Bubu ataka Kusema,
Mkuu, kwanza ningeomba mada hii iunganishwe na zile nyingine tunajaza ukumbi tu...
hata hivyo, haya madudu ndio nayazungumza - hakuna mtu CCM, sasa kama wewe unataka kupinga hoja kwa nini unajigubika na blanketi usionekane!.. Ndo unafiki huo, wajitokeze hadharani waseme ukweli wananchi wawasikie na wafahamu kwamba wapo watu wanaweza kusimama na Rostam/Lowassa na Mkapa ktk ufisadi..
Kumbuka mkuu wangu labda unasahau nguvu ya Mtandao, kumbuka Mzee Es alituambia nini wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2005 ndani ya chama CCM.. Mkapa, Kawawa na Mwinyi walifungwa midomo...Malecela alitupwa nje kama mbwa na hakuna mtu aliyesimama kuettea, leo unambie ati kuna watu CCM wanataka mafisadi washughulikiwe..
Ikiwa bungeni tu wameshindwa kunyoosha vidole vyao kupendekeza mafisadi wakidai Usalama wa nchi utapotea, leo unambie ati kuna watu wanataka JK asisimame.. Hawa wote ni Wanafiki wametumwa na Rostam/Lowassa, sio habari ya awamu mbili kwa sababu KJK kashindwa kazi.. nakwambia hakuna kati yao, hakuna hata mmoja angeweza kuwa ondoa madaraka hata watu wa usalama kina Apson au Mahita - Hakuna... that is the fact..