The Radar Scandal: Investigation & Progress



Maneno yake ya kushitaki vyombo vya habari hayana tofauti na yale ya Boss wake kudai atashitaki kisa wamesema kachukua pesa Iran za Uchaguzi .Hivi ile nayo imeishia wapi vile ? Je huyu Masha na matisho yake ya hivi majuzi kesi kesha fungua ?
 
Ndugu yangu TUAMNDAMANE pole sana kwa uchungu ulionao. Naona mheshimiwa sana INVISIBLE tayari ameweka maoni yako kapuni. Ila naungana nawe kwa hasira na uchungu kwa nchi yetu inavyovurugwa na hawa "WAJANJA" wachache wanaojiita VIONGOZI. Na kwa mtaji huu nadhani hasira za wengi zitafikia kufikiria kufanya yale yaliyo sawa na wanayofanya raia wenye hasira kwenye mitaa ya DAR wanapomkamata kibaka - kumfunga tairi na kumpiga moto. Naombea tusifike hapo, lakini i'm sorry to say that we are heading for that sad but swift street justice.
 
Mkuu Halisi,

Huyu Chenge Mwizi, karudi mwenyewe au karudishwa? Nilitegemea angeelekea USA na muungwana.

Kweli sasa tumemfunga paka kengere, hivi alikuwa na nguvu hata ya kuwaangalia Watanzania usoni?


Lunyungu yuko US na msafara wa Rais kanitonya kwamba the guy has been sent back baada ya kuona mambo yamewaka .JK kasema kawajibu nikija kuwe kumetulia na si zaidi ya hapo .
 
Binafsi naelewa sana kuwa mambo haya yanaudhi mno! Inafikia hatua mtu unatamani kutukana lakini lazima tutambue kuwa maandishi hufunga... Think of it buddy. Pandisha munkari na bamiza keyboard kwa nguvu zote lakini jaribu kukumbuka kuwa maandishi hayo yataendelea kuwepo hata baada ya hasira yako kupoa. Ni suala la muda... Inakera, inaudhi, inatia uchungu, inasababisha hasira sana...
 
Bilioni moja zinaitwa vijisenti....
Nina wasiwasi na akili na huyu AC...is he mentally ok? I am in a big doubt.
USIWE NA WASIWASI NA AKILI YA JAMAA IS CLEARY IN SHOCK, HE WAS NOT EXPECTING THIS HIYO QUOTE BELOW INATOKA GAZETI LA MWANANCHI
 
CHENGE CHENGE NGE EEH! Tunakulilia wenye nchi! rejesha HAZINA zetu na uwape taarifa wenzako kuwa tuko nao! "List of shame" na orodha nyingine zitaibuka na kuleta mabadiliko ambayo yalikuwa hayafikiriki siku za nyuma!

JF Oyee eh!
 

Kwanza asnte sana mkuu hawa jamaa wanatupeleka huko street justice kama hakuna aneongea, kilakitu wanabisha kuwa hawajafanya, mkapa kanyamaza tuu watu hawakamatwi wakajibu mashtaka etini bora warudishe hela, watu watakapo chukua sheria mkononi watawashangaa kweli??? najua maandishi hufunga lkn ukweli unabaki palepale kwa mwendo ni wao wenyewe wanatulazimisha tuongee kwa vitendo
 
Maneno yake ya kushitaki vyombo vya habari hayana tofauti na yale ya Boss wake kudai atashitaki kisa wamesema kachukua pesa Iran za Uchaguzi .Hivi ile nayo imeishia wapi vile ? Je huyu Masha na matisho yake ya hivi majuzi kesi kesha fungua ?

Na Nchimbi nae kasha shitaki tanzania daima?
 
Jamni hapa sidhani kama Chenge atakuwa na kesi wala nini

(source ThisDay April 17 08)

It has been reported that Chenge’s local legal representative in the matter is Dar es Salaam lawyer Joseph Mbuna, who incidentally is also the father-in-law of Nicholas Mkapa (the son of ex-president Mkapa) and chairman of the board of directors of Kiwira Coal and Power Company Limited.

The formerly state-owned coal mine was sold in 2005 under dubious circumstances to Tanpower Resources Limited, a private company jointly owned by the Mkapa family, former energy and minerals minister Daniel Yona, Mbuna himself, and other closely-connected shareholders.

At the same time, there are reports that Nicholas Mkapa is currently in the employ of the Director of Public Prosecutions (DPP) office - a fact that again raises fears that he may interfere in a potentially-pending prosecution of high-profile individuals linked to the dubious privatization of the lucrative Kiwira mine.

Investigations by THISDAY have established that although Chenge may have not been directly involved in the negotiations with Britain’s arms manufacturer BAE Systems for purchase of the radar, he did give crucial legal advice to the Tanzanian government in favour of the deal.
 
ok, kuna chenge, then who next?
Tunataka sasa mwingine mpyaaaaa!! hebu pekueni huko kwenye kumbukumbu zenu najua mafisadi wako wengi, tuwafichue wote halafu tuanze upya na mafisadi wachanga. (samahani just joking)

NOT FUNNY,ESPECIALLY ON AN EMPTY STOMACH,EVEN IF YOUR POCKETS ARE FULL LIKE THOSE OF THE MAFISADI.
 
Kumbukeni kuwa huyu Chenge ndio mwenyekiti wa kamati ya maadili ya CCM.

Kama mwizi huyu anaweza kupewa nafasi ya kwenda kuangalia maadili ya wenzake ndani ya chama na kuyakemea hivi hapo kuna chama kweli?

Kwa moyo wa dhati kabisa nawaomba wana CCM waliopo hapa wawe wa kwanza kuhoji na hata kumtaka walau aondoke kwenye kamati ya maadili kama mwenyekiti na hata mjumbe kwa masilahi ya taifa.

Nchi hii kuna siku inaweza kulipuka kwenye list yetu ya mafisdadi tunaona timu inapungua kila siu hivyo huienda tukaweka wachezaji wa ziada kama 7 hivi karibuni stay tuned.

Pia tumeweza kumpata kocha msaidizi wa first 11 yetu hivyo huenda tukawa tunashinda kila wakati na kila mechi.
 
tanzania ufisadi hauwezi kwisha yalianza zamani sana lakini hii ya AC inatia aibu kwani inaonyesha ni namna gani watanzania wakikabidhiwa madaraka wanavyotumia vibaya, AC inatakikana kama kweli huu ufisadi kaufanya na afilisiwe

Zungu, tunachokiona hapa ni tip of an iceberg, tumejua ya chenge sbb imetoka UK laiti kama wote wangechunguzwa na kujulikana (which ndocho kifuatacho) kwa mtindo huu hii nchi hapata kalika, I just give u a year hatutakuwepo hapa tulipo maana mengi tutakuwa tumeshayaju
 
Kumbukeni kuwa huyu Chenge ndio mwenyekiti wa kamati ya maadili ya CCM.

Kama mwizi huyu anaweza kupewa nafasi ya kwenda kuangalia maadili ya wenzake ndani ya chama na kuyakemea hivi hapo kuna chama kweli?

Kwa moyo wa dhati kabisa nawaomba wana CCM waliopo hapa wawe wa kwanza kuhoji na hata kumtaka walau aondoke kwenye kamati ya maadili kama mwenyekiti na hata mjumbe kwa masilahi ya taifa.

Nchi hii kuna siku inaweza kulipuka kwenye list yetu ya mafisdadi tunaona timu inapungua kila siu hivyo huienda tukaweka wachezaji wa ziada kama 7 hivi karibuni stay tuned.

Pia tumeweza kumpata kocha msaidizi wa first 11 yetu hivyo huenda tukawa tunashinda kila wakati na kila mechi.
 

NN
Hivi hujui kwa sasa tuko DUNIA YA NNE?!. Maana hataile third world tumeachwa.
 
Haya Bwana...."Andrew John Chenge is Tanzanian politician and a Member of Parliament in the National Assembly of Tanzania. After serving as Attorney-General, he was appointed as Minister of East African Affairs in the Cabinet named on January 4, 2006. He was then appointed as Minister of Infrastructure on October 15, 2006,retaining that post in the Cabinet named on February 12, 2008"

...Kwamba alikuwa mtumishi wa Serikali tangu wakati wa Azimio la Arusha...kwa hiyo vijisent alivyonavyo..kama anavyoviita" ameanza kuvikusanya wakati gani?..wakati wa Ruksa ama wakati wa Uwazi na Ukweli? ...muda wa kufanya biashara ulikuwa saa ngapi na wakuitumikia Serikali ni Saa ngapi..labda ni traveling allowances...kwenu wafuatiliaji wa Account!
 
Kwa kusema hizo hela ni vijisent inaonyesha ni kiasi gani kazoea kuiba na hiasi hicho cha pesa ni sehemu ndogo sana yamapesa aliyonayo. kama kweli hizo hela si za maajabu hebu we chenge niambie kwann uzipeleke kuzihifadhi mbali huko badala ya hapa home zizunguke kujenga nchi kuna mkuna mabenk mengi tuu hapa?
 
Huyu jamaa ana dharau sana yaani nimesoma mahojiano yake na waandishi, billioni moja anaziita "visent"? yaani mi simpatii picha,
 
Chenge kufuru tupu, amiliki bilioni 25

*Amchotea kigogo bilioni moja
*Amwashia indiketa Ben Mkapa


Na Saed Kubenea



Follow the money....source http://www.halihalisi.co.tz/08/04/16/
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…