Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,325
33,131
muwashoo.jpg

Sehemu ya uke iliyoathirika kwa viuvimbe kutokana na ugonjwa unaosababishwa na na virusi ujulikanao kama Human Papillomavirus (HPV). Ni moja ya magonjwa yanayosababisha muwasho sehemu za siri. Picha kwa hisani ya Taasisi ya Mutrition Facts.

Muktasari:​

Gazeti hili limepokea maswali mengi kuhusu tatizo la kuwashwa sehemu za siri. Kupitia makala hii daktari anayajibu, akielezea chanzo, tiba na namna ya kujitunza dhidi ya maambukizi.
Kuwashwa sehemu za siri kunaweza kuwa dalili ya maradhi fulani bila kujali jinsi, muwasho unaweza kuwa umesababishwa na ugonjwa wa ngozi, zinaa au mzio.
Kuwashwa hutokea pale ngozi inapokereketa ikiambatana na hamu ya kutaka kupakuna. Muwasho huongezeka pale unapokaa na kukiwa na unyevunyevu.
Sababu kuu za kuwashwa kwenye njia ya haja kubwa inaweza ikawa ni sababu fulani kama vile kutojisafisha vizuri baada ya haja, kula vyakula vyenye viungo vingi, kuharisha, vidonda kwenye njia hiyo, maambukizi ya fangasi, bawasiri (hemorrhoids) au minyoo.
Baadhi ya vitu vinavyosababisha muwasho huhitaji matibabu ya hali ya juu zaidi ili kuvikabili. Ikiwa unawashwa kwa muda mrefu ni vyema kumuona daktari.

Kwa wanaume
Kuwashwa uume au sehemu zingine za siri za mwanamume husababishwa na sababu zilezile zinazosababisha muwasho sehemu nyingine za mwili.
Maambukizi hasa ya magonjwa ya zinaa, ndio chanzo kikuu cha kuwashwa uume. Sababu nyingine ni maradhi ya fangasi, ugonjwa wa upele (scabies), chawa, mzio na maambukizi ya bakteria.

