Tido Mhando atemwa TBC

Tido Mhando atemwa TBC

Jamani nafasi yake ilikuwa ngumu sana, na alivyokuwa BBC ni tofauti sana na TBC, wengi mnalaumu lakini ukifikiria kwa undani utagundua haikuwa rahisi na kama wengi mngepewa hiyo nafasi mngefuata matakwa ya ccm kwa asilimia 100.

Hongera Tido you will be remembered if there was any weakness, believe me your performance outweighed those weakness by large scale!

Tido ni mtu mzima kama nafasi ya BBC ilikuwa rahisi kuliko TBC why he accepted the job.
Tido ndiye huyu huyu aliyeendesha mahojihano na Kikwete yaliyokuwa na maswali yanayo mfavour Kikwete
Tido huyuhuyu aliyerudiarudia mkutano wa Kikwete na wazee wa Dar es Salaam siku Rais alipowatukana na kuwatusi wafanyakazi
Tido huyuhuyu aliyekatisha matangazo ya Bungeni siku Dr Slaa alipokiuwa anaipa fact serikali
Ni Tido huyuhuyu aliyekatisha matangazo siku chadema walipokuwa wanafanya uzinduzi wa kampeni, na baadaye kutetea uamuzi wake huo
Tido aliyekuwa anatoa matangazo yaliyokuwa yanaonyesha kazi za jeshi na mafanikio ya Jeshi katika kipindi cha Kikwete kipindi cha kampeni
Tido huyuhuyu aliyekuwa anaendesha matangazo ya kuonyesha mafanikio ya CCM kipindi cha kikwete wakati wa kampeni (si kosa kuonyesha mafanikio ya serikali ya CCM lakini alikuwa wapi mpaka kipindi cha uchaguzi)
Bado Tido alijitahidi kujaribu kufanya mahojiano na Lowasa kutaka kumuosha
Mwisho bado aliipendelea CCM ukifuatilia alipokuwa anaweka kuonyesha kampeni za vyama pinzani utaona alikuwa hawaonyeshi wakiongea point ni either wakisalimu halaiki iliyofika au kuonyesha helkopta ikifika

Sikatai toka afike TBC imekuwa na muonekano wenye kuvutia lakini matangazo yenye kukibeba chama cha wala nchi
Sawa atakuwa kamwagwa kimizengwe lakini ni wale aliowabeba ndio waliomwaga, here comes Suzan
 
Send to a friend Friday, 17 December 2010 06:34 0diggsdigg

Sadick Mtulya, Patricia Kimelemeta
BAADA ya kufanya kazi nzuri ya kuboresha matangazo na uendeshaji wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), serikali imeamua kuachana na mkurugenzi wa chombo hicho, Tido Mhando baada ya mkataba wake kuisha, lakini mtangazaji huyo maarufu ameielezea uamuzi huo kuwa kuwa ni wa utata.
Kuenguliwa kwake kumefanyika takriban miezi miwili baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu ambao TBC iliripoti kwa kina na bila kupendelea chama chochote na hivyo kujivunia sifa kemkem kutoka kwa watazamaji wa TBC1 na wasikilizaji wa redio hiyo ya umma.

“Hatua hii imenishtua kidogo na hata hivi ninapoongea na wewe wafanyakazi wengi wamepata mshtuko na wengine wanalia," alisema Tido alipoongea na Mwananchi jana. "Ni juzi (Jumatatu) ndio niliandikiwa barua na serikali ya kutakiwa kuondoka.... ilikuwa kinyume kabisa na uratatibu wa serikali.
“Barua ya kutakiwa kuondoka niliipata mara baada ya kukutana na kuzungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Michezo, Utamaduni na Vijana , Seti Kamwanda.’’

Tido, ambaye kabla ya kujiunga na TBC alikuwa mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Habari la Uingereza (BBC), alisema kwa mujibu wa taratibu mfanyakazi anayemaliza mkataba wake anatakiwa kujulishwa suala hilo miezi sita kabla.
"Kimsingi (barua) hukumbusha kwamba mkataba unamalizika na kama serikali inakusudia kuuendeleza au la. Sasa hilo halikufanyika kwangu," alisema.
Kwa mujibu wa Tido, hatua hiyo inaweza kutafsiriwa tofauti na wananchi hasa ikizingatiwa kwamba imefikiwa miezi miwili tu tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu.
Wafanyakazi walipata taarifa ya kuondolewa kwa Mhando jana baada ya mkurugenzi huyo kubandika tangazo la kuwataarifu kuwa anaondoka na kwamba ametakiwa akabidhi ofisi kwa Joe Rugabaramu.

