Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 877
- 4,101
Tido mzee wa watu katika utumishi wake alijenga CV nzuri ndani na kimataifa. Walipoona anafanikiwa na anazidi kupata jina Duniani wakamwita na kumkabidhi TBC. Akaweka mikakati kiwe chombo cha umma kinachozingatia maadili. Akakataa miradi ya rushwa mara TBC ikaanza kupata watazamaji wakiwemo wa mpira. TBC ikaanza kuingia kwenye ushindani wa tenda za matangazo na ikawa na uwezo wakupewa tenda husika.
Baada tu yakuonekana kodi za wananchi zinatumika vizuri na matunda yanaonekana. Mawaziri na wanasiasa wengine wakaanza kumwonea wivu as if na wao wanaweza kufanya kama yeye. Wakamchongea kwa Magu kisha wakamtwisha makesi ya jinai. Wakamfukuza ukurugenzi huku wakitoka adharani nakumtusi kuwa ni fisadi na mwizi.
Vyombo vya habari vikahusika kumkaanga ikiwemo TBC aliyokuwa anaongoza. Wakamleta Ayubu nadhani mnaona tofauti ya TIDO na Ayubu. Kwamba tunamtaka Dr. na siyo mkurugenzi. TBC imepotea kwenye ramani , imebaki na nyimbo za asili na vipindi vya marudio. As long watumishi wanalipwa mishahara chakufia nini bora liende.
Wanaomfahamu TIDO na wacha Mungu wa kweli wakamchukua nakumkabidhi ofisi. Leo AZAM ni chombo kikubwa Afrika linapambana na DSTV kwenye baadhi ya maudhui. Mzee Bakharesa tofauti na pesa pia amepewa Moyo wakumtukuza Mungu kila anapopata nafasi. Kila jambo analofanya linafanikiwa kwa sababu anayo hofu Mungu ndani yake.
Hao wanasiasa walioshangilia kutumbuliwa kwa TIDO jana nimewaona wamejazana tena Azam wakimpongeza. Tofauti ya TIDO na wao ni kwamba wao wanaishi kwa dhuluma na Majungu na kuwaachisha wenzao kazi ila TIDO anaishi kwa taaluma na kipawa cha Mwenyenzi Mungu.
Tido siyo bosi basi amebeba vision na kila aliyepo chini yake atamshape aweze kuifikisha vision panapotakiwa. Natambua kazi hii anamkabidhi Salimu Kikeke ila bado viatu vitakuwa vikubwa sana.
Cha kujifunza: KUITWA WAZIRI AU KIONGOZI WA KISIASA HAINA MAANA WEWE UMEBEBA BARAKA ZA UNAOWAONGOZA. NI SUALA LA MUDA TU, ISHI VIZURI NA WATU, TAMBUA WENZAKO PIA WANAFAMILIA NA ELEWA NI PUMZI YA MUNGU NDIYO IMETUFANYA TUWE HAI. USIUMIZE WENZAKO ILI WEWE UNUFAIKE.