The Rise and Fall of Augustine Lyatonga Mrema

The Rise and Fall of Augustine Lyatonga Mrema

By the way,
Muungano usingeweza kuleta upinzani wa kweli na wenye afya kwa kuwa lika chama kina sera yake na malengo yake. Tunachohitaji ni upinzani wa kweli, na sasa ni nafasi nzuri kwa kila vyama vyenye kuhitaji ushirikiano vikavunjwa na kuwa na kujenga chama kimoja baada ya marekebisho ya sheria.

Vyama vifanye siasa za kuwaletea maendeleo Watanzania. Viwe vyama vya kutoa mtizamo mbadala kwa chama tawala ili kiweze kujisahihisha/kupokonywa madaraka, lengo kuu likiwa ni kuwaletea maisha yawe bora watanzania.

Ni aibu kuwa badala ya kumwaga sera zitakazowawezesha kunyakua jimbo la mbeya rural, mnaendelea kumsakama CHADEMA. Angekuwa ameingiza majeshi nyuma ya ccm kama alivyofanya Mtikila sijui ngesema je.

CHADEMA endeleeni na mipango yenu thabiti ya kukijenga chama kitakacho toa sera mbadala. Hakuna haja ya kuendeleza malumbano yasiyokuw na mwenyewe, kazi ni moja tu sasa, "SANGARA" kuitangaza CHADEMA.

Vyama visivyofahamu nafasi yao katika siasa, visubiri kufa kifo cha mende!!
 
Mkakati wa siri unaendelea Mbeya kuna mazungumzo makubwa sana yanaendelea kufanyika huko ili CHADEMA iwaunge mkono CUF wanaona bila kuungwa mkono hali ni ngumu sasa wao wanafanya kihuni wanataka kuwarubuni baadhi ya viongozi wa CHADEMA local wawaunge mkono.

Nimeona niwapenyezee ili muweze kuangalia na hilo pia.
 
Mkakati wa siri unaendelea Mbeya kuna mazungumzo makubwa sana yanaendelea kufanyika huko ili CHADEMA iwaunge mkono CUF wanaona bila kuungwa mkono hali ni ngumu sasa wao wanafanya kihuni wanataka kuwarubuni baadhi ya viongozi wa CHADEMA local wawaunge mkono.

Nimeona niwapenyezee ili muweze kuangalia na hilo pia.

Huo ndio unafiki wenyewe kwanini tusiamini Chadema wamepewa "kitu kidogo"
 
Neither Chadema no CUF walio na strategic plan ya kuchukua nchi hata baada ya miaka kumi kuanzia sasa. Else;
1. Tusingeweza kuona makosa ya kizembe kama yaliyoafanywa na Chadema Mbeya.
2. Chadema wasingeshindwa kung'amua katika strategy yao kuwa vyama vingine vya Upinzani ni key stakeholders (and competetors of course) na hivyo wangekuwa makini katika mahusiano nao kwani yana athari kwa wananchi wa kawaida.
3. CUF wasingefanya ubahili na kutotoa pesa nyingi bara ili zikiimarishe Chama. Wanasahau kuwa bila kuwa na nguvu bara ukuu wao wa upinzani unakuwa na mapungufu.

Kama Chadema wangekuwa na experienced visionary leaders na CUF wakaacha kujali Zanzibar (Pemba?) tu tungeweza alau kuimarisha upinzani bungeni na kuanza kuchagiza mabadiliko ya katiba.

NN
 
NN,

Inawezekana ktk vyama vyote vya Upinzani kuna mapandikizi...!!! Bahati Mbaya wao wanaona bora kupakana matope Hadharani....kwanini both parties wasi concentrate kupigana na CCM ktk majukwaa yao, kuliko kuendelea kuwashambulia wao kwa wao ambao hawana nguvu(serikali)....wanamuuacha adui CCM wanabaki kutiana vidole machoni....
 
Mapandikizi ndugu yangu yamewekwa kila chama,utayajua kwa matendo na maneno. Inachukua muda kuyajua na tayari wakati huo yanakuwa yametuchelewesha sana.
 
Mrema anaweweseka bure tuu,watu makini walishamuona kuwa ni mbabaishaji anayetafuta riziki ndani ya siasa pasipo dhamira ya kweli.
Kuhusu CHADEMA, ni kweli kuwa kuna mapungufu ya kiuongozi kama chama chochote kilicho kichanga. Hata hivyo la msingi ni dhamira waliyonayo viongozi dhidi ya kile wanachokizungumzia ambapo kwa CHADEMA walao hilo linaonekana. Nadhani badala ya kuwalaumu kwa hayo mapungufu ya kiuongozi yanayoonekana, tunapaswa kuwasaidia kwa kushirikiana nao na kuwapa ushauri pamoja na support.
 
Tumefika pabaya. Siku zote huwa naamini ushirikiano wa vyama si suluhisho. Kila mmoja ni msindani kwa kwa mwenzake, dhana ya kuwataka waungane ndio huleta matatizo kama haya.

Nimeshuhudia mkutano mmoja wa operesheni sangara pale Manzese ambapo mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alikuwa anahutubia, sikumsikia akitukana vyama vingine. Alitoa hotuba nzito ilioyowataka wananchi kuweka mkazo wa kujitafutia maendeleo na kutokubali kugawanywa na vyama!

Kesho yake Jusa wa CUF alienda pale kuporomosha matusi! CUF wanalalamika nini bado? Viongozi wa CHADEMA wameondoka mbeya wiki kadhaa na wapo kwenye opereshni sangara hapa Dar?

CUF, mrema na Mbatia wajitahidi kutoa suluhisho kwa wananchi wa mbeya vijijini. wazungumzie mbolea, umeme na mikakati mingine ya kimaendeleo. Wanayoyafanya sasa huko mbeya ni hujuma kubwa kwa upinzani zaidi ya CHADEMA kukataa kuwaunga mkono.

Suala la CHADEMA waendeleze badae sasa hivi watumie uwezo wao kuhakisha wanashinda huko,na hiyo itawasaidia sana kusukuma 'ajenda' yao dhidi ya CHADEMA. Ni Jambo la ajabu kutumia jukwaa la uchaguzi mdogo mbeya vijijini kumshambulia mtu ambae hawatashindana nae huko.


Kazi ipo
 
Neither Chadema no CUF walio na strategic plan ya kuchukua nchi hata baada ya miaka kumi kuanzia sasa. Else;
1. NN

Hivi strategic plan si ndio Mpango Mkakati au nimekosea jamani? Kama ndio mi naona CHADEMA tunayo, viongozi wetu walisema hapa kwenye uzinduzi kuwa walizindua pia strategic plan, unaweza kuiona humu kwa ufupi: Uzinduzi wa Chama Agosti 2006

Nungu Nungu, nini maoni yako kuhusu hiyo plan?


Asha
 
Hiyo paper iliyoandikwa inaweza kuwa sehemu ya input na sio mpango mkakati wenyewe kwani haikidhi vigezo vya chini kabisa ili iweze kuitwa hivyo.

Nimepitia ukurasa wa mwanzo hadi mwisho siamini vijana kama Zitto au Mnyika hawajayaona mapungufu hayo ya kiufundi kama kukosekana kwa Strategic Objectives, SWOT/SWOC na Stakeholders analysis nikitaja machache tu.

Na kama upo mwingine, tunachoweza kukiona wengine ni harakati na matokeo ya utekelezaji wa mkakati huo. Matukio ya karibuni yameonyesha vinginevyo.

Otherwise, hicho kilichobandikwa kwenye website ya Chadema hauwezi kuwa mpango mkakati wa chama kinachokusudia kuongoza nchi.

NN
 
Hivi unaweza kuniambia CUF Tarime waliunga mkono chama gani, NCCR au CHADEMA

Kama waliunga Mkono CHADEMA, kwa nini hawakutoa tamko la kulaani NCCR kutoiunga mkono CHADEMA?

Kama Waliunga mkono NCCR, kwa nini leo watake kuungwa mkono na CHADEMA?

hivi suala la kuunga mkono chama si mapendekezo ya chama chenyewe, mi sidhani kama ni sawa kulazimisha au kumuunga mkono mtu ambaye mnajua hataweza ku produce, Kwanza vyama vya upinzani halahala msije mkatujazia bora viongozi bungeni kwa ajili ya huo muungano wenu wakizushi, sisi tutawapima kama wamemuona kiongozi huyo hafai hawana haja ya kuunga mkono maana Mwaka kesho ni uchaguzi kama Chadema wamemuona anafaa na kumuunga mkono basi hawana haja ya kusimamisha mgombea kwani tunaamini mwaka mmoja hauwezi kum judge mtu,. ni kama nitakavyoshangaa kama mgombea wa CCM akishinda halafu 2010 wasimamishe mwingine, Chadema nawafagilia sana wameliona hilo..WANAAMINI MGOMBEA WAO NDIYE MWENYE UWEZO WA KUONGOZA NA AMESHINDWA KWA SABABU SIZIZOWEZA KUZUILIKA THEN WATAMSIMAMISHA 2010, SASA WAUNGE CHAMA KINGINE MKONO 2010 WATATUAMBIA NINI ....
 
Hapa kuna mtu kasema maneno ya msingi hivi kama Mponzi ambaye aligombea kura za maoni CCM na akawa wa mwisho ndani ya CCM kati ya kura 1000 yeye aliambulia 23 anafaa kweli kuungwa mkono ?

Mponzi ambaye hadi leo mabaunsa wa CUF wanamlinda usiku na mchana eti wakimuacha anaweza kurubuniwa na CCM na hivyo kuamua kuachana na CUF anafaa kuungwa mkono kuwatetea wananchi wa Mbeya?

Mponzi ambaye hajasema anataka kufanya nini ama kuwafanyia nini wananchi wa ,Mbeya anafaa kuungwa mkono? ama mtu akiwa upinzani hata kama hafai kwa sababu tuu ni mpinzani basi aungwe mkono?

Kila la kheri.
 
Kabla sijasema kama naunga mkono CHADEMA kujitoa kwenye Ushirika nina Maswali ambayo naomba wana bodi mnisaidie ili niweze kuwa katika maamuzi sahihi nataka nijue nani MNAFIKI.
1: Ni lini na ni wapi Ushirika huu ulikaa na kuamua ni chama gani kisimame Tarime
2: Na nini lilikuwa Azimio la Kikao Hicho?

No,and they have never agree about any thing.
 
Nawaunga mkono CHADEMA kwa hatua yao ya kuamua kujitoa kwenye muungano wa kinafiki wa kambi ya upinzani. CCM imepandikiza mamluki wa kutosha kwenye vyama vya upinzani hili limethibitishwa pia na Mhe Tendwa ambaye ni msajiri wa vyama vya siasa. Kwa kuwa CHADEMA wamedhamiria kufanya siasa za kweli na siyo za kuganga njaa ni dhahiri hawawezi kufanya siasa na mamluki. Wote mnakumbuka jinsi ambavyo Mbatia na NCCR- Magauni yake alivyowahi kuwawekea pingamizi wagomea wa CUF kisiwani Pemba wakati chama chake kikiwa hakina hata tawi kisiwani humo. Pia naamini wana ukumbi bado hamjasahau Mrema alivyosambaratisha kwa ustadi mkubwa NCCR. Sasa mabo yote hayo hayakutokea kwa bahati mbaya ni mambo ambayo yalipangwa vizuri kitaalamu kabisa kwa lengo la kuinufaisha CCM. Nawasihi CHADEMA wasirudi nyuma katika hili kwani hao TLP,NCCR ni matawi ya CCM
 
Nawaunga mkono CHADEMA kwa hatua yao ya kuamua kujitoa kwenye muungano wa kinafiki wa kambi ya upinzani. CCM imepandikiza mamluki wa kutosha kwenye vyama vya upinzani hili limethibitishwa pia na Mhe Tendwa ambaye ni msajiri wa vyama vya siasa. Kwa kuwa CHADEMA wamedhamiria kufanya siasa za kweli na siyo za kuganga njaa ni dhahiri hawawezi kufanya siasa na mamluki. Wote mnakumbuka jinsi ambavyo Mbatia na NCCR- Magauni yake alivyowahi kuwawekea pingamizi wagomea wa CUF kisiwani Pemba wakati chama chake kikiwa hakina hata tawi kisiwani humo. Pia naamini wana ukumbi bado hamjasahau Mrema alivyosambaratisha kwa ustadi mkubwa NCCR. Sasa mabo yote hayo hayakutokea kwa bahati mbaya ni mambo ambayo yalipangwa vizuri kitaalamu kabisa kwa lengo la kuinufaisha CCM. Nawasihi CHADEMA wasirudi nyuma katika hili kwani hao TLP,NCCR ni matawi ya CCM. Tunaweza kujiuliza hivi Mrema na Mbatia wanaishije mjini bila ajira wala biashara yoyote, ukipata jibu utajua ni kwanini ni muhimu kwa CHADEMA kujiepusha na watu hao. Mrema anaogopa sana endapo wananchi wa Mbeya wataitikia wito wa CHADEMA wa kususia uchaguzi kwani anajua itasababisha mgombea wa CCM ashinde kwa kura chache.
 
Hiyo paper iliyoandikwa inaweza kuwa sehemu ya input na sio mpango mkakati wenyewe kwani haikidhi vigezo vya chini kabisa ili iweze kuitwa hivyo.

Nimepitia ukurasa wa mwanzo hadi mwisho siamini vijana kama Zitto au Mnyika hawajayaona mapungufu hayo ya kiufundi kama kukosekana kwa Strategic Objectives, SWOT/SWOC na Stakeholders analysis nikitaja machache tu.

Na kama upo mwingine, tunachoweza kukiona wengine ni harakati na matokeo ya utekelezaji wa mkakati huo. Matukio ya karibuni yameonyesha vinginevyo.

Otherwise, hicho kilichobandikwa kwenye website ya Chadema hauwezi kuwa mpango mkakati wa chama kinachokusudia kuongoza nchi.

NN


Mpango Mkakati kamili hauko kwenye website ya chama, huo ni muktasari tu wa maeneo ya juu kwa ajili ya umma wa wanachama. Mpango Mzima ni siri. Hara sisi kwenye mafunzo ya Zanzibar hatukupewa mpango mzima lakini nyaraka tuliyowepewa ilikuwa na SWOT, Objectives, Stakeholders na Targets za CHADEMA za mwaka 2010. Sasa hizi ni silaha za ushindi haziwezi kumwagwa hadharani wewe. Jiunge na CHADEMA utapata hayo kwenye vikao vya ndani.

Haya hebu tupe japo kwa ufupi Strategic Plan ya vyama vingine tulinganishe na CHADEMA.

Halafu mbona waliokupongeza wote ni wanaCCM tu waliojitambulisha humu JF? Inaelekea maoni yako yamewakuna sana wenzako eeehhhhh

Asha
 
Back
Top Bottom