The road towards 2010 Elections

The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
...maandamano bila sababu za msingi ni uthibitisho tosha wa uvivu wetu wa kufikiri. Kama tunataka demokrasia ya kweli, ugombea pekee maana yake nini?
 
Kweli Tumerogwa. Badala ya kujadili namna ya Kuendelea Kwanza Tumtafute Mchawi Wetu. Seriously Nimekubali kuwa Watanzania Tumerogwa. Seriously , Seriously , Seriously !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kweli Watanzania Tumerogwa. Badala ya kujadili namna ya Kuendelea Kwanza Tumtafute Mchawi Wetu. Seriously Nimekubali kuwa Watanzania Tumerogwa. Seriously, Seriously , Seriously !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Swali: Nani Katuroga Watanzania Jamani?????????????????
 
Kweli Tumerogwa. Badala ya kujadili namna ya Kuendelea Kwanza Tumtafute Mchawi Wetu. Seriously Nimekubali kuwa Watanzania Tumerogwa. Seriously , Seriously , Seriously !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Mr 0, hakuna aliyerogwa labda wewe mwenyewe. Watu wako kazini. Unategemea nini baada ya madudu yote haya! Lazima kwanza mtu apime upepo na mikwara kibao ili aone ni kiasi gani amekalia kuti kavu. Sina hakika, ila naamini walikuwa na mkutano na mzee kabla ya kuja kuwachefua wananchi kupitia kwa waandishi wa habari! Kazi inaendelea na katika hii miezi kama 12 iliyobaki tutaona mengi sana.
 
Kwa kifupi ni kwamba hatuna wazee!! Hao ndio washauri? Haishangazi tupo hapa tulipo.
 
Sasa Mnadhani atasema nini wakati yeye nd' anayepigiwa debe na kukingiwa kifua kama hivyo hata ningekuwa mimi nisingesema kitu! mi natamani siku nijitoe mhanga nife na FISADI mmoja wapo tena mzizi mkuu!
 
Ukifa kwa njia hiyo mimi nitaitunza familia yako maisha yote
 
tatizo kipato chao kilikuwa kinatoka hapo ccm kwa ufisadi na sasa hapo kwenye system wanajaribu kutafuta influence ili endaspo mzee mwenyewe akiwa kwenye power aweze kuwakumbuka ni umbumbavu mtumpu,
wanapigania maslahi binafsi
 
Sikusema popote kwamba nadhani, bali nimesema naamini kwamba ndani ya CCM anaweza kupatikana kiongozi bora mara 1,000 zaidi ya huyu Kikwete ambaye tangu aingie madarakani nchi imekuwa ikiyumba kuliko wakati wowote ule tangu tupate uhuru.

Mkuu BUBU, Kuyumba kwa nchi sidhani kama kuko kama unavyataka tuamini. Nahitaji kuelimishwa kilicho tofauti kati ya wakati wa Mkapa na huu wa Kikwete> Suala la mijadala na kufichua maovu naomba Tafadhali usilioredheshe kwani naamini kuwa hili lipo kwa kuwa Demokrasia na uhuru wa kutoa maoni unaofanya hayo umeachiwa makusudi na huyohuyo JK kwa lengo la kuwa wazi. Kulikuwa na wakati hapa uliopewa jina la ukweli na uwazi lakini ilikuwa ndio wakati wa kufungwa midomo wananchi.
 
Ndugu WJM, BAK kaweka wazi kwamba kuna watu walio bora kuliko JMK ambao CCM inaweza kuwasimamisha and that is very very clear statement kwa hiyo sijaona mkanganyiko hapo. May be let me slow down: anasema ukipanga mstari wa viongozi kwa ubora katika viwango vya Ki-CCM JMK hawezi kusimama natumai sasa umeipata picha na ujumbe kamili!

Bubu bado kashindwa kuwataja hao anaowaona kuwa wanafaa kutoka CCM kama alivyoombwa na Gozigumu. Hata mimi nakubaliana na William kuwa tunapozungumza CCM na mkakati wake wa kuweka mgombea tuzungumzie CCM kwa ujumla kwani wanaetuletea ni chaguo lao katika kuendeleza sera zao. Uzowefu unaonyesha kuwa mashujaa wa CCM wana mambo wanayaficha ama yao au ya viongozi wao, sasa watu kama hao tutasema kuwa wanatufaa? Lakufanya ni moja tu CCM na walete mtu yeyote wampendae lakini sisi tusimpe kura KESI IMEKWISHA>
 
Huyu ni mmoja wa kambi ya "Ni Mwenzetu huyu" hivyo kazi yake hapa ni kutaka kuonyesha kinachoandikwa na yeyote yule ambacho yeye hakiafiki kina kasoro. Tunajua fika kutokana na dalili za wazi kabisa kwamba upinzani hauna dalili ya kuchukua Urais 2010, lakini pamoja na hayo haina haja ya kumpa tena Kikwete. Katiba ya CCM inaruhusu wagombea wengine wanaotaka kufanya hivyo kuchukua form, sasa hivi vitisho dhidi yao vya nini tena? Na lini katiba ya CCM ilibadilishswa na kuruhusu vitisho kwa wale ambao wanataka kumpinga Rais!? Haya mambo ya unafiki ndiyo yanaifikisha nchi yetu pabaya. Rais kama kuna mazuri aliyoyafanya yawekwe hadharani, lakini hakuna hivyo Watanzania tunastahili kabisa kupata Rais mpya ambaye ataweka maslahi ya nchi mbele kwa manufaa ya Watanzania.

BUBU.
Ni hawahawa CCM kwa umoja wao walikaa na kutuletea JK kuwa ni chaguo lao. Ni hao hao CCM wana utamaduni wa kiongozi lazima amalize vipindi viwili (kumbuka Karume/Gharib kule Z'bar). Ni CCM hawa hawa ndio mafisadi, CCM haweahawa wana mashujaa wanaomiliki Biashara zao. CCM hao hao wanayajuwa mabaya dhidi ya Taifa wanaficha, Ni CCM hawa hawa walio wengi katika Bunge wakichukuwa maposho wasioyafanyia kazi.
Nashindwa kuona mwana CCM aliebora (labda yule Mwarabu Watanzania tusiemtaka) alie bora kuliko KIkwete. Nafikiri tuwe wazi kama ulivyoombwa huko nyuma kuwa jaribu kutaja wachache ili tuthibitishe hiyo dhana yako kuwa yuko alie mbora zaidi ya Kikwete katika kutekeleza sera za CCM.
Sio kweli kuwa mtu aieleza mtazamo wake anakusudia kuonyesha kasoro ya mwengine bali kuna wakati mtu hutaka kitu halisia badala ya nadharia na kwa hili Mkuu kunali kuwa bado unapiga chenga kuwa muhalisia na kuwataja mifano ya watu bora CCM kuliko JK.
 
"Kwa kifupi ni kwamba hatuna wazee!! Hao ndio washauri? Haishangazi tupo hapa tulipo."

*************************

Mpigafilimbi: Correct kabisa, hatuna wazee, waliishia enzi yaJKN. Nakumbuka mapema miaka ya 90 wakati Mwinyi ananadi sera ya kuchangia eklimu ya juu, ktk mkutanio mmoja wa ndani na wazee wa Mbeya, alikuwa anakatizwa kwa kupigiwa makofi na vigelegele ktk hotuba yake ya kuwataka wazazi wachangie.

Hivi sasa wazee hao wanajisikia vipi watoto wao wanatimuliwa hovyo Vyuo Vikuu kwa kukosa hela za kuchangia ada! Wazee wetu siku hizi hawana maana yoyote, hawa wa CCM waliotoa tamko juzi wanaganga njaa tu, na bila shaka utakuta wamehongwa na mafisadi ili kusema.

Kwa mtindo huu tutasikia mengi siku zijazo na wengi kujitokeza ktk kampeni ya kunadi "JK TENA": Viongiozi wa walemavu, vijana, wanawake wanawake, machinga, vijana, wanafunzi etc watapewa hela na mafisadi ili waende ukumbi wa maelezo kutoa matamko ya kiajabuajabu!

Hadi sasa sijamsikia mzee yoyote wa CCM akisimama jukwaani na bila kigugumizi kuwashambulia mafisadi. Hakuna! labda Warioba na Butiku, lakini angalia jinsi mafisadi wanavyojaribu kuwageuzia vibao!
 
Last edited:

Msekwa: Enzi za kulindana,kubebana CCM zimekwisha

Basil Msongo

HabariLeo; Sunday, November 18, 2007 @00:03

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Pius Msekwa amesema enzi za kulindana, ‘mwenzetu' na kubebana katika chama hicho zimekwisha.

...hawa wazee wanajifanya wana tafsiri mpya ya kubebana!

Jamani njaa ni kitu kibaya sana........dah

...hivi, njaa au uvivu wa kufikiri, nini kinatangulia?

