The road towards 2010 Elections

The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
MwK'

Hili ni tatizo dogo na limekwishajulikana. Iliyobaki ni kwa wapinzani kuitangazia Tanzania yote kungali mapema kabisa kwamba upuuzi huu hauwezi kuendelea kuvumiliwa. Hayo yote na yaliyotokea Kiteto upinzani ni lazima wajiweke tayari kuyakabili kwa nguvu zote zinazowezekana. Wakati wa kulialia tu ili kuonewa huruma umepitwa na wakati.

Tatizo kubwa ni kuwaelimisha wananchi ili wawakatae CCM.

Aliyezungumzia suala la kiteto nafikiri kidogo hakujua ni jinsi gani CCM waliwekeza nguvu zao zote ambazo hazitaweza kuonekana wakati wa uchaguzi 2010. Hili lilitokea kwa sababu CCM yote, vyombo vyote vya dola vilielekezwa kiteto. Kwa njia hii hakukuwa na uwezo wowote wa kushinda.

Walio angalia uchaguzi uliopita vizuri watakubaliana nami kuwa CCM inashindika ni mikakati tu. Uchaguzi uliopita wabunge wengi wa CCM walipita siyo kwa kupendwa hila ilikuwa ni nguvu ya Kikwete na nguvu ya pesa alizokuwa nazo.

Watanzania walimchagua kikwete kwa pesa na ushawishi aliyokuwa amewaonyesha kuwa angeweza kufanya kazi na kuwaletea neema. Lakini kwa sasa ameingia uwanjani mpaka miaka mitano inaonekana tayari sina uhakika atajiteteaje kwa wananchi.

Labda tu kikwete ataweza kuwashawishi vizuri watanzania akiwatoa kafara rafiki zake(EL, RA, KAra, nk)ambalo pia haliwezekani. Vinginevyo wapinzania wanapoint nyingi sana za kuweza kufunika CCM kila mkoa.

Kikwete 2010 hatakuwa na influence yoyote ya kumrudisha mbunge wa CCM maana nayeye atakuwa hoehae. Kikubwa sana ambacho wapinzani wanatakiwa wafanye ni kuunda mkakati mapema sana.
 
Hakuna cha kungoja wakati ni huu, CCM imeshavurunda vya kutosha, CCM has to go, Hatuwezi kukubali kuendelea kuongozwa na Mafisadi na Majambazi. Kwa hiyo nadhani 2010 ni muda muafaka kabisa wa kutumia kila mbinu kuwatoa madarakani CCM. Dr. Slaa for President.

Yes there is an opportunity. But even with that, it doesn't just happen because you said so. Wapinzani have got to prepare and not just whine out after the outcome.
 
Who are wapinzani? if you the citizen who does not agree with the existing situation(which dejure makes you one of wapinzani), sits back and just whine? You should be part of the preparations and determine the outcome. Otherwise, you better shut up!

Asha
 
Hakuna lolote hapa.

Linalotakiwa, iwe ni Mexico, Paraguay, Kenya, Zambia, Malawi, n.k., ni kumpata/kuwapata viongozi katika upinzani wenye 'charisma', ushawishi na kuaminiwa na wapiga kura. Tunataka wajitokeze akina Slaa na wengine, tumpate huyo kiongozi tutakayempa jukumu la kuwavuta wananchi.

Yote hayo unayoyasema kukosa ushirikiano na kufanya maandalizi kungali mapema, yote yanahusiana na kukosa kiongozi/viongozi hawa tunaowalilia wajitokeze mapema. Lakini wewe unawapinga wasijitokeze. Hueleweki msimamo wako upo wapi!

Ninakushangaa kama huoni somo lolote katika mifano ya Mexico na Paraguay! Nadhani unaishi katika dunia ya kipekee, au mambo ya siasa hunayo habari kabisa.

Kalamu,
  1. Hapajawahi kuwepo kiongozi mwenye hizo sifa ulizozitaja kwenye upinzani kama Mrema. Mpaka wasomi wa UDSM walimkubali awe kiongozi wao, matokeo - akapigwa chini.
  2. Kama unafikiria wapinzani wana muda, basi ngoja waendelee kusubiri mpaka 2010 ndio waanze kujipanga, hala tutasikia matokeo.
  3. Mimi sipingi yeyote yule kujitokeza, ninachopinga ni kuwatoa kafara mtu kama Dr.Slaa, wakati vyama vyenyewe havijajiweka sawa.
Tunaweza tukaongelea mifano ya nchi hata 30, labda kwa vile tunaipenda, lakini hakuna hata mmoja ambao utatusaidia either kujenga upinzani wa dhati au kuiondoa CCM madarakani. Vyama kujisafisha na kuwa na maandalizi yanayofaa ndio solution peke yake.
 
Believe me or not; mwaka 2010 [endapo wapinzani hawataleta products zinazouzika] CCM watapata ushindi wa kishindo tu.

Wapinzani wanatakiwa kuleta vichwa vipya for God's sake. Think of it Kitila

Tungekuwa na electorate iliyo sophisticated wapinzani wangeingia ikulu huku wakitembea. Yaani hamna cha wao kuleta products zinazouzika wala nini.

Kwanza CCM wangetuheshimu sisi wananchi na kuachia kabisa hiyo nafasi ya uraisi kwa kutokuweka mgombea. Wapinzani wakishindwa sitawalaumu, wa kulaumiwa watakuwa wananchi wanaowapigia kura watu wanaowaambia kula nyasi/ majani.
 
Kalamu,
  1. Hapajawahi kuwepo kiongozi mwenye hizo sifa ulizozitaja kwenye upinzani kama Mrema. Mpaka wasomi wa UDSM walimkubali awe kiongozi wao, matokeo - akapigwa chini.
  2. Kama unafikiria wapinzani wana muda, basi ngoja waendelee kusubiri mpaka 2010 ndio waanze kujipanga, hala tutasikia matokeo.
  3. Mimi sipingi yeyote yule kujitokeza, ninachopinga ni kuwatoa kafara mtu kama Dr.Slaa, wakati vyama vyenyewe havijajiweka sawa.
Tunaweza tukaongelea mifano ya nchi hata 30, labda kwa vile tunaipenda, lakini hakuna hata mmoja ambao utatusaidia either kujenga upinzani wa dhati au kuiondoa CCM madarakani. Vyama kujisafisha na kuwa na maandalizi yanayofaa ndio solution peke yake.

Kubwa jingajinga

Hivi upinzani ni nini na wapinzani ni wakina nani?

Asha
 
Who are wapinzani? if you the citizen who does not agree with the existing situation(which dejure makes you one of wapinzani), sits back and just whine? You should be part of the preparations and determine the outcome. Otherwise, you better shut up!

Asha

Asha,
When angry count to ten before you speak. If very angry, count to one thousand in your case. Just take a note that not everyone who is dissatified with CCM is a CHADEMA. Some are even Democrats.
 
Asante kubwa jingajinga

Nawe hesabu mpaka elfu kumi kabla ya kuandika ili upate muda wa kufikiria jamani. Nashukuru walau sasa umepunguza ule msimamo wako wa awali wa kwamba upinzani hawana kabisa uwezo wa kushinda na kwamba CCM ni lazima itashinda 2010. Sasa tuko ukurasa unaokaribiana kwamba ni vyema upinzani ukajiandaa zaidi.

Ila nimeuliza swali upinzani ni nini na upinzani ni nani, hujanijibu

Hata mimi ni mwanaCHADEMA, ninaungana na KJ kuwa kwa wapinzani mambo baaaaaaado, labda 2020. Kwa sasa tugombee ubunge tupate wafuasi wengi, tutoe elimu ya kutosha kwa wananchi waelewe kwa nini waibwage CCM.

Nadhani wengi wa wananchi wa Tanzania hawajui kwa nini wanaichagua CCM, nadhani wanafanya tu kwa mazoea.
 
Asante kubwa jingajinga

Nawe hesabu mpaka elfu kumi kabla ya kuandika ili upate muda wa kufikiria jamani. Nashukuru walau sasa umepunguza ule msimamo wako wa awali wa kwamba upinzani hawana kabisa uwezo wa kushinda na kwamba CCM ni lazima itashinda 2010. Sasa tuko ukurasa unaokaribiana kwamba ni vyema upinzani ukajiandaa zaidi.

Ila nimeuliza swali upinzani ni nini na upinzani ni nani, hujanijibu

Asha

Asha, Mimi sina upendeleo kwenye misimamo yangu kama ilivyo ya kwako. Kama Chadema wanaboronga utanisikia. Kama ni wengine bakora yangu ni ileile.

Tokea awali nimesema hapa waziwazi kuwa kama Chadema wataingia kwenye uchaguzi na mgawanyiko wa vyama kama ulivyo hivi sasa, itakua ni ndoto za mchana kudhania kuwa watashinda, hata kama Asha anataka iwe hivyo.

Kutaka tu Chadema ishinde 2010, haina maana itakuwa hivyo. Wanatakiwa wajipange sio kwa maneno tu bali kwa vitendo. CCM sio goi goi, hata ukijumlishia ufisadi wao. They are organized and have resources.
 
Asha,
Mimi sina upendeleo kwenye misimamo yangu kama ilivyo ya kwako. Kama Chadema wanaboronga utanisikia. Kama ni wengine bakora yangu ni ileile.

Tokea awali nimesema hapa waziwazi kuwa kama Chadema wataingia kwenye uchaguzi na mgawanyiko wa vyama kama ulivyo hivi sasa, itakua ni ndoto za mchana kudhania kuwa watashinda, hata kama Asha anataka iwe hivyo.

Kutaka tu Chadema ishinde 2010, haina maana itakuwa hivyo. Wanatakiwa wajipange sio kwa maneno tu bali kwa vitendo. CCM sio goi goi, hata ukijumlishia ufisadi wao. They are organized and have resources.

Tatizo letu sie wanachama na viongozi wa nyama vya siasa hatukubali kukosolewa bali tunapenda na kujua sana kukosoa. Kukubali kukosolewa kunasaidia kujua udhaifu na kujua njia mbadala ya katika kujiimarisha.
 
Hata mimi ni mwanaCHADEMA, ninaungana na KJ kuwa kwa wapinzani mambo baaaaaaado, labda 2020. Kwa sasa tugombee ubunge tupate wafuasi wengi, tutoe elimu ya kutosha kwa wananchi waelewe kwa nini waibwage CCM. Nadhani wengi wa wananchi wa Tanzania hawajui kwa nini wanaichagua CCM, nadhani wanafanya tu kwa mazoea.

Murra,
Angalau umeiona hii picha ya 2010. Lakini mawazo yangu ni zaidi ya Chadema kutoweka mgombea uraisi. Nilishauri kuwa kama vyama vya upinzani haviko tayari kuungana, basi haitakuwa vema kuwatoa mhanga wale ambao wana nafasi ya kuwa wabunge, ili wakashindwe kwenye uraisi halafu wawe kama Mrema, i.e. Watakosa jukwaa, bunge, la kuikosolea serikali.

Lakini kama wapinzani wakiungana, then sio vibaya kumtoa kafara hata Dr. Slaa, maana wakati huo upinzani utakuwa na nguvu na msimamo mmoja.

Lakini kuna wanaojidanganya na huu umaarufu wa hivi karibuni ambao Chadema imejipatia na kufikiri kuwa wao sasa wana ubavu wa kupambana na CCM. Hizi ni ndoto za alinacha na tamaa ya haraka haraka kwao ya kushika madaraka bila kufikiria historia na kifua cha CCM.

Uwezo wa kifendha wa Chadema ni mdogo sana na kama hizo kidogo zilizopo zikitumiwa vibaya kwenye uraisi, uwezo wa Chadema kushindana na CCM unapungua, na sio ajabu wakapoteza viti kama ilivyokuwa kwa Dr. Kaborou.
 
Kalamu,
  1. Hapajawahi kuwepo kiongozi mwenye hizo sifa ulizozitaja kwenye upinzani kama Mrema. Mpaka wasomi wa UDSM walimkubali awe kiongozi wao, matokeo - akapigwa chini.
  2. Kama unafikiria wapinzani wana muda, basi ngoja waendelee kusubiri mpaka 2010 ndio waanze kujipanga, hala tutasikia matokeo.
  3. Mimi sipingi yeyote yule kujitokeza, ninachopinga ni kuwatoa kafara mtu kama Dr.Slaa, wakati vyama vyenyewe havijajiweka sawa.
Tunaweza tukaongelea mifano ya nchi hata 30, labda kwa vile tunaipenda, lakini hakuna hata mmoja ambao utatusaidia either kujenga upinzani wa dhati au kuiondoa CCM madarakani. Vyama kujisafisha na kuwa na maandalizi yanayofaa ndio solution peke yake.

Kwa vigezo vya nani unatumia kusema kuwa hapajawi kuwa na kiongozi kama Mrema peke yake? mtu mwenye chuki za kikabila na kidini kama wewe hufai kuweka viwango vya kugombea uraisi maana unaweza kuua watu kwa chuki zako.
 
Who are wapinzani? if you the citizen who does not agree with the existing situation(which dejure makes you one of wapinzani), sits back and just whine? You should be part of the preparations and determine the outcome. Otherwise, you better shut up!

Asha

Da Asha,

sidhani kama analijua hili. Upinzani ni matokeo ya neno kupinga na sasa ona yeye anakimbilia kumwaga rants bila kufikiri.
 
Tungekuwa na electorate iliyo sophisticated wapinzani wangeingia ikulu huku wakitembea. Yaani hamna cha wao kuleta products zinazouzika wala nini. Kwanza CCM wangetuheshimu sisi wananchi na kuachia kabisa hiyo nafasi ya uraisi kwa kutokuweka mgombea. Wapinzani wakishindwa sitawalaumu, wa kulaumiwa watakuwa wananchi wanaowapigia kura watu wanaowaambia kula nyasi/ majani.

Kweli kabisa Ngabu,

badala ya Kubwajinga kuanza kuwaambia wapinzani wawaachie ccm nafasi ya uraisi, inabidi aanze kuwaambia ccm kuacha kutoa mgombea wa urais maana kuanzia mwaka 95 ccm wanatoa mabomu tupu
 
Hata mimi ni mwanaCHADEMA, ninaungana na KJ kuwa kwa wapinzani mambo baaaaaaado, labda 2020. Kwa sasa tugombee ubunge tupate wafuasi wengi, tutoe elimu ya kutosha kwa wananchi waelewe kwa nini waibwage CCM. Nadhani wengi wa wananchi wa Tanzania hawajui kwa nini wanaichagua CCM, nadhani wanafanya tu kwa mazoea.

Hakuna aliyekuuliza chama chako hapa maana haisaidii katika huu mjadala for now. Unaweza kuanza na hiyo elimu yako kwa sasa ili kusaidia watu wasichague kiongozi anayeuza nchi badala ya kutoa hoja za kujichanganya hapa.
 
Murra,
Angalau umeiona hii picha ya 2010. Lakini mawazo yangu ni zaidi ya Chadema kutoweka mgombea uraisi. Nilishauri kuwa kama vyama vya upinzani haviko tayari kuungana, basi haitakuwa vema kuwatoa mhanga wale ambao wana nafasi ya kuwa wabunge, ili wakashindwe kwenye uraisi halafu wawe kama Mrema, i.e. Watakosa jukwaa, bunge, la kuikosolea serikali.

Lakini kama wapinzani wakiungana, then sio vibaya kumtoa kafara hata Dr. Slaa, maana wakati huo upinzani utakuwa na nguvu na msimamo mmoja.

Lakini kuna wanaojidanganya na huu umaarufu wa hivi karibuni ambao Chadema imejipatia na kufikiri kuwa wao sasa wana ubavu wa kupambana na CCM. Hizi ni ndoto za alinacha na tamaa ya haraka haraka kwao ya kushika madaraka bila kufikiria historia na kifua cha CCM.

Uwezo wa kifendha wa Chadema ni mdogo sana na kama hizo kidogo zilizopo zikitumiwa vibaya kwenye uraisi, uwezo wa Chadema kushindana na CCM unapungua, na sio ajabu wakapoteza viti kama ilivyokuwa kwa Dr. Kaborou.

Kama uwezo wa chadema kifedha ni mdogo je nini kitawasaidia kwenye ubunge pekee badala ya kwenye uraisi pia. Inaonekana wewe una tatizo na CHADEMA kuweka mgombea wa uraisi na sio swala la upinzani.

Nina wasiwasi ungefurahi sana kama mgombea uraisi angekuwa yule rafiki yako mdini mwenzako ambaye ulikuwa unampigia debe kipindi kile.
 
Back
Top Bottom