Tido Mhando atemwa TBC

Jamani Tido ni kichwa kizuri sana kile kwenye ile fani yake,tunapoteza mtu potential,mi nafikiri kama kuna redio na TV zinazoweza kumlipa hapa bongo achukue kazi au kama vp afungue yake

potential kwa lipi?msipende kuwapa watu sifa wasizostahili...machunu aliyotufanyia wakati wa kampeni hayasahauliki ..Noo siwezi kumsamehe hata kidogo mwache aende zake bana
 
Ahamie Star tv, au ITV, tatizo ni hata pewa ukurugenzi, by the way mie namtakia mafanikio atakapo enda.
 


Nilikuwa nafuatilia magazeti ya leo yalivyokuwa yanasomwa pale TBC, lilipofika gazeti la Mtanzania, mtangazaji hakuisoma ile habari ambayo ndiyo imebeba gazeti hilo badala yake akasoma nyingine ndogo. Jambo hili limenifanya nijiulize sana, si rahisi kuiacha habari kuu. Suala lingine linalonifanya nijiulize, ni kwa nini gazeti la Mtanzania limeweka font size kubwa sana kwenye hiyo habari? Imesomeka "Tido ang'olewa TBC"
 
wako wapi wale waliokua wanailaani TBC nao waseme yakwao?? maana hapa naona zimejaa sifa wakati very short while ago nilizoea kusoma mabaya kuhusu TBC na huyu baba??

Au ndio wale mbayuwayu sisi??

Tido Mhando, Samuel Sitta ni walewale, unafiki ndio unawasumbua kuna kipindi alijikomba kwa kina EL, then akashituka kwenye kampeni nadhani ni masharti ya wafasdhili akawaudhi CCM haya ndio malipo yake.

All in all aende tu!
 
Hivi wananchi hatuna say katika hili? Can someone tell me what lipi tunaweza kufanya kuhakikisha tido stays?

Sasa maana ya mkataba nini. Kama kamaliza mkataba, wala hajafukuzwa. Kuongezwa kipindi cha mkataba si lazima.
 
Hivi wananchi hatuna say katika hili? Can someone tell me what lipi tunaweza kufanya kuhakikisha tido stays?

Acha upupu...ulikuwa involved in the first place? kama alivyokuja ndio kaondoka...tuma application...mambo kwa merit tu hamna ku sympathise na mtu hapa
 
<b><i>tido ameisaidia chadema? Alikuwa akitangaza bila upendeleo wakati wa uchaguzi mkuu? Hii mbona siielewi?</i></b>
Tido hajaisaidia Chadema kama Tido bali kutokana na kusisitiza impartiality wakati wa uchaguzi mkuu the biggest benefactor ni upinzani na Chadema ndio the lead.

Tido amewakatalia CCM kutangaza vile vipindi vya kampeni vilivyokuwa vikitangazwa na Kipozi.

Every thing has a price, kwa kumeintain objectivity na impartiality, that is the price Tido has to pay!.
 
Tido kapigwa chini TBC1. Tusubili labda na hao akina Mhando wengine nao watapigwa chini pia!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kina Aci mnakosea mnaposema watu wamegeuka, hapa kuna watu wengi sana na maoni yetu pia ni mengi na tofauti sana, pamoja na kuwa yanaweza kugeuka pia. ...!
Afadhali umeliona hilo. Ninashangaa watu humu wapokuwa general kwamba "watu wamegeuka"! Ni lini JF ilitoa msimamo kwamba haimpendi Tido? Ni vyema Acid na wenzako mkajua kwamba hapa kuna watu wengi sana, kwa hiyo kutoa judgement kuwa watu wana msimamo fulani inabidi uwe specific sana. Heri ungesema "Sinkala umegeuka" au "Invisible umegeuka" na ukaweka quotes za misimamo ya zamani. Kuna watu humu hawachangii mara kwa mara, kwa hiyo ukiwaita kuwa wamegeuka wakati hawakuchangia hiyo hoja unayosema wamegeuka, utakuwa haujawatendea haki!
 
Sababu mkataba haujawa renewed watu mnaanza sympathy. Wakati wa uchaguzi most members hapa walikuwa wakilalamikia TBC.

Kwa nini watu tunakuwa ka vinyonga.

Mshahara wake ulikuwa shilngi ngapi?
 
Nilishawaambia mkwere kwa visasi hajambo, mbona tutaona mengi, sijui JF tutasalimika kweli? si ndio tutaitwa weekleaks wa bongo?
 
Send to a friend Friday, 17 December 2010 06:34 0diggsdigg

Sadick Mtulya, Patricia Kimelemeta
BAADA ya kufanya kazi nzuri ya kuboresha matangazo na uendeshaji wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), serikali imeamua kuachana na mkurugenzi wa chombo hicho, Tido Mhando baada ya mkataba wake kuisha, lakini mtangazaji huyo maarufu ameielezea uamuzi huo kuwa kuwa ni wa utata.
Kuenguliwa kwake kumefanyika takriban miezi miwili baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu ambao TBC iliripoti kwa kina na bila kupendelea chama chochote na hivyo kujivunia sifa kemkem kutoka kwa watazamaji wa TBC1 na wasikilizaji wa redio hiyo ya umma.

