The road towards 2010 Elections

The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
Mimi naamini ndani ya CCM tunaweza kabisa kupata kiongozi jasiri atakayeweka mbele maslahi ya Tanzania na Watanzania badala ya mafisadi na chama cha mafisadi. Haiwezekani nchi ya watu 40 millioni kushindwa kumpata kiongozi bora kuliko Kikwete. Kikwete siyo kiongozi hata kidogo alitaka kuwa Rais bila kujua uzito wa kuwa Rais sasa kila kitu kinamshinda ahadi zote alizotoa wakati wa kampeni hadi sasa hakuna hata moja aliyoitekeleza, halafu mnataka tena aendelee kuwa madarakani hadi 2015!!!!!?. WE CAN DO BETTER THAN THAT!!!! 🙁

Mkuu BUBU hili la kudhani haliwezi kuwa msaada kwa Watanzania. Kinachotakiwa kuwa na watu tunaowajua kuwa hawa watafaa lakini kwa safu ya CCM tunashindwa kumuonesha kidole mtu fulani. Mara zote wanapochaguliwa hawa wakubwa huwa tunawapanga kuwa labda huyu au yule na hilo ndio lilitakiwa kujulikana. Tukiwataja tutakuwa na wasaa wa kuwjadili na kama kuna kasoro zitaanikwa mapema.
 
Gozogumu
Tatizo la CCM wanapenda kumchagua mtu watakae weza kula pamoja au MKUU unasemaje?
 
You should have known by this time that; "politicians are like diapers, they are alike and they have same uses. Change 'em and keep changing them but the end is always the same, none ends clean"

....what is the way forward then?
In my humble opinion, anything associated with the so called CCM should be uprooted and burned and ashes thrown in deep sea (no trace to be found)!!
Let's start a fresh, plant new seeds, cultivate new hearts, conceive new ideas. Theirs have failed us so far! It's pity they don't even realize that!
Meanwhile they should be busy watching, as our country needs more than the power of the ballot box, because they know how to manipulate minds of ordinary people.
Are we the last generation in Tanzania? who told them? If not why are they trying to ruin everything before they die?
with this mentality we are in deep deep trouble.
The second phase of Mkapa was terrible compared to the first (politicians tend to be humble when they know they would need a vote from the wananchi, you will hear them even give a person far younger than them the famous "Shikamoo"), once they are done with your vote, forget it!!
It is the same with the JK, he has failed when he tried very hard to please voters, do you really expect this guy to perform in the next 5yrs?
The guy has reached his peak, out of ideas and very old/lazy to learn new tricks and so are people around him, the so called washauri, kadas, and whatever you call them.
Tanzania belongs to us all, we are not aliens from another planet, so at the end of the day, it's a shame to all of us to have allowed things to reach this far!!!!
I guess it's not too late, tufanye kazi kwa bidii, na tuondoe huu ubwanyenye ndani ya nchi, kwa kuwa mwisho wa siku Kiongozi mzuri pia aongoze watu smart au, sio kutwa kwenye kijiwe na kusema tuna Raisi genious maendeleo yatakuja tu!!
 
TZ needs a new direction 2010, they need to mbeki-nize him and choose a new leader
 
Ninatuma ombi maalum kwa Raisi Jakaya Mrisho Kikwete apuuze hizi sauti za giza na za kinafiki na asikubali kusimama tena kugombea. Yaliyotendeka na yanayoendelea kutendeka chini ya utawala wake, ameyaona na ameyashuhudia. Hivi leo akitangaza kuwa hatasimama tena 2010, atakuwa na hakika ya ku "salvage" kaheshima kadogo mbele ya UMMA wa Watanzania na atakumbukwa kwa Uungwana wake huo.
 
Ninatuma ombi maalum kwa Raisi Jakaya Mrisho Kikwete apuuze hizi sauti za giza na za kinafiki na asikubali kusimama tena kugombea. Yaliyotendeka na yanayoendelea kutendeka chini ya utawala wake, ameyaona na ameyashuhudia. Hivi leo akitangaza kuwa hatasimama tena 2010, atakuwa na hakika ya ku "salvage" kaheshima kadogo mbele ya UMMA wa Watanzania na atakumbukwa kwa Uungwana wake huo.

Mkuu ni sawa na kulazimisha ng'ombe kunywa maji,labda Lowassa wa kwetu Monduli ambaye kuna kila dalili ya kumrithisha mtoto wake ubunge Mmmmh kukaa Back benchers kuna hitaji moyo haswa pale unapokuwa kinara wa shughuli za bunge kisha ghafla unakuwa Back benchers Loh!

Ahadi ya Fred Lowassa kupitia kampuni yake ya Alphatel ni kupeleka watu South Africa 2010 haya nipe nikupe.
 
- Wakuu ufike wakati tujadili alternative, otherwise politically tunakuwa tunakubali kwamba ni CCM, au hakuna,

- Tutoe mapendekezo ya kuelekeza wananchi kwenye mabadiliko, na pia tuseme mchango wetu utakua ni nini hasa katika njia hiyo ya kuwabadilisha mawazo wananchi wapiga kura, au tujiunge na vyama vya siasa now.

Respect.

FMES!
 
Kwa mtaji huu wa kupindisha katiba na kutisha watu ambao katiba ya nchi na hata ya CCM zinawaruhusu kugombea Urais, Tanzania haitapiga hatua yoyote kimaendeleo hata kwa miaka mingine 50. Watakuwa wanachaguliwa Marais dhaifu na hivyo mafisadi kuendelea kupeta bila woga wowote maana wanajua kiongozi wa nchi ni dhaifu na hana ujasiri wa kuwafanya chochote. Maskini Tanzania!!! 🙁 🙁 🙁

CCM: Atakayempinga Kikwete 2010 kukiona

• Waonywa wanaotumia vita ya ufisadi kama mtaji

na Sauli Giliard

Tanzania Daima~Sauti ya Watu

WAKATI kukiwa na taarifa zisizo rasmi za kuwapo baadhi ya watu kujipanga kupambana na Rais Jakaya Kikwete ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika uchaguzi mkuu mwakani, wenyeviti wastaafu wa mikoa wa chama hicho wamejitokeza na kuapa kupambana na wanachama wenye nia hiyo kwa kutumia uzoefu wao ndani ya chama.

Kauli hiyo ya wazee imekuja kuku baadhi ya wanachama wa chama hicho tawala, wakiwa wameonyesha nia ya kutoa upinzani kwa Rais Kikwete akiwamo Mbunge wa Maswa, John Shibuda ambaye amekwishatangaza wazi nia yake ya kugombea nafasi hiyo ya juu zaidi katika uongozi wa nchi.

Akisoma msimamo wa wazee hao jana katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo), jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoani Dodoma na Mwenyekiti mstaafu wa Wenyeviti wa chama hicho mikoa yote nchini, Pancras Ndejembi, alisema hawamzuii mtu kugombea kiti hicho, lakini hawaoni sababu ya kuwapo upinzani wakati Rais Kikwete anatarajia kumalizia kipindi chake cha pili.

Ndejembi ambaye aliambatana na Mwenyekiti mstaafu CCM Mkoa wa Iringa, Tasil Mgoda, Mwenyekiti mstaafu Mkoa wa Dar es Salaam, Hemed Mkali na Mwenyekiti mstaafu Mkoa wa Pwani, Jumanne Mangara, alisema kamwe hawatakubali kuwapo wagombea wengine watakaojitokeza kumpinga Rais Kikwete.

