Kubwajinga,
Hayo mawazo yako ya kukatisha tamaa vyama vya upinzani nilikuwa nayo sana, kabla ya Kikwete haja-prove beyond doubt kwamba hana uwezo wa kuleta mabadiliko ya maana Tanzania.
Kwa taarifa yako, nadhani haitapata kutokea tena wakati mzuri kwa wapinzani kama wakati huu tunapoelekea katika uchaguzi mwingine hapo 2010. Yaani wapinzani wasitegemee tena kuwepo na udhaifu mkubwa katika chama cha CCM pamoja na serikali yake kama ulivyo wakati huu. Kazi tu inayowakabiri wapinzani wakati huu ni kuwapata viongozi wenye uwezo na ushawishi wa kuwavuta wananchi wakubali kuwatelekeza CCM. We need our own Railas now, the rest would be history.
Kusema kwamba CCM haiwezi kung'olewa hata kwenye urais, sio kweli hata kidogo. Kuna mifano mingi na mizuri tu inayopingana na hiyo dhana yako. Chama cha PRI kule Mexico ilikuwa kama ni 'institution' tena iliyoimarika zaidi kuliko hii CCM yetu hapa. Lakini waling'olewa, tena hata 2006 wakaendelea kucharazwa na Felipe Calderon.
Ni juzi tu, kule Paraguay - Chama cha ASUNCIO, chama kilichotawala nchi hiyo miongo sita mfululizo kiling'olewa madarakani na kumchagua Fernando Lugo(askofu aliyeng'atuka) kuwa rais wa nchi hiyo.
CCM si lolote, hasa wakati huu ambapo imekuwa dhahiri kabisa kuwa kimekuwa ni chama cha wenye pesa na wanachama wanaochagua viongozi kwa kukubali hongo.
Akipatikana kiongozi mwenye kuaminika huko kwenye wapinzani, na mtu ambaye atakuwa na uwezo wa ku-articulate vizuri matatizo yanayowakabili wananchi, na ambayo CCM imeshindwa kuyasimamia, CCM wataanguka vibaya mno! Ndio maana sisi wengine tunakazania ajitokeze/wajitokeze viongozi huko kwenye upinzani (akiwemo na Dr. Slaa ambaye amependekezwa hapa) ili tuweze kuangalia wasifu zao na kuwashawishi wajitokeze kugombea urais hapo 2010.
Bila hawa watu kujitokeza, bila shaka, ninakubaliana na wewe kwamba 'we are stuck with these CCMs eternaly.'