Mkuu Jmushi,
Labda sasa tukubaliane tuu kuwa tunataka kubishana.Yaani hapo ulipoandika habari za Mahita ndo SIJAKUELEWA KABISA na umenishangaza kweli kweli kusikia madai hayo ya uzushi.Kaka inaonekana hata riot hujui inafanywaje na hao maaskari.Labda nikusaidie tuu kuwa,askari polisi wakienda kwenye riot ama tuseme kutuliza fujo huwa kunakuwepo makamanda.Utaona kuna askari waliobeba bunduki za risasi za moto,mabomu ya machozi.virungu,machela nk pia utaona kama wana magari ya maji nk.Utaona pia kunakuwa na mwingine ana kipaza sauti.So inaanza kwa huyo mwenye kipaza sauti kuwaamuru watu watawanyike ama sivyo nguvu itatumika.Atatangaza na hilo li tarumbeta lake mara tatu,wakikataa inatoka amri ya kamanda kuwaagiza askari wa virungu,wakishindwa anaamuru wa mambomu ya machozi wakishindwa maji ya kuwasha wakishindwa mlolongo unaendelea.
Sasa kaka hebu nambie kati ya hao ni wapi mahita alionekana akiwa na bukta na kuamru askari wampige mrema?????Wewe unasema eti akiwa nyumbani anatoa amri????hivi kweli ni wewe au umepitiwa???Tunajua protokali ya kijeshi ilivyo ndo maana huwa tunamhusisha mahita na mabomu aliyopigwa mrema moshi.Lakini kwa statement yako hiyo sina la kuongeza bali kusema tu kuwa labda unataka uwe ubishi tuu humu tujaze idadi za threads.
Labda nikukumbushe kuwa kipolisi mkoani wote wanatii kwa RPC,weka mastafu kisha njoo RCO,kisha njoo kwa vikosi as FFU,trafic nk baada ya hapo shuka wilayani kwa OCD na OC CID hadi OCS.Narudia tena wote wanatii kwa RPC sasa kaka siku nyingine njoo na utetezi wa kina kuliko kudanganya watu kuwa mahita alitoa amri na bukta za kumpiga Mrema akiwa nyumbani.
Narudia kusema kuwa Mrema na Mtikila wanafanana sana.Kufanana kwao ni katika nyanja zifuatazo:-Wote ni watu wa kupenda sifa,wote ni wakurupukaji,wote hawashauriki,wote wanapenda umaarufu,wote ni watu wa kulipa visasi,wote ni watu wenye hasira,wote ni watu wanaoganga njaa,wote wanapenda kuona upepo kisiasa unaenda vipi na kulalia huko,wote hawana dira,wote wana uchu wa madaraka na wote unaweza kuongeza zingine.
Tofauti yao ni moja tu kuwa Mrema aliwahi kuwa kiongozi wa Serikali wakati mtikila hajawahi.THATS IT.
Mrema ana historia ya kupigania maslahi ya walalahoi toka akiwa chama tawala...Nani anajuwa mtafanya nini nyie mkipewa nchi?
Kama mpinzani mwenzenu mnapinga kuliko hata fisadi mwenyewe nyie ni watu wa kuaminika kweli?
Kumfananisha na Mtikila na kukomalia kichwa kwenye pointi hiyo ni dalili za wazi za chuki miongoni mwa wanasiasa wa upinzani.
Halafu unasema eti tofauti ya Mrema na Mtikila ni simply kuwa mmoja kafanya kazi serikalini na mwingine hakufanya....Halafu umeishia hapo na conclusion kuwa yule ambaye hakufanya kazi serikalini ni sawa na yule aliyefanya kazi serikalini na kusolve matatizo ta wananchi na kusimama kinyume na mwenendo mchafu wa kifisadi.
Unafananisha watu ambao wameupiga ufisadi ndani ya ngome ya ufisadi na wameonyesha hilo kwa vitendo bila woga wa kufa kisiasa.
Nani asiyejuwa kila mwana ccm mwenye kutaka kujiunga na upinzani anatumia kigezo cha Mrema kama kisingizio?
Nani anayetaka kuja kukosewa fadhila kama ilivyo sasa...Wanaona ni bora wakae tu humo ndani na wafuate flow almuradi mkono unaenda kinywani na mambo ni safi.
Kama upinzani ndio kuna watu kama nyie basi hakuna upinzani.
Kuhusu hilo la Mahita ni ukweli na inaonyesha huujui...So habari ndiyo hiyo...Unajifanya hujui kuwa polisi kama hao wako juu ya sheria hapo bongo..Kwa taarifa yako Mahita wakati huo alikuwa anaishi mahali ambapo ni njia yangu ya kila siku kwenda shule primary pale Kibo....Na baadhi ya marafiki zangu walikuwa wanishi jirani yake tu na wakati mwingine tunatembea tu hadi kwao wakati wa kwenda nyumbani....Na wakati mwingine Mahita utamkuta yuko nje na bukta akipiga tizi la hapa na pale na mawasiliano kama kawaida.
Wewe unajaribu kunielezea utaratibu wanaoufuata wanausalama hao wakati wa kudeal na riot...Kama hujui kuwa Mrema alikabidhiwa kwa Mahita then kuna issue ambazo hauzitilii maanani kutokana na kuwa umeshaamuwa kuwa Mrema ni mtu mbaya na hafai.
Kama ulivyodai kuwa umeshawahi kukutana naye nk..Inawezekana wewe ni mwanasiasa..So sishangazwi....Siwezi kushangazwa kwasababu umesema ana uchu wa madaraka...Ni kina nani hao huko upinzani wasiokuwa na uchu wa madaraka? NI neno "Uchu" ndio linalokushtuwa?
Nani asiyetaka kwenda ikulu huko upinzani kwa style ambayo tunaweza kusema ni uchu?
Ama unataka kusema wanataka madaraka lakini hawayatamani?
Mtikila aliyechukuwa pesa za Rostam unasema Mrema na yeye ana njaa? Sifa? what is sifa? Mwanasiasa gani asiyependa sifa...Ebu acha utani bana.