"Sisi hatusemi wengine wasijitokeze kugombea, la hasha! Tunasema tunamuunga mkono Kikwete. Akipata mpinzani kwenye kuomba ridhaa ya wana-CCM ya kugombea tena, basi sisi tutatumia fursa na uzoefu wetu katika uongozi kama wazee, kuielezea jamii ni kwa nini Kikwete bado anafaa," alisema Ndejembi na kuongeza: '‘Anayetaka kuchukua fomu achukue kama alivyotangaza Shibuda, hatumzuii ni ruksa. Akichukua, tutatumia uzoefu wetu."

Mwenyekiti huyo mstaafu wa wenyeviti wa CCM wa mikoa yote nchini, aliwataka wanachama hao kufuata utamaduni ambao chama hicho kimejiwekea cha kuruhusu kiongozi katika ngazi ya urais kutumikia miaka 10 na kuendelea kusisitiza kuwa kwa Rais Kikwete, haoni kitakachowafanya wampinge kutokana na uwajibikaji wake kwa taifa na mapambano dhidi ya rushwa.

'‘Utamaduni wetu ndani ya chama unafahamika, Mwinyi tulimpa miaka kumi, Mkapa naye vile vile, lipi baya alilofanya Kikwete hata tumnyime asiendelee kwa kipindi kingine?" alihoji.

Wastaafu hao wamesema CCM imekuwa na bahati ya kuongozwa na Rais Kikwete, kwani amekuwa mvumilivu wa kukosolewa, msikivu na ni mtu anayeipenda nchi yake kwa moyo wote na si kiongozi wa visasi.

'‘Sisi tunaamini kwamba usalama na amani ya nchi yetu upo salama leo na kesho chini ya uongozi wake. Kwa maana hiyo, nasi tunaungana na wale wengine kumuunga mkono kwa kipindi cha pili cha urais," alisema.


Wazee hao pia walieleza kukerwa na tabia ya baadhi ya wanachama wa CCM, walioamua kujitokeza hadharani na kulumbana kwani kufanya hivyo, kunakidhoofisha chama, huku kikijenga mgawanyiko miongoni mwa wananchi na kuendeleza chuki na uhasama.

Waliwaonya viongozi hao wa CCM kuacha tabia ya kushutumiana na kunyoosheana vidole, kuwekeana visasi kwani wanakidhohofisha chama kutokana na hulka zao za malumbano na kukipunguzia heshima.

'‘Lakini pia kufanya hivyo hadharani, kwa nia ya kutaka kuungwa mkono katika shutuma na visasi hivyo, kunajenga chuki, uhasama na mgawanyiko katika jamii. viongozi hawatakiwi kuwajaza watu chuki uhasama ndani ya mioyo yao," alisema Ndejembi.

Katika kauli yao ya pamoja, wazee hao, pia walisema wanakerwa na tabia iliyoibuka kuyatumia vibaya mapambano dhidi ya ufisadi kama mtaji wa kujinufaisha kisiasa na kwamba tabia hiyo inapotosha maana halisi ya mapambano hayo.

'‘Lakini sasa tumeanza kushuhudia baadhi ya viongozi wa CCM kurushiana maneno wenyewe kwa wenyewe kwa kutaka kuonyeshana nani zaidi na nani vinara kuliko wengine katika mapambano dhidi ya rushwa. Hii si sawa.

'‘Mapambano dhidi ya rushwa nchini yanaongozwa na chama chetu katika kutekeleza ilani yetu ya uchaguzi, si shughuli ya kikundi cha watu wachache," alisema Ndejembi.


Waliongeza kuwa mapambano ya ufisadi, yasiwe kichaka cha kuficha ubovu wa viongozi na kuonya kuwa, wakati huu taifa linapoelekea katika uchaguzi mkuu, neno ‘mafisadi' lisitumike kuwatishia wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali katika chama hicho.

Pamoja na tofauti kadhaa zilizojitokeza miongoni mwa wanachama ambao wako katika Halmshauri Kuu ya Chama (NEC), wazee hao walisema ni jambo la kawaida ndani ya chama chochote cha siasa na kuonya kuwa wanaosubiria CCM imeguke, wanapoteza muda.

'‘Ni makosa kudhani kuwa tutakuwa na chama ambacho viongozi wake wanafikiri sawa na wana maoni sawa. Hao watakuwa ama hawafikirii au ni wanafiki wanaojipendekeza badala ya kuchangia kwa uwazi kurutubisha sera, mwelekeo na utendaji kwenye chama," alisema mwenyekiti huyo mstaafu wa Dodoma.

Kauli ya wenyeviti hao wastaafu inakuja huku taifa likijiandaa kuingia katika uchaguzi mkuu hapo mwakani.

Tayari Shibuda alishatangaza na hata karibuni alirejea wito wake kuwa amejipanga kuchukua fomu ya kuomba kuwania urais mwaka kesho.

Shibuda ambaye alikuwa miongoni mwa wagombea 11 waliojitokeza ndani ya CCM kuchuana na Rais Kikwete katika uchaguzi mkuu uliopita, alisema si lazima wala hakuna sheria inayotamka kuwa lazima rais aliyeko madarakani, atawale kwa vipindi viwili.
 
HTML:
“Sisi hatusemi wengine wasijitokeze kugombea, la hasha! Tunasema tunamuunga mkono Kikwete. Akipata mpinzani kwenye kuomba ridhaa ya wana-CCM ya kugombea tena, basi sisi tutatumia fursa na uzoefu wetu katika uongozi kama wazee, kuielezea jamii ni kwa nini Kikwete bado anafaa,” alisema Ndejembi na kuongeza: ‘‘Anayetaka kuchukua fomu achukue kama alivyotangaza Shibuda, hatumzuii ni ruksa. Akichukua, tutatumia uzoefu wetu.”

Hey enyi waheshimiwa wa CCM wake up! take note that If the only tool you have is a hammer(JMK), you tend to see every problem as a nail.We have other people who need to exercise their democratic rights within the party and outside the party. Au ndo yale yale ya baniani mbaya kiatu chake dawa?

 
Mkuu BUBU hili la kudhani haliwezi kuwa msaada kwa Watanzania. Kinachotakiwa kuwa na watu tunaowajua kuwa hawa watafaa lakini kwa safu ya CCM tunashindwa kumuonesha kidole mtu fulani. Mara zote wanapochaguliwa hawa wakubwa huwa tunawapanga kuwa labda huyu au yule na hilo ndio lilitakiwa kujulikana. Tukiwataja tutakuwa na wasaa wa kuwjadili na kama kuna kasoro zitaanikwa mapema.

Sikusema popote kwamba nadhani, bali nimesema naamini kwamba ndani ya CCM anaweza kupatikana kiongozi bora mara 1,000 zaidi ya huyu Kikwete ambaye tangu aingie madarakani nchi imekuwa ikiyumba kuliko wakati wowote ule tangu tupate uhuru.
 
Gozogumu
Tatizo la CCM wanapenda kumchagua mtu watakae weza kula pamoja au MKUU unasemaje?

Wanataka mtu ambaye hana ujasiri, muoga na ameweka mbele maslahi ya CCM na mafisadi badala ya yale ya Tanzania na Watanzania. Si unaona mafisadi sasa hivi wanapata nguvu maana hata hao waliofunguliwa kesi wanajua fika uchaguzi wa 2010 ukiisha tu baso wote wako huru kabisa na hivyo kuendelea kutafuna mapesa yao ya kifisadi.
 
Sikusema popote kwamba nadhani, bali nimesema naamini kwamba ndani ya CCM anaweza kupatikana kiongozi bora mara 1,000 zaidi ya huyu Kikwete .

- Sometimes hapa Forums kunachanganya kweli, maana kuna wakati tatizo linakua CCM as a whole, halafu wakati mwingine kumbe CCM ile ile tena inaweza kutoa kiongozi bora kuliko rais wa sasa, kwa kweli inachanganya.


William.
 
