The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
Ndugu zangu wana JF there's something i wanna share with you...

Tuchukulie mfano wa Raila Odinga huko Kenya!
Jaramogi mwenyewe alikuwa akipambana na Moi kishujaa!

Wakenya hawajaweza kuyafikia haya mabadiliko kama sio baadhi a watu kujitoa muhanga! Kina Robert Ouko ni mfano hai!

Jaramogi Oginga Odinga alikuwa akiwapelekea wananchi maendeleo!

Leo unasikia amejitolea kuanzisha miradi ya kuwaajiri wananchi na kuwekeza kwenye kuwapa huduma mbali mbali!

Moi naye licha ya ufisadi alikuwa at least akijibu mapigo na kufanya tumambo flani flani kwa wananchi!

Wakati huo kulikuwa na rumrours..Sijui kama ni true or not lakini Jaramogi alitaka kufungua bomba za maziwa wananchi wawe wanakunywa bure!

Kama sikosei alikuwa akijibu mapigo ya moi kuanza kuwapa watoto maziwa mashuleni!

Tunataka viongozi wa upinzani muanze kuwekeza kwa wananchi na si hotuba and then mitini..And then press meeting!

Na wananchi siku hizi wanaona kama magazeti ni udaku tu!

Mifwedha ya misaada ya kimaendeleo inatolewa kwa CCM ama kwa taifa?
Mmechukua hatua gani kuona kuwa na nyie mna haki kama taasisi ya kupokea fedha hizo na kujijengea imani zaidi kwa wananchi pale mnapo kwenda kuanzisha shughuli za kimaendeleo!


Everyday nasikia mabilioni ya JK, mabilioni ya JK!
Hayo mabilioni yametoka wapi na tunaambiwa kila siku sisi ni masikini?

JK kafungua hiki, JK kazindua kile..Na nyie mnafungua nini?
At least mnawakomalia kwenye ufisadi na kwa hili mtapata kura yangu!

Mmeshawaelimisha wananchi kuwa sisi ni matajiri?

Kwani hamjui kuwa njaa ni tatizo la kisaikolojia kabla halijawa la kimwili?
Picha inayomjia mtanzania ni ile ya yule aliyempa chakula!


Chakula ni anasa bongo mnatakiwa mtambue hilo!

Self actualization bado so mjue namna ya kutafuta kura base on mazingira!

Pelekeni mikate mashuleni, vyakula, anzisheni sehemu za vijana kukutana social services..Michezo,elimu..mjikite kwenye fikra na sio matusi kwa viongozi everyday! Mtawawin wabongo! Nyie mnatukana wao wanatoa pilao, kandambili na kanga! Halafu mnategemea picha gani itawajia the moment wakiwa kwenye ballot box!?
Kwanza wakati huo tumbo maybe linaunguruma! Yani mkono unaenda wenyewe tu..Kikwete tik!

Nyie hamuoni Pinda kafungua Taifa Cup..Mnafikiri CCM ni pumbavu?
Ama mnafikiri haina maana?
Wana imprint!
 
Kazi ipo!..
Yaani naona dalili kubwa Kikwete anapita bila kupingwa wakati wadanganyika wanaendelea kumchambua kuku..
 
Kazi ipo!..
Yaani naona dalili kubwa Kikwete anapita bila kupingwa wakati wadanganyika wanaendelea kumchambua kuku..

kweli lakini, umeona chenge alivyopokelewa kama shujaa, Jakaya jee si atakuwa kama mungu mtu
 
Hii thread imesummarize the main problem that we have in Tanzania. Some have argued that Slaa apewe reward yakuwa RAIS kwakuwa Shujaa... Hiyo sio point, mpeni medali.. Elimu inaumuhimu lakini sio elimu in itself that is important but rather the vision that comes with it.

Africa has the most wealth on this planet lakini sisi ndio tunaongoza kufa na ugonjwa uliokuwa invented, njaa, tunashindwa kusomesha watoto wetu...!? this is a fundamental problem! Wazungu wanatudharau na kututumia... Why is that so?

Kwasababu mpaka sasa hatujaonyesha akili ya kukabiliana na matatizo yakimsingi yanayo tukabili.. Ufisadi, Ufisadi.. that seems to be all that we think of... U want to know the truth, hata mtu aliemsafi kiasi gani, mkimuweka awerais lazima atawaibia angalau kidogo.

Kinamkapa wameenda over the top kwasababu they suffer from acute greed, lakini no one is a saint and those who know the people on the political scene Tanzania sasahivi will know that these people will steal at some level wakipata nafasi, CCM is already doing it and has for a while. Alietumia mfano wakenya naomba afanye research Raila and Kibaki are elitists kazi yao ni kuprotect the status quo.