“Hatua hii imenishtua kidogo na hata hivi ninapoongea na wewe wafanyakazi wengi wamepata mshtuko na wengine wanalia," alisema Tido alipoongea na Mwananchi jana. "Ni juzi (Jumatatu) ndio niliandikiwa barua na serikali ya kutakiwa kuondoka.... ilikuwa kinyume kabisa na uratatibu wa serikali.
“Barua ya kutakiwa kuondoka niliipata mara baada ya kukutana na kuzungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Michezo, Utamaduni na Vijana , Seti Kamwanda.’’

Tido, ambaye kabla ya kujiunga na TBC alikuwa mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Habari la Uingereza (BBC), alisema kwa mujibu wa taratibu mfanyakazi anayemaliza mkataba wake anatakiwa kujulishwa suala hilo miezi sita kabla.
"Kimsingi (barua) hukumbusha kwamba mkataba unamalizika na kama serikali inakusudia kuuendeleza au la. Sasa hilo halikufanyika kwangu," alisema.
Kwa mujibu wa Tido, hatua hiyo inaweza kutafsiriwa tofauti na wananchi hasa ikizingatiwa kwamba imefikiwa miezi miwili tu tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu.
Wafanyakazi walipata taarifa ya kuondolewa kwa Mhando jana baada ya mkurugenzi huyo kubandika tangazo la kuwataarifu kuwa anaondoka na kwamba ametakiwa akabidhi ofisi kwa Joe Rugabaramu.

Tido alipojiudhuru BBC nilisikitika na kufurahi kwa upande mwingine na kujiuliza maswali haya, 1. Kasukumwa na uzalendo? 2. Pesa ya serikali aliyohaidiwa ilikuwa nyingi zaidi? 3. Amechoka kukaa huko ughaibuni?.

Nakumbuka kusikiliza mahojiano yake BBC kabla ya kuondoka, na alikariri kuwa bado mkataba wake pale BBC ulikuwa unamruhusu kuendelea na ikumbukwe alikuwa mwafrika wa kwanza kuongoza Idhaa. Imani ilijengeka kwamba TBC ingeimarika kwa ujio wake na ki kweli amefanya mengi, kuanzia uboreshaji wa vipindi mpaka vitendea kazi!

Japo anamafanikio makubwa lakini wakati mwingine alitenda kisiasa zaidi, labda hii haiepukiki!. Mojawapo ya tukio ambalo sitalisahau ni siku alipokuwa na JK wakati wa kipind cha maswali na majibu kutoka kwa raia. Tido hakuuliza maswali kama yule Mhando tunayemjua, vile vile TBC iliendelea kupendelea chama tawala katika chaguzi japo si kama zamani. Sitaki kumpa lawama sana hapa kwavile huenda alikiwa katika kipindi cha mpito, nilitamani utendaji wa TBC uwe kama wa BBC. Hii ni TV ya umma.

Nimeshangaa kuona Tido haamini kilichotekea (angalia kwenye Bolded sentensi), hakujua hapa bongo kuwa wanasiasa watakubembeleza alafu wakiona huwatimizii matakwa yao basi wanatimulia mbali kama vile hujui chochote. POLE SANA TIDO MHANDO!
 
ILA KAZI NZURI AMEIFANYA, KWANI AMESaidia TBC IMEKUWA YA KISASA INAYOENDA NA WAKATI.
 
Hili ni mfano wa jambo ambalo katika nchi nyingine wananchi wangekuwa mitaani wanaandamana.

Ni mfano wa matumizi mabaya ya madaraka na kiashiria kwamba watendaji wa serikali ni watendaji wakuu wa chama tawala.

Ni mfano wa sababu kubwa sana kwa watendaji wa serikali kuunga mkono mabadiliko ya katiba ili kuhakikisha their job security
 
....aende zake tu,mnafiki mkubwa yule! alianza kuigeuka CCM baaada ya watu kumpigia kelele pia alisoma upepo ulivyokuwa unaenda. mchumia tumbo tu!
 
Leo hii mnamuona Tido hakuwa na upendeleo katika kurusha vipindi vyake wakati wa kampeni huu ni unafiki mkubwa na ndivyo watanzania tulivyo ni watu wa kusahau haraka sana. Ni wangapi walikilalamikia chombo cha habari cha TBC wakati wa kampeni kwa kukibeba chama Tawala leo Watanzania hao hao wanamsifu kuwa hakuwa na upendeleo? Sijui kama haya ya kumsifia ni ya kweli.
 
Nyambala, mikataba yote huongozwa kwa vipengele vya mkataba ambavyo ni points za kisheria, hivyo kisheria, Tido amemaliza rasmi mkataba wake tangu tarehe 15/12/2010.

Lakini licha ya kuwepo kwa mkataba husika, TBC ni shirika la umma, hivyo mikataba yake yote hutekelezwa kwa kufuata kanuni za utumishi wa umma zinazosisitiza six months notice prior to exipire date ya mkataba wake.

Kwa vile Tido was not served with leter of intent toka serikalini, tena siku hiyo ametoka kuonana na Katibu Mkuu wake asimweleze chochote kuhusu barua ya kumtaka kukabidhi ofisi, huu ni uthibitisho wa "malice ".
Sheria zimefuatwa lakini taratibu hazikufuatwa na kanuni zimekiukwa.
Smooth transition ni zile zinazo zingatia sheria, taratibu na kanuni.

Thanks mkuu nilikuwa sifahamu hili, lakini je usipopewa hiyo notice inamaanisha unakuwa automatically eligible kwa mkataba mwingine? Na mwajiri akikosa confidence na wewe say wakati mwezi mmoja wa kumaliza mkataba umebakia na 6 months notice haikutolewa inakuwaje hapo?
 
Back
Top Bottom