Apo juu inamaana wasiokuwa na elimu hawawezi kugombea nafasi za kisiasa ? Ukizingatia kila siku mikoa,wilaya,vijiji ,kata,mitaa ,majimbo yanagawanywa hivyo uwezekano wa kukosa elimi ya mijishahada inaweza kabisa isipatikane katika sehemu hizo mpya. Pia kuna maneno maneno eti wasomi wanakimbilia kwenye siasa ,sasa kuanzisha huo utaratibu wa kudai vyeti vya wagombea si kutawafanya wasomi wote waelekee huko na mashahada yao ! Kwa vielelezo vilivyopo sioni sababu ya kudai vyeti wakati kuna ushahidi wa hao mnaowaona wamesoma kutafuta wataalamu na makampuni ya nje kuja kuwafanyia mahesabu na mauchunguzi ,tuiondoe CCM tu ndio dawa matibabu si kudai vyeti kwani ugonjwa ni Chama kiliopo madarakani. Je tukubali kuwa Chama kilichopo madarakani hakina wasomi wenye mashahada ya juu ,hizi ni hila za Sultani CCM kutafuta kisingizio cha kuiendesha Nchi hii kwa madai ya vyeti bandia kumbe wao ni wezi mafisadi.
Hoja ya TCU siyo kutaka watu wenye shahada ndiyo wagombee nafasi za kisiasa peke yao, bali lengo la TCU ni kuondoa utapeli wa kugushi vyeti ama kudanganya wapiga kura kwamba mimi ni msomi wa ngazi fulani na kumbe ni ulaghai mtupu. Acha wapiga kura wamchague mtu kulingana na sifa zake za kikweli. Kama mtu kaishia darasa la 7, kwanini ajikweze kwamba amemaliza F6?
Katiba ya nchi iko wazi, kwamba wagombea wa Ubunge wanatakiwa kujua kusoma na kuandika, haijalishi ni darasa la nane, Form 7 (darasa la msingia saba) ama F4 ama F6 au diploma.
Siku hizi kwenye siasa elimu imekuwa ni deal kubwa sana na inaonekana ni mtaji. Pale OUT (Open Univ) kulikuwa na wimbi kubwa sana la wana siasa kujiandikisha kusoma na wote wameishia mitini, waliofanikiwa kumaliza ni wachache sana. Matokeo yake kuna uyoga wa PhD fake za correspondence zimejaa huko Bungeni pamoja na nyeti vingine vya kugushi ambavyo watu wamejiwekea kwenye CV zao.