The story of my life: Ukweli mchungu baada ya kugundua mtoto tulie naye hakuwa mtoto wangu

banzy

Member
Sep 2, 2012
22
140
Habari zenu wana jamii forum

Leo naomba niwaletee kisa cha ukweli kilichotokea miaka kama 9-10 iliyopita wakati wa kuhangaika na Maisha, naomba nikiri mimi sio mtu wa kupost sana mara Nyingi ni mtu wa kusoma tu content za watu.

Mtaniwia radhi kwa uandishi mbovu mana sio mtaalamu sana wa uandishi na pia kisa chenyewe ni kirefu kidogo ila nitajitahidi kukimaliza chote kwa kuhide baadhi ya information ili wahusike wasijulikane.



MWANZO WA MAHUSIANO YETU

Miaka kama kama 9-10 iliyopita nilikuwa nimetoka kumaliza shule nipo mtaani nasaka ajira,nikabahatika kupata kazi kwenye company X iliyopo maeneo ya Dar wakati huo huo pia nikawa naendelea pia kufanya kazi nyingine za mtaani kutokana na field niliyosomea ilikuwa inaruhusu kazi za ukishoka.

Kuna siku kukawa kuna kazi nimepata ya mteja mmoja nikamfanyia kazi yake ikaisha baada ya kumtaarifu aliniomba nimpelekee hiyo kazi ofisini kwake kumkabidhi,basi nikapanga nikiwa job ile mida ya jioni nitoroke ili nimpitishie yule mteja then niondoke zangu kurudi mtaani ninapoishi.

Baada ya kuwasiliana na jamaa alinielekeza ofisini kwake ilikuwa maeneo ya posta nikafika pale nikakuta wapo kwenye kikao ilikuwa ni evening session wanatoa updates za kazi zao za siku,jamaa alikuwa kama supervisor wao (hili nililijua badae) coz yeye ndio alikuwa anaongoza hicho kikao chao.Baada ya muda akaomba kidogo kikao kisimame wamsubiri anione mimi then waendelee na uzur walipokuwa wanafanyia kikao ni meeting room ambayo me nilikuwa nimekaa kwa pembeni tu kwa nilisikia yaliyokuwa yanaendelea.Jamaa akaja nikamwoyesha kazi yake akaridhika nayo iko poa akanipa mshiko wangu basi nikaaga pale nikaondoka zangu,jamaa baada kurudi kwenye kikao nasikia aliniongelea vizur kuwa nimemsaidia issue yake iliyokuwa inamsumbua kwa muda Mrefu (hii nilijua badae)

Kwenye kile kikao kulikuwa na watu kama 6-7 hv wanaume na wadada kama wa3 hv na mmoja wa hao wa dada ndio nilikuja kuwa nae kwenye mahusiano.Basi kama nilivyosema nilitoroka job kwetu ilikuwa mida ya jioni na nilikuwa na njaa sikula mchana nikaona nipitie mahali nipige msosi then nikapande dala dala niingie mtaani.

Baada kupiga msosi nikaenda moja kwa moja kupanda dala dala za posta-makumbusho na Bahati nikmkuta yule dada kwenye ile daladala basi nikamsalimia then nikapita nikaa siti ya nyuma yake kumbe na wao baada ya ile session wakaondoka ndio nikamwona kwenye daladala baada hapo mwisho wa gari kila mtu alishika njia yake.

Ikapita kama siku 3-4 hv nikaja kuonana nae tena makumbusho pale asubuh anasubiria daladala za kwenda posta,nakumbuka by that time daladala za makumbusho -posta mida ya asubuh kupata seat ilikuwa issue kweli kweli,basi nikamsalimia pale then nikakaa kusuburi daladala ikaja nikaondoka,so nikawa naendelea kubahatisha kuonana nae kama mara 4-5 hv tukawa tunawasiliana fresh halafu naendele na mambo mengine ya kusubiri daladala nakumbuka kunasiku daladala zilikuwa shida sijui ilikuwa kuna mvua au foleni sana tulipanda pamoja zile bajaji za buku 3 kwenda posta.

