi coz inayokatwa ni ngozi na si penis yenyewe

Ufupi au urefu unatokana na genetics
 
Wataalamu wa afya huelezea umuhimu na faida za kufanyika kwa tendo hili kwa wanaume.

Baadhi ya sehemu wanaume huwa hawatahiriwi kabisa, na wengine wanaotahiri husubiri hadi mtoto afikishe walau miaka 12 ndipo afanyiwe tendo hilo kwa uoga wa kupunguza ukubwa wa viungo hivyo.

View attachment 2410644

Madai haya yamekuwepo kwa muda mrefu, na majibu sahihi bado hayajatewa. Ni kweli kuwa tohara hupunguza ukubwa wa via vya uzazi vya mwanamme?
Ndio kwani kinachotolewa ni prepuce sasa hapo lazima vpimo visiwe sawa kama prepuce itabakia
 
Mkuu nimesoma lakini naona hakuna hoja nzito Sana juu ya swala Hilo

Kikubwa kama wanavyosema Ile ngozi ya juu ikiondolewa inapunguza urefu WA penis Hilo liko wazi kwakuwa kulikuwa na linyama la ziada,lkn si kwamba inapunguza urefu WA penis excactly

Wanasema kuna upungufu WA 3/8 inches hata kama ni kweli sio big ishu coz tofauti ni ndogo Sana kana kwamba hakuna tofauti

Lkn nimechoka zaidi kuona wenye utafiti wao kushindwa kuona athar za kiafya kama mtu akiwa hajataahiriwa, nimejiuliza hata kama ni sahihi kuamini watu kama hawa.

Lakini vile vile wamesema Hali hiyo pia husababishwa na mambo ya genetics,hormonal imbalances na matatizo mengine ambayo huwakumba watoto udogoni

Kwa upande wangu sikubaliani na utafiti wao naona hauna mashiko.
Athari ni zipi za kiafya kwa mtu asiyetahiriwa ?
 
Athari ni zipi za kiafya kwa mtu asiyetahiriwa ?

# hupata tatizo la phimosis,Hali ya Ile ngozi kutokaa mahala pale baada ya kuvutika

# hupata ugonjwa WA balanitis, ngozi ya juu katika kichwa cha uume kuvimba na kuleta maumivu kama Moto hivi

# kupata magonjwa ya njia ya mkojo kirahisi

# ni rahisi kuambikizwa magonjwa ya zinaa

# ni vigumu kuufanyia uume wako usafi
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom