Miaka yote ya kumuhukumu Rostam na hili jambo rahisi mlikuwa hamjafanya... whats up with you guys?
TCU wametoa tamko kwamba kuanzia uchaguzi mkuu wa mwakani wagombea wote watapaswa kupeleka vyeti vyao kwenye hiyo kamisheni ili iweze kuthibitisha kama sifa walizojaza kwenye fomu zao zinaendana na vyeti walivyo navyo na siyo mtu kusema ana BA Economics ama PhD na kumbe ni utapeli mtupu. Nina hakika TCU wamegundua mengi na ili ku-deal na hayo mahali pa kuanzia ni huko kwenye kuthibitisha vyeti vya wagombea.
Wakati mwingine hata ukienda na FACTS as long as mhusika mkuu yuko kwenye anga za watawala hakuna kitu kitafanyika. Ukweli ni kwamba vyombo husika vya kufuatilia haya mambo navyo vimekuwa corrupted kiasi kwamba wao ndiyo wahusika wakubwa wa kuharibu ushahidi ama kufunika ushahidi.
Swala la Chenge (radar) linasukumwa kwa kuwa SFO wako frontline kulifuatilia. Isingekuwa SFO hilo swala lingekuwa limeishafukiwa na Chenge angekuwa bado yuko madarakani mpaka leo hii. TAKUKURU yetu na polisi wako kimya kabisa. Subiri ukisikia MwanaHalisi lina info za account za Benki za watu fulani walio serikalini utaona Polisi ambavyo hawasubiri ushahidi, ila wao wenyewe ndiyo watakwenda kwenye ofisi za MwanaHalisi na nyumbani kwa Kubenea kwenda kusaka huo ushahidi. Kwanini tuhuma nyingine wanadai ushahidi na tuhuma nyingine hawadai ushahidi?
Swala la Chitalilo lilishughulikiwa na polisi kwa kuwa lilihusisha INTERPOL na polisi walipopeleka report kwa DPP, mkurugenzi wa mashitaka akasema hakuna case. Hivi kweli kunaweza kuwa hakuna case kwa mtu ambaye ameapa kwamba kasoma sekondari hii na ile na kwamba kamaliza High School na kumbe ni darasa la saba tu! Na alijaza fomu ambayo aliapa mbele ya Hakimu (siyo kwa wakili).
Kasheshe pamoja na kuwatetea hao watu wako, sometimes wananchi tunapata shida sana kuamini hata pale ambapo FACTS zinakuwa ziko uchi utawakuta wanakwepa kwepa tu.
RA kapeleka tuhuma za Mengi PCCB na tayari jamaa wameishaanza kuzichunguza. Je, ulishawahi kusikia kwamba RA anachunguzwa na chombo chochote cha dola?
Kilichoandikwa kwenye report ya Mwakyembe kuhusu Dowans kutumia sanduku la barua la Caspian na anuani ya barua pepe ya Caspian kilikuwa kinatosha kabisa kuwa-alert PCCB na Polisi kumchunguza RA kama ana mahusiano ya aina yoyote na Dowans. RA anajitetea kwamba aliwaruhusu watumie e-mail address ya caspian na sanduku la posta kwa sababu ya mahusiano ya kibiashara kwamba walishawahi kumpa kazi ya ujenzi pale Ubungo. Hakuna mfanya biashara mjinga ambaye anaweza ku-risk ku-expose information zake kwa kutumia sanduku la barua la kampuni nyingine na kutumia anuani pepe ya kampuni nyingine, kwa kuwa kitendo hicho kinampa huyo mtu access ya info zote za barua za posta na barua pepe. Je, wafanyakazi wanapokuwa waajiriwa wa Caspian na Dowans kwa wakati mmoja bado hilo nalo halitoshi kuwa-alert hao watu wa PCCB na Polisi na kutaka kujua kulikoni?
Mchg Mtikila aliwahi kumtuhumu Sumaye kwamba ni mla rushwa namba moja Tanzania. Hoseah akiwa Director wa Operations pale PCCB akasema kwamba wamesoma tuhuma za Mtikila na kwamba wameanza kuzifanyia kazi. Mkurugenzi Mkuu (Kamazima) akaja after few days akasema hakuna tuhuma zinazofanyiwa kazi na PCCB zinazomhusu Sumaye. Baada ya hapo sikuwahi kumsikia tena Hoseah akiongelea mambo ya rushwa mpaka alipokuja kuteuliwa kuwa DG wa PCCB.
Waunganisha dots walisema wazi kwamba Mtikila katumiwa na mtandao na Hoseah nae alikuwa mtu wa mtandao na hivyo ilikuwa ni kampeni za kummaliza Sumaye. Dots zilikuja kuwa wazi pale ambapo uteuzi wa Hoseah ulifanyika wakati Muungwana akiwa nje ya nchi (wajuba wanasema ni Brother EL ndiye aliyemteua). Dots zikakamilika mwaka jana pale ambapo Mtikila aliumbuliwa na RA kwamba alishikishwa shilingi milioni 3. Je, hiyo ni coincidence tu ama ni kitu kilichokuwa kimefanywa strategically?