The Radar Scandal: Investigation & Progress

hahaha lazima dola milioni moja aite vijisenti!
pia ameviita vijisenti kwa kuwa anajua kuwa katika serikali ya ccm yeye sie anaeongoza kwa pesa za ufisadi.
kikwete mwenye fisadi, na angekuwa si fisadi asingewakingia kifua mafisadi wa namna hii
 
hahaha lazima dola milioni moja aite vijisenti! pia ameviita vijisenti kwa kuwa anajua kuwa katika serikali ya ccm yeye sie anaeongoza kwa pesa za ufisadi.
kikwete mwenye fisadi, na angekuwa si fisadi asingewakingia kifua mafisadi wa namna hii

Kabisa man!
Kama anamiliki bilioni zaidi ya 25 lazima hio moja iwe vijisenti.
Bado najisikia kupigana.
 
Did you believe katika ari, nguvu & kasi mpya? Just hopes and dreams .......
Chenge will definetly go, but how? Resign? Be sacked? Lets wait and see.

Mkuu wa kaya is definitely going to ask AC to step down akigoma naamini atam-sack tu. Kwanza atamwambia apime uzito wa tuhuma halafu ajiuzulu, akishindwa kujiuzulu atamtimua tu. Siku hiyo nanunua Champagine na kusherehekea. Hivi wana JF, kwa nini Mkuu wa Kaya anang'anga'nia kumtenga Magufuli asichukue Wizara ya Miundo Mbinu where we know Magufuli he can at least show results as compared to this AC aka VIJISENTI aka Fisadi(tukiweka kando dhambi ya Magufuli ya kumsikiliza BMW na kuuza nyumba za serikali bila kutoa protest yoyote)?? Naomba aliye na jibu anitoe vumbi kwenye macho.
 
hahaha jamani msimzoze sana chenge, kwa kwe yeye ni vijisenti tu japo kuwa vinaweza kufanya yote hayo alotaja mkjj. yeye kwake ni vijisenti tu manake ana bilioni nyingi sana nyengine kapuni
 
Mkuu Jf Hii Habari Ya Visenti(mijisenti)ya Ac Hakika Unaweza Kudhani Ni Riwaya Lakini Inataka Moyo Wa Mwehu Kuisoma Otherwise Unaweza Kupata Presha.kaaazi Kwelikweli Tz Hii.
 
ukistaabu ya mussa utayaona ya firauni, just go through this SMART text and see how our beloved country inavyotafunwa


By The Citizen Reporter

As allegations of grand corruption continue to rock the nation, with some prominent politicians and government officials suspected of having billions in foreign bank accounts, it has emerged that such transactions contravene BoT financial regulations.

Central Bank officials yesterday confirmed to The Citizen that for any Tanzanian to hold an overseas bank accounts, he or she must be given that authorisation by the Governor of the Bank of Tanzania (BoT).

Debate on whether or not Tanzanians can operate overseas bank accounts has been sparked by revelations in the UK's Guardian newspaper that Insfrastructure minister Andrew Chenge was found by British investigators to have $1 million (Sh1.2 billion) in an offshore account in Jersey.

The embattled minister, who returned home on Wednesday, from Beijing, vowed to fight the mounting corruption allegations against him, and declared that he would not quit his position as investigations were still going on.

Mr Chenge admitted that he was being investigated over allegations that he and some government officials had received bribes from a UK company, BAE System, to influence a Sh50 billion deal to sell a radar system to Tanzania.

Asked by reporters whether he has billions in a foreign account, the Harvard University-trained lawyer, who served as the Attorney-General until 2005, when quit to join politics, said: ?I, too, want to know the truth about these grave allegations?I hope that this investigation will reveal the truth.

His bank records, he said, would prove that "there is no connection to the BAE's Tanzanian radar deal".

According to The Guardian, Mr Chenge does not dispute the money in his Jersey accounts, but said, ?The obvious inference (of the investigation) is that I have received for my benefit ?corrupt payments? from BAE. This is untrue.?

Yesterday, a source told The Citizen that in 1998, BoT issued a circular, stating clearly that no Tanzania is allowed to hold an overseas bank account while residing in Tanzania.

The circular titled, ?Foreign Exchange Secular No 6000/DEM/EX.REG/58 of 1998 states: ?It should be noted that operation of offshore accounts by residents is prohibited.?

The circular made available to The Citizen says that to operate an offshore account, one must seek permission from the BoT Governor.

The Citizen established that for BoT to issue such special permission, the bank must satisfy itself that the applicant has "clean money, obtained through legal channels".

The statement adds: ?It should be noted that portfolio investment, foreign lending operation in favour of non residents or acquisition of real estates, upward direct investments are subject to restrictions.?

Asked whether the circular was still in use, the BoT deputy governor responsible for Foreign Exchange and Foreign Banking, Mr Juma Reli, confirmed that the order was still in force.

?This circular is still valid and operational,? Mr Reli told The Citizen by telephone. Besides holding offshore accounts, some top former and current government leaders are said to own posh homes abroad, especially in South Africa, Dubai, the United Kingdom, the US and Switzerland.

Some of the huge scandals that have caused a public uproar lately, include construction of $400 million BoT Twin Towers, the Sh133 billion EPA account rip-off, the 28 million pound sterling radar purchase from UK?s BAE company, and $172.9 million emergency power supply contract awarded to Richmond Development Company. Early this month, Switzerland offered to help Tanzania recover any EPA money that may have been deposited in that country.

Swiss Ambassador Adrian Schlaepfer was quoted by the media in Dar es Salaam recently as saying his country "was committed to working closely with Tanzania on the issue".

So far, the special team investigating the EPA scandal is said to have recovered more than Sh60 billion, of the Sh133 billion, believed to have been swindled by 22 companies. According to Finance minister Mustapha Mkulo, the culprits in the BoT scandal have returned to the Government more than Sh60 billion.

The target, Mr Mkullo said, was to recover by June at least 70 per cent of the illegal payments made in the 2005/06 financial year.

Speaking on Wednesday at Julius Nyerere International Airport in Dar es Salaam on his return from Beijing, Mr Chenge promised to co-operate fully with local and UK sleuths investigating whether the $1 million found in his account was in any way linked to $12 million kickback paid to runaway businessman Sailesh Vithlani in the Sh70 radar deal.

The Bariadi MP denied any wrongdoing, insisting that "I am clean, and as a citizen of this country I have the right to be heard".
 
kwa kweli naona hata mie tutakuwa wenda wazimu, lakini kama alivyandika mwenzetu hapo juu, dola la tanzania ndo linatarajia kuanguka kwa kuwa limekuwa jeuri machoni mwa Mungu, kamwe MUNGU hatakubali jeuri za wezi mbele pa machoni mwake, kila senti iliyoporwa wanyonge wanaotaabika kote nchini sasa itahesabika na kuwarudia walala hoi hao.kitanzi kinawasubiri kwa hamu mafisadi hawa
 
unajua nashindwa kuamini kama hiki ninachokisoma sahihi au naota!
siamini hali ni hii roho inauma sana lakin je ni chenge peke yake?
nini kifanyike kurekebisha hali hii?
ni bora vijisenti hivi vingekaa kwenye vijibanki vyetu tungeweza nauhakia vingerekebisha maisha ya watu
hebu fikiria vijisenti hivyo vingekopeshwa kwa wajasilimia mali wadogo wadogo kwa kiasi cha shs 1000000 kila mmoja kwa riba ya asilimia mbili kwa mwezi in reducing rate zingezungushwa kwa watu wangapi
tusiwe wapumbafu we should do some thing
 
Yna mwisho haya, tena mwisho wao hawa mafisadi wala hauko mbali. Nina imani ipo siku tutawapeleka pale mnazi mmoja, mchana wa jua kali, tuwapige mawe mpaka wafe.
 
Dah!! kweli bilioni moja ni vijisenti babake..ila uyu kubenea sasa naona kashakata tamaa ya maisha....watamficha sasa ivi uyu..System bana!!!
 
hivi kwanini tunamtaka ajiuzuru? ili apate heshima? tumshinikize mkuu wake aliyemchagua amfukuze kwasababu that is what he deserve an lot more, mi ningekuwa na uwezo ninge organize mgomo wa nchi nzima, ah lakini who am i kidding, zimbabwe wenyewe wako kwenye very desparate situation mgomo haujafanikiwa itakuwa hapa!
 
Wao wenyewe wana skendo zao zinasubiri zinatafuta jinsi ya kutoka halkafu wajamp kwenye skendo ya mtu mwingine. Hii issue kama ingekuwa ya mtu mdogo wangekuwa wameshamkamata. Sijui Prof. Mahalu anajisikiaje sasa baada ya kupata mwenzie.


The thing here is like bongo artist ( kila mmoja anajitahidi kutoa singo yake ) tunangoja singo za wengine then tuone ya nani ime hit sana. Kwa sasa hakuna singo kama Anita feat Lady Jay Dee hii naifananisha na CHENGE.
 
Jamani, kwa wenye kujua mambo hebu tuambieni hawa waliopata faraja ya mshiko toka kwa paymaster general ni kina nani hawa, kwa nini wao, je kulikoni?


Kutoka kwenye akaunti ya binafsi ya Chenge, mamilioni ya shilingi yamelipwa kwa watu mbalimbali wakiwa ni pamoja na Janet Mashale, Mary Nchimbi, Mary Chitanda na Livingstone Ruhere.

Wengine ni Getrude Mtiga, Hawa Kiama, Leocardia Kalumuna, Athumani Sheha na David Sanga.
 
Tunangojea tuone Mramba anangapi pengine ndio maana AC akasema ile 1 mil $ vijisent pengine kina Mramba waliramba pesa nzuri kwenye dili ya Rada na Ndege ya Rais. si mnakumbuka ilibidi tule nyasi Rais anunuliwe ndege? au mmesahau? Maana wabongo kwa kusahau wamevunja rekodi.
 
Dah!! kweli bilioni moja ni vijisenti babake..ila uyu kubenea sasa naona kashakata tamaa ya maisha....watamficha sasa ivi uyu..System bana!!!

Kubenea ana moyo mgumu kama wa mwendawazimu vile.....Yaani he is the real guy who dares to talk openly, in a day light.

Tunahitaji vichwa vingine kama yeye kama 10 hivi nchi hii mambo yanaweza angalau kunyooka.

Mungu amlinde na kumbariki sana.
 
lets take action basi, tukilalamika sana watatuzoea itakuwa makelele ya chura hayamzuii tembo kunywa maji, tuanze kupanga mkakati sasa.
 
Na Mbasha Asenga
YAPO mambo mengi aliyozushiwa Andrew Chenge, Waziri wa Miundombinu ambayo mengi watu waliyaona kama mambo ya mtaani tu. Kwa mfano, niliwahi kusikia Chenge alikuwa akisafirisha suti zake kwa DHL kwenda London, Uingereza kufuliwa.

Hii ilikuwa wakati akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akiamini Tanzania kulikuwa hakuna kampuni ya kueleweka ya ufuaji nguo.

Lakini pia lipo jingine la kilimbukeni alihusishwa nalo; kila alipokuwa akisalimiana na watu alitafuta upenyo na kwenda kunawa mikono yake na kupaka mafuta laini.

Chenge alipata kuhusishwa na ukiukaji wa misingi ya utendaji, alipokuwa kiongozi wa Salander Bridge Club. Inadaiwa baada ya kushindwa kwa muda mrefu kuitisha mkutano wa wanachama, baadhi ya wanachama waliamua kujiorodhesha ili kushinikiza mkutano uitishwe.

Wakati orodha hiyo ikiwa ukutani na watu wengine wakihamasishwa kujiandikisha ili kumlazimisha bwana mkubwa kuitisha mkutano, Rais Ali Hassan Mwinyi alimteua Chenge kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Habari zinasema kutokana na unafiki wa Kitanzania, orodha ile ilipotea kitatanishi. Hakukuwa tena na shinikizo la kumtaka aitishe mkutano kwa sababu si tu kwamba ujasiri wa wanachama ulikuwa umeyeyushwa na madaraka mapya aliyopewa, bali sasa wengine walianza kukaa mkao wa kupata lolote kutoka kwake.

Hayo ni simulizi. Haya yanayofuatia, nina uhakika nayo maana niliyashuhudia. Kwamba Chenge amejaa kiburi si jambo la kuuliza! Ni kiburi kikubwa kwani aliwahi kukionyesha kwa wabunge kati ya 1995-2005 akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Nitaeleza machache.

Baada ya Bunge kupitisha sheria ya kuvunjwa iliyokuwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na kuundwa NBC 1997 Limited na National Microfinance Bank (NMB) mwaka 1997, pamoja na kuanzishwa kwa kampuni tanzu ya NBC Hodings Limited ili kusimamia mali za iliokuwa NBC ambazo hazikugawiwa kwa NBC 1997 wala NMB, ofisi ya Mwanasheria Mkuu ilicheza faulo.

Faulo hiyo ni kutunga sheria kinyemela kwa kuiondoa iliyokuwa National Bureau De Change kutoka NBC Holdings ili ionekane kama ni taasisi inayojitegemea.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ilijipa jukumu la kupora Bureau kinyemela bila shaka, ili kujinufaisha katika harakati za kupora mali za umma zilizopamba moto wakati wa utawala wa Benjamin Mkapa. Wabunge makini akiwamo Philip Magani, wakati huo akiwa ndiye Mwenyekiti wa Bodi ya NBC, na Arcardo Ntagazwa, walishtukia suala hilo na kuwasha moto mkali bungeni.

Baada ya Bunge kuchunguza suala hilo, ilithibitika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliingilia kazi za Bunge kwa kurekebisha sheria bila ya kuifikisha bungeni, ikilenga kupora Bureau hiyo iliyokuja baadaye kuwa Twiga Bankcorp. Wabunge walichachamaa wakitaka maelezo ya serikali.

Nakumbuka Waziri Mkuu wakati huo, Frederick Sumaye, alisimama na kuomba radhi kwa niaba ya serikali kuhusu ukiukwaji mkubwa wa taratibu uliotokea na kuahidi kurekebisha kasoro hiyo. Sumaye alikuwa muungwana ambaye kwa mara ya kwanza katika kipindi cha utawala wake nilimuona akiwa mkweli kwa alilokuwa akilisema.

Lakini pamoja na hatua ya Sumaye, Chenge aliibuka. Akasema, “kiti cha Mwanasheria Mkuu wa Serikali kimejaa!” Kebehi iliyoje dhidi ya wabunge pamoja na Waziri Mkuu aliyekuwa ameshasawazisha kasoro.

Kiburi cha Chenge kilijidhihirisha jinsi asivyoheshimu Bunge, wabunge na hata Waziri Mkuu amabye ndiye kiongozi wa shughuli za serikali bungeni.

Katika hali ya kawaida, Sumaye alikuwa na kazi moja tu, kumwomba Rais amuondoe Chenge kwenye wadhifa kwa kuwa alikuwa anafanya kazi yake kuwa ngumu. Hili halikufanyika, Chenge akaendelea kutesa hadi bwana mkubwa Mkapa alipomaliza kipindi chake Novemba 2005.

Baada ya kusikia hivi karibuni Chenge anachunguzwa kwa ukwasi aliojiwekea kwenye kisiwa cha Jersey, Uingereza akiwa na zaidi ya dola milioni moja za Marekani, kwenye akaunti yake, nimeanza kujua kiburi cha ofisa huyu kinakotoka!

Ni kiburi cha mtu aliyeshiba na kuvimbiwa, na unajua ukivimbiwa kuna uwezekano mkubwa wa kuharibu hali ya hewa. Chenge hakumtii Sumaye wala wabunge wa chama chake. Hakuwa na sababu za kuwatii maana yeye na bwana mkubwa walikuwa wanaruka mruko mmoja wa ndege wenye mabawa (manyoya) ya kufanana.

Bwana mkubwa Mkapa naye ukwasi wake haramu umekuwa ni mapambo kwenye magazeti ya Tanzania kwa zaidi ya mwaka sasa. Yeye (Mkapa) ameamua kukaa kimya. Kiburi kile kile cha swahiba wake. Kiburi cha ukwasi, cha kupumua, cha shibe, shibe iliyomlevya kiasi cha kushindwa kujua yeye ni Mtanzania na kwamba kujilimbizia fedha nyingi kiasi hicho ughaibuni ni usaliti kwa nchi masikini kama Tanzania.

Chenge alipochaguliwa kuwa waziri na Rais Jakaya Kikwete Januari 2006, watu walijiumauma na kuuliza, inakuwaje Kikwete ampe uwaziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Chenge wakati zikiwapo tuhuma nyingi mitaani za uchafu unaomgusa.

Mikataba kama ya IPTL, uuzaji wa NBC iliyotolewa kwa Makaburu wa ABSA sawa na bure! Watu waliguna lakini Rais Kikwete naye si tu alipuuza miguno yao, aliwazaba kibao wananchi mwaka jana alipofanya marekebisho madogo katika baraza lake la mawaziri kutokana na kuchemka kwa sakata la Richmond. Chenge aliondolewa Afrika Mashariki na kupelekwa Miundombinu, wizara nyeti na yenye kazi kubwa ya kujenga barabara ambazo ni kilio cha kudumu kwa wananchi na wawekezaji.

Hakuishia hapo tu. Alipolazimika kuvunja baraza la mawaziri ya Edward Lowassa na mawaziri wawili wengine kujiuzulu, kutokana na sakata lilelile la Richmond, Rais Kikwete alimrejesha Chenge pale pale miundombinu katika baraza jipya! Miguno mipya ikaendelea kuzizima.

Sasa Waingereza wametusaidia kumweka hadharani Chenge kuhusu namna alivyopata ukwasi mkubwa. Shaka iliopo si ya kwamba amepataje ukwasi huo, bali pia kwa kuwapo uwezekano wa kuhusiana na mabilioni ya rada iliyouziwa Tanzania kwa bei ya juu na Waingereza haohao wa kampuni ya BAE Systems.

Chenge yuleyule wa kusafirisha suti kwa DHL kwenda kufuliwa Uingereza, hadi kuogopa kuchafuliwa mikono kwa sababu ya kusalimiana mpaka kwa Chenge wa kiburi kwa Waziri Mkuu na wabunge, ni Chenge huyohuyo wa kumiliki ukwasi wa kutosha kula hadi aingie kaburini.

Haya yote yakitokea, Chenge anawajibika kueleza umma alivyopata ukwasi huu. Ni vema akatambua kuwa wakati umefika wa kuwa muungwana na kutambua kuwa ulevi wa ukwasi unaompa kiburi hautamsaidia kitu. Angeamua tu kuachia ofisi ya umma akaendelea na yake. Chenga na kiburi, safari hii havitamponya!


Source: MwanaHalisi
 
What more do you folks expect? Tanzania may be a stable "state" but the truth is Tanzania remains a very WEAK state ("weaker than clock radio speakers" as GZA would have put it) even after almost 50 years of political independence.

Whats worse, people like Chenge, Lowassa, Balali, Mkapa et al are by all conceivable measures "the state". Looting, plunder, and pillage of national resources is a matter of course for Big Men of their stature without any legal, political or economic consequences.
 
Kutamka vijisenti,ameudhalilisha sana utu wetu umma wa watanzania.

Hongera watu wa Dom kwa mshikamano mlioanza tayari kumtoa huyu nyoka AC pangoni.
 
Nadhani jinalake ni baab kubwa kama lingekua Andrew 'Billionea' Chenge.

Manake amewezxa kuita bilioni moja vijisenti kweli majina mengine hayamfai huyu ni 'The Billz'

Kibri kitakwisha tu halafu wazalendo wenzangu huko Dodoma wanahakikisha hatingi Bungeni yaani pale alipokula kiapo cha uaminifu
 
Back
Top Bottom