Ili wazungu waendelee kuchukua chao... Hakuna kiongozi yoyote niliosikia akiaddress the real problems of the people ... Tunataka constructive politics sio watu wanaotuambia kwanini waliopo niwabovu.. but wao watafanya nini?? CCM imeoza na wapinzani hawana vision or substance... Tunahitaji ku breed a new generation of patriots not capitalists watakao operate from Luthuli street in an ANBEM fashion.

We need to educate ourselves, and I dont mean elimu ya Mungu but bringing ourselves closer to reality. Watanzania tunaline mitaa kushangilia 700 Million dollars?

DO u know how sickening that is... Watu wanachukua resources on an incalculable level, wanarudisha visenti alafu tunawashangilia nakuwalamba miguu? Huu ni ungonjwa wa akili.

Watoto wetu wanafundishwa mzungu kagundua Mt. Kilimanjaro..hehehe.. I make it my personal mission to gather support for a new wave of thought and ideas which will in time spawn a new breed of Patriots to whom stealing from Tanzania will feel like an act of incest with their own mother. Only then can we have leaders with a satisfactory degree of moral fiber.

Corruption manifests in the mind primarily, only then does it move to the Swiss Bank accounts.. Its the mentality that we must fight..

Anyone anaebisha answer me this.. The biggest critics of the government that we all love so much... ukikutananao barabarani hawana hayo ma VX yanayokopeshwa kwa wabunge and do they not take the posho and the highly disproportionate salaries compared to the teacher anaefundisha watoto wakitanzania, or the officer who is daily accused of taking bribes or the farmer who's the 'backbone' of the economy.. literally because they do work to the point of rendering their backbones useless.. JAMANI EEH KILIO CHANGU NIKWAMBA TUNAOMBA VIONGOZI AMBAO WATAKUWA NA VISION... SO FAR SIJAONA.... and by vision I dont mean populist rhetoric of the "Maisha Bora..kwakila.." type or the "Change we ca believe in" type but real vision.. exemplified by the lifestyle of the leader, the accomplishments, ethics and overall their determination.

Watanzania tuamke, Ufisadi is not the disease that we suffer from but a mere symptom. Panadol releaves the headaches but does not cure malaria.. We need to cure our way of thinking by educating our children about the reality of this world and the values they should hold.

TUAMKE
 
So far Tanzania katika suala la RAIS wa tanzania kinachotukabili si Elimu ya RAIS muhusika, si diplomasia, si uongeaji nk

Tatizo kubwa linalotukabiri ni kutokuwa na RAIS mwenye uwezo wa kusimamia yale anayoaamini, RAIS mwenye kutoa maamuzi mazito kulingana na nguvu alizopewa kikatiba, Rais ambaye si mwoga.

Ukiangalia machache hayo tu ambayo nimeyataja na nafikiri wengine mnaweza kuongezea, watu ambao wana CV nzuri na record za uongozi unakuta wanakosa kitu kimoja nacho ni woga.

Kwa mfano labda JK anaweza kuwa kiongozi Mzuri lakini nikiangalia bado ana woga fulani. Bado sijaona akisimama, kidete wakati mwingine kusimamia yale anayoyaamini. Mwalimu nyerere pamoja na mapungufu yake hakuwa mwoga ndio maana wakati mwingine alikuwa hachelewi hata kumwambia waziri Mkuu kuwa umekosea(John, Kolimba issue).

Kwa nini watu wameona kuwa labda Slaa anaweza, ni kwa sababu si mwoga. Aliyoyafanya ni wachache wanaweza. Kuna mtu mwingine ambaye mimi huwa najua Si mwoga pamoja na kwamba hayuko kwenye siasa siku hivi na huyu ni Jenerali Ulimwengu.

Tanzania inaanguka kwa sababu ya kuwa na viongozi waoga, lakini kuna aliyesema hata sisi ndo tulivyo kwa hiyo viongozi wanareflect tabia za watu wanaowatawala.
 
SLAA anafaa hana kipingamizi...ni SHUJAA wa kuigwa
 
slaa ajaonyesha vision if u ask me.. he's a good critic which is needed... ni shujaa lakini sio rais unless he can prove otherwise
 
slaa ajaonyesha vision if u ask me.. he's a good critic which is needed... ni shujaa lakini sio rais unless he can prove otherwise


Siraa hafai kuwa raisi aendelee kuwa mbunge, mimi nasisitiza hiki kila siku watu kama siraa na zito lazima waendelee kuwa bungeni na sio kutafuta uraisi.
 
Siraa hafai kuwa raisi aendelee kuwa mbunge, mimi nasisitiza hiki kila siku watu kama siraa na zito lazima waendelee kuwa bungeni na sio kutafuta uraisi.

Naona una sound kama Mwanajeshi mkiritimba.
Naona ni bora uje na hoja badala ya viroja!
Hivi mtu akiweza kuchaguliwa na wananchi kuwa mbunge hawezi kuchaguliwa na wananchi hao hao kuwa rais?


Ama unaanza kama za mafisadi kwenda huko majimboni na kuanza kuwa divide watanzania kwenye issue nyeti!
We nani unayesema eti unasisitiza kuwa hawafai na wao ni wabunge tu!?

Wewe sasa ndio mrithi wa Mwalimu Nyerere aliyesema kuwa Mrema anafaa kuwa mbunge lakini si Rais!?


Urais kwasababu Mwalimu aliufanya kuwa ni Umungu mtu!
Characteristic aliyoipenda toka wakati akiwa waziri mkuu wa nchi hii ikiwa bado mikononi mwa mkoloni mpaka pale alipopewa full madaraka!


Hivi bado ile nyerereism ya a single person or group wanaamua kuwa nani na kutoka wapi..Kabila gani etc etc ndio wanafaa kuwa marais!

Hapa kwenye kuamua mambo yanayolisibu Taifa letu ni watanzania wote wenye responsibility and say!
 
slaa ajaonyesha vision if u ask me.. he's a good critic which is needed... ni shujaa lakini sio rais unless he can prove otherwise
Tunaomba pia uje na hayo maoni kuwa aprove kivipi!
 
Siraa hafai kuwa raisi aendelee kuwa mbunge, mimi nasisitiza hiki kila siku watu kama siraa na zito lazima waendelee kuwa bungeni na sio kutafuta uraisi.

Kwanza kabisa ,

jina lake ni Slaa na sio Siraa kama unavyojaribu kuharibu jina lake hapa damn it....... grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
 


Mkuu wangu,

Kwa hizi tabia zako za ukabila na ubaguzi,jaribu kutafuta uraia hapo nchi jirani wenye tabia ya ukabila ukaishi huko.Wewe sina hakika kama Tanzania inakufaa.


Mbowe ukimsikiliza akiwa anaongea na jinsi anavyojenga hoja hata usingekua na ujasiri wa kuulizia CV yake,vinginevyo ungekimbilia kuulizia au kutafuta uhalali wa CV za akina Nchimbi,Deodorus Kamala na akina Kikwete. Unless kama lengo lako lingekua tu kuelezea chuki zako za kikabila hapa
 


HAina maana kwa CV hii ndio kiongazi mzuri rejea mfano wa Chenge
 

1)Be specific on number one pls! Medali unayozungumzia ni ipi? Ya civilian honor or what? Pls specify!

2)Hapo umeharibu! Hizo ni fikra mbovu na very negative kuzikumbatia! Beliefs kama hizo ndio zinatukwamisha kubadilisha viongozi believing kuwa everybody ni fisadi in one way or another!

3)Sijamtaja Kibaki!
Nilimention Jaramogi ambaye ni baba yake Raila pamoja na Moi back in a day Baba Moi ile Jogoo ya Kenya ikiwa madarakani!

4)Wanachotakiwa ni kufanya the opposite of what the current leaders and the rulling party are doing! To undo the injustices!

Na kwa taarifa yako the new generation can only be built under their ledership which lifts us up instead of letting us down by speaking loud on our hears everyday..WERE POOR! Kwani sasa we now sisi ni matajiri!

New frikras wataziongoza wenye kupinga ufisadi wakiwa madarakani huku wale waliotolewa wakikaa pembeni kusubiri zamu yao kama na hawa wapya wakichemsha! THE PEOPLE are the ones to call the shots!
So therefore if we decide to change the regime...What about the knew leaders?
THEY WILL DO WHAT WE'RE FED UP WITH... NOT TO BE FISADIS!
NB:UFISADI NI UKIMWI WA MAENDELEO YA TANZANIA-JMushi1

5)Wale waliowafichua mafisadi wakichukua resources ndio hao wanaotakiwa wamalizie kazi waliyoianza!

Na kama tukiwapa madaraka hawawezi kuthubutu kuiba kwani CCM nao watakuwa pembeni wakivizia na wao wafanye blanda!
HAPO TAIFA JIPYA LENYE KUSONGA MBELE LINAZALIWA!