Kwa kipindi chote hicho sikuwah kumuuliza jina lake wala sikuwa na contact zake ila alikuwa anarespond kwa uchangamfu sana pale tunapoona,baadae Akili za kiuanaume zikaniambia “embu acha uboya omba no. mtoto wa watu asije akakuona hamna kitu bure” na ukizngatia dada mwenyewe alikuwa mzuri tu ila sikuwa nataka niingie kwenye relationship coz nilikuwa na vigoals vyangua kwanza nivitimize kwa utulivu.Basi siku moja nikamwomba no.akanipa then nikamtext kumpa no yangu then tuakendelea na Maisha mengine.

From that day sikumpigia wala kumtext ikapita kama week hv hatukuonana kwasababu me nilisafiri mara moja kama week hv then nikarud baada kama ya siku 2 hv naenda job ile asubuh nakuta kuna daladala imeshajaa wengine wamesimama ndio inakaribia kutoka na me siku hiyo sikuwa na haraka nikakaa pembeni kuichunia ili iondoke niskilizie nyingine nipande,kumbe kwenye ile daladala alikuwepo yule dada kasimama so yeye aliniona me sikumwona,kidogo nikasikia simu inavibrate kuna text basi kuitoa nakuta ni yeye

Yeye:Mambo

Mimi:poa za kwako

Yeye:Salama za siku huonekani?nimekuona hapo kwa nje nipo kwenye hii daladala inayotoka

Mimi: Nipo tu, aah okay nilikuwa sijakuona unaendeleaje?

Yeye: Niko poa , hupandi hii daladala?

Mimi:Hiyo imejaa sana na leo sina haraka sana ngoja niskilizie nyingine.

Basi tuliendelea kuchat kidogo nikamuuliza jina lake kiushahidi kwasbabu jina lake nilikuwa nimeshalipata kupitia ile ya kutest kufanya transaction kwa simu, akanitajia jina lake na mie nikamtajia la kwangu,akaniuliza ninapopigia job namie nikamuuliza anapoishi akanitajia ikawa ndio imefungua mawasiliano baina yetu.

Tukawa tunaanza kuchat mara Nyingi mida ya usiku na tukaanza kuzoeana kidogo kidogo na nikaanza kuvutiwa nawe nikmwomba outing akanikubalia kwa kipindi chote hicho tulikuwa tumeshakuwa very good friends ila sikumuapporach bado nilitaka tufahamiane Zaidi,ikawa ni wale lazima kuchekiana asubuh,mchana na jion daily.

Nikaja kufaham kuwa anaishi na dada yake na amebakiwa na mzazi mmoja (mama) na yupo mkoani,ikafikia mahali tukaulizana relationship status zetu me by that time nilikuwa kwenye long distance relationship ambayo ilikuwa inaelekea kaburini kwasababu nilikuwa na girlfriend ambaye nilikuwa nae wakati nipo chuo na yeye alikuwa alikuwa anafanya kazi Tayari sasa Bahati mbaya au nzur company yao walianzisha office za zones huko mikoani na yeye akahamishiwa huko na pia nikapata habari zake huko mkoani kutoka kwa washkaji zangu na kuna kipindi nilienda kwa hela ya boom kwa siri huko nilichokiona ilikuwa balaa (hii nitaisimulia siku nyingine),

So nikamwambia kuwa nipo kwenye long distance relationship na yeye akaniambia pia yupo kwenye mahusiano ambayo sio serious sana, basi nikaja nikamuapproach akakubali then tukaanza kudate kwa condition za kupeana timeline kila mtu amalize makando kando yake baada ya muda Fulani ili tuendelee sisi wawili tukiwa huru.

Basi tulidate mambo yakawa moto moto kiukweli tulipendana sana na pia hii ilichagiza na ile close friendship ambayo tulianza nao (na ndio ambacho huwa naamini),basi mahusiano yetu yalikuwa poa sana,kuongozana ,outings,kutaniana kwa sana kukutana mara chache chache mida ya lunch maeneo ya ofisini kwao kwenda kupata lunch kwa hiyo that was our life.

Nikamkaribisha kwangu akapajua na mie alipeleka kwa dada yake niliona nae kama mara 2-3 hv nikafahamiana nae.

Mimi kwenye Maisha yangu ya mahusiano huwa napenda nimpe uhuru na huwa sipendi nimfatilie mtu kwasababu naaminini mtu mzima na utash wa kujua kipi kizur na kibaya na pia huwa napenda nimpe uaminifu wa 100% hadi pale yeye mwenyewe atakapoanza kuishusha hiyo trust kutokana na matendo yake.

Basi tuliendelea na relationship for almost a year na miez kadhaa na kwa kipindi chote hicho when it comes to sex niliweka msimamo tuwe tunatumia kinga kwasababu me nilikuwa mwoga na Maisha.

Kiukweli tulishauriana na yeye alinishauri vitu vingi sana vya msingi na maendeleo ambavyo vilinisaidia sana to mention some of them nilikuwa na viside hustle mtaani akanishauri kuviweka in a proper way, badae akanishauri sehemu nilikuwa nimepanga ilikuwa chumba self na sebule ila jiko tulikuwa tunashare na wapangaji wenzangu wa2,hapo mwanzo kwangu haikuwa shida mana jiko lenyewe nilikuwa silitumii yani sipiki me kula restaurant ghetto ilikuwa ni kulala na kupumzika au kununua kuja kulia getho,yeye akashauri tutafute nyumba nyingine ya kupanga yenye kajiko chake ili tuwe free kupika na kuweza kusave matumizi mara moja moja ofcourse niliona inamake sense tukatafuta nyumba tukapata sio mbali na tulikuwa tunaishi tukahamia hapo nikanunua na vitu vya kupikia jiko na vitu vingine.

Nakumbuka baada kama yam waka mmoja na nusu hv tukiwa kwenye mahusiano nakumbuka siku hiyo tunazungumzia issue ya kupima HIV, of course huwa ilikuwa inatokea huko nyuma but that day mada ilipamba moto tukakubaliana tukapime then tukaset date tukaenda kupima fresh majibu yakatoka wote tupo salama.

Baada ya haya majibu mimi kidogo nikalegeza msimamo wa kutumia ndom na pia yeye alisema huwa zinamuumiza basi tukaanza kwenya dry ila kwa precaution kubwa ya kuogopa mimba na mara Nyingi nilikuwa nawith draw siku za hatar na hii hadi aliniuliza nawezaje kwasababu ex wake alikuwa hawez (hii nilikuja kuconnect dot badae),basi nikawa pia nikawa najua mzunguko wake kuliko yeye nakumbuka ofisi niliyokuwepo kipindi hicho walikuwa wanatupa calendar za kwenda home so nikawa nacircle zile date kwenye calendar kwa umakini.

Kuna kipindi ofisini kukawa na project ya kuzunguka almost nchi nzima so ikabidi nisafiri so tulikuwa nje ya dar kama miezi 2 hv kazi moja ilikuwa ya kuchosha sana nakumbuka nilitoroka kama mara 2 kurudi dar lakini sikuonana nae tulipisha nay eye alikuwa amesafiri kwenda mkoani kikazi ila fungua nyingine ya nyumbani pale alikuwa nazo so alikuwa anaenda kufanya usafi na sometimes kupumzika akibioreka.

Baada kama ya mwez since kurud dar akaniambia ni mjamzito nikafurah sana kuwa tunaanza new chapter so tukaanza process za kifamilia na mambo ya kupeleka barua kwao na nini ila tukashauriana kuwa tuatendelea na harusi baada ya yeye akishajifungua,so tukashauriana atoke kwa dada yake aje tuishi nae tukaanza kukaa pamoja tukapata baraka ya pande zote 2 fresh kabisa kwa mimi kwa familia yangu hasa bimkubwa kwasababu mshua alishafariki nay eye bimkubwa wake na ndugu zetu wengine.

Bi mkubwa wangu alivyosikia huyu mchumba wangua ana ujauzito alifurah sana kesho yake tu akapanda bus kuja dar kaja na mazaga zaga kibao tukampokea akatupa nasaha zake pale then akaondoka



Itaendelea soon ………
 
HISTORIA YA MAISHA YANGU

Naomba nielezee historia ya familia yangu kwa ufupi kidogo ili kuja kupata picha nzur badae.

Mimi ni mtoto wa 3 kwenye familia ya Watoto 5 nina dada ka kaka yangu ambao wakubwa kwangu na wana familia zao na Maisha yao na pia nina wadogo 2,mzee alishafariki tumebaki na bmkubwa.

Bi mkubwa alikuwa amesharetire na anafanya shughuli zake ndogo ndogo za ujasiliamali,kingine ni mtu ambae anapenda sawa Watoto/wajukuu yani yeye hiyo ndio Furaha wajukuu wajae home wale wanywe maziwa (anajishughulisha na ufugaji pia) waondoke wamenenepa basi hiyo ndio Furaha yake.na pia kwenye kila familia alitoa ahadi ya wajukuu zake anawapa asset ye alilkuwa anasema kabla hajafa so kwa brother mkubwa (ana mtoto 1) na sister (2)wale Watoto akawapa Mashamba watagawana wakikuwa na wazazi marufuku kuuza hadi wajukuu wakue basi ikawa hivyo.

Tuendelee

Sasa alivyosikia mchumba wangu mjamzito akaja nyumbani akatoa nasaha zake akaondoka.

Tukaendelea na Maisha pale muda ukafika wa kuanza clinic mchumba wangu akapata gyno mmoja huwa nakuwa na session za clinic kwenye hospital moja ipo maeneo ya mikocheni,basi tukaanza safari za kuattend clinic hapo.Tukashauriana tutafute kausafiri kwa ajili ya sasa ye mjamizto na pia mtoto akija kuzaliwa ili kusiwe tunapata challenge ya usafiri toka sehem moja kwenda nyingine.Nilikuwa na kaakiba changu kama 5m na pia nikachukua mkopo kwenye mfuko wa office kama 2m so nikawa kama na 7m tukaona kwa hii price gari tutakayoweza kuimudu ni kuchukua mkononi kwa mtu.

Bahati nzur on that time pale ofisini kwetu kulikuwa n bro mmoja huyu yeye nilimkuta kazini alikuwa amepata scholarship anaenda nje kusoma na nilikuwa nimezoeana nae sasa katika maongezi yetu siko moja nikamwambia natafuta kigari cha kuzugia nichukue mkononi kwa mtu mana sina budget ya kutosha.Jamaa kama Bahati akaniambia yeye ataondoka kwa hiyo kama vipi aniuzie gari yake yeye alikuwa na ist ilikuwa bado mpya mpya tu kwa makubaliano nimpe 8m nyingine nitammalizia mdogo mdogo,nikapambana nikapata 8m yule mchumba wangu alikuwa na akiba alichangia 500k tukampa jamaa akatuachia gari na Maisha mapya ya kumiliki kausafiri yakaanza kidogo ikawa inatusaidia zile trip za clinic na mizunguko michache.

Baada yah apo nikawa nafikiria means ya kuongeza kipato kwasababu gari inahitaj mafuta/service na huku mshahara wangu ulikuwa umepungua kwasababu ya kukatwa kwa ajili ya ule mkopo,katika kufuria idea ya nncha kufanya nikapata story ya uber ndio ilikuwa imetoka kuanza anza enzi hizo tulikuwa tunatumia hata number plate za njano sharia hazikuwa ngumu sana kama siku hz kwa hiyo nikaanza kula vichwa.

Kwa hiyo ratiba yangu ilikuwa weekdays asubuh naenda job natoka ile saa 11 sharp narud home hapo gari nakuwa nimeiacha nyumbani kusave mafuta then nalala kidogo hadi saa moja the naamka naanza kula vichwa hadi saa 5-6 ndio narud home kulala na weekends nilikuwa naamsha siku nzima na nashkuru nilifanikiwa kuongeza kipato kidogo Maisha yakawa yanaenda.

Siku moja nimempeleka clinic mchumba wangu pale ile hospital amabyo huwa tunaenda nilionana na class mate wangu wa primary school ni madada mmoja alikuwa nurse pale mda huo mchumba wangu alikuwa ndani basi tukasalimiana pale akanitambulisha kwa manurse wenzake na mchumba wangu alivyotoka alikuwa amsharud mezani kwake kwa hiyo nilimuaga kwa mbali tukaondoka.

Huyu dada nilikuwa nimezoeana nae sana kwasababu primary me nilikuwa mtu wa utani mwingi na utundu mwingi kwa hiyo ilikuwa rahisi kuzoeana na watu wengi sana hasa kwenye darasa letu

Miezi ikaenda tukawa tunaenda pale clinic yule classmate nilikuwa simkuti tulikuwa tunapishana yeye alikuwa anaingia shift nyingine so sikuonana kwa muda na me nilikuwa naendelea na ratiba zangu za job na uber na badae nilikuwa nampeleka clinic ila naishia nje akiwa Tayari ananishtua namfata tunarud nyumbani.

Miezi ikaenda ikaenda akakaribia kujifungua nashkuru alijifungua salama wkati anakaribia mama yake alikuja home so tukawa na mama mkwe na dada wa kazi na alipojifungua bmkubwa wangu akafunga safar akaja ila hakukaa sana kwasababu pale nyumbani palikuwa padogo kupokea watu wengi na pia mchumba wangu aliniomba yupo comfortable kuhudumiwa na bmkubwa wake so mama hakukaa sana akarud nyumbani.Sasa kama mnavyojua mtot akizaliwa story za hapa na pale sijui kafanana na nini zinakuwaga Nyingi ila ilionekana hakuwa amefanana na baina yetu wawili yani mimi au huyo mchumba wangu kuanzia rangi na vitu vingine me nilikuwa sijui hayo mambo kwasababu sina uzoef ila wakongwe wale wanaokuja kutembea wanaongea pale, na hiyo wala haikunipa shida nilikuwa najua mambo ya genetics tulisoma shule so nilichukulia kawaida huwa inatokea.

Sasa nakumbuka hapo kabla nyuma nakumbuka tulikuwa tunataniana (kuna muda nilikuwa namuita dogo) kulikuwa na meme flani ya pic sikumbuki vizur ila ilikuwa wazazi wamebeba mtoto halafu mtoto alikuwa amefanana sijui na kiongozi wa dini sijui wa serikali sikumbuku vizur, sasa nikamtania kwa kumtumia ile pic then nilimwambia “mdogo wangu ukileta mtotos copy yangua nakutoa mbio hadi kijijini kwenu nilitaja jina la Kijiji chao”.Lakini ile story tu wala haikuwa hivyo.

Sasa bwana kumbe bmkubwa alivyokuja pale mwanzoni kuna kitu alinotice lakini hakusema akaona ajipe muda mtoto akuwe aone kama kuna kitu aliona utofaut au vp (hii nilikuja kuambiwa badae sanaaa),na pia alibaki nayo moyoni hayo mawazo bila kusema kitu kwa sababu alihisi labda ningeumia au ningeleta shida na kiukweli bimkubwa wangu kwa mujibu wa ndugu na jamaa na majirani wanasema katika makuzi yangu mimi ndio nilikuwa kipenzi chake kwa hiyo akaona areserve comments zake ili kuepusha kuniumiza mimi kwasababu huku mwanae nilishaoza na hivi kuna mtoto mpya basi hauniambii kitu.Kwa hiyo alikaa baada ya miezi kadhaa alirudi tena akatusalimia hii mara ya pili alikaa tena siku kadhaa akaondoka.

Tukawa tuanendelea na maisha baadae tena alirudi baada ya miezi kadhaa alikuja kutusalimia mara hii alikuja na aunt yangu yeye ni dada yake na marehem mzee wangu wanafatana, huyu alikuwa ni nurse huko mkoani ila alikuwa amesharetire kipindi hicho,sasa wakatusalimia wakaondoka, wakazuga kuna mgonjwa walikuja kumuona muhimbili by that time kulikuwa na baba yangu mkubwa mmoja alikuwa anaumwa so wakaniambia yule aunt alikuja kwa sababu hiyo na bmkubwa yeye alimsindikiza na wakaona waje kumsalimia mmjukuu wao.

-Kumbe hicho kipindi chote walikuwa wanaangalia tu me sina hili wala lile,tukawa tunampeleka mtoto clinic na nini.sasa kuna kitu kilijitokeza hapo kika nipa mashaka sana



Itaendelea …………..
 
Back
Top Bottom