The road towards 2010 Elections

The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
[urambotabora;354523]Jamani katika haka ka list kangu haka mnaona Nani anaweza kuliongoza taifa letu angalau tukawa na imani na serikali yetu ?

Bernard Membe

Edward Lowasa

Dr.Wilbard Slaa

Ibrahim Lipumba

Samwel Sitta

Mizengo Pinda
Mark Mwandosya

Jakaya kikwete

Mizengo Pinda. Wengine wote ni siasa tu.
 
Mgombea binafsi wa uRais? Yaani mtu atoke huko na hisia zake binafsi na aongoze nchi? Yaani tuongozwe na hisia binafsi? Kwa kisa gani hasa?

Siamini kuwa kuna tija yoyote zaidi ya madhara kama tukiwa na Rais atakaechaguliwa bila kutoka kwenye chama au taasisi yenye mfumo thabiti wa uongozi. Kuwa na mgombea wa kuteuliwa na chama chake, inatuhakikishia kuwa anafuata sera zinazoaminika, zinazokubalika, zinazoweza kudumu na zenye tija kwa Taifa. Mtu binafsi akichaguliwa kuwa Rais anaweza kuji-control hasa katika masuala ya ethics, policies na kutekeleza mambo sustainably? I doubt.

Recta,
Haya mawazo yako ndio yale yale yaliyotufikisha hapa tulipo.
Sisi wote ni wanadamu tu. Kila mmoja anatawala kwa mawazo na hisia zake.
Hata Kikwete pia hapa anatawala kwa hisia na matakwa yake. Ndio sababu alilala siku moja akaamua vile visenti walivyokwiba na kuvirudisha ziende kwenye benki fulani na zisaidie wakulima.

Ndio sababu aliamua kutoa mipesa kwa kila mkoa shilingi bilioni. Nadhani kwa kuigiza ile sera ya John Cheyo (LOL).

Ni mawazo yake na hisia zake tu zilikuwa zikimtuma kufanya yote hayo.
Sasa unaposhikia bango mgombea binafsi kwa hoja zako ninazoziona hapa naona unaturudisha kule kule kwamba kama unataka kuwa kiongozi wa nchi hii ni lazima utoke kundi fulani. Tena kama wewe si wa kundi hilo au kundi hilo halikulidhii basi usiote kupata uongozi wa nchi hii.

Huku ni kujidanganya tu!
 
Recta,
Haya mawazo yako ndio yale yale yaliyotufikisha hapa tulipo.
Sisi wote ni wanadamu tu. Kila mmoja anatawala kwa mawazo na hisia zake.
Hata Kikwete pia hapa anatawala kwa hisia na matakwa yake. Ndio sababu alilala siku moja akaamua vile visenti walivyokwiba na kuvirudisha ziende kwenye benki fulani na zisaidie wakulima.
Ndio sababu aliamua kutoa mipesa kwa kila mkoa shilingi bilioni. Nadhani kwa kuigiza ile sera ya John Cheyo(LOL).
Ni mawazo yake na hisia zake tu zilikuwa zikimtuma kufanya yote hayo.
Sasa unaposhikia bango mgombea binafsi kwa hoja zako ninazoziona hapa naona unaturudisha kule kule kwamba kama unataka kuwa kiongozi wa nchi hii ni lazima utoke kundi fulani. Tena kama wewe si wa kundi hilo au kundi hilo halikulidhii basi usiote kupata uongozi wa nchi hii.
Huku ni kujidanganya tu!

Mchukia Fisadi, nashukuru kwa kijibu maelezo yangu vizuri. Nakuhakikishia kuwa tuko pamoja. Ili kuweka maelezo yangu vizuri zaidi, labda niseme hivi, Mimi siamini kuwa ni vyema kuwa na mgombea u-Rais binafsi. Naamini ni vyema na haki kuwa na wagombea binafsi katika nafasi nyingine zote (Ubunge/Udiwani n.k.). Sababu za mimi kudhani hivyo ni nyingi.

1. Mapungufu makubwa yaliyopo kwenye katiba yetu. Ambapo Rais anakuwa na kinga kubwa, na nguvu nyingi sana

2. Ni kushindwa kwetu kukataa kurubuniwa na wanasiasa wenye pesa. Chaguzi za siku hizi zinaonyesha kuwa ukiwa na pesa (Kwa u-Rais, unaweza kuzipata nje ya nchi), unakuwa na nafasi kubwa ya kushinda.

3. Fikra binafsi kwa 100% haziwezi kuwa na maslahi kwa Taifa. Maana zinatokana na mipango ya mtu binafsi na zenye kulenga mahitaji ya kufikirika kibinfsi zaidi.

Mathalan, Rais (aliechaguliwa kwa ugombea binafsi) anaweza kuamua kuelemea makundi (kidini, Kikabila ama vinginevyo) atakayoona yeye kuwa na maslahi kwake zaidi ya kitaifa (kwa kuwa yeye ndio sera). Rais huyo atahakikisha anakidhi haja za makundi hayo ili kuendelea kubaki madarakani (kwa kuwa hata yeye ana nunulika). Misimamo yake itaangalia zaidi maslahi ya makundi atakayoyachagua yeye (watu binafsi). Hivyo kuzua kwa ukabila, udini n.k.

4. Udikteta mkubwa Afrika ulisababishwa na viongozi walioingia madarakani kwa nguvu binafsi (kupindua nchi). Sidhani kama walifanikiwa sana zaidi ya Kumwaga damu nyingi.

Ni hayo tu mkuu kwa sasa.
 
...Something is Definitely Cooking! Kwenye taarifa ya habari ya ITV ya saa mbili usiku kuna habari tatu zilizotokea maeneo tofauti nchini lakini zenye muelekeo mmoja:

1. Vijana CCM Dodoma wameandamana kuunga mkono maneno ya Mzee Cigwiyemisi ya kutaka Mheshimiwa Kikwete apewe nafasi nyingine tena ili kumaliza kazi alizoanza e.g kupiga vita Ufisadi, wauaji wa Albino.

2. Akina mama wa Wilaya moja ya Moshi nao wametoa tamko kama hilo hilo la kutaka Kikwete kuwa mgombea pekee wa Urais kutoka CCM

3. Kuna wazee kutoka Wilaya nyingine nchini ambayo bahati mbaya sikusikia jina lake nao wametaka Mheshimiwa Kikwete kupewa nafasi ya kumaliza kazi alizoanza!

Nafahamu kwamba hakuna tatizo lolote kwa taarifa moja ya Habari kuwa na matukio matatu kutoka maeneo matatu tofauti nchini TZ yote yakihusu Mheshimiwa Kiwete kuwa mgombea pekee wa Uraisi kutoka CCM, but it just makes one raise an eyebrow....!
 
Last edited by a moderator:
Wameamua kuchagua zimwi walijualo....Typical miafrika.Kwani ni lipi kuu amelifanya kwenye mauaji ya albino?Pls msijeniambia zile kura za maoni&ile jino kwa jino ya PM.Vita dhidi ya ufisadi???Wapi kagoda,meremeta,mwananchi,deepgreen et al.Hao waandamanaji watakuwa wameahidiwa "ubwabwa" tu.
 
Wanabodi, nini kinaendelea ndani CCM kwa sasa? Kunani? Takribani wiki mbili sasa, wana CCM, kuanzia Malecela hivi majuzi alipokuwa akiongea na waandishi wa habari, na sasa makada mbalimbali wa CCM wiki hii wameendelea kuibuka na kusisitiza kuwa mgombea wa CCM 2010 ni JMK pekee, hakuna mwingine. Is this necessary, especially now?

Huu ujumbe wanamfikishia nani? Au habari za mitaani ndio habari kamili? Kunani? Kwa kumbukumbu zangu, bado sijamskia mwanaCCM yeyote (hata JMK mwenyewe) kutamka waziwazi kwamba atagombea 2010, japo inatarajiwa.

CCM, siku hizi wamekuwa watu wa kufikishiana ujumbe kwenye mikutano ya hadhara na vyombo vya habari. Zamani, wimbo ulikuwa ni kwamba, ukiwa na jambo, fuata utaratibu rasmi wa vikao. Katiba ya CCM kwa sasa inasemaje? Je, majukwaa ya hadhara na vyombo vya habari ni sehemu ya utaratibu wao wa kupashana habari?

Who is Scaring Who, this Early?

Can someone one tell us What's Going On?
 
Ka-nchi ketu na siasa!
Yaani tayari mumeshaamua tuache agenda zingine, tuanze kuongelea uchaguzi?
Hivi hakuna siasa zingine zaidi ya uchaguzi?
 
Vipi yule mheshimiwa aliyesema kuwa yeye ni mfungwa ndani ya CCM???
 
Mkuu Sekenke... si wewe peke yako mwenye dukuduku. Hii nayo ni thread aliyoanzaisha BabaDesi

...Something is Definitely Cooking! Kwenye taarifa ya habari ya ITV ya saa mbili usiku kuna habari tatu zilizotokea maeneo tofauti nchini lakini zenye muelekeo mmoja:

1. Vijana CCM Dodoma wameandamana kuunga mkono maneno ya Mzee Cigwiyemisi ya kutaka Mheshimiwa Kikwete apewe nafasi nyingine tena ili kumaliza kazi alizoanza e.g kupiga vita Ufisadi, wauaji wa Albino.

2. Akina mama wa Wilaya moja ya Moshi nao wametoa tamko kama hilo hilo la kutaka Kikwete kuwa mgombea pekee wa Urais kutoka CCM

3.Kuna wazee kutoka Wilaya nyingine nchini ambayo bahati mbaya sikusikia jina lake nao wametaka Mheshimiwa Kikwete kupewa nafasi ya kumaliza kazi alizoanza!

Nafahamu kwamba hakuna tatizo lolote kwa taarifa moja ya Habari kuwa na matukio matatu kutoka maeneo matatu tofauti nchini TZ yote yakihusu Mheshimiwa Kiwete kuwa mgombea pekee wa Uraisi kutoka CCM, but it just makes one raise an eyebrow....!
BabaDesi
 
Wanabodi, nini kinaendelea ndani CCM kwa sasa? Kunani? Takribani wiki mbili sasa, wana CCM, kuanzia Malecela hivi majuzi alipokuwa akiongea na waandishi wa habari, na sasa makada mbalimbali wa CCM wiki hii wameendelea kuibuka na kusisitiza kuwa mgombea wa CCM 2010 ni JMK pekee, hakuna mwingine. Is this necessary, especially now?

Huu ujumbe wanamfikishia nani? Au habari za mitaani ndio habari kamili? Kunani? Kwa kumbukumbu zangu, bado sijamskia mwanaCCM yeyote (hata JMK mwenyewe) kutamka waziwazi kwamba atagombea 2010, japo inatarajiwa.

CCM, siku hizi wamekuwa watu wa kufikishiana ujumbe kwenye mikutano ya hadhara na vyombo vya habari. Zamani, wimbo ulikuwa ni kwamba, ukiwa na jambo, fuata utaratibu rasmi wa vikao. Katiba ya CCM kwa sasa inasemaje? Je, majukwaa ya hadhara na vyombo vya habari ni sehemu ya utaratibu wao wa kupashana habari?

Who is Scaring Who, this Early?

Can someone one tell us What's Going On?

Hawa unaowasikia wanampinga Karume ,maana Karume anatayarishwa kuchukua nafasi ya Kikwete ,ikiwa Kikwete ataamua kuachia ngazi ,ila wapo katika kutoa ishara kuwa hakuna sababu ya Kikwete kuachia ngazi, kama unakumbuka Mwinyi alipomaliza kuwa Raisi wa Zanzibar alipewa wa Tanzania na ndio hivyo hivyo ,kama unavyofahamu taratibu za CCM ,ili kujificha na ile dhana kuwa Zanzibar haipewi uongozi wa Tanzania ,ndio inaonekana kuwa Karume apishwe katika kipindi hiki au hata Kikwete akimaliza miaka kumi yake kama akiipata apewe Karume.Ni utaratibu wanaosema wamejipangia au wameamua kuurudisha ili kudumisha muungano.
 
Hayo ni mambo ya kawaida tu na hayo aliyoyasema mzee Malecela ni mawazo yake binafisi na hata yale mawazo yanayotolewa na baadhi ya makada pia ni mawazo binafsi hilo la vikao ni suala linalojadiliwa katika vikao na wakati utakapofika vikao vitajadili na kufanya maamuzi
 
Wewe Mwiba, nani kakuambia Karume anasifa za kuwa rais wa Tanzania? Unaacha kuangalia watu wenye uwezo na mtizamo? huyo sana sana labda kuwa mkuu wa mkoa tu.

Hawa unaowasikia wanampinga Karume ,maana Karume anatayarishwa kuchukua nafasi ya Kikwete ,ikiwa Kikwete ataamua kuachia ngazi ,ila wapo katika kutoa ishara kuwa hakuna sababu ya Kikwete kuachia ngazi, kama unakumbuka Mwinyi alipomaliza kuwa Raisi wa Zanzibar alipewa wa Tanzania na ndio hivyo hivyo ,kama unavyofahamu taratibu za CCM ,ili kujificha na ile dhana kuwa Zanzibar haipewi uongozi wa Tanzania ,ndio inaonekana kuwa Karume apishwe katika kipindi hiki au hata Kikwete akimaliza miaka kumi yake kama akiipata apewe Karume.Ni utaratibu wanaosema wamejipangia au wameamua kuurudisha ili kudumisha muungano.
 
Wewe Mwiba, nani kakuambia Karume anasifa za kuwa rais wa Tanzania? Unaacha kuangalia watu wenye uwezo na mtizamo? huyo sana sana labda kuwa mkuu wa mkoa tu.

Hata ukuu wa mkoa ni kumpendelea tu tena upendeleo wa wazi na hasa mkoa wenyewe ukiwa kama dar = chaos ... maana idadi ya watu ni zaidi ya mara tatu ya wale wanaomshinda kuwaongoza sasa, kwa hiyo inafaa kumuonea huruma na kumpumzisha kabisa, au kama anapenda sana madaraka awe mshauri wa mgambo... tosha

-----------
Tuna kazi ya kutafuta kazi
 
Hawa unaowasikia wanampinga Karume ,maana Karume anatayarishwa kuchukua nafasi ya Kikwete ,ikiwa Kikwete ataamua kuachia ngazi ,ila wapo katika kutoa ishara kuwa hakuna sababu ya Kikwete kuachia ngazi, kama unakumbuka Mwinyi alipomaliza kuwa Raisi wa Zanzibar alipewa wa Tanzania na ndio hivyo hivyo ,kama unavyofahamu taratibu za CCM ,ili kujificha na ile dhana kuwa Zanzibar haipewi uongozi wa Tanzania ,ndio inaonekana kuwa Karume apishwe katika kipindi hiki au hata Kikwete akimaliza miaka kumi yake kama akiipata apewe Karume.Ni utaratibu wanaosema wamejipangia au wameamua kuurudisha ili kudumisha muungano.

