Anajuta kuwa mtoto wa waziri!

joseph2

Senior Member
May 31, 2015
126
251
Wana Jami forums naomba ni wasalimu wote kwa heshima zote. Leo nakuja na story ya kweli ya mtoto wa waziri maarufu kwenye awamu ya nne.

Huyu kijana ambaye Sasa ni mtu mzima. Nimekutana naye ugaibuni kwenye jiji maarufu, NY. Huyu baba Nimekutana naye kwenye Hari ya kusikitisha. Mimi huwa ni mtu ambaye Sina marigo huwa na ongea na watu wa kila Aina.

Hasa huwa na napenda kusalimia watu waliopo kwenye Hari ya chini kabisa kimaisha kama homeless. Sasa Leo nikiwa natarii kidogo kwenye jiji la New York wakati nikiwa natafuta hiki na kile kwaajiri ya safari yangu ya kurudi Nyumbani. Ni kaona mahomeless wamekaa kwenye kijiwe Chao karibu na times Square.

Mimi nikajisikia moyoni nataka kufanya kitu chema kwa mtu yoyote. Basi nikasogea pale mahomeless waliopo kuwa wamekaa. Nikaanza kuwa salimimia kwa kingereza. Mara tu baada ya kusalimia kama watatu Kuna mmoja akaja kuongea na mimi. Akanisalimia. " what's up man." what's up brethren. "NOTHING MUCH" can you spare me some changes brother?

Nikamuuliza unataka cheji za nini. Akanijibu nataka nikusanye kusanye cheji nikanunuwe sandwich. Maana sijala tangu Jana. Nikamwambia basi kama ni hivyo twende wote pale kwenye mgahawa nikununulie chakula tule wote. Nilifanya hivyo kwasababu najuwa mahomeless wengi wa naomba hela ya kula lakini wakipata hela wanakwenda kununuwa madawa ya kulevya.

Hivyo dhamira yangu iliniambia nikimpa hela akaenda kununuwa madawa ya kulevya nitakuwa nimeshiriki kumharibia maisha. Basi akakubari kufuwatana na mimi kuelekea kwenye mgahawa. Sasa wakati tunatembea akaazisha maongeze kwa kuniuliza ninako tokea. Nikamwabia mimi natokea Tanzania. Basi akashituka. Tanzania! Yes Tanzania. Oh men, I got story to tell you.

Mimi ni kasema really? Akaanza kuongea kwa kiswahili kumbe wewe ni mtanzania mwezangu. Nikamjibu ndio. Basi tukawa tumefika kwenye mgawa tukaaa, na nikamwambia aagize chochote anacho taka nitalipa. Basi akaagiza sandwich ya nyama ya kuku na chips na soda. Nami nikaangiza soup ya maharage. Inatwa "chill soup" basi tukaanza kula huku tunaongea kwa kiswahili. Basi akaniambia kuwa baba yake alikuwa waziri maarufu Tanzania kwa mda mrefu Jina (kampuni).

Akanielezea history ya maisha yake yote. Na akaniambia nikifika nyumbani nisiseme Hali yake. Akaniambia alipofika kimaisha, Alishakata Tamaa ya maisha ila angependa story yake iwekwe wazi ili iwe fundisho kwa wengine. Kwa ufupi akaniambia maisha ya utoto wake yalikuwa ya anasa Sana kwani baba Yao alikuwa ni waziri na alikuwa anaiba hela nyingi zauma kiasi kwamba nyumbani kwao waliona pesa kama makaratasi. Na hakuwahi kujuwa kuwa ipo siku atakuja kuwa omba omba. Kwenye nchi za wengine.

Kaka nakwambia tulidekeshwa Sana. Kusoma tulisomeshwa kwenye shule za kifahari. Natuliamini maisha yataendelea kuwa Mazuri. Tukiona watu masikini tulikuwa tunafikiri wamejitakia wenyewe. Kwasababu kwetu hela zilikuwa Zina patikana wakati wowote tukizihitaji. Pamoja na baba kuwa na hela nyingi sikuwahi kujuwa kwanini alikuwa na hela nyingi kwani sikumuona akifanya biashara yoyote.

Kitu nilichoona kwenye utoto wangu ni kuona baba akichukuliwa na Gari na kurudi na Gari Nyumbani. Nyumbani tulikuwa na Madreva watatu mmoja wa kuendesha Watoto kuwapeleka shuleni. Na mwingine wa mama na mwingine wa kuendesha baba kwenda kazini na kurudi.

Nilivyo kuja Marekani kusoma baba alikuwa ananilipia kila kitu. Nilikuwa naishi kwenye apartment ya kifahari. Ambayo baba alikuwa ananilipia kodi. Nilisoma nikamaliza shule vizuri. Nikapata kazi kwenye kampuni nzuri, na nilikuwa nalipwa mshahara mzuri Sana. Kwasababu baba alikuwa bado anahela nyingi aliendelea kunilipia rent. Hivyo bado nikaendelea kuishi kama mtoto wa waziri. Mambo yalikuja kubadilika kwenye awamu ya tano hela kutoka nyumbani zikawa zimekoma ghafla. Maisha yakaanza kuniwia magumu. Mke wangu wa kizungu niliye kuwa nimeowana naye kwa miaka kumi na tatu akaanza ukorofi. Badaye tukatengana. Mimi ikabidi nitoke kwenye nyumba tuliyo kuwa tunaishi. Mwanamke akanipeleka mahakamani kudaiwa matunzo ya Watoto. Mtoto wa waziri nikaaza KUJIFUNZA kuishi kwa shida ukubwani. Nikapatwa na msongo wa mawazo nikaanza kuwa mlevi. Badaye nikashindwa kulipa matunzo ya Watoto nikakamatwa na kuweka JELA miezi mitatu.

Nilivyo toka JELA nikawa nimepoteza kazi nikaaza kuwa homeless. Lakini haya yote yamenipata kwasababu ya malezi mabaya ya kuwa mtoto wa waziri. Kama baba yangu asinge kuwa waziri akaendelea na kazi yake ya uhasibu huwenda angetulea vizuri na tungejuwa ugumu wa maisha tukiwa bado wadogo. Changamoto zimenikuta uzeeni, kuzikabili siwezi. Mzee akaanza kulia huku akitetemeka. Watu pembeni yetu wakasema huyo anahitaji vodka. Sisi tuna juwa akikaa bila pombe anakuwa kama anataka kufa. Maongeze yetu yakaishia hapo. wenye mgahawa wakaita police. Jamaa wakaja kumchukuwa na Gari la wagojwa. Police wakaniuliza kama nilikuwa naye mimi nikawambia jinsi tulivyo kutana wakachukuwa maelezo yangu. Na mimi nikawa uliza wanampeleka wapi? Wakaniambia wanampeleka kwenye hospital iliyo karibu na hapa. Kesho yake nikaenda kumjulia Hali hospital . Basi siku hiyo nikaamka asubuhi Sana kwenda kumjulia Hali huyo mtoto wa waziri. Kama mjuwavyo desturi zetu za KITANZANIA, mtu huendi kutembelea mgojwa ukiwa na mikononi mtupu. Hivyo ikabidi nipitie kwenye mgahawa ulio karibu na hospital kumchukulia kifunguwa kiywa. Kwa vile ilikuwa bado asubuhi Sana. Bahati nzuri wakati nafika tu hospital, naye ndio alikuwa anaruhusiwa kutoka hospitalini. Kwani tatizo lake lilikuwa siokubwa, ilikuwa Hali tu ya ulevi. Hospitalini, baada ya kuangaria record yake wakajuwa kuwa ni homeless wa siku nyingi (clonic homeless) hivyo ikabidi wamwache alale hospitalini kwani walimaliza kumhudumia jioni Sana. Na mashariti ya shelter za mahomeless mwisho kuipokea watu ni saa moja za usiku. Baada ya kumuona Tena nikafurahi Sana. Nikamkabidhi chakula nilicho mletea. Naye aka pokea kwa furaha tele. Basi nikamomba tukae kwenye mgahawa wa hapo hospitalini. Nilikuwa na shauku ya kusikiliza story yake pia nilikuwa maswali mengi kichwani ya kumuulizi. Kusema kweli huyu baba pamoja na ulevi wake lakini ni muongeaji mzuri. Nafikiri shida zimemfundisha mengi. Story zake hazichoshi kusikiliza. Anyway, tuka endelea na maongeze. Mimi nikamuliza: kwanini hasa unasema unajuta kuwa mtoto wa waziri? Ni wapi hasa unaona uliko sea? Jamaa akanijibu hivi: sikiliza mdogo wangu. Japo kuwa hujaniambia umri wako, kwa kuku angaria tu najuwa kabisa nimekuacha mbali kwa umri. Bwana mdogo nataka nikwambie kitu kuhusu maisha. Pamoja na kwamba niko k wenye Hali hii lakini nimejifuza mengi hizi changamoto zangu za maisha. Kitu ambacho kinanifanya nijute kuwa mtoto wa waziri ni kwamba Sasa ninaelewa mambo mengi Sana kuhusu maisha. Najuwa Hali yangu ni mbaya, watu wengi hawapendi kusikiliza watu masikini hata kama masikini ni genius kiasi gani , hakuna wa kumsikiliza. Unajuwa dogo, mtu wanapo pewa dhamana ya kuwa waziri. Huwenda aliye mtuamini kwa nafasi hiyo kubwa. Kaona kama anauwezo wa kutatuwa matatizo ya wengi. Sasa nikikumbuka baba yangu aliaminiwa kutatuwa matizo ya watu masikini wa taifa letu. Lakini nikikumbuka alivyo kuwa anahela nyingi kawaida. Naweza kusema bila shaka kuwa alikuwa wanatengeneza matatizo badala ya kutatuwa matatizo. Huwenda alikuwa anaiba hela za Uma akidhani anasaidia familia yake. Lakini ukweli alikuwa anaangamiza familia yake bila yeye mwenyewe kujuwa.
.



Nitaendelea kuongea naye. Itaendelea....
 
Maisha haya sio fair kabisa, mimi nina mwandiko safi ila niko hapa kwa Mtogole mwenzangu anaandika kama mtoto wa chekechea yupo NY huko!
Mzee wa NY, kiswahili kinakupiga chenga.Halafu, jifunze kusimulia kwa kwenda kwenye hoja.Unasimulia vitu vingi hata havina maana.
Tatizo lake kubwa ni R na L. Makosa mengine ni dictionary ya simu yake inabadili maneno na kumuharibia anacho andika.
 
Hapana, makosa ni mengi sana. Maneno kwa usahihi wake, kuunga na kutenganisha maneno n.k.
Hata bila kuangalia makosa hayo, uandishi wenyewe ni mgumu sana kwake. Mpangilio na mtiririko wa hadithi, na namna ya kueleza jambo lionekane kuwa ni la kweli, kwake ni shida kubwa.

Unakutana na "kundi la homeless", New York, unaamua kwenda kujitambulisha kwao, na wewe ni mgeni, tena toka mbali kabisa?
 
Hata bila kuangalia makosa hayo, uandishi wenyewe ni mgumu sana kwake. Mpangilio na mtiririko wa hadithi, na namna ya kueleza jambo lionekane kuwa ni la kweli, kwake ni shida kubwa.

Unakutana na "kundi la homeless", New York, unaamua kwenda kujitambulisha kwao, na wewe ni mgeni, tena toka mbali kabisa?
Ameona kutufunga kamba hakutoshi. Ameamua kutufungasha kwenye sandarusi.
 
Hata bila kuangalia makosa hayo, uandishi wenyewe ni mgumu sana kwake. Mpangilio na mtiririko wa hadithi, na namna ya kueleza jambo lionekane kuwa ni la kweli, kwake ni shida kubwa.

Unakutana na "kundi la homeless", New York, unaamua kwenda kujitambulisha kwao, na wewe ni mgeni, tena toka mbali kabisa?
Kama vile ameenda NY kusalimia homeless..hahaha
 
Hata bila kuangalia makosa hayo, uandishi wenyewe ni mgumu sana kwake. Mpangilio na mtiririko wa hadithi, na namna ya kueleza jambo lionekane kuwa ni la kweli, kwake ni shida kubwa.

Unakutana na "kundi la homeless", New York, unaamua kwenda kujitambulisha kwao, na wewe ni mgeni, tena toka mbali kabisa?
Hujaelewa au umekurupuka as usual ya JF na kizazi cha 1990's to 2000's. Soma vizuri wametambulishana wakiwa wawili japo story hii ni chai ukiangalia anavyoiandika.
 
Taja wizara ya huyo waziri, bila hivyo unajifunza kuandika hadith, japo watoto wa vingozi wapo wenye maisha hayo lkn yako ni hadith tu.
 
Back
Top Bottom