Ningekuwa ndo mimi JMK ningeachia madaraka ya nchi 2010.
Sababu kuu ni hizi;
Mambo mengi ya ufisadi yametokea katika kipindi kifupi tu cha utawala wake, Richmond, Buzwagi, Tume ya mawasiliano nk.
Kushindwa kuushughulikia ufisadi wa EPA
Kushindwa kuushughulikia ufisadi wa Richmond na Buzwagi
Kusainiwa mikataba tata ya Richmond na Buzwagi
Hali ya maisha ya wananchi imeendelea kuwa duni na mbovu kuliko wakati wote.
Ikulu kupoteza kauli na kila mtu kuwa na kauli zake ambazo hufuatwa na watendaji.
Kuwa na maswahiba wenye nguvu zaidi kiasi kwamba kauli zao ndio kauli za Ikulu
Kuporomoka kwa uchumi wa nchi
Dalili za kukosa uvumilivu kati ya makundi mbalimbali katika Jamii
Mpasuko mkubwa ndani ya chama kufuatia mtandao ulioanzishwa na maswahiba wake walomweka Ikulu
Hatari ya kuvunjika kwa Muungano uliodumu kwa zaidi ya miaka 44 sasa kufuatia rais kokosa ushawishi na ahadi ya kuupatia ufumbuzi wa mgogoro wa ZNZ ambayo haijatimizwa.
Yote kabisa ni hili la nchi kukosa Dira, Kiuchumi na kisiasa. Bora liende.
Ningekuwa JMK, mzalendo, ninayeipenda nchi yangu, nikiwa na akili timamu, bila kushawishiwa na mtu yeyote, ningekiomba chama changu cha SISI EM kisiniteue kwenye nafasi nyeti kama hiyo kwa maslahi ya kizazi kijacho na pia kulinda heshima yangu na kuwatosa Mafisadi ambao wengi ni maswahiba wangu
Je ingekuwa wewe ndo JMK ungechukua uamuzi gani 2010?