Kuna kitu kinaitwa Ilani za CCM moja kati ya ilani hizo ni kuwa mtu kugombea uraisTANZANIA ijapokuwa hii inatumia Mainland ni lazime apate elimu ya UNI kwa upande wa ZANZIBAR wao huwambiwa hawahitaji mtu mwenye elimu alimradi awe na akili tu isiyopunguwa kiwango cha muuza Gederi kwa mana nyingine uzowefu sasa narudi kwenye hili la karume kuwa Rais TANZANIA sidhani wasomi wa kule bara kama wapo tayari kupandishwa Rikwama (Mkokoteni )hasa katika dunia ya leo
 
, especially now?
Huu ujumbe wanamfikishia nani? Au habari za mitaani ndio habari kamili? Kunani? Kwa kumbukumbu zangu, bado sijamskia mwanaCCM yeyote (hata JMK mwenyewe) kutamka waziwazi kwamba atagombea 2010, japo inatarajiwa.
Nikukumbushe tu kuwa John Shibuda alishatangaza nia yake ya kugombea hiyo nafasi ya urais mwaka 2010.
 
Hata ukuu wa mkoa ni kumpendelea tu tena upendeleo wa wazi na hasa mkoa wenyewe ukiwa kama dar = chaos ... maana idadi ya watu ni zaidi ya mara tatu ya wale wanaomshinda kuwaongoza sasa, kwa hiyo inafaa kumuonea huruma na kumpumzisha kabisa, au kama anapenda sana madaraka awe mshauri wa mgambo... tosha

-----------
Tuna kazi ya kutafuta kazi

Kwi kwi kwi kwi kwi, teh teh teh walahi Mwiba lazima arushe ngumi akiiona hii
 
Mkuu CCM washaona candidate wao hana sifa kwahilyo inabidi watumie mabavu kuhakikisha anaendelea
 
Heshima mbele sana,

- Wakuu tunapokata ishu tuwe tunajali kwamba hoja zetu zinawafikia wananchi wengi wanaokuja hapa kutafuta elimu ya taifa lao, sasa tukiwa-mislead ndio matokeo yanakuja kuwa tofauti na wananchi kukatishwa tamaa. Hivi ni kikao gani cha CCM leo mwaka 2009 kitakacho mpitisha mgombea mwingine over the sitting president? Toeni mifano, tizama nchi fulani rais aliondolewa na chama chake kabla ya kumaliza term ya pili, hivi yamewahi kutokea wapi zaidi tu ya SA ambako hata na wao hakieleweki?

- Mimi binafsi reading between the lines, kwa maoni yangu ni kwamba ndani ya CCM kumekua na makundi ya kisiasa na in itikadi, I see nothing to be wrong with that, isipokuwa kuna kundi moja ambalo limekuwa likihangaika sana na kutaka urais by 2010, sasa walichokosea so far katika nia yao ni kushindwa kushawishi makundi mengine dnani ya CCM kuwaunga mkono, infact wala hawakuwahi kujaribu kuwa-consult, beleiving kwamba wanazo nguvu za kutosha, sasa ninachoona ni kwamaba kuna rebellious ya makundi mengine against hili linalotaka urais na inatokana hasa na tabia zao walizokwisha zionyesha tayari katika uongozi wa juu.

Lakini kuna kitu kimoja muhimu sana hapa, miezi 8 iliyobaki, ni mingi sana kisiasa, anything can happen, ila for now hao wanaotaka kupingana na rais wa sasa, wamehairbu big time kwa sababu sasa wamempa mwanya rais wa sasa ku-mobilize wana CCM wote kwa kisingizio cha kutaka kuharibiwa na mafisadi, in the process hakuna atakayeuliza record yake, ila itakuwa wimbo wa kupigana na mafisadi tu, atakusanya wote maana ni wimbo mzuri sana kwa wasioelewa kitu.

Mungu Aibariki Tanzania.

FMES!
 
Ni kazi gani gani jmk aliyoianza inabidi amalizie? What?
 
Back
Top Bottom