Kwa wale ambao hamkusoma vizuri, please soma tena hii hizi points muhimu, wana-JF tusilaze damu jamani tunahitaji kwauajua hao waliotajwa kupewa mgawo ni kina nani? Waandishi waliomegewa ni kina nani? Halafu tizama wakurugenzi wa hiyo kampuni waliokuwa na idhini ya kuidhinisha malipo ya kampuni, wazee kazi ndio kwanza imeanza mpaka kileweke hapo:-
In the meantime, ni vyema Waziri Chenge, akajiuzulu badala ya kuendelea kumpa mzigo mzito rais wa jamhuri wa kujibu maswali yake kila kona, ili pia atupe nafasi taifa turudi kwenye kujadili mambo muhimu kwa taifa letu!
1. WAZIRI wa Miundombinu, Andrew Chenge anaogelea katika utajiri wa zaidi ya Sh. 25 bilioni zenye utata huku Rais Jakaya Kikwete akiendelea kumkumbatia,
2. Chenge amekuwa mfanyakazi serikalini kwa karibu miaka 30 na hafahamiki kuwa mfanyabiashara. Kiwango kinachotajwa ni pamoja na fedha zilizogunduliwa na makachero wa Uingereza katika akaunti zake za nchi za nje.
3. Fedha zilizoko kwenye akaunti yake ya nchini, Na. 011101006950 katika benki ya NBC Limited, ni Sh. 25,794,805.89 za Tanzania hadi Ijumaa iliyopita, tarehe 11 Aprili 2008.
4. Katika akaunti yake ya Uswisi, ambako ana akaunti ya fedha za kigeni, Chenge amehamishia dola za Marekani 467,000, sawa na zaidi ya nusu bilioni kwa fedha za Tanzania.
5. Chenge ni Mkurugenzi wa kampuni ya TANGOLD Limited ambayo ina dola 12,997,950.84 sawa na Sh. 15 bilioni za Tanzania katika NBC Limited tawi la Makao Makuu.
6. makachero wa Uingereza wanafuatilia uhalali wa Euro 3 milioni (sawa na zaidi ya Sh. 8 bilioni za Tanzania) Chenge alizipeleka kwenye akaunti zake nje ya nchi.
7. Chenge alihamisha kwa mkupuo dola 600,000 za Marekani kwenda kwenye akaunti ya ofisa mwandamizi mmoja aliyekuwa Benki Kuu miaka kadhaa iliyopita, na ambaye kwa sasa anaongoza shirika la umma nchini.
8. Wakurugenzi na waidhinishaji malipo wengine wa kampuni hiyo ni, Daudi Ballali, Gray Mgonja, Vincent Mrisho na Patrick Rutabanzibwa.
9. Kutoka kwenye akaunti ya binafsi ya Chenge, mamilioni ya shilingi yamelipwa kwa watu mbalimbali wakiwa ni pamoja na Janet Mashale, Mary Nchimbi, Mary Chitanda na Livingstone Ruhere. Wengine ni Getrude Mtiga, Hawa Kiama, Leocardia Kalumuna, Athumani Sheha na David Sanga.
10. Miongoni mwa waliolipwa ni viongozi wa CCM, waandishi wa habari na wengine. Muhimu ni kwamba karibu fedha hizo zote zililipwa wakati uchaguzi wa CCM mwaka jana ambapo Chenge aliwania ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC). Alishinda kwa kura nyingi.