Wazee hao pia walieleza kukerwa na tabia ya baadhi ya wanachama wa CCM, walioamua kujitokeza hadharani na kulumbana kwani kufanya hivyo, kunakidhoofisha chama, huku kikijenga mgawanyiko miongoni mwa wananchi na kuendeleza chuki na uhasama.

...'dongo lako' hilo mheshimiwa Mwakyembe, wazee weshakugeuka hawa!

Kwa wale wanaomshutumu bure Bw. Shibuda na kuwatishia wengine, naendelea kumnukuu Bw. Msekwa;

"Suala la kukosoa, kujikosoa na kukosoana katika chama ni njia ya kukijenga na kukiimarisha chama chetu. Lakini ni kweli pia kuwa hatujajenga tabia hii ipasavyo. Mara nyingi tumependelea kuteteana na kufichiana makosa, awamu hii itaondokana nayo," alisema Msekwa.

...Sambamba na kukiri kulindana, Msekwa pia alikiri kuwa rushwa imetawala katika uchaguzi ndani ya chama hicho na kubainisha kwamba CCM haikumbatii rushwa ila utekelezaji na usimamizi wa sera ya chama hicho kupambana na rushwa umekwama.
 
Shadow naona sasa nchi inaelekea kwenye udikteta, maana hata failure kubwa ya uongozi wa Kikwete ambayo ni kupambana na ufisadi wale wanaotaka kuitumia kupambana naye wameshatishwa kwamba wasitumie ufisadi dhidi ya Kikwete!!! Wao wako tayari kutumia 'utamaduni wao' wa kumuachia Rais akae madarakni kwa awamu mbili, lakini wale wanaotaka kumpinga na kuleta vigezo vya kuonyesha kwamba Rais hastahili kuendelea kuwa madarakani kwa sababu kadhaa wa kadha wanatishwa!!!!

Bubu bado hatujafika huko unakosema kwani hili si geni hapa kwetu. Nilitowa mfano wa Karume/Bilali na huu ulitendwa na wana CCM wote(mafisadi na mashujaa) na sikumbuki kama yupo hapa aliesimama na kuuzungumza huo upotevu wa Demokrasia. Ni CCM hii hii kwa kupitia Wazee hao hao waliosimama na kusema hawataki kutawaliwa na 'Mwarabu" na vyombo vya habari vikashajiisha ubaguzi huo. Wakati huo Demokrasia ilikuwa na maana.?
Nafikiri Wazee walichosema si cha uongo kuwa ni desturi yao CCM kuwaweka viongozi wao kwa vipindi viwili, na wazee hao hawakusema kuwa watamfukuza mtu kwenye chama, walichosema ni jambo la kawaida kuwa watamtetea wanaemuona anafaa. Tusilazimishe yule tunaemuona hafai kwa nadharia yetu kuwa hafai bali kama tuna hoja za kuuza kwa wananchi wenzetu na tufanye hivyo ili tuwafanye wakubali msimamo wetu.
Kulitangazia Taifa kuwa liko katika udikteta si sahihi kwani Si hivi tunajadili kwa uwazi bila oga na kumnanga kiongozi wa juu kabisa sasa demokrasia gani tunaihitaji. Tumuangushe JK kwa kura na kama kura ni demokrasia hili la kungangania nje ya kura lina maana gani?
 
Mr 0, hakuna aliyerogwa labda wewe mwenyewe. Watu wako kazini. Unategemea nini baada ya madudu yote haya! Lazima kwanza mtu apime upepo na mikwara kibao ili aone ni kiasi gani amekalia kuti kavu. Sina hakika, ila naamini walikuwa na mkutano na mzee kabla ya kuja kuwachefua wananchi kupitia kwa waandishi wa habari! Kazi inaendelea na katika hii miezi kama 12 iliyobaki tutaona mengi sana.

DC,

Wewe amabaye hujuwi kuwa tumerogwa ndiye ndumba lilikukorea kisawasawa. But trust me WTZ Tumerogwa!!!!!!!!!

I wish ningekuwa Madagascar, kule mambo poa, Rais akileta za kuleata hata DJ anapewa madaraka. Lakini Bongo sijui huyu mkoloni CCM ataondoka lini????
 
Bubu bado hatujafika huko unakosema kwani hili si geni hapa kwetu. Nilitowa mfano wa Karume/Bilali na huu ulitendwa na wana CCM wote(mafisadi na mashujaa) na sikumbuki kama yupo hapa aliesimama na kuuzungumza huo upotevu wa Demokrasia. Ni CCM hii hii kwa kupitia Wazee hao hao waliosimama na kusema hawataki kutawaliwa na 'Mwarabu" na vyombo vya habari vikashajiisha ubaguzi huo. Wakati huo Demokrasia ilikuwa na maana.?
Nafikiri Wazee walichosema si cha uongo kuwa ni desturi yao CCM kuwaweka viongozi wao kwa vipindi viwili, na wazee hao hawakusema kuwa watamfukuza mtu kwenye chama, walichosema ni jambo la kawaida kuwa watamtetea wanaemuona anafaa. Tusilazimishe yule tunaemuona hafai kwa nadharia yetu kuwa hafai bali kama tuna hoja za kuuza kwa wananchi wenzetu na tufanye hivyo ili tuwafanye wakubali msimamo wetu.
Kulitangazia Taifa kuwa liko katika udikteta si sahihi kwani Si hivi tunajadili kwa uwazi bila oga na kumnanga kiongozi wa juu kabisa sasa demokrasia gani tunaihitaji. Tumuangushe JK kwa kura na kama kura ni demokrasia hili la kungangania nje ya kura lina maana gani?

Mkuu, Nadhani Suala sio kwamba walisema uongo ama la, Suala ni How They Said It: "Mwanachama yeyote anaruhusiwa kuchukua fomu ili kugombea lakini akijitokeza sisi tutatumia uzoefu wetu kuwaeleza wanachama wetu kwa nini Kikwete ndio anafaa kupewa Kura!" kwa mtazamo wa kawaida, hii ni kauli ambayo haina matatizo yoyote lakini ukiisoma katikati ya mistari unaona kabisa kuna onyo linatolewa kwa atakayejitokeza kufanya hivyo! Je Huo uzoefu Unaosemwa Utaishia katika Kuwaeleza tu Wanachama wao ama kuna la ziada ambalo aliyejitokeza atakumbana nalo??
Anyway, hiyo ni kwa jinsi nilivyoelewa mimi.
Mwisho wa Yote ni kama Ulivyosema, CCM na wamchague mtu yoyote wampendaye lakini kama wao wenyewe wanadai wako Milioni 4 tu, sisi Mamilioni wengine tuliobaki tunaweza kabisa tukawapiga chini wao na mtu wao waliyemteua! Tatizo ni How Do We Do That Katika Muda Uliobaki???
 
Mbu,
...maandamano bila sababu za msingi ni uthibitisho tosha wa uvivu wetu wa kufikiri. Kama tunataka demokrasia ya kweli, ugombea pekee maana yake nini?
__________________

Mkuu uvivu wa kufikiri unaanza na sisi hapa JF.. Mimi nashindwa kabisa kuelewa kinachogomba hapa kwani hawa wazee ni wanachama walezi wa chama CCM ambao wana kila sababu kulingana na mtazamo wao kuwa Kikwete ndiye mgombea pekee wanayemtaka kwa tiketi ya CCM..Wana kila sababu ya kufanya kampeni hizo kwa sababu wanajua kinachoendelea ndani ya chama.. Wewe na mimi hatufahamu kitu. Hayo madogo aliyoyafanya Kikwete wameridhika nayo na pengine wanaelewa zaidi kinafuatia baada ya misafara na umaarufu...

Sisi hapa tumeanza kupinga hoja hiyo na kuita ni Udikteta kama vile ndio kwanza tunakuwa na mgombea urais kwa vipindi viwili..Halafu kinachonishinda kabisa kuelewa ni mtu kama BAK ambaye siku zote analia na CCM waondolewe madarakani kama vile ni mpinzani lakini inapofikia swala la Kikwete kusimama tena inamwasha sana, Kisha basi ameshindwa kutupa mgombea ambaye anaweza kufikisha salamu za hayo maombi yake.

Kikwete ameshindwa kufuta Ufisadi na ikiwa kweli Ufisadi ndiye adui yetu mkubwa kwa nini bado mnafikiria CCM?.. kwa nini bado watu wanafikiri kiongozi bora atatoka CCM kama huu sii uvivu wa kufikiri kitu gani?..
Binafsi sioni big deal kabisa chaguo la wazee hao na kusema kweli sioni kiongozi bora ndani ya CCM ambaye ataweza kutimiza yale nayoyataka..Wengi ambao ningefikiria pengine wanaweza kuleta mabadiliko wameondoka ktk kurupushani za siasa..Waliobakia wote wanaogopa Mtandao kama anavyoogopa Kikwete mwenyewe!

