Sasa chukulieni gari hili la CCM limekwama, nanyi mnataka kubadilisha dereva kwa sababu gari limekwama... hii kweli inaingia akilini jamani..Shukeni, tatizo sio dereva kuna gari jingine pembeni linasubiri abiria tena bureee hakuna gharama zaidi...Sambamba na kukiri kulindana, Msekwa pia alikiri kuwa rushwa imetawala katika uchaguzi ndani ya chama hicho na kubainisha kwamba CCM haikumbatii rushwa ila utekelezaji na usimamizi wa sera ya chama hicho kupambana na rushwa umekwama.
Jamani mweee, muambiwe vipi ikiwa makamu mwenyekiti wa chama CCM mwenyewe amekiri kwamba UTEKELEZAJI na USIMAMIZI wa sera za chama kupambana na Rushwa Umekwama!..
Utekelezaji na Usimamizi wa sera ndio sifa kubwa ya UTAWALA wowote ule, sasa kama hawa wamekwama bado mna tumaini lipi..