Tatizo kwanini hawakati kamba na kuelekea kwengine ,Mwalimu Nyerere alikwishawambia kuwa huwezi kupinga wakati umo ndani ya CCM ni lazima utafute uwe nje ya Chama ndio upinge,kubakia CCM ni kuendeleza makundi yao,kila siku ninapiga makelele kama unaamini unawatumikia wananchi na wewe umo ndani ya CCM ,basi ukiona uchafu na hakuna linalotokea toka kwenye CCM ,kuna vyama tele vya upinzani na wananchi watakujua kwamba ulisimama kidete na umefanya kweli katika kuzikataa na kupinga hila za Chama cha mafisadi ,kwa msimamo wa Nyerere huwezi kuwemo ndani na ukawa mkweli kwa unayoyasema ,zaidi itaonekana ni majungu ,toka CCM na watu wasikie kuwa umetoka kwa sababu unazozipigia makelele kwa ufupi hakuna utawala wa sheria ndani ya CCM ,au sheria ni kwa walala hoi tu ,vibosile.
Ondoka huko CCM ,sasa kama kuna kundi linaona utawala uliopo ni wawachache kwanini halimeguki na kuongezea nguvu zao kwa upinzani ,wanabakia humo humo kuzozana ,zaidi itakuwa mmezidiana kete hamna ukweli wa kuwatendendea kuwaletea wananchi kile wanachokitafuta na kukisaka ,ugonvi wa matatizo yenu na machozi yenu ya mamba unatafuta huruma za wananchi ,lakini mnapiga makelele kwa sababu mmepigwa buti na kuzidiwa na wajanja miongoni mwenu.
Zaidi wananchi waelewe hawa wanaopigia makelele ndani ya CCM dhidi ya wenzao nao pia ni mafisadi ,dawa yao ikiwa mtu atabakia ndani ya CCM basi apigwe buti la nguvu katika uchaguzi ,aidha wapewe uhuru wa kujiengua ikiwa imebaki siku moja kupiga kura ili kuonyesha kupinga kwao , ila wanaubavu wa kufanya hivyo inataka mtu ambae amejitolea kupambana na CCM mpaka dakika ya mwisho. Kubaki na makelele yao ni hila za kuwadanganya wananchi.