6)Ugonjwa wa akili ni watanzania kuwarudisha mafisadi madarakani!

7)Namba 7 nakubaliana!
 
Kwa kuanza tuu huyu Mwandosya alichukua(alitoa amri) magari ya TRC yote yatumike kwenye kampeni za uchaguzi wa uraisi Mbeya wakati ule alipokuwa akigomea uraisi pale TRC kazi zote zilizotegemea magari yale zilisimama..
 
Nauliza tena wakulu:
FREEMAN ANAFAA AMA HAFAI?
If so why? and if not then why not?

Mkuu wangu,

Huyu Freman anafaa sana kuliongoza taifa hili kwani ni mtu anaejua kiini cha matatizo yanayolikabili taifa kuliko Ex PM aliekaa madarakani for ten years and still anakuja kusema 'SASA NAJUA KWA NINI TANZANI NI MASKIN' baada ya kwenda semina huko Harvard.

Pia zaidi ya hyu mkuu wa Kaya ambae aliushangaza ulimwengu kwa kusema Hajui kwani nini Watanzania ni maskini.

mkuu wangu,hayo maneno ya hao wakuu yalikua shocking news.

Freeman kupitia kampeni zake na makala yake mbalimbali ameonyesha ni mtu jasiri na mzalendo wa kweli kulikomboa taifa hili.


Najua kuna watu watakuja kuuliza kuhusu mambo ya NSSF hapa,but hata kama angekua nabii asingekubali kufanyiwa ufisadi ambao walikua wanamfanyia.Yeye ni kiongozi anaepigania haki ikiwa ni pamoja na kuwapa hell mafisadi wasinyonye wananchi,je,angekubali yeye kufanyiwa ufisadi?


Leo hii CHADEMA imekua popular kwa sababu ya wao chini ya Mbowe kujijenga kitaasisi tofauti na CCM ambayo JK ni maarufu zaidi kutokana na yeye kujijenga peke yake tena kisanii.

Ukiangalia mafanikio ya Mbowe huko Hai enzi akiwa mbunge since 2000-2005 ni makubwa ukilinganisha na ya mtu kama Jk huko Chalinze pamoja na kuwa mbunge wa huko miaka mingi.Kufeli kwa JK katika jimbo lake ndicho chanzo cha sisi kuongozwa na rais asiye na uwezo.Pia mbowe kuliwakilisha jimbo la Hai vizuri na kuongoza chama kitaasisi ndicho chanzo cha sisi kumuona kuwa na uwezo,pamoja kutambua kiini cha matatizo yetu
 
Kazi Za Raisi Wetu Nini?
Sifa Za Raisi Wetu Nini?

Sisi Tunapenda Rais Mwenye Sifa Ipi?
Mi Naona Kwa Sasa Tunazingatia Opposites Ya Watu Tusiowapenda, Mfano Jk Ni Weak, Tunataka Jasiri, Mkapa Mjeuri, Tukamchukua Jk Mpole, Nyerere Mkristu, Mwinyi Muislamu.
Sasa Tunatafuta Mtu Ambaye Hafanani Kabisa Na Jk.
Mi Nadhani Hili Ni Kosa, Na Tutakuwa Tunarudia Kosa Tulilofanya Kwa Mkapa/mwinyi/jk
Bora Tujue Tunataka Nini, Watu Tupo Tu Wengi.
 
Jamani eeh! haya mambo ya CV sawa lakini kubwa la kuangalia pia ni kwa jinsi gani mtu ni mwadilifu, mchapakazi na mzalendo wa kweli mwenye uchungu na atakaekerwa na shida za wa-tz na atafute njia ya kuzitatua.

Kuwa na mavyeti hata kama yanajaa pick-up sio issue!!!... Nyerere nadhani hakuwa na ma-CV makubwa kiasi hiki lakini kwa kweli alikuwa ni mtu mwenye uchungu na nchi na uadilifu uliotukuka licha ya several failed attempts za kujenga mazingira ya usawa, haki, amani.

Sasa mkiwa mnatekwa na ma-CV nina wasiwasi tukarudi pale pale...Tupanue mitazamo zaidi..
 
CV inatisha ...sijajua kama politics fitna za mtandao ataziweza hata baada 2015...maana nimesikia anaweza kuchukua form za kugombea na mwenyekiti wake...ila onyo kwake akikosa...atapotea kisiasa kabisaaaaaaaa..aaaangalie hilo kwa makini sana...ushauri wangu bureeee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…