Tuna watu kama Dr. Slaa akienda sambamba na Mafisadi, akichukua kila kitu hatua kwa hatua lakini ameshindwa kwenda mbele kwa sababu hana ubavu..Now, just imagine mtu huyu anakuwa Rais au Waziri Mkuu wa Tanzania!..Matatizo yetu yote yamekwisha!
Kwa nini bado mnafikiria CCM!
 
Mbu,

Mkuu uvivu wa kufikiri unaanza na sisi hapa JF.. Mimi nashindwa kabisa kuelewa kinachogomba hapa kwani hawa wazee ni wanachama walezi wa chama CCM ambao wana kila sababu kulingana na mtazamo wao kuwa Kikwete ndiye mgombea pekee wanayemtaka kwa tiketi ya CCM..Wana kila sababu ya kufanya kampeni hizo kwa sababu wanajua kinachoendelea ndani ya chama.. Wewe na mimi hatufahamu kitu. Hayo madogo aliyoyafanya Kikwete wameridhika nayo na pengine wanaelewa zaidi kinafuatia baada ya misafara na umaarufu...

Sisi hapa tumeanza kupinga hoja hiyo na kuita ni Udikteta kama vile ndio kwanza tunakuwa na mgombea urais kwa vipindi viwili..Halafu kinachonishinda kabisa kuelewa ni mtu kama Bubu ambaye siku zote analia na CCM waondolewe madarakani kama vile ni mpinzani lakini inapofikia swala la Kikwete kusimama tena inamwasha sana lakini pia ameshindwa kutupa mgombea ambaye anaweza kufikisha salamu za hayo maombi yake,,
Kikwete ameshindwa kufuta Ufisadi na ikiwa kweli Ufisadi ndiye adui yetu mkubwa kwa nini bado mnafikiria CCM?.. kwa nini bado watu wanafikiri kiongozi bora atatoka CCM kama huu sii uvivu wa kufikiri kitu gani?..
Binafsi sioni big deal kabisa chaguo la wazee hao na kusema kweli sioni kiongozi bora ndani ya CCM ambaye ataweza kutimiza yale nayoyataka..Wengi ambao ningefikiria pengine wanaweza kuleta mabadiliko wameondoka ktk kurupushani za siasa..Waliobakia wote wanaogopa Mtandao kama anavyoogopa Kikwete mwenyewe!

Tuna watu kama Dr. Slaa akienda sambamba na Mafisadi, akichukua kila kitu hatua kwa hatua lakini ameshindwa kwenda mbele kwa sababu hana ubavu..Now, just imagine mtu huyu anakuwa Rais au Waziri Mkuu wa Tanzania!..
Matatizo yetu yote yamekwisha!

Mkandara hakuna uvivu wa kufikiri, huu unafiki tulionao Watanzania ndiyo unaipeleka nchi yetu pabaya. Kumpigia Rais debe ili aendelee kuwepo madarakani kutokana na mazuri aliyoyafanya si kitu cha ajabu, lakini Kikwete hakuna MAZURI yoyote aliyoyafanya hata ahadi zake zote hakuna hata moja aliyoitimiza na hii ni ukweli mtupu na tangu lini kusema ukweli kuhusu kiongozi dhaifu imekuwa ni uvivu wa kufikiri!!!!?
 
Bubu Ataka Kusema,
Mkuu swali langu rahisi sana.. kama yeye hafai nani anafaa?.. ambaye wewe una hakika atayaleta yale unayoyataka.. mwenye kutimiza ahadi zake maanake nijuavyo Mimi sii Mwinyi wala Mkapa walitimiza lolote..
Ukishindwa hilo bila shaka ni kutokana na uvivu wa kufikiri..Unapinga kitu ukiwa na solution mkononi, kama huna wewe pia mvivu vile vile, ndio nachosema mimi..
 
Wazee hawana kosa wapo sahihi kabisa maana wanajua mtu yeyote atakaepita ataukwaa uraisi kuongoza Tanzania ,maana Katiba ya nchi ni ya Chama kimoja,Mahakama ni za Chama kimoja,Tume ya uchaguzi ni ya Chama kimoja ,kila kitu kilichopo kilitokana chini ya mfumo wa Chama kimoja hakuna hata kitu kilichobadilishwa ,sasa hizo kelele za wazee ni kuwambia watoto wale kwa heshima haina haja ya kunyang'anyana tonge mdomoni ,wamuache mwenzao ale miaka kumi yake halafu hapo ajitokeze yeyote yule na kwa kutumia taratibu zao atakaefanikiwa ni zamu yake kutesa.
 
Back
Top Bottom