The road towards 2010 Elections

The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
Andindile,
Kikwete anastahili kugombea kipindi cha Pili?..
Jibu langu nni NDIYO!..
...

Mkandara umejibu vyenma, unaweza kutoa sababu kwa nini unafikiri Kikwete anastahili kugombea/kuongoza kipindi cha pili? na klama sababu ni uhuru wa kikatiba , so unafikiri kila mwenye uhuru wa kikatiba anafaa kuwa rais?
 
Nimeshindwa kupiga kura. Sikuona mahali panasema "none of the above."
 
nimeshindwa kupiga kura. Sikuona mahali panasema "none of the above."


kwani karatasi la kura tz kuna sehemu inayosema non of the above.
Non of the above ni sawa na kukaa nyumbani na kutokwenda kupiga kura
 
Rais awe Dr.Salim Ahmed Salim halafu waziri mkuu piga ua ni John Pombe Magufuli
Kikwete anaweza kupewa wizara ya habari,utamaduni na michezo
nasema baada ya miezi 6 tu Mabadiliko chanya yataanza kuonekana Tanzania!
 
Andindile,
Mkuu kwanza unakosea kusema hivyo kwa sababu utakuwa unakiuka demokrasia inayokupa wewe nafasi ya kuchagua kiongozi pamoja na kwamba wagombea ni wengi..Na kati yao wapo wasiofaa kuongoza na ndio maana hatawachagua kuongozi nchi..
Unapochaguliwa kuongoza nchi, ni matokeo ya kufaa kuongoza sio sababu leading to kugombea, na unaposhindwa ina maana hufai kuongoza nchi kutokana na sababu za wapiga kura waliokutosa....sio kwamba hukufaa kugombea urais.
Upo babuuu!

Waberoya,
Labda nifafanue vizuri mtazamo wangu hapa. Kikwete anafaa kugombea Urais kwa sababu ya kikatiba na sio kweli kabisa kwamba anyefaa kugombea basi bila shaka anafaa kuongoza nchi.. ndio maana tumeweka Kura za wananchi.. Kila kitu hatua sasa unaposema asiyefaa kugombea ni lazima uzitazame sheria za kikatiba zinasema nini kuhusiana na mgombea.. Sasa kama Kikwete hana sifa hizo za mgombea bila shaka hafai kugombea..Kuna watu wengi sana wanafaa kuongoza, pengine hata wewe unfaa kuongoza nchi lakini kwa sababu huna chama basi hufai kugombea urais..mgombea urais binafsi hafai kugombea haina maana hafai kuongoza nchi!

Kikwete hafai kuwa rais wa nchi kwa awamu ya pili ndio mtazamo wangu na ndivyo nilivyosema wakati wa Mwinyi, Mkapa lakini bado waliendelea kutawala..Hivyo walifaa kutawala ndio maana wakatawala -inabidi nikubali mfumo wa wengi wape au sio?..

Mimi kama Mpinzani nawakilisha hoja yangu kwenu kwamba CCM haifai kuongoza nchi na mbora kati yao lazima atakuwa hafai kuongoza nchi.. Siwakatazi kugombea nafasi ya Urais hata kidogo lakini hawafai.
Hii inatokana na sera na mrengo wa chama na sio mtu atakaye teuliwa... Historia ya chama hicho inatakiwa kutufundisha na sii kufikiria kuna mbora kati yao ambaye anaweza kuleta maendeleo hata kama chama kimekuwa hijacked!.. Hizi ni fikra finyu, ni mawazo mgando ambayo ndiyo kila siku yametuweka ktk matatizo. Ni sawa na tumeshindwa kuelewa nini maana ya kuwepo vyama vingi badala yake tunatazama watu wengi toka chama kimoja..Ni akili ya Kikomunist

Sasa nizungumze kama mtu nje ya imani yangu ya chama.. Ikiwa sina choice nje ya CCM kumteua mtu kuongoza nchi basi hakuna zaidi ya Kikwete.. kwa sababu mbili muhimu..
1. Hakuna mtu mwingine alojitokeza kugombea nafasi hiyo. Siwezi kwenda na nchi isiyokuwa na uongozi kama Somalia ila nitahitaji mtu kuniongoza na nitaweza tu kuwapima watu hawa kama wamejitokeza..
Ni jambo la ajabu mtu kutaka kubadirisha tairi la gari kwa sababu linatoa upepo, wakati huo huo huna spare tyre..Ndipo niliposimama mimi na busara za mjadala huu.

2. Mbinu ya kudhoofisha uongozi wa Kikwete ndani ya gari bovu la CCM imeundwa na mafisadi ambao mimi nakataa kabisa kuwa nyuma yao. NI bora nibakie na Kikwete ambaye kawageuka kuliko kuendeshwa na mmoja wa watu toka kundi la Mafisadi.. Kwa sababu naifahamu nguvu ya Dola.. atakayeingia Ikulu kama nim mtu wa Rostam tumekwisha.. Bora zimwi likujualo..
 
Andindile,
Mbinu ya kudhoofisha uongozi wa Kikwete ndani ya gari bovu la CCM imeundwa na mafisadi ambao mimi nakataa kabisa kuwa nyuma yao. NI bora nibakie na Kikwete ambaye kawageuka kuliko kuendeshwa na mmoja wa watu toka kundi la Mafisadi.. Kwa sababu naifahamu nguvu ya Dola.. atakayeingia Ikulu kama nim mtu wa Rostam tumekwisha.. Bora zimwi likujualo..

Mkandara, ni ukweli usiopingika kuwa viongozi wengi wametumia kipindi chao cha mwisho madarakani kujinufaisha bila aibu - for they have nothing to lose. Kama ni kweli kuwa Kikwete kawageuka Mafisadi na wao wameamua kuunda mbinu ya kudhoofisha uongozi wake, umeridhika na hatua ambazo mpaka sasa amechukua kuwashughulikia ?. Na kama hajaweza kuchukua hatua madhubuti dhidi ya Rostam na wezake, atawezaje akiongezewa kipindi cha mwisho ambapo hatakuwa tena na haja ya kubembeleza kura ? Naomba tuwe honest katika mitizamo yetu - leo hii huwezi ukamshikia bango Rostam na hapo hapo ukamfagilia Kikwete, that is being a little disingenuous.
CCM na Mafisadi, lao moja.
 
kwani karatasi la kura tz kuna sehemu inayosema non of the above.
Non of the above ni sawa na kukaa nyumbani na kutokwenda kupiga kura

Kama wagombea ni hao pekee, heri nikae nyumbani nisiharibu kura yangu. But on a serious note - kwa nini usiweke hiyo sehemu ya none of the above. Nina hakika hii itasadidia kujua wengine tusivyo na imani na hiyo listi - some of us already have in mind someone capable of bringing change na mtu kama huyo mtu yupo mbali kabisa na hiyo listi.
 
Watu wengi mmekua mkimpinga jk kutokana na udhaifu wake, na sasa jk ameanza kampeni yake kutumia wazee.


JINSI MAJINA NILIVYO YACHAGUA
SAS - ANAWAKILISHA WATU AMBAO HAWAKO KWENYE SYSTEM.
SHIBUDA & MWAKYEMBE - WABUNGE
MWANDOSYA & MAGUFULI - TISHIO NDANI YA BARAZA LAKE
MEMBE & MKULO - MBEGU ZA JK
PINDA, KARUME - SIO MAADUI WA JK BALI WANAMALENGO YA CHEO CHA JUU (AMBITION ZA KUWA RAIS)
DR SHEIN - MTU WA MKAPA

NIMESHINDWA KUONA MWANAMKE AMBAYE ATATOA USHINDANI/ AU KIONGOZI MZURI

Je swali ni nani kati ya hawa awe badala ya jk?

piga kura hapo juu.
Ongeza option ya 'Mwingine', kwani wengine tuna 'watu wetu' pia. Au option ya 'none of the above'.
 
Abeid Karume mbona ameshakufa 1972 ,huu ni upigaji kura wa kiCCM mpaka maiti wamo dah ,au daftari halijaboreshwa. 😀
 
Kwa list hiyo hapo juu bado naona Tanzania tupo mbali sana kupata maendeleo ya kweli. Hayo ndiyo maoni yangu. Kama walivyoshauri members wengi, tafadhali ongeza None of the above kama ilivyokuwa enzi za Chama kimoja Mgombea kupambana na Kivuli.
 
abeid karume mbona ameshakufa 1972 ,huu ni upigaji kura wa kiccm mpaka maiti wamo dah ,au daftari halijaboreshwa. :d

unajua abeid ni jina kubwa sana na ni rahisi kulifunika amani kwa hiyo mtu unajikuta unasema abeid badala ya amani.
 
2. Mbinu ya kudhoofisha uongozi wa Kikwete ndani ya gari bovu la CCM imeundwa na mafisadi ambao mimi nakataa kabisa kuwa nyuma yao. NI bora nibakie na Kikwete ambaye kawageuka kuliko kuendeshwa na mmoja wa watu toka kundi la Mafisadi.. Kwa sababu naifahamu nguvu ya Dola.. atakayeingia Ikulu kama nim mtu wa Rostam tumekwisha.. Bora zimwi likujualo..

hii kitu haipo kabisa, una maneno mengi mkuu, lakini hapa wadanganye hao hao, kumbe na wewe ni wa aina ya mhariri wa mwanahalisi!

1. Kikwete ni fisadi, hivyo swala la kuwa kuna mafisadi wanaomdhoofisha ni uongo, na kama umedanganywa hivi waambie hao watu kuwa kuna watu wanapinga.

2. Mafisadi wote utakaowataja kuwa wanamdhoofish JK ni marafiki wa karibu wa JK! hata kama wamegeukana, JK kashika nchi!

3. Hatujasikia mbiu ya Kikwete kuhusu mafisadi. tunamsemea, tunamlazimisha kuchukua hatua,mpaka nchi wahisani wanamlazimisha achukue hatua!

4. Kusema CCM haifai! at the sama time unasema afadhali JK kuliko Rostam, ni utoto wa-wakwetu, unachanganya mambo, na siasa za ukweli haziendi hivyo! kwani Rostam ana nini, Rostam ana matatizo gani?? si naye ana haki ya kugombea urais?? UKISEMA ROSTAM FISADI INA MAANA MAMBO YOTE ULIYOANDIKA KWENYE POINT YAKO YA MWISHO NI YA UONGO, KAMA KIKWETE HATAKI UFISADI, BASI WALE WASHUKIWA WOTE WA UFISADI WANGEKUWA WAMESHAENDA JELA, KESI MAHAKAMANI, HATA KULAZIMISHWA KUJIONDOA!

UNASEMA KIKWETE ANAPINGA UFISADI, KAMATI KUU YA CCM WAKO AKINA NANI??, KWA MAMLAKA YA KIKWETE ATISHWE NA MAFISADI??

5. Kama wewe umefunguka macho si kila anayechaguliwa kwa kura nyingi ni watu wengi wameamua! labda unasema kuwa hamna wezi wa kura, na hao wanamchagua kwa wingi ni wangapi kati ya wanaotakiwa kupigiwa kura??

Hakuna mbinu yeyote ya kumdhoofisha JK, ila kuna mbinu ya kuwachanganya watu kama wewe!

JK FISADI, NARUDIA JK FISADI.... I repeat JK fisadi........kumsupport yeye hakukupi jina lingine lolote zaidi ya fisadi tu!
 
Hata mimi nimeshindwa kupiga kura kama Jasusi, hakuna none of the above, kwa sababu hakuna anayefaa kati ya hao.

Hakuna mtu anaetaka majambazi kutoka CCM.
 
Mugo"The Great";420253 said:
Kwa list hiyo hapo juu bado naona Tanzania tupo mbali sana kupata maendeleo ya kweli. Hayo ndiyo maoni yangu. Kama walivyoshauri members wengi, tafadhali ongeza None of the above kama ilivyokuwa enzi za Chama kimoja Mgombea kupambana na Kivuli.

Mi nachagua option X: News3Online is your breaking news center

lol ...
 
Nani kati ya wanajanvi alijua kuwa Lowassa angeachia ngazi ya uwaziri mkuu kabla ya kipindi cha kwanza cha urais wa Kikwete kwisha? Hivyo basi nadhani ni mapema mno kuzungumzia juu ya kipindi cha pili cha urais wa Kikwete kwani Mwenyezi Mungu anamipango yake ya kuikomboa nchi hii toka kwenye makucha ya mafisadi wanaolindwa na muungwana!!
 
JMK inafaa asigombee bali aombwe na vyama vyote apite bila kupingwa. Maendeleo anayotuletea sasa yalibidi yaletwe miaka 40 iliyopita .
 
Watu wengi mmekua mkimpinga jk kutokana na udhaifu wake, na sasa jk ameanza kampeni yake kutumia wazee.


JINSI MAJINA NILIVYO YACHAGUA
SAS - ANAWAKILISHA WATU AMBAO HAWAKO KWENYE SYSTEM.
SHIBUDA & MWAKYEMBE - WABUNGE
MWANDOSYA & MAGUFULI - TISHIO NDANI YA BARAZA LAKE
MEMBE & MKULO - MBEGU ZA JK
PINDA, KARUME - SIO MAADUI WA JK BALI WANAMALENGO YA CHEO CHA JUU (AMBITION ZA KUWA RAIS)
DR SHEIN - MTU WA MKAPA

NIMESHINDWA KUONA MWANAMKE AMBAYE ATATOA USHINDANI
/ AU KIONGOZI MZURI

Je swali ni nani kati ya hawa awe badala ya jk?

piga kura hapo juu.

And how do you analyse this:

...The fact is, Sumaye, who had been Kikwete’s unsuccessful rival contender for the CCM investiture for the 2005 presidential election, could try his chance again in 2010. He has not yet publicly announced his decision, but sources inside the CCM suggest that certain high-ranking officials ousted by Kikwete or still in their posts but discontent with the President’s anti-corruption campaign, do not want to see Kikwete obtain a second mandate. In that case, Sumaye could become a replacement candidate for this wing of the CCM. Especially if Kikwete’s backers and financers, such as Rostam Aziz, who had been subject to attacks in Parliament for their supposed links with a company implicated in a shady affair, decide to drop the outgoing President for the 2010 election.

Source: Kikwete mad at Membe - THE INDIAN OCEAN NEWSLETTER

How has political tectonic plates realigned themselves at the moment. Is Sumaye, or Lowassa for that matter vying for the high office? And when we start hearing cries of ooh, its only JK in 2010, is this a fight-back strategy against the "real power" and king-maker, Rostam Aziz, mentioned in this article, who determines, and not Wananchi, who becomes the President of Tanganyika?
 
naamin kabisa unamaana mbadala wa jk ndani ya ccm

katika tuwajuao yupo anayeweza kuperform vizuri zaid na zaid kuliko jk. huenda anaweza kuharibu zaid na zaid pia. lakin ni muhimu kujua kuwa yupo the best president somewhere - miongon mwa tuwajuao

semilong,

pengine ungeanza kwa kuwataka watu wapendekeze nani katka watz waliopo anafaa kuwa president. wangepatikana best 10 say, tungewapigia kura wote

kwasasa umetufunga. si mbaya tukiwa as free as air
 
Back
Top Bottom