The Radar Scandal: Investigation & Progress

The Radar Scandal: Investigation & Progress

Halafu unaambiwa hilo ni deal moja tu! bado kuna deal kibao ambazo hatujazifahamu! kweli wajinga ndio waliwao! hapo bado hujajua madeal ya Mramba,Mkapa,Sumaye,Karamagi,Rostam Aziz,Lowasa na wengineo!..ndiyo maana hawa watu huwa wanakiburi sana kumbe ni kwa sababu ya mimali waliyojilimbikizia.

Halafu na Rais Kikwete bado hajui ni kwanini nchi yetu ni masikini?

-Wembe

JF hipo hapa kumwambia ukweli JK maana anajiuliza maswali ambayo majibu yake anajua, kwanini nchi ni masikini wakati mawaziri wake na watangulizi wake anaosema waachwe wapumzike wamejirundikia mimali kibao wakati watanzania wanakufa na njaa.
 
Kama Tanzania ni nchi inayoomba omba mpaka Rais wetu kila Siku yuko kwenye Nchi za watu anaemea inakuwaje kumbe tu matajiri mpaka Milioni za dola ya USA tunayaita vijisenti?

Chenge anataka kutwambia nini hapa? Kumbe ndo alivyo na kiburi



Itabidi bajeti ya mwaka huu hayo mapesa Chenge aliyoyaiba yaingizwe kwenye bajeti kwa vile wafadhili wanaelekea kugoma kucontribute
 
Jamani msing'oane meno bure. Habari mpya nilizozipata hapa ni kwamba kumbe hizo hela za Chenge ni dola za Zimbabwe. Du, tuendeleeni na mijadala mingine tuachane na hivi vijisenti vya chenge.


Kwi kwi kwi, Nuru unajaribu kushusha pressure za watanzania kwa kuwaliza kihivyo eeh
 
Wale wanyama wakubwa wa Kale Dinosaurus walitoweka wote.

Dinosaurus walitoweka sababu mojawapo ikiwa ukubwa wa matumbo yao na miili, haikuwa rahisi kwao kukwepa aina yeyote ya kimbunga.

Tabia ya wanyama hawa wakubwa ilikuwa ni kula kula kula, kama walikuwa wakipumzika kidogo basi walikuwa wakienda Msalani, baada ya hapo ni kula ni kula tu.

Kwa sababu ya ukubwa wa maumbo yao na vishindo vyao, walidhani hawana maadui. Kwa mtaji huo waliendekeza kula kuliko kuandaa plan itakayo wasaidia wakati wa dharura.


Ukubwa wa matumbo yao,
Ukubwa wa umbo lao na,
Kushindwa kuwa na Emergency plan,
ni moja kati ya vitu vilivyowaangamiza milele Dinosaurus.

Mijitu kaa Chenge ni MiDinosaurus.

Inakula inakula inakula inapumzika tu kama iko chooni kunya au kuharisha kwa kuvimbiwa.

Inajivunia ukubwa, ukubwa ambao hivi punde utakuwa chanzo cha maangamizo yao.

Ukimya wa mijitu kaa Chenge si Busara, ni kibri chenye dharau hata kwa wajomba zake kule Usukumani.

Mijitu kaa Chenge Haina plan ya leo wala kesho plan yao kubwa ni kula kula kula na kunya kunya kunya tu.


sishabikii wizi wala sina simile nao.
Lakini nasema hivi,angeiba mtu mwenye akili isiyofanana na ya Dinosaurus wizi wake pengine ungewafaa wengine.

Billioni 20 nifedha ambayo ingetosha kuanzisha utitiri wa viwanda vya kusindika vyakula aina zote na togwa aina zote kutoka katika matunda kibao nchini Tanzania.

Aidha Fedha hizo zingeweza kuleta ajira kubwa kwa watanzania walio wengi.
Kuiba na kuiacha fedha ikigaagaa kwenye account za watu walioshiba huko Ulaya ni Dalili moja ya Udinosaurus.

Mimi nadhani Aina ya Ubongo walio kuwa nao wale wanyama wakubwa kwa umbo lakini duni wa mawazo bado unaendelea kujisimika katika vichwa vya watu kama Chenge.

Akina Chenge wako wengi sana,wengine kwa kuona hili so la Dinosaurus mwenzao limebumbuluka wako karibu kwenda haja ndogo kwenye kaptula zao.

Mtakoma kulinga.
 
Huuu....!!
Bila wahalifu police watakosa kazi!!...Bila kesi mahakimu Watakosa kazi...
Bila mafisadi!!!?............sijui

Nafikiri tuanze kutathimini haya mambo kwa logic!!Tusi jiachie sana!! kama kiongozi ana iba basi hata mimi mfuasi nitafanya hivyo!!

viongozi wangu!!
Im sorry



Bila mafisadi Tanzania ingekuwa DEVELOPED COUNTRY na sio AMONG THE MOST POOREST COUNTRY OF THE WORLD. Usiige matendo ya viongozi wako, fanya wajibu wako Mungu atakulipa na utakumbukwa kwa mema siku zote.
 
Shilingi bilioni moja na laki mbili kwa fisadi Chenge ni vijisenti sasa sijui hao waliopata mshiko mnono akina fisadi Mkapa, Mramba na wengineo wana balance kiasi gani katika bank accounts zao za nje.

Bubu:
Hapana, 1.2 bn, ni sh. billioni moja na million mia mbili' sio bilion na laki mbili!
 
Chenge Ni Mtu Gani!!!! Kaifanyia Nini Tanzania,hakuna Kumchunguza Mtu Kama Huyo,kwani Jina Lake Lilikuwa Serikalini Muda Mrefu,hakuna Hata Jambo Au Kazi Hata Moja Ya Maana Kalifanyia Taifa Hili!!!! Bora Kikwete Sasa Ateue Mawaziri Toka Upinzani Kidogo Tutakuwa Na Imani Na Yeye,tumechoka Na Scandal Za Serikali Yake,mawaziri Wote Wameoza Kwa Rushwa,je Wabunge Wake Cha Chake "ccm" Chukua Chako Mapema,nchi Inaelekea Wapi Hii,nani Atusaidie Kwa Yote Hayo,epa,richmond,kiwira.....tusali Sana Mungu Atufungulie Mengi,na Pesa Zetu Zirudishwe Haraka...
 
Itabidi bajeti ya mwaka huu hayo mapesa Chenge aliyoyaiba yaingizwe kwenye bajeti kwa vile wafadhili wanaelekea kugoma kucontribute

Hahahahh Chenge, Lowassa alisema tukiamua kufatilia hakuna mwanasiasa atakayepona na aliye msafi....Chenge amepitiwa na kimbunga, more are coming, RA, Mkapa, Yona, Mramba, Karamavi etc etc...
 
Hahahahh Chenge, Lowassa alisema tukiamua kufatilia hakuna mwanasiasa atakayepona na aliye msafi....Chenge amepitiwa na kimbunga, more are coming, RA, Mkapa, Yona, Mramba, Karamavi etc etc...

Acha wafuate wote, kwa kweli hakuna sababu ya kujikomba kwa wazungu kuwaomba watusaidie kutunisha bajeti yetu wakati uwezo tunao. Hawa mafisadi ndio wametufanya tuko omba omba na unajua ukiwa omba omba matokeo yake ni kudharualiwa na kusimangwa.

Sijui huwa wanajisikiaje wizara muhimu kama elimu, afya, kilimo n.k zinapopewa mafungu kiduchu wakati wenyewe wana mafedha ambayo yawaweza kujazia penye upungufu
 
Hahahahh Chenge, Lowassa alisema tukiamua kufatilia hakuna mwanasiasa atakayepona na aliye msafi....Chenge amepitiwa na kimbunga, more are coming, RA, Mkapa, Yona, Mramba, Karamavi etc etc...

Chenge Kesho hana haja ya kwenda ofisini inabidi akae ndani tu. Tanzania nchi aliyoiasisi Mwalimu bado ni nchi Masikini inatakiwa watu wenye uwezo wa kuitoa katika dimbwi la Umasikini. Mliona hata Ministers wa UK walichachamaa kuona pesa kama hiyo inamilikiwa na Mtu mmoja. Yeye anaona ni VIJisenti.

Tunahitaji Mtu aliye tayari kutumikia watanzania siyo Mtu ambaye ameisha ridhika wakati watanzania waliowengi hawawezi kula milo miwili kwa siku.

Mr. Chenge inatosha kama ni Uongozi aende akaongoze nchi za matajiri. Huo utajiri kwanza ametoa wapi kama siyo WIZI wa Rasilimali zetu?

Leo hii baada ya kutuibia na kutunisha mfuko anageuka na kujiona tajiri? Biashara gani anafanya WIZARANI?
 
Kwa hakika huyu nadhani ni mtu mzito sana kuliko hata alivyokuwa gavana wa benki kuu!!!

Aliyekuwa mwanasheria mkuu wa nchi kama kweli akijulikana bila shaka ametuibia... Then kama taifa tuna tatizo kubwa... maana kama ni ethics, kufuata sheria mwanasheria mkuu wa serikali ndiye angekuwa mtu wa kwanza kwa usafi immediate after head of the state... sasa kama yeye kweli atajulikana ametuibia... du kazi ipo...


Hapana, ni waTanzania 'wapumbavu' au 'Tanzania kuwa nchi ya wapumbavu' remember!
 
Mwanakijiji,

Fafanua maana nimetoka kapa hapo.

Naona Wazungu wamekosea, hizo milioni ni shilingi sio pounds au dola
kwi kwi kwi!!!!!

Si ajabu Chenge alikuwa analundika tu, alisahau ni dola na akadhani ni pesa za madafu.

mwaka jana katika kuendelea na harakati hizo nilitoa ahadi kadhaa kwa upande wangu kuhusu wale "watuzugao". Niliandika hivi katika Makala ya tarehe 19 Disemba:

Vinginevyo, mwaka ujao tutaendelea kuwakalia kooni kama nira na kama ndege wanavyotua juu ya wanyama malishoni ndivyo na sisi tutavyotua katika migongo yenu. Tutawadonoa kwahoja na kuwaparua hadi makupe na viroboto yaishe kati yenu. Kama mwaka huu mmetushinda kwa kuwarudisha vijana wetu toka Ukraine kusoma na kuwaacha Solemba, na mkatangaza ushindi, basi mwaka ujao ni zamu yetu! Tunawatangazia mapema kuwa kama mlifikiri Tanzania ni yenu peke yenu na sisi wengine ni wakimbizi tu na wahamiaji mjue kuwa wakati wa njozi yenu hiyo umefikia kikomo!

Unapokuja mwaka mpya, hatutakubali tena kuzugwa kwani kuzuga kwa miaka 46 iliyopita kumetosha na wananchi wanajiandaa kwa mwaka 2010! Mmepewa nafasi nyingi ya kusahihisha na kujisahihisha na mara zote mmekuwa na majibu na mikakati ya kizugaji. Watanzania wamechoka, na wakati waja na tena upo ambapo wataonesha uchovu wao kwenye sanduku la kura. Safari ya kuelekea huko ndiyo imeanza. Mtatuzuga tena? I don’t think so!

Na pia niliandika na kusema mwakani tutafuatilia akaunti zao siyo zile za Uswisi (ambako wengi wanafikiri wameziweka) lakini hata zile za Hapa US, na zile ambazo zimefichwa Cayman Islands na kwenye "offshores" accounts. Walidhani tunawatania.

Nakulilia na Mtanzania; nilichozungumzia ukiondoa hii ni suala la RA (kuna makala mbili ziko Mwanahalisi)...
 
Hawa walio leak data za Chenge ku-divert attention from Richmond na EPA wanadhani Mwanahalisi nalo halina data dhidi yao. Wamefungua Pandoras box, maana Chenge hataanguka mwenyewe hivi hivi, lazima afe na mtu. Sit back and enjoy the show.
 
Mzee Mwanakijiji;176063 Nakulilia na Mtanzania; nilichozungumzia ukiondoa hii ni suala la RA (kuna makala mbili ziko Mwanahalisi)...[/QUOTE said:
JF raha tupu maana magazeti yote yanakuja na habari ambazo tayari tumeshazipata hapa. JF always behind the news maker
 
Hawa walio leak data za Chenge ku-divert attention from Richmond na EPA wanadhani Mwanahalisi nalo halina data dhidi yao. Wamefungua Pandoras box, maana Chenge hataanguka mwenyewe hivi hivi, lazima afe na mtu. Sit back and enjoy the show.

mtumie salamu, wote watakaoanguka pamoja naye walipaswa kuanguka pamoja naye! kwa hiyo kama kwa jiwe moja tutaangusha ndege wawili au watatu.. why not?
 
Wakuu,

Hivi hawa watu ni akina nani?

Kutoka kwenye akaunti ya binafsi ya Chenge, mamilioni ya shilingi yamelipwa kwa watu mbalimbali wakiwa ni pamoja na Janet Mashale, Mary Nchimbi, Mary Chitanda na Livingstone Ruhere.

Wengine ni Getrude Mtiga, Hawa Kiama, Leocardia Kalumuna, Athumani Sheha na David Sanga.


Hapa kuna ndoa za watu zitaota mchanga. Mtu unaweza kufikiri mama anajituma, anakuja na mlo safi, kumbe ni mafisadi yamekuingilia hata nyumbani kwako.
 
Mtanzania... naamini kuna mtandao mkubwa wa kifisadi kiasi kwamba wameingiliana hadi mwisho wameanza kuumbuana. Halafu unajua Bongo siyo kazi kuweza ku"mtengeneza" mtu anaitwