The Rise and Fall of Augustine Lyatonga Mrema

TLP chasambaratika mkoani Kilimanjaro

Na Victor Kwayu, PST Moshi

Zaidi ya viongozi na wanachama 100 wa Tanzania Labour Party (TLP) mkoani Kilimanjaro wakiongozwa na Mwenyekiti wao mkoani hapa, Rose Masuruali wamekihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Akizungumza na viongozi wa kata mbalimbali za Kirua Vunjo, Masuruali alisema amefikia uamuzi wa kuihama TLP baada ya kubaini mapungufu kadhaa ya uongozi ndani yake.

Alisema TLP pamoja na viongozi wake wa ngazi za juu akiwemo Mwenyekiti wake, Augustine Mrema, wamekosa mwelekeo ikiwa ni pamoja na kutokuwa na sera mbadala za kumkomboa Mtanzania.

`` hama chetu (TLP) kimekosa mwelekeo, viongozi wa ngazi za juu wamekosa dira na ndio maana hatuna hata mbunge wala diwani, chama kimefilisika kisiasa na badala yake yamebakia majungu yanayosababisha kukigawa, sasa tumeamka,`` alisema Mwenyekiti huyo ambaye kabla ya kuukwa Uenyekiti wa mkoa alikuwa Mwenyekiti wa Wanawake Kata ya Kirua Vunjo.

Wanachama na viongozi wa kata waliokihama chama hicho na kujiunga na Chadema ni waliotoka katika vijiji vya Nganjoni, Mrumeni, Kireuwo pamoja na kijiji cha Mero ambao kwa pamoja walipitisha azimio la kukihama cha hicho.

Naye Mwenyekiti wa TLP Kata ya Kirua Vunjo, Joseph Assey alisema kutokana na Mwenyekiti wa chama hicho, Augustine Mrema kuonekana kukosa sera mbadala, wameamua kukihama chama hicho na kujiungana na Chadema katika kupambana na vita vya mafisadi sanjari na zoezi la kuwasakama mafisadi la Operesheni Sangara linaondelea Kanda ya Ziwa.

Alisema kimsingi Chadema imeonyesha nia ya dhati ya kupambana na viongozi wasio waadilifu na kwa msingi huo wameona chama pekee kinachoweza kuing`oa CCM madarakani ni Chadema pekee.

``Operesheni Sangara imeitikisa nchi, viongozi na mafisadi ndani ya serikali matumbo joto...kuingia kwetu Chadema kutasaidia kuonyesha nia ya dhati ya kuendelea na mapambano dhidi ya mafisadi na viongozi wasio makini, lengo ni kumkomboa mwananchi na lindi la umasikini,`` alisema Assey.

Naye Katibu Mwenezi wa Chadema Manispaa ya Moshi, Augustine Makelele alisema kundi la wanachama hao pamoja na viongozi wa TLP kuamua kujiunga na chama hicho, limedhihirisha ni namna gani chama hicho kinavyokubalika hivi sasa.

Alisema kwa msingi huo, chama hicho kimeazimia kuhakikisha kinahamishia zoezi la Operesheni Sangara katika Mkoa wa Kilimanjaro ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wananchi kuhakikisha wanajiunga na chama hicho ambacho alikiita kama chama chenye mwelekeo wa kumtetea mnyonge dhidi ya vita ya umasikini wa kipato.

Alisema kutokana na TLP kuonyesha udhaifu kiutendaji ikiwa ni pamoja na kukosa sera ya kweli, wanachama kadhaa wa vyama kadhaa vya siasa mkoani Kilimanjaro wamekuwa wakituma maombi kadhaa ya kujiunga na chama hicho.

``Tumekuwa tukipokea maombi mengi kutoka kwa wanachama wa vyama vya siasa kikiwemo chama tawala cha CCM...kutaka kujiunga na chama chetu, sera na mwelekeo wa Chadema umekuwa ukikubalika na kuwa na mvuto mkubwa, hivyo tunawakaribisha kwa mikono miwili,`` alisema Makelele.

Aidha, alisema viongozi na wanachama hao waliojiunga na chama hicho wakitokea TLP, watakabidhiwa kadi rasmi na Mwenyekiti wa chama hicho kitaifa, Freemani Mbowe hivi karibuni mjini hapa.

SOURCE: Nipashe

Kule Iringa ilikuwa ni CUF na sasa Kilimanjaro ni TLP...Kaazi kweli kweli.
Masuruali anasema hivi Makelele naye anasema vile...Wakati wa furaha hiyo ya kukabidhiwa kwa kadi ikiendelea...Makelele yeye anadai kuna maombi ya CCM kutaka kujiunga na CHADEMA....Ila hajataja vichwa zaidi ya furaha ya wanachama hao wapya wa kutoka TLP huko Vunjo.
Mbona sisikii kabisa kuhusu hao wa CCM?
Ama wananchi wote ni upinzani tu?
Hiyo Sangara si ianzie huko CCM? Ama macho yangu?
Hao kina Assey nao wanakuja wanadai Mrema hana sera mbadala...Ni TLP hakina sera mbadala ama ni individual this time mwenyekiti? Sababu walizozitaja za kuhama hazina nguvu...Lakini dhambi ile ile ya CCM isijekuwa ndiyo dhambi inayowatafuna wapinzani.
Ama na wao wanajiposition tu...Cha muhimu muungane.
 
MWENYEKITI wa TLP Augustino Mrema, amesema anaukataa unafiki wa CHADEMA wa kudai walifanyiwa hila na kusababisha aliyekuwa mgombea wao wa ubunge jimbo la Mbeya Vijijini, Sambwee Shitambala kuenguliwa.

Alisema nchi inatakiwa kutawaliwa kisheria, hivyo pingamizi walilowekewa CHADEMA kwa mgombea wao kuapa kwa wakili badala ya kwa hakimu kama sheria ya uchaguzi inavyotamka lilikuwa la haki.

"CHADEMA hawakuwa na nafasi ya kutwaa jimbo hili... wananchi tunaomba mtutetee, kwani inaonyesha hawa CHADEMA wanalo lao jambo," alisema Mrema.

Mrema alisema hayo juzi alipohutubia mkutano wa hadhara wa kampeni kumnadi mgombea ubunge wa CUF, Daud Mponzi. Mkutano huo uliofanyika katika stendi ya mabasi, iliyopo mji mdogo wa Mbalizi.

Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi huo, kimemsimamisha Mchungaji Luckson Mwanjale, wakati mgombea wa SAU ni Subi Mwakipiki.

Mrema aliwataka wananchi wa jimbo la Mbeya Vijijini, kuvipima vyama vya upinzani ili kubaini vyenye malengo ya ubabaishaji.

Mrema alisema CHADEMA ndiyo wanaovuruga muungano wa vyama vya upinzani, kwani katika uchaguzi wa jimbo la Tunduru, chama hicho kilivipinga vyama vitatu vilivyomo katika muungano huo.

Kwa mujibu wa Mrema, hali haikuishia hapo, kwani hata katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kiteto, CHADEMA walidai wanamsimamisha mgombea wao kwa maelezo kuwa wana mtandao mkubwa, kitu ambacho walibaini baadaye kuwa ni unafiki.

"Tarime nako walitupiga chenga... kwa unafiki huu wa CHADEMA ninyi wananchi ndio mtatupima. Kama kuna mtu angekuwa na kinyongo katika jimbo hili la Mbeya Vijijini basi ni TLP," alisema Mrema.

Alisema TLP ina wenyeviti wa vitongoji takriban 95 katika wilaya ya Mbeya Vijijini, hivyo kama mtandao basi wao ndiyo walitakiwa kusimamisha mgombea, lakini wakaamua kuiunga mkono CUF.

Mrema alisema katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, ambao marehemu Richard Nyaulawa (CCM), alishinda mgombea wa CUF, Amina Jacob, alishika nafasi ya pili, huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na mgombea wa TLP.

Alisema kwa takwimu za uchaguzi huo uliopita, CHADEMA hawakuwa na nafasi katika jimbo la Mbeya Vijijini, hivyo, kusema walikuwa na nafasi kubwa ya kushinda ni unafiki mtupu.

Kwa mujibu wa Mrema, CHADEMA kushawishi wananchi wa jimbo hilo wasijitokeze kupigia kura si halali, kwani inaonyesha chama hicho kinataka jimbo hilo lisiwe na mbunge hadi mwaka 2010.

"Wananchi msidanganyike na porojo zao za kuwataka msijitokeze kupiga kura, kwani hamtakuwa mnatenda haki," alisema Mrema.
 
Hiyo ndiyo siasa ya TZ wapinzani kutafunana wenyewe kwa wenyewe,upinzani wenye umoja wa kweli usio na mamluki itapatikana lini TZ.Kazi kwenu Watanzania kuangalia msema ukweli katika kutetea maslahi ya wengi katika TZ.
 
Chadema baada ya kushinda Tarime wanafikiri wanahaki ya kumiliki akili na maamuzi ya wapinzani wote,Chadema waliachiwa jimbo la Kiteto na Tarime lakini hawataki kuachia jimbo la Mbeya Vijijini ,kulikoni yaani vyama vingine visifanye siasa ?.Bila ushirikano wa usawa wa wapinzani wote hadithi ya kushindwa vibaya itaendelea kuwapo katika chaguzi zinazokuja.
Najua hapa jamvini washabiki wa Chadema ni wengi laiti ingekuwa ni chama kingine kimekataa ushirikiano hoja za kukijadili zingekuwa nyingi sana.
 
Mara NYINGI huwa niko against na CHADEMA, lakini kwa hili sipati picha haina mgombea lakini mtu anasimama kweny jukwaa na kuanza mashabulizi kwa chama ambacho hashindani nacho kwenye kitimu timu hicho???

hivi ameacha zile stori zake za kukamata dhahabu uwanja wa ndege? nakumbuka kwenye mdahalo wake na akina mkapa akiulizwa swali yeye anakazana kweny dhahabu tu na sio kujibu alichoulizwa. mmmh toka siku ile nilinawa mikono, kabla ya hapo nilkuwa muumini wa mrema.
 
Chadema baada ya kushinda Tarime wanafikiri wanahaki ya kumiliki akili na maamuzi ya wapinzani wote,Chadema waliachiwa jimbo la Kiteto na Tarime lakini hawataki kuachia jimbo la Mbeya Vijijini ,kulikoni yaani vyama vingine visifanye siasa ?.Bila ushirikano wa usawa wa wapinzani wote hadithi ya kushindwa vibaya itaendelea kuwapo katika chaguzi zinazokuja.
Najua hapa jamvini washabiki wa Chadema ni wengi laiti ingekuwa ni chama kingine kimekataa ushirikiano hoja za kukijadili zingekuwa nyingi sana.

Ngongo, ni kweli binafsi huwa nafagliia sana CHADEMA hasa kwa mambo mazuri wanayo yafanya hususani kuwabana mafisadi na kuiwajibisha serikali bila woga, lakini kwa hili kukataa kuwaunga mkono CUF hasa baada ya wao kubugi step na kuondolewa katika kinyanganyiro, nadhani si sahihi na silifagilii hata kidogo!

Hata kama CUF walishiriki kuwawekea pingamizi lakini wanapashwa tambua kwamba ADUI yao No moja ni CCM; na kuunganisha nguvu ili kumuondoa huyo ni muhimu kuliko tofauti ndogo walizo nazo. Ni afadhali wawaunge mkono CUF, jimbo liende CUF kuliko kuliacha rirejee kwa CCM.
 
Hivi unaweza kuniambia CUF Tarime waliunga mkono chama gani, NCCR au CHADEMA

Kama waliunga Mkono CHADEMA, kwa nini hawakutoa tamko la kulaani NCCR kutoiunga mkono CHADEMA?

Kama Waliunga mkono NCCR, kwa nini leo watake kuungwa mkono na CHADEMA?
 
Inaelekea hawa jamaa wa CHADEMA wana nguvu kubwa sana mbeya vijijini ndio maana wanaendelea kushambuliwa badala ya CCM. Mgombea wa CUF 2005 alipata asilimia 8 ya kura, Nyaulawa alishinda zaidi ya asilimia 80. Hali imebadilika sana kisiasa kati ya 2005 mpaka 2008, miaka mitatu. CHADEMA ilikuwa tishio sana kwa CCM. Mgombea wa CUF 2005 sio huyu aliyegombea sasa, yule wa mwanzo ni Amina. Sasa hakupita kura za maoni, si mnakumbuka yule mchungaji wa CUF aliyelalamika uteuzi ulivyokwenda kwa kupendelewa Mponzi aliyetoka CCM. Mama Amina aliambiwa aondoe jina lake, Mbeya kiasi kikubwa ni wakristu walimwambia kuwa kama akisimama kupitia CUF chama chao kitapata asilimia ile ile 8 tu. Sasa huko tumepeleka timu kubwa ya kina Malecela, ushindi uko wazi baada ya CHADEMA kuondolewa.

......ndiyohiyo
 
Mrema ndio mnafiki zaidi dhidi ya CHADEMA:

a. Aliahidi kwenda Kiteto kuunga mkono CHADEMA, hakwenda aliishia DSM. Chaguzi za CUF zote huenda mwenyewe

b. Tarime, Mrema aliunga mkono NCCR Mageuzi. Kwanini hakuunga mkono CHADEMA iliyokuwa na nguvu zaidi?

c. Huyu ndiye aliyeshiriki kusema Mbowe alimuua Wangwe, na naibu katibu Mkuu wake akaandika barua kwa IGP kuwa Mbowe alifanya sherehe Afrika Kusini. Mrema akamsifu kwa barua hiyo

Kwa ujumla ni hasira zake kwa Mbowe na CHADEMA kwa kuchukua nafasi ambayo yeye na TLP walikuwa nayo katika siasa za Tanzania.

Hivi kwanini vyama vyote vinaishambulia CHADEMA jamani? Ina nini cha pekee, CCM, CUF,TLP, NCCR nk

Asha
 
Ninaunga mkono hatua ya CHADEMA kujitoa katika ushirika wa vyama hivi vya upinzania kwani vingi ni vya kinafiki na havina muelekeo. Kwa sababu malengo, imani na muelekeo wa CHADEMA ni tofauti na ule wa TLP na CUF. Tatizo huyu Mrema na wenzake wanataka kutumia mgongo wa CHADEMA kurudisha heshima yao ya kisiasa ambayo imeshapotea kutokana na uongozi wao usio na malengo.

Mrema ulikiua NCCR-Mageuzi sasa ya nini leo uyanye ushirika na kiongozi kama huyu mrokaji tu na asiye ya political vision.

Sasa hivi kila mtanzania anajua nini CHADEMA wanafanya tofauti na hao wababaishaji wa TLP na CUF. Mrema tumeshamzoea ni mropokaji tu, TLP chama gani hakina hata mbunge mmoja.

Isitishe, kwa nini CHADEMA mina wauma sana hawa TLP na CUF wakati hata hawamo kwenye ushindani. Kuna tatizo hapa.

KEEP IT UP CHADEMA ,NEVER MESS UP WITH VISIONLESS TLP and CUF
 
Ngongo, ni kweli binafsi huwa nafagliia sana CHADEMA hasa kwa mambo mazuri wanayo yafanya hususani kuwabana mafisadi na kuiwajibisha serikali bila woga, lakini kwa hili kukataa kuwaunga mkono CUF hasa baada ya wao kubugi step na kuondolewa katika kinyanganyiro, nadhani si sahihi na silifagilii hata kidogo!

Hata kama CUF walishiriki kuwawekea pingamizi lakini wanapashwa tambua kwamba ADUI yao No moja ni CCM; na kuunganisha nguvu ili kumuondoa huyo ni muhimu kuliko tofauti ndogo walizo nazo. Ni afadhali wawaunge mkono CUF, jimbo liende CUF kuliko kuliacha rirejee kwa CCM.

Kabla sijasema kama naunga mkono CHADEMA kujitoa kwenye Ushirika nina Maswali ambayo naomba wana bodi mnisaidie ili niweze kuwa katika maamuzi sahihi nataka nijue nani MNAFIKI.
1: Ni lini na ni wapi Ushirika huu ulikaa na kuamua ni chama gani kisimame Tarime
2: Na nini lilikuwa Azimio la Kikao Hicho?
 
`Ndoa` ya Chadema, TLP, CUF yavunjika

2008-09-13 09:40:54
Na Simon Mhina

Ushirikiano wa kisiasa kati ya vyama vinne vya upinzani, umesambaratika baada ya vyama vitatu kati ya hivyo kuamua kusimamisha mgombea mmoja katika uchaguzi mdogo wa Tarime.

Wenyeviti wa vyama hivyo, Augustine Mrema (TLP) Profesa Ibrahim Lipumba (CUF) na James Mbatia (NCCR- Mageuzi) juzi walifanya kikao cha kujadili uchaguzi huo, na kumtenga mwenzao wa Chadema, Freeman Mbowe.

Japokuwa Profesa Lipumba alisema kwamba taarifa za kumwalika Mbowe zilitumwa, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilibrod Slaa, alisema hakuna mwaliko wowote uliotumwa kwa bosi wake na Chama chake hakina mawasiliano yoyote na viongozi wa vyama hivyo vitatu.

Hata hivyo, Profesa Lipumba hakuweza kueleza kwamba walitumia njia gani kumpelekea Mbowe taarifa.

``Unajua hapa katikati kumetokea sintofahamu zilizosababishwa na kifo cha Wangwe (Mbunge wa zamani wa Tarime, Chacha), kuna kamgogoro baridi kanafukuta ndio maana hawakuhudhuria,`` alisema.

Alisema vyama vitatu vimeamua kuweka mgombea mmoja ili kuhakikisha wanapata ushindi mkubwa Tarime.

Lipumba alisema baada ya kikao cha viongozi wakuu, wamepeleka madaraka yao kwa viongozi wa vyama vyao Jimbo la Tarime.

``Vikao vya wenyeviti wa taifa havitoshi, tunataka wenzetu wa Tarime nao wakutane, wao wanajuana na wanaelewa mazingira yao zaidi. Tunataka nao watuletee mapendekezo yao,`` alisema.

Hata hivyo, kiongozi huyo alisema kwamba ushirikiano wa vyama hivyo, hauondoi haki ya kila chama kufanya shughuli zake kwa mujibu wa sera na katiba yake.

Awali akitoa taarifa za kikao hicho, Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Uchaguzi wa NCCR, Faustine Sungura, alisema kwa kauli moja, viongozi hao wamependekeza mgombea wa Chama hicho apitishwe.

Alimtaja mgombea aliyependekezwa kuwa Enock Haruna Marwa maarufu kwa jina la Macho Manne.

Sungura alisema kikao hicho kilichofanyika siku nzima, viongozi wa Chadema waliingia mitini.

Alisema haelewi ni kwanini viongozi wa Chadema waliingia mitini bila kutoa taarifa yoyote.

Awali akizungumzia sakata hilo, Dk. Slaa alisema pamoja na kutengwa na wenzao, wataendelea na maandalizi yao ya kuingia vitani.

``Tutaingia vitani kivyetu vyetu, hatuwezi kurudi nyuma. Lazima jimbo la Tarime tutalirudisha mikononi mwetu,`` alisema.

Alisema kutokana Chadema kutengwa ghafla na wapinzani wenzake, kitachukua hatua kadhaa kuhakikisha Jimbo hilo haliendi CCM kama ilivyokusudiwa.

Alisema Tarime kuna rasilimali nyingi ambazo zinaporwa, hivyo waporaji wanaweza kuhakikisha wanasaidia mkakati wowote wenye lengo la kuifanya Tarime iwe ya CCM.

Mbunge huyo alisema Chadema kina mtaji mkubwa wa kisiasa Tarime, hivyo hakitishwi wala kubabaishwa na uamuzi wa kutengwa.

Vyama vya Chadema, TLP na CUF vilianza ushirikiano rasmi bungeni na kuunda kambi rasmi ya upinzani ambayo inatambulika rasmi bungeni.

Tangu kifo cha Wangwe kilichotokea kwa ajali ya gari Julai 28, 2008 iliyotokea kijiji cha Pandambili, Kongwa mkoani Dodoma akiwa safarini kwenda Dar es Salaam, kumekuwa na mvutano wa wazi baina ya viongozi wa kambi hiyo.

Tukio la kipekee lililotokea ni pale mazishi ya Wangwe yalipoahirishwa Julai 31, 2008 kutokana na familia kutaka uchunguzi wa kujitegemea juu ya chanzo cha kifo cha mbunge huyo, hali iliyowagawa viongozi hao kwenye makundi mawili.

Chadema wamekuwa wakilaumu wenzao kwamba walitaka kutumia msiba huo kupata faida ya kisiasa Tarime na kukiangamiza chama hao. Lawama ambazo pia zimeelekezwa kwa CCM.

* SOURCE: Nipashe
 
MWENYEKITI wa TLP Augustino Mrema, amesema anaukataa unafiki wa CHADEMA wa kudai walifanyiwa hila na kusababisha aliyekuwa mgombea wao wa ubunge jimbo la Mbeya Vijijini, Sambwee Shitambala kuenguliwa.

Alisema nchi inatakiwa kutawaliwa kisheria, hivyo pingamizi walilowekewa CHADEMA kwa mgombea wao kuapa kwa wakili badala ya kwa hakimu kama sheria ya uchaguzi inavyotamka lilikuwa la haki.

"CHADEMA hawakuwa na nafasi ya kutwaa jimbo hili... wananchi tunaomba mtutetee, kwani inaonyesha hawa CHADEMA wanalo lao jambo," alisema Mrema.

Mrema alisema hayo juzi alipohutubia mkutano wa hadhara wa kampeni kumnadi mgombea ubunge wa CUF, Daud Mponzi. Mkutano huo uliofanyika katika stendi ya mabasi, iliyopo mji mdogo wa Mbalizi.

Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi huo, kimemsimamisha Mchungaji Luckson Mwanjale, wakati mgombea wa SAU ni Subi Mwakipiki.

Mrema aliwataka wananchi wa jimbo la Mbeya Vijijini, kuvipima vyama vya upinzani ili kubaini vyenye malengo ya ubabaishaji.

Mrema alisema CHADEMA ndiyo wanaovuruga muungano wa vyama vya upinzani, kwani katika uchaguzi wa jimbo la Tunduru, chama hicho kilivipinga vyama vitatu vilivyomo katika muungano huo.

Kwa mujibu wa Mrema, hali haikuishia hapo, kwani hata katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kiteto, CHADEMA walidai wanamsimamisha mgombea wao kwa maelezo kuwa wana mtandao mkubwa, kitu ambacho walibaini baadaye kuwa ni unafiki.

"Tarime nako walitupiga chenga... kwa unafiki huu wa CHADEMA ninyi wananchi ndio mtatupima. Kama kuna mtu angekuwa na kinyongo katika jimbo hili la Mbeya Vijijini basi ni TLP," alisema Mrema.

Alisema TLP ina wenyeviti wa vitongoji takriban 95 katika wilaya ya Mbeya Vijijini, hivyo kama mtandao basi wao ndiyo walitakiwa kusimamisha mgombea, lakini wakaamua kuiunga mkono CUF.

Mrema alisema katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, ambao marehemu Richard Nyaulawa (CCM), alishinda mgombea wa CUF, Amina Jacob, alishika nafasi ya pili, huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na mgombea wa TLP.

Alisema kwa takwimu za uchaguzi huo uliopita, CHADEMA hawakuwa na nafasi katika jimbo la Mbeya Vijijini, hivyo, kusema walikuwa na nafasi kubwa ya kushinda ni unafiki mtupu.

Kwa mujibu wa Mrema, CHADEMA kushawishi wananchi wa jimbo hilo wasijitokeze kupigia kura si halali, kwani inaonyesha chama hicho kinataka jimbo hilo lisiwe na mbunge hadi mwaka 2010.

"Wananchi msidanganyike na porojo zao za kuwataka msijitokeze kupiga kura, kwani hamtakuwa mnatenda haki," alisema Mrema.
aha ya kunguru

Mhh, vita vya panzi (Wapinzani) furaha ya Kunguru (CCM). Huyu Mrema badala ya kupiga kampeni dhidi ya mshindani wao CCM anapiga kampeni kunyume cha CHADEMA ambacho hakina mgombea. Any way, Mrema aliyaanza hayo tangu Uchaguzi mdogo wa Tarime. Wananchi watawapima kwa matokeao ya Uchaguzi wa Mbeya Vijijini na ole wake Wapinzani washindwe.
 
`Ndoa` ya Chadema, TLP, CUF yavunjika

2008-09-13 09:40:54
Na Simon Mhina

Ushirikiano wa kisiasa kati ya vyama vinne vya upinzani, umesambaratika baada ya vyama vitatu kati ya hivyo kuamua kusimamisha mgombea mmoja katika uchaguzi mdogo wa Tarime.

Wenyeviti wa vyama hivyo, Augustine Mrema (TLP) Profesa Ibrahim Lipumba (CUF) na James Mbatia (NCCR- Mageuzi) juzi walifanya kikao cha kujadili uchaguzi huo, na kumtenga mwenzao wa Chadema, Freeman Mbowe.

Japokuwa Profesa Lipumba alisema kwamba taarifa za kumwalika Mbowe zilitumwa, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilibrod Slaa, alisema hakuna mwaliko wowote uliotumwa kwa bosi wake na Chama chake hakina mawasiliano yoyote na viongozi wa vyama hivyo vitatu.

Hata hivyo, Profesa Lipumba hakuweza kueleza kwamba walitumia njia gani kumpelekea Mbowe taarifa.

``Unajua hapa katikati kumetokea sintofahamu zilizosababishwa na kifo cha Wangwe (Mbunge wa zamani wa Tarime, Chacha), kuna kamgogoro baridi kanafukuta ndio maana hawakuhudhuria,`` alisema.

Alisema vyama vitatu vimeamua kuweka mgombea mmoja ili kuhakikisha wanapata ushindi mkubwa Tarime.

Lipumba alisema baada ya kikao cha viongozi wakuu, wamepeleka madaraka yao kwa viongozi wa vyama vyao Jimbo la Tarime.

``Vikao vya wenyeviti wa taifa havitoshi, tunataka wenzetu wa Tarime nao wakutane, wao wanajuana na wanaelewa mazingira yao zaidi. Tunataka nao watuletee mapendekezo yao,`` alisema.

Hata hivyo, kiongozi huyo alisema kwamba ushirikiano wa vyama hivyo, hauondoi haki ya kila chama kufanya shughuli zake kwa mujibu wa sera na katiba yake.

Awali akitoa taarifa za kikao hicho, Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Uchaguzi wa NCCR, Faustine Sungura, alisema kwa kauli moja, viongozi hao wamependekeza mgombea wa Chama hicho apitishwe.

Alimtaja mgombea aliyependekezwa kuwa Enock Haruna Marwa maarufu kwa jina la Macho Manne.

Sungura alisema kikao hicho kilichofanyika siku nzima, viongozi wa Chadema waliingia mitini.

Alisema haelewi ni kwanini viongozi wa Chadema waliingia mitini bila kutoa taarifa yoyote.

Awali akizungumzia sakata hilo, Dk. Slaa alisema pamoja na kutengwa na wenzao, wataendelea na maandalizi yao ya kuingia vitani.

``Tutaingia vitani kivyetu vyetu, hatuwezi kurudi nyuma. Lazima jimbo la Tarime tutalirudisha mikononi mwetu,`` alisema.

Alisema kutokana Chadema kutengwa ghafla na wapinzani wenzake, kitachukua hatua kadhaa kuhakikisha Jimbo hilo haliendi CCM kama ilivyokusudiwa.

Alisema Tarime kuna rasilimali nyingi ambazo zinaporwa, hivyo waporaji wanaweza kuhakikisha wanasaidia mkakati wowote wenye lengo la kuifanya Tarime iwe ya CCM.

Mbunge huyo alisema Chadema kina mtaji mkubwa wa kisiasa Tarime, hivyo hakitishwi wala kubabaishwa na uamuzi wa kutengwa.

Vyama vya Chadema, TLP na CUF vilianza ushirikiano rasmi bungeni na kuunda kambi rasmi ya upinzani ambayo inatambulika rasmi bungeni.

Tangu kifo cha Wangwe kilichotokea kwa ajali ya gari Julai 28, 2008 iliyotokea kijiji cha Pandambili, Kongwa mkoani Dodoma akiwa safarini kwenda Dar es Salaam, kumekuwa na mvutano wa wazi baina ya viongozi wa kambi hiyo.

Tukio la kipekee lililotokea ni pale mazishi ya Wangwe yalipoahirishwa Julai 31, 2008 kutokana na familia kutaka uchunguzi wa kujitegemea juu ya chanzo cha kifo cha mbunge huyo, hali iliyowagawa viongozi hao kwenye makundi mawili.

Chadema wamekuwa wakilaumu wenzao kwamba walitaka kutumia msiba huo kupata faida ya kisiasa Tarime na kukiangamiza chama hao. Lawama ambazo pia zimeelekezwa kwa CCM.

* SOURCE: Nipashe

Asante dada Asha!
Kwa mujibu wa Maelezo hayo ina maana CHADEMA haikuungwa mkono na chama chochote TARIME.
Sasa:
1: Hii kauli ya CUF iliiunga mkono CHADEMA Tarime ina maana gani!
2: Kama kweli CUF watakuja hapa kuthibitisha kwamba waliunga mkono CHADEMA Tarime,
Waeleze walichukua hatua gani kwa NCCR kwenda kinyume na kusimamisha mgombea
Tarime!
3: Kwa NCCR, Kama CUF iliunga mkono CHADEMA Tarime, kwa nini basi mnailaumu CHADEMA
Na kuwaona CUF ni Watakatifu ilhali hawakuwaunga mkono TARIME
 
Naipenda hali hii. sasa ndio vyanma vijue kuwa hakuna mteremko kwa mgongo wa ushirikiano. nadhani itakuwa ni challenge kwao kujijenga kivyaovyao bila kutarajia kuwa kutakuwa na mjomba wa kushirikiana naye. Unafiki umeshaonyesha hali halisi na ni wakati wa vyama makini kupanga mipango yao. Uchaguzi wa serikali za mitaa unakaribia, wafahamu hivyo katika mipango yao na mwakani si mbali sana
 
Nakwambia! Wanalialia tu badala ya kupiga kampeni, ningeweza kwenda huko ningewapa Madhiwa;hivi Mrema bado unatembea na mkewe na chupa ya uji kwenye mikutano? Manake alikuja hapa Kibanda Maiti kila akizungumza kidogo anakunywa uji!

Asha
 
Hivi kwanini vyama vyote vinaishambulia CHADEMA jamani? Ina nini cha pekee, CCM, CUF,TLP, NCCR nk

Asha
Chadema haina lolote jipya, tena CCM huwa hawaishambulii Chadema zaidi ya kuwapa ukweli wao kuwa wanaongozwa na kilaza.
 
Hizo zote ni kelele tu. Hivi nchi hii kweli tuikabidhi CHADEMA chini ya Mbowe!!! Yaani rais awe Mbowe !! Acheni ufinyu wa kuangalia mbali.
 
Heri ya Mwaka Mpya,

Hali ya Mbeya Vijijini inaweza kuelezewa kwa maneno mengi sana kuhusiana na suala hili la hivi vyama vya CUF,TLP,NCCR NA PPT -MAENDELEO kwenda kufanya kampeni Mbeyaq na badala ya kumnadi mgombea wao wao wamekuwa wakikazania ya kuwa CHADEMA inawahujumu wakati CHADEMA inaendelea kujipanga kimya kimya DSM kwenye opersheni sangara.

Imefikia mahali sasa baada ya CUF kuona moto wa Sangara DSM na wao wameamua kujitokeza hadharani kufuatilia mikutano ya CHADEMA kila inapofanyika mikutano ya CHADEMA siku inayofuata JUSSA wa CUF huwa anapita pamoja na viongozi wengine wa CUF kuwashambulia viongozi wa CHADEMA na haswa ZITTO, DR.SLAA NA MBOWE.

Anafikia mahali pa kusema kuwa viongozi wa CHADEMA ni mafisadi na hawapaswi kuungwa mkono hata kidogo, na hili jana lilipelekea miongoni mwa kiongozi wa CUF kuzomewa na wananchi alipokuwa anauliza swali hilo kuwa amemsikia JUSSA akisema hivyo , hali iliyomfanya kunyamazishwa na wananchi eneo la kwa Tumbo kata ya TANDALE.

Kuna mengi yatakuwa yanajitokeza wakati huu na haswa baada ya hivi vyama vingine kutokuwa na programu maalum ya kujipanga kwa ajili ya kuelekea 2009 na 2010.
 
Back
Top Bottom