“Sisi hatusemi wengine wasijitokeze kugombea, la hasha! Tunasema tunamuunga mkono Kikwete. Akipata mpinzani kwenye kuomba ridhaa ya wana-CCM ya kugombea tena, basi sisi tutatumia fursa na uzoefu wetu katika uongozi kama wazee, kuielezea jamii ni kwa nini Kikwete bado anafaa,” alisema Ndejembi na kuongeza: ‘‘Anayetaka kuchukua fomu achukue kama alivyotangaza Shibuda, hatumzuii ni ruksa. Akichukua, tutatumia uzoefu wetu.”

- Wangesema haya tu halafu wakanyamaza.

William.
 
- Sometimes hapa Forums kunachanganya kweli, maana kuna wakati tatizo linakua CCM as a whole, halafu wakati mwingine kumbe CCM ile ile tena inaweza kutoa kiongozi bora kuliko rais wa sasa, kwa kweli inachanganya.


William.

Ndugu WJM, BAK kaweka wazi kwamba kuna watu walio bora kuliko JMK ambao CCM inaweza kuwasimamisha and that is very very clear statement kwa hiyo sijaona mkanganyiko hapo. May be let me slow down: anasema ukipanga mstari wa viongozi kwa ubora katika viwango vya Ki-CCM JMK hawezi kusimama natumai sasa umeipata picha na ujumbe kamili!
 
- Wangesema haya tu halafu wakanyamaza.

William.

Wanyamaze na wao wana wasi wasi kwamba mgombea wao anaweza kubwagwa!!! Ni lazima waweke vitisho pia!!! sasa sijui watamfanya nini huyo atakayempinga Kikwete sijui atafukuzwa chama au kubambikiwa zengwe la hali ya juu yeye na familia yake yote!! Tanzania kweli inaelekea pabaya
 
Naomba kuuliza BAK, Je, hivyo vitisho ilivyotolewa na hao wastaafu wa CCM ni vya kuganga njaa au? Spati picha katika ulimwengu wa kidemokrasia watu kusimama na kutoa hoja zisizo na makanyagio.
 
- Sometimes hapa Forums kunachanganya kweli, maana kuna wakati tatizo linakua CCM as a whole, halafu wakati mwingine kumbe CCM ile ile tena inaweza kutoa kiongozi bora kuliko rais wa sasa, kwa kweli inachanganya.


William.

- Mkuu ukisoma tena post yangu, utaona haina uhusiano wowote na ya kwako, hebu soma vizuri post yangu hapo juu.

William.
 
Ndugu WJM, BAK kaweka wazi kwamba kuna watu walio bora kuliko JMK ambao CCM inaweza kuwasimamisha and that is very very clear statement kwa hiyo sijaona mkanganyiko hapo. May be let me slow down: anasema ukipanga mstari wa viongozi kwa ubora katika viwango vya Ki-CCM JMK hawezi kusimama natumai sasa umeipata picha na ujumbe kamili!

Huyu ni mmoja wa kambi ya "Ni Mwenzetu huyu" hivyo kazi yake hapa ni kutaka kuonyesha kinachoandikwa na yeyote yule ambacho yeye hakiafiki kina kasoro. Tunajua fika kutokana na dalili za wazi kabisa kwamba upinzani hauna dalili ya kuchukua Urais 2010, lakini pamoja na hayo haina haja ya kumpa tena Kikwete. Katiba ya CCM inaruhusu wagombea wengine wanaotaka kufanya hivyo kuchukua form, sasa hivi vitisho dhidi yao vya nini tena? Na lini katiba ya CCM ilibadilishswa na kuruhusu vitisho kwa wale ambao wanataka kumpinga Rais!? Haya mambo ya unafiki ndiyo yanaifikisha nchi yetu pabaya. Rais kama kuna mazuri aliyoyafanya yawekwe hadharani, lakini hakuna hivyo Watanzania tunastahili kabisa kupata Rais mpya ambaye ataweka maslahi ya nchi mbele kwa manufaa ya Watanzania.
 
Back
Top Bottom