Kwa wanawake

Kinachosababisha muwasho katika sehemu za siri za mwanamke ni maambukizi ya fangasi ukeni, kuvimba uke wakati wa hedhi na usio wa hedhi, trikomonasi, minyoo, tatizo la shingo ya kizazi, wasiwasi, tatizo la mfumo wa kinga na kisukari.
Maambukizi ya fangasi ni moja ya tatizo kwa wanawake linalosumbua. Tatizo hili husababishwa na fangasi waitwao Candida. Dalili kuu ni kuwashwa ukeni, kuvimba na kutoa uchafu mweupe kama maziwa.
Ugonjwa wa kuvimba uke kitaalamu unajulikana kama Vulvovaginitis. Ni ugonjwa unaoathiri kwa kusababisha sehemu za nje za uke na uke wenyewe kuvimba. Dalili kuu ni kuwashwa ukeni, maumivu wakati wa haja ndogo, kukereketa unapokojoa na kutokwa na uchafu ukeni.
Kuvimba uke baada ya hedhi kukoma ama Postmenopausal Atrophic Vaginitis.
Kwa kawaida hutokea baada ya hedhi kukoma. Hali hii huongeza maambukizi ukeni na huweza kusababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa.
Maambukizi ya trikomonasi. Ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na kimelea aitwaye trichomonas. Dalili kuu ni muwasho katika uke au uume na kutokwa na uchafu ukeni.
Ugonjwa wa minyoo wajulikanao kama pinworm. Ni maambukizi ya minyoo wadogo wenye umbo la pini wanaoweza kuambukiza kwenye utumbo na kusambaa maeneo mbalimbali. Ugonjwa huu huwatokea zaidi watoto wa kati ya miaka mitano na 10.
Uvimbe wa mrija wa urethra ama kwa kitaalamu urethritis. Ni maambukizi kwenye njia ya kutolea mkojo nje inayoungana na kibofu. Dalili kuu ni mkojo kuchoma, maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kutokwa uchafu.
Tatizo la warts. Hivi ni viuvimbe vidogo vinavyotokea juu ya ngozi sehemu za siri.
Vinaweza kuota kama kamba au vimikia vidogovidogo vinavyokua kwa kurefuka. Ugonjwa unaoenezwa kwa njia ya kujamiiana na husababishwa na virusi vijulikanavyo kama Human Papillomavirus (HPV). Vivimbe vinaweza kusababisha muwasho na maumivu na hata kuvuja damu vikikandamizwa.
Saratani sehemu ya nje ya uke. Hutokea nje ya uke na kuambatana na hisia za kuwashwa sehemu hizo.
Ugonjwa wa wasiwasi ama Generalized Anxiety Disorder (GAD). unaotokana na hofu ya matukio fulani. Wakati mwingine husababisha kujikuna sehemu mbalimbali hata za siri.
Ugonjwa wa Sjogren. Ni tatizo katika mfumo wa kinga ya mwili unaoathiri tezi zinazosaidia mwili kutengeneza unyevunyevu kwenye macho na mdomo. Ugonjwa huu huathiri wanawake zaidi kuliko wanaume.
Tatizo la kisukari pia huweza kumuathiri mwanamke sehemu za siri. Ni ugonjwa sugu wa mfumo wa kuzalisha nishati mwilini unaosababishwa na kasoro katika utengenezaji wa insulini au utendaji kazi wake.
Kisukari kilichokomaa kinaweza kusababisha maumivu ya tumbo, kichefuchefu, kizunguzungu na kuwashwa sehemu za siri.
Njia za kuepuka kuwashwa
Wanaume wanapaswa kufuata hatua mbalimbali ili kuepuka kuwashwa sehemu za siri. Miongoni ni kuosha vizuri uume na kwa wale ambao hawajatahiriwa wanapaswa kuosha kwa umakini zaidi hadi sehemu za ndani za govi.
Namna nyingine ni kuweka sehemu za siri katika hali ya usafi na ukavu, kwa maana unyevunyevu unaweza kusababisha maambukizi. Matumizi ya poda yanaruhusiwa hasa kipindi cha joto kali.
Vaa nguo isiyobana sana, iliyotengenezwa kwa vitu asilia kama pamba. Badili nguo ya ndani angalau kila siku na vaa kondomu kila unapofanya ngono na mwanamke usiyejua hali yake kiafya.
Wanawake wanapaswa kila baada ya kukojoa au kujisaidia haja ndogo kuosha sehemu za siri kuanzia mbele yaani ukeni na baadaye nyuma kwenye njia kubwa. Huu ni mfumo wa kuzuia maambukizi ya bakteria walioko kwenye njia ya haja kubwa kwenda ukeni.
Mwanamke aepuke matumizi ya vitu vyenye kemikali kama marashi katika kusafisha uke kwa maana huharibu hali ya asidi ya uke na kuua bakteria wanaolinda maeneo hayo na kufanya iwe rahisi kushambuliwa na maradhi.
Weka sehemu zako za siri katika usafi na ukavu. Tumia sabuni kidogo katika kusafisha sehemu zako za siri na maji mengi. Kausha sehemu zako za siri kila baada ya kuoga au kuogelea na epuka kukaa na nguo mbichi kwa muda mrefu.
Vaa nguo isiyobana, iliyotengenezwa kwa pamba ili unyevunyevu usitokee.
Badili nguo za ndani kila baada ya saa 24. Epuka ngono bila kinga hasa ukiwa na hofu na mpenzi kuwa ana maradhi. chanzo. Fahamu sababu, tiba ya muwasho sehemu za siri
 
Attachments

  • Fahamu sababu, tiba ya muwasho sehemu za siri.jpg
    Fahamu sababu, tiba ya muwasho sehemu za siri.jpg
    24.1 KB · Views: 4
View attachment 2713169

Okay me imetokea hivyo Kwa mke wangu harafu ni mjamzito
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom