Tido Mhando atemwa TBC

nimeamka na mshangao, huyu huyu Tido.....he was once a bad guy akiwa TBC, leo naona sifa nyiingi na watu tuna sympasize......suddenly he is a nice guy!
Kazi kweli kweli

Kwanza tunajadili kuhusu MAPINDUZI aliyoyafanya katika kitengo husika, Kubali kwa TVT to TBC jamaa amefanya mapinduzi.

Alafu kwa suala la ubaya wake , kwa sasa ni rahisi kujua hata kama jamaa alikuwa ni mbaya........ kwa picha halisi tukubali kuwa alikuwa anafanya mambo mmengine under pressure..... thats why kwa yalipo fikia na ubaya wake ndo tunaona kuwa msukumo wa mambo mengine ulikuwa unatika kwa wakubwa so amefika mwisho na anaweza kuonekana shujaa.... Ni mtazamo wangu tu.
 
Unajua tusiiperekee hii nchi kama ya watu fulani hii nchi ya kwetu sote na inaongozwa kwa sheria . Kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa umma ya 2008 na kanunu zake katika ajira za mikataba mwajiri lazima atoe notes/taarifa b4 six month mkataba kumalizika na anatakiwa kueleza kuwa je ataongeza mkataba au ndo mkatba utakuwa umekwisha. Tunajua wako watanzania wengi wanaoweza kuliongoza shirika hilo lakini tufuate sheria na haki za mtumishi. Tido ana haki zake za kiutumishi thus y hata yeye anashanga sana kwa kitendo hicho.
Hii nchi inako elekea si kuzuria kama mambo yenyewe yanakwenda huko kwamba lazima ufanye kazi kwa matakwa ya watu fulani hatuwezi fika na mimi naawambia watanzania huyo mkurugenzi atakayeletwa hatakuwa kama tido atalipeleka shirika kama ccm wanavyotaka.tido ndiye aliyefanya tbc ipendwe na watanzania walio wengi kutokana na kuboresha vipindi kuwa vya kisasa zaidi na kuweka wigo mpana wa watu kutoa maone yao.
Tbc kwishedeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee sasaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa tunarudi enzi za tvt ,rrd.
 
i
Thanks mkuu nilikuwa sifahamu hili, lakini je usipopewa hiyo notice inamaanisha unakuwa automatically eligible kwa mkataba mwingine? Na mwajiri akikosa confidence na wewe say wakati mwezi mmoja wa kumaliza mkataba umebakia na 6 months notice haikutolewa inakuwaje hapo?
Kanuni zilitaka apewe notice of reminder kuwa amebakisha miezu 6 mkataba wake kuisha barua hiyo ingeandamana na kipengele cha intent iwapo mwajiri alikuwa bado anahitaji huduma yake hivyo kumpa fursa kutafakari kama yuko tayari kuendelea.

Kwa vile sheria imefuatwa kilichokiukwa ni kanuni tuu, hivyo kitakachofamyika ni kumpatia barua ya reminder ambayo ita act retro respectively six months back kuonyesha taratibu zimefuatwa au to be fair kwake wangepaswa kumpa six months notice extention.

Hata hivyo, kila mkataba lazima una pande mbili. Baada ya kuona miezi sita imepita bila mwajiri kumletea leter of intent, ilipobaki miezi mitatu, (90 days)Tido naye kwa upande wake alipaswa kumremind mwajiri kuwa amebakiza miezi mitatu na yeye angeonyesha nia ya kurenew na kumwachia mwajiri kuamua hatma yake.
 
Mkuu Pasco, huo msimamo wako ni chini ya taratibu gani. kanuni hizo unazo-refer ni zipi? Mkataba umekwisha, hakuna dhamira ya renewal iliyotolewa. Sasa hapo kuna u-ghfla gani wakati mkataba ulikuwa definate kuhusu tarehe ya kumalizika kwake. He should have known kwamba kufika tarehe 15 December yeye si mfanyakazi tena na hivyo angejiandaa kuondoka, unless awe amepewa taarifa ya kuendelea, ambayo kwa kesi hii hakupewa. Kuishi kwa matumaini kwamba labda nitapewa halafu usipewe haiwezi kuwa sababu ya msingi ya kulalamika. Let him go and he should let people to assess the positives and negatives of his regime. Hatuwezi kumsifia kufanya kitu alichoajiriwa kukifanya. Aliyemteua alijua uwezo wake ndo maana alimpa kazi na ingekuwa de-service kama asingeifikisha TBC hapa ilipofikia because that is what he was paid for. The guy is well above 60, when is he going to rest and enjoy life after more than 30 years of hard work?
 
i will never do this if i love my country... politicizing professions!!!

Kazi itangazwe na yeye aombe... kwani alikujaje kutoka huko UK, was the process competitive??

Kila kazi lazima ishindanishwe....

Acid, I always thought Mkuu wa TBC ni presidential appointee na sio kazi ya kutangaza......Mwenye uhakika na hili atujuze.
 
nilishawaambia mkwere kwa visasi hajambo, mbona tutaona mengi, sijui jf tutasalimika kweli? Si ndio tutaitwa weekleaks wa bongo?

katiba na sheria ,mambo ya ndani,wameblock jamii forum . Katika server zao mwenyewe nimekumbana na masaibu haya .pia posta mpya jengo jipya la posta .kuna huduma ya intarnet washenzi nao pia wameblock jamii forum .
 
Kina Aci mnakosea mnaposema watu wamegeuka, hapa kuna watu wengi sana na maoni yetu pia ni mengi na tofauti sana, pamoja na kuwa yanaweza kugeuka pia. Ila wale wasiomkubali pia wapo, na waliokuwa wanamkubali pia wapo.
Pia kuna kina sie ambao hatuangalii jina, bali vitendo, mie nakubali baadhi ya vitendo vyake na baadhi sikuvikubali, nakubali amefanya kazi kubwa mpaka TBC imekubalika. Huyu ni mwana CCM, na alijitahidi sana kujivua ili aweze kuifanya kazi ya umma, kuna wakati alishindwa. Binafsi nilikuwa napenda vipindi vyao wakati bunge linaendelea, watu tulipata uchambuzi wa wiki nzima bungeni.
Documentaries za kitanzania zimekuja juu ukiacha za STAR tv ambazo kwangu ni za juu zaidi.
Ametupa thamani ya kodi yetu kwa TBC.
Ilinipa hofu wakati walipokuwa wanamtuma Shelembi mitaani huko na mambo ya ajabu ajabu yanafunuliwa na wananchi nilianza kuhisi hiki kitu hakitadumu, na kweli naona ndio basi tena. Ila moto uliouwasha hautazimika. pamoja na mapungufu yako, I hope watu uliowascout hawatatolewa kukufuata!!!!

u have said it all, and most recently swala la ukeketaji huko mara ambalo wameibua and it seemed very challenging toward the govt..
 
Ukiacha kina kimei-crdb ,dau-nssf, tido ni kati ya watanzania wanaotakiwa kupongezwa kwa kuonyesha kwa vitendo kaichukua tbc ikiwa tvt,tbc taifa ikiwa rtd lakini leo huwezi amani ndo taasisi zile za zamani ni zimekuwa bora sana na kupendwa na watu wengi sn na watanzania ni mashahidi tumeona mabadiliko kwa vitendo. Si wako watanzania wamepewa mashirika sasa yako wapi si yamekufa???????????????? .
Ushauri watu kama hawa si vyema wakatolewa kwa njia kama aliyofanyiwa tido mhando!!!!!!!!!!! Mimi naamini kwa ushenzi aliofanyiwa tido hata makabidhiaono hayatakuwa mazuri na kuna vitu vingi sn huyo atakayekuja atakavikosa ambavyo alitakiwa kusaidiwa na tido .
Tananzia inatakaa kupiga hatua mbele lakini wale amaboo wanaonekana wanaweza ndio haoo wanakuwa fired.
 
nowadays mi naona ni makopo ya maji tu yaweza kuwa renewable, so im not sure with the toilet paper, ukishananihiii unaifrash then unaweka ingine, ni mtazamo wangu tuuu.
 
mimi nilishangaa sana siku ile jk alopoenda cloud fm kipindi cha kampeni............kumbe wanasababu zao....

tido nenda baba.......... waache tuone kama watadumu........huyu rugalabamu ni ndugo na salva rweyemamu?
 
Wakati anazima mikutano ya Chadema pale jangwani alifikiri ni vizuri. Mifisadi itakuwa ilikasirishwa na midahalo ya wagombea kwenye uchaguzi wa 2010.

Mimi naona watakaoumia kwa dhati kabisa katika wapinzani ni CUF, maana CHADEMA tayari wanachombo chao cha ITV ambacho kiliapa kutotangaza kampeni za CUF na kujikita kidhati kabisa kui promote CHADEMA! sasa hii itakuwa imekula kwa CUF!!! ndio siasa hizi waache walale tu na siasa zao za Unguja na Pemba....
 
Hili ni mfano wa jambo ambalo katika nchi nyingine wananchi wangekuwa mitaani wanaandamana.

Huu sasa ni upuuzi tuache kuandamana kwa kukosa dawa mahospitalini, shule kukosa vifaa na waalimu weledi, sera mbovu za makazi na miundombinu duni......alafu tuandamane eti kisa Tido kaondolewa TBC!!

Nina shaka sana na ufikirivu wako!!
 
Afadhali umeliona hilo. Ninashangaa watu humu wapokuwa general kwamba "watu wamegeuka"! Ni lini JF ilitoa msimamo kwamba haimpendi Tido? Ni vyema Acid na wenzako mkajua kwamba hapa kuna watu wengi sana, kwa hiyo kutoa judgement kuwa watu wana msimamo fulani inabidi uwe specific sana. Heri ungesema "Sinkala umegeuka" au "Invisible umegeuka" na ukaweka quotes za misimamo ya zamani. Kuna watu humu hawachangii mara kwa mara, kwa hiyo ukiwaita kuwa wamegeuka wakati hawakuchangia hiyo hoja unayosema wamegeuka, utakuwa haujawatendea haki!

Sinkala usemalo ni kweli kuwa watu hawachangii mara kwa mara, lakini kama alivosema Acid kipindi cha uchaguzi Tido hakuwa fair kabisa kwa vyama vya upinzani, watangazi wengi walikuwa wanaonesha msimamo wa wazi kabisa kuwa wanashabikia CCM (eg mama Kimaro) na Tido hakuchukua hatua yoyote acha yaliyomkuta yamkute.
 
Kumpiga chura teke ni kumuongezea mwendo(waswahili),huwezi kujua kujua ukubwe wa chura mpaka atakapo kufa (waghana)anayebisha na adishe tbc itakufa mda si mrefu umaarufu wa itv katika habari utarudi kama zamani,................alafu tunashangaa la tido je la yule wa itv...............nani yule alikuwa akirusha kipindi cha matrafiki na rushwa ameishia wapi.........hii ndo bongo unacheza na mafisadi wewe................2tumbuke kuanda jf nyingine hii itafungwa mara 2....................unakumbuka ze utamu/yuko wapi kama si jela..............hatujui tu ni nani na kina nani hawa.............wanaofanya yote haya nimekumbuka rai alipoinunua kada anaedaiwa kuwa fisadi na bwana mengi,,,,,,,,ilikufa hakuna kitu pale tena............tido ulitakiwa uwe na jicho la tatu lenye kuona mbali lakini umeshaona sasa sio mbaya......
 


Nilikuwa nafuatilia magazeti ya leo yalivyokuwa yanasomwa pale TBC, lilipofika gazeti la Mtanzania, mtangazaji hakuisoma ile habari ambayo ndiyo imebeba gazeti hilo badala yake akasoma nyingine ndogo. Jambo hili limenifanya nijiulize sana, si rahisi kuiacha habari kuu. Suala lingine linalonifanya nijiulize, ni kwa nini gazeti la Mtanzania limeweka font size kubwa sana kwenye hiyo habari? Imesomeka "Tido ang'olewa TBC"

niliona mi mwnyw yule mama alivyoruka ile habari + gazeti lililo ripoti ile habari (la mafisadi) ,made me want to connect the dots to get a bigger and brighter picture!
 
Mimi naona watakaoumia kwa dhati kabisa katika wapinzani ni CUF, maana CHADEMA tayari wanachombo chao cha ITV ambacho kiliapa kutotangaza kampeni za CUF na kujikita kidhati kabisa kui promote CHADEMA! sasa hii itakuwa imekula kwa CUF!!! ndio siasa hizi waache walale tu na siasa zao za Unguja na Pemba....
madrasa bwana daa!
 
Pole Tido nadhani sasa utakuwa na utashi zaidi juu ya nchi hii ikoje? Ulijitahidi kubalance ili usionekane mnafiki kwa wananchi na CCM lakini juhudi zako bado hazikuonekana. Hebu fikiria walivyokufanyia kama mfanyakazi wa kiwanda cha Urafiki Urafiki ukifika asubuhi unakuta bango leo hakuna kazi. Wewe ulijitahidi kufuata sheria walizotunga kama sheria ya Uchaguzi kwa kukatiza matangazo mara kwa mara pindi jamaa waliopokuwa wakishambuliwa lakini wao wameshindwa hata kukupa notice ya miezi sita kabla kwamba hawatarenew mkataba.

Kiukweli wananchi tunakupenda sana uendelee kuwa mkurugenzi wa TBC1 lakini CCM wamekupenda zaidi!!!
 
Back
Top Bottom