Bubu Ataka kusema na Recta,
Wakuu zangu vipi lugha inawapa shida?...
Hivi kweli hamfahamu matumizi ya neno a thin line between Love and Hate?..
Sikusema unamchukia JK ila nasema mapenzi yako yanaweza tafsirika kama Chuki kutokana na mtazamo wa upande huo -shilingi wakuu zangu, ina pande mbili..
Nitarudia kwa ufasaha zaidi..
Kikwete na Kundi lake wameacha kuwafikisha mahakamani Mafisadi kwa sababu wanahofia usalama wa nchi..
Fikra au maneno haya kwa mtazamo wao yanatokana na Mapenzi ya nchi yao ndiyo yanawasukuma kuona kwamba ni bora wamezee hili kuliko kuingia ktk vita ya ndani..On the other hand, mimi binafsi, nauchukia Ufisadi na naweza sema namchukia fisadi yeyote bila kificho kutokana na mapenzi ya nchi yangu na naomba kila siku Mafisadi wafikishwe mahakamani.. Fikra au imani hii inatokana na CHUKI (ya Ufisadi) hivyo, pia inaweza tafisrika kuwa ni chuki..na badala ya watu wa upande ule wa pili kutumia chuki yangu kwa vitendo vya Ufisadi wakaitumia jina au majina ya watu kupindisha ukweli - mathlan Mkandara anamchukia Rostam..(simchukii Rostam ila nachukia vitendo vyake)
Pili ktk vitendo vya Kikwete kuwaachisha kazi baadhi ya viongozi ni kutokana na mapenzi yake kwa nchi yetu lakini kuna baadhi ya watu watatazama hiyo kama chuki yake kwa watu hao..na matokeo ya migogoro yote ndani ya CCM inatokana na maneno haya mawili.. LOVE and HATE kutafsirika jinsi watu wanavyojisikia..
Wakuu zangu hawa jamaa wanalindana na sasa hivi wameamua kutoleana Uvivu - tumesikia wakisema fulani tumemsitiri kwa madhambi ya mkewe angekuwa akiozea Jela kama sio sisi..Maneno kama haya badala ya kujenga hoja ya wahusika hao ni lazima yatushtue toka usingizini kuhusiana na vitendo hivyo.. viongozi wa CCM sio kweli hawafahamu kwamba wanavurunda isipokuwa maadili yao yanawahimiza kulindana hata kama wakivunja sheria..now, Why hope something good itatoka huko! ndilo swali langu.
Jamani kwa miaka mitatu tumekuwa tukizingumza humu kuhusu utawala wa CCM, leo inashangaza sana watu mnafikiria kwamba tatizo sio CCM isipokuwa ni Kikwete wakati chama kizima kinampongeza kama alivyopongezwa Mwinyi na Mkapa.. haya madudu na akili ya kushikiwa itaisha lini?.. kwa nini msifikirie kumtafuta rais toka vyama vingine ambavyo kwa kauli zao wamesema watahakikisha Mafisadi wanafikishwa mahakamani!..
Utawala bora hauwezi kutanguliwa na kitu chochote ikiwa bado kuna watu Untouchbles, watu wanaopinga na kusherehekea Ufisadi au unafiki wa kuzungumzia ktk vijiwe wakati wanashindwa kusimama kupinga Ufisadi na watu kama Lowassa, Rostam, Karamagi wafikishwe mahakamani..Hawa Mafisadi bado wabunge, bado ni wana kamati wa chama tena wanaheshimika na kuabudiwa,leo mnafikiria kuna mtu ndani ya chama hiki anaweza kuifanya kazi kubwa aloshindwa baba lao Kikwete..
Bisides, Tuache reality, tuzungumzie mathlan kama kuna mtu ataweza kushindana na Kikwete na pengine kushinda..basi vita ya matokeo hayo sidhani kama kuna mtu hujmu ndani anayaombea, ndio hapo Usalama wa taifa utakuwa hatarini na nakuhakikishieni kwa lugha yenu na mtazamo wenu..Kama kweli kuna mtu huyo au nafasi hiyo ikitolewa - mgombea atakuwa Puppet wa Mafisadi!... And U all don't wanna that!