"Tangazo linasema kuwa amefanya kazi na sisi kwa miaka minne na sasa mktaba wake umeisha na kwamba ametakiwa akabidhi ofisi kwa Rugarabamu," alisema mmoja wa wafanyakazi wa TBC.
"Baadaye alitushukuru kwa ushirikiano wetu kazini na akatuambia tusubiri hadi hapo mkurugenzi mpya atakapotangazwa."
Mfanyakazi mwingine alisema kuwa walitarajia kuwa Mhando angetimuliwa mapema kabla ya uchaguzi kwa kuwa wanadai kuja kwake nchini kulitokana na uhusiano wake na kigogo mmoja wa CCM ambaye kwa sasa hayuko madarakani.
"Angetimuliwa hata kabla ya Desemba 15, lakini ikaonekana kuwa isingekuwa sahihi," alisema mfanyakazi huyo ambaye alieleza kuwa Mhando aliwasiliana pia kwa simu na mfanyakazi mmoja mmoja kumuelezea uamuzi huo wa serikali.
Habari za Tido kuondoka TBC zilianza kuvuma wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wakati iliposemekana kuwa alikuwa akipigana vijembe vya chinichini na vigogo wa CCM kutokana na vyombo hivyo vya umma kutangaza habari bila ya upendeleo.
Baadhi ya mambo yaliyoibua hisia kuwa mtendaji huyo wa shirika la umma angeondolewa ni msimamo wake wa kuendelea kurusha hewani kipindi cha "Jimbo kwa Jimbo" ambacho kilikutanisha wagombea ubunge wa vyama mbalimbali vya siasa kwenye mdahalo kuhusu maendeleo ya eneo lao.

Kipindi hicho kilichorushwa kwa wakati mmoja na vituo vya televisheni na redio kilianza kwa kushirikisha wagombea wote wa ubunge kwenye jimbo, lakini katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba akaandika waraka wa kuzuia wagombea wa CCM kushiriki kwenye mdahalo huo akidai kuwa chama hicho tawala kina njia zake za kufanya kampeni.
Pamoja na CCM kujitoa, TBC iliendelea kurusha vipindi hivyo hadi kumalizika kwa uchaguzi ambao uliisha kwa CCM kupoteza viti vingi Tanzania Bara, ikiwa ni mara ya kwanza tangu serikali iruhusu mfumo wa vyama vingi.

"Ilikuwa aondoke kabla kampeni hazijaanza ingawa mkataba wake ulikuwa umalizike Desemba 15. Lakini serikali ilikuwa inarekebisha mambo yake na kumtafuta mtu anayeweza kurithi nafasi yake," chanzo cha habari cha ndani serikalini kilidokeza.
Chanzo kingine alisema: "Kuna watu wanaajiriwa pale TBC ambao malipo yao yanayotokana na Saccos ya shirika hilo, kitu ambacho ni kinyume na taratibu za serikali zinazotaka mwajiriwa alipwe na Hazina."
Jitihada za gazeti hili kumpata katibu mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Seti Kamhanda hazikuzaa matunda.
Alipoulizwa endapo atakubali kurejee kwenye wadhifa huo ikitokea serikali ikamwita tena, Mhando alijibu: "Nitalazimika kuchukua muda zaidi kutafakari hilo kwa kina.

“Nitafanya maamuzi ya kazi ya kufanya kulingana na wakati utakavyokuwa, lakini itanichukua muda kidogo kutafakari hilo kwa kuwa nimefanya kazi mfululizo.’
Kuhusu utendaji wa shirika hilo, Tido alisema amefarijika kwa kiasi kikubwa na mafanikio ya kiutendaji yaliyofikiwa.
“Nilikuwa na mipango mikakati mingi ya kuendeleza shirika hili hususani kulifanya lijiendeshe kwa kujitegemea bila ya kuhitaji ruzuku serikalini," alisema na kuendelea:

“Lakini nimefarijika vya kutosha na utendaji wangu na mafanikio yaliyofikiwa na TBC hadi wananchi kukiamini chombo hiki na ‘reaction’ imekuwa nzuri kutoka kwao na kwa vyama vya siasa.’’
Mbali na kurusha taarifa za kampeni katika njia iliyoonekana kuwa si ya upendeleo hata kwa chama tawala, TBC ilifanikiwa sana katika urushaji wa moja kwa moja wa matangazo ya mechi za mpira wa miguu na matukio makubwa ya kisiasa na kijamii.
Mechi za michuano mbalimbali ya kimataifa na ya ndani, urushaji wa matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge, urushaji wa moja kwa moja wa matukio makubwa na staili ya utangazaji ulilifanya shirika hilo kuwa na mvuto mpya na hivyo kuweza kupambana na vituo vingine vya redio na televisheni vya kampuni binafsi
kwenye red si kweli kwa mujibu ELRA 2004/6/7 mfanyakazi anatakiwa apewe notice ya siku 28 as well as mfanyakazi naye anatakiwa atoe notice ya siku 28 kwa mwajiri,hili pia la muhando linakubaliwa badala ya kukupa notice ya siku hizo,unakuwaterminated lkn unalipwa haki zako zote
 
Pole Tido ulishindwa kuwalidhisha mabwana wawili kwa wakati mmoja.
 
Mwacheni akapumzike jamaniiiiiiiiiiiii,maneno mengi ya nini?:teeth::teeth::whoo::whoo::whoo::whoo::whoo:
 
Amewajua mafisadi. Wanakutumia baada ya hapo wanatupa jalalani. Bado Zitto!
 
nyambala, mikataba yote huongozwa kwa vipengele vya mkataba ambavyo ni points za kisheria, hivyo kisheria, tido amemaliza rasmi mkataba wake tangu tarehe 15/12/2010.

Lakini licha ya kuwepo kwa mkataba husika, tbc ni shirika la umma, hivyo mikataba yake yote hutekelezwa kwa kufuata kanuni za utumishi wa umma zinazosisitiza six months notice prior to exipire date ya mkataba wake.

Kwa vile tido was not served with leter of intent toka serikalini, tena siku hiyo ametoka kuonana na katibu mkuu wake asimweleze chochote kuhusu barua ya kumtaka kukabidhi ofisi, huu ni uthibitisho wa "malice ".
Sheria zimefuatwa lakini taratibu hazikufuatwa na kanuni zimekiukwa.
Smooth transition ni zile zinazo zingatia sheria, taratibu na kanuni.

pole sana suzan mongi hiyo ndio sisiemu iliowarudisha tanzania....
Mnakaribhswa chaddy
 
Frankly speaking, TIDO kaibadilisha TBC sana and thus, kaacha bonge la legacy!!! These days, TBC wanapata a lot revenue through matangazo contrary to the past. Hii ni baada ya jitihada za Tido ku-raise public image ya iliyokuwa TVT(now, TBC) ambapo alifanikiwa sana.

Naona supremacy ya ITV katika tasnia ya habari kupitia TV hakika itarudi kwa kasi!!! Why? Kwa TIDO kuondolewa TBC ni dhahiri kwamba CCM wanataka kuendesha TBC kichama zaidi kuliko kitaifa and thus tusitarajie muujiza wowote kutoka kwa mkurugenzi mpya!!!
mkuu nimewaza na kuwazua lakini nimekosa jibu

Typical
 
wakubwa huu ndio ufisadi wa ccm ulivyo. Hakuna urafiki wa kweli wala uadui wa kweli as long as mna interest zinazo fanana. Tido kawasaliti walitaraji kua atawapa favours zaidi, then matokeo yake akasoma alama za nyakati na kuona jamii inataka then akatoa nafasi. Mi namshauri tido asirudi tena ili alinde heshima yake kuliko kulazimisha then aondoke kwa scandel si mnajua ccm walivyo wazuri kwa kazi hiyo?
 
pole mzee Tido but hiyo isikusumbue sana, Mungu ni mwaminifu atakupa sehemu nyingine,
bt umeiweka wazi ccm kwamba haifanyi kitu ikiwa madarkani, tumechoka sana
 
wakubwa huu ndio ufisadi wa ccm ulivyo. Hakuna urafiki wa kweli wala uadui wa kweli as long as mna interest zinazo fanana. Tido kawasaliti walitaraji kua atawapa favours zaidi, then matokeo yake akasoma alama za nyakati na kuona jamii inataka then akatoa nafasi. Mi namshauri tido asirudi tena ili alinde heshima yake kuliko kulazimisha then aondoke kwa scandel si mnajua ccm walivyo wazuri kwa kazi hiyo?
 
alijitahidi kuitangaza injili pale shirika la habari la TAIFA!
 
Mi naona watu wanaruka ruka tu kweye hoja zao. Members wa JF tunakuwa ka vinyonga. Hii ni kama siku ya msiba wa marehemu hutasikia mabaya yake.

Tujiulize

  • Kwani Tido alijiriwa kwa kufuta sheria za ajira mashirika ya umma? Iweje alipata ajira kwa sheria nyingine alafu watu watake mkataba wake usitishwe kwa sheria tofauti.

  • Je mshahara wa tido ilikuwa kwenye viwango vya hayo mashirika ya umma??

  • Pia naomba kuelimishwa hivi TBC iko chini ya Ofisi wa Waziri mkuu au Wizara ya habari.?
 
Tido ni mtu mzima kama nafasi ya BBC ilikuwa rahisi kuliko TBC why he accepted the job.
Tido ndiye huyu huyu aliyeendesha mahojihano na Kikwete yaliyokuwa na maswali yanayo mfavour Kikwete
Tido huyuhuyu aliyerudiarudia mkutano wa Kikwete na wazee wa Dar es Salaam siku Rais alipowatukana na kuwatusi wafanyakazi
Tido huyuhuyu aliyekatisha matangazo ya Bungeni siku Dr Slaa alipokiuwa anaipa fact serikali
Ni Tido huyuhuyu aliyekatisha matangazo siku chadema walipokuwa wanafanya uzinduzi wa kampeni, na baadaye kutetea uamuzi wake huo
Tido aliyekuwa anatoa matangazo yaliyokuwa yanaonyesha kazi za jeshi na mafanikio ya Jeshi katika kipindi cha Kikwete kipindi cha kampeni
Tido huyuhuyu aliyekuwa anaendesha matangazo ya kuonyesha mafanikio ya CCM kipindi cha kikwete wakati wa kampeni (si kosa kuonyesha mafanikio ya serikali ya CCM lakini alikuwa wapi mpaka kipindi cha uchaguzi)
Bado Tido alijitahidi kujaribu kufanya mahojiano na Lowasa kutaka kumuosha
Mwisho bado aliipendelea CCM ukifuatilia alipokuwa anaweka kuonyesha kampeni za vyama pinzani utaona alikuwa hawaonyeshi wakiongea point ni either wakisalimu halaiki iliyofika au kuonyesha helkopta ikifika

Sikatai toka afike TBC imekuwa na muonekano wenye kuvutia lakini matangazo yenye kukibeba chama cha wala nchi
Sawa atakuwa kamwagwa kimizengwe lakini ni wale aliowabeba ndio waliomwaga, here comes Suzan

Tido ulianza kugusa pabaya baada ya kufanya kosa la kiitifaki. Na kama ungekuwa mjanja ungeliona hilo mapema. Siku uliyomhoji Pinda kabla ya kumhoji Lowasa. Ilionekana kwako Lowasa Kiitifaki yuko juu ya Pinda. Hilo ni kosa kubwa sana kiitifaki. Alitakiwa Pinda akimaliza, kama utamhoji mtu mwingine awe ni JK mwenyewe. Ila sidhani kama Pinda ana vinyongo vya hivyo ila najua watu wa itifaki walilifanyia kazi.

Pia usilalamike ila ukumbuke wakati Hawa Ghasia anamtukana Prof Baregu kuhusu kunyimwa mkataba kwa staili kama ulivyofanyiwa, hilo hukuliona ni tusi na uliruhusu majibu ya Ghasia kurudiwa TBC. Nafikiri wengi mnakumbuka Ghasia alimwambia Baregu akajiuze nje kama anaona anauzika. Tido hakuliona hilo kuwa na yeye yuko kwenye mkataba ambao nao utaisha. Mkumbuke Jay Dee kaimba siku hazigandi. Hayo si yamekukuta wewe tu bali hata vyuoni maprof kibao wamefanyiwa kama wewe.

Pia ukumbuke kuwa ulikataa kurusha malalamiko ya wahadhiri wa vyuo vikuu na shirika lako likuyapotosha ati wanadai mishahara zaidi wakati suala lilikuwa ni pension ndogo inayotolewa na PPF pamoja na tabia ilozuka serikalini ya kukatisha mikataba bila utaratibu. Ungekuwa umeruhusu mahojiano ya TBC na wahadhiri kurushwa, wananch wangejua ni nini unacholalamikia.

Mwisho tu nakukumbusha kuwa mwanasiasa akishakutumi, mwisho anakufanya kama toilet paper. Huwa anakutupa na kukuflashi bila hata ya kuangalia umechafuka au la.
 
Mi naona watu wanaruka ruka tu kweye hoja zao. Members wa JF tunakuwa ka vinyonga. Hii ni kama siku ya msiba wa marehemu hutasikia mabaya yake.

Tujiulize

  • Kwani Tido alijiriwa kwa kufuta sheria za ajira mashirika ya umma? Iweje alipata ajira kwa sheria nyingine alafu watu watake mkataba wake usitishwe kwa sheria tofauti.

  • Je mshahara wa tido ilikuwa kwenye viwango vya hayo mashirika ya umma??

  • Pia naomba kuelimishwa hivi TBC iko chini ya Ofisi wa Waziri mkuu au Wizara ya habari.?

Kuna post ilikuwa humu jamvini ilikuwa imeletwa na Zito Kabwe mwaka jana au mwaka juzi ikionyesha mishahara ya akina Tido. Tido alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wanalipwa vizuri sana katika nchi hii. Kama kuna mtu anayeweza kuirudisha au kutupa link atusaidie
 
Hata kama siyo ndg. inaonekana anapenda sana jina MUHANDO liskike hewani
Hivyo moja ya vigezo vya kuingia TBC labda uwe unaitwa Muhando!
Hapo imekaaje?:loco:
 
Jamaa analalamika walivyom fire bila notice ya miezi sita kwa mujibu wa taratibu/kawaida za serikali

Mkataba unasema nini kuhusu non-extension of the contract, sio habari ya kawaida ya serikali.

Hukusoma mkataba? Walisema lazima wakupe notice ya miezi sita?
 
The amazing thing about politics is this: Depending on circumstances, a politician can turn a stone into bread, and vice versa!!!
Tido ulianza kugusa pabaya baada ya kufanya kosa la kiitifaki. Na kama ungekuwa mjanja ungeliona hilo mapema. Siku uliyomhoji Pinda kabla ya kumhoji Lowasa. Ilionekana kwako Lowasa Kiitifaki yuko juu ya Pinda. Hilo ni kosa kubwa sana kiitifaki. Alitakiwa Pinda akimaliza, kama utamhoji mtu mwingine awe ni JK mwenyewe. Ila sidhani kama Pinda ana vinyongo vya hivyo ila najua watu wa itifaki walilifanyia kazi.

Pia usilalamike ila ukumbuke wakati Hawa Ghasia anamtukana Prof Baregu kuhusu kunyimwa mkataba kwa staili kama ulivyofanyiwa, hilo hukuliona ni tusi na uliruhusu majibu ya Ghasia kurudiwa TBC. Nafikiri wengi mnakumbuka Ghasia alimwambia Baregu akajiuze nje kama anaona anauzika. Tido hakuliona hilo kuwa na yeye yuko kwenye mkataba ambao nao utaisha. Mkumbuke Jay Dee kaimba siku hazigandi. Hayo si yamekukuta wewe tu bali hata vyuoni maprof kibao wamefanyiwa kama wewe.

Pia ukumbuke kuwa ulikataa kurusha malalamiko ya wahadhiri wa vyuo vikuu na shirika lako likuyapotosha ati wanadai mishahara zaidi wakati suala lilikuwa ni pension ndogo inayotolewa na PPF pamoja na tabia ilozuka serikalini ya kukatisha mikataba bila utaratibu. Ungekuwa umeruhusu mahojiano ya TBC na wahadhiri kurushwa, wananch wangejua ni nini unacholalamikia.

Mwisho tu nakukumbusha kuwa mwanasiasa akishakutumi, mwisho anakufanya kama toilet paper. Huwa anakutupa na kukuflashi bila hata ya kuangalia umechafuka au la.
 
TBC ni ya watanzania...

Tido aliharibu siku alipokataa kurusha matangazo ya ufunguzi wa chadema. Alifavor CCM. Kwahiyo serikali imemuona kwamba hafai! Let him go!
Xcuse u me!!!! Serikali ipi hiyo?
 
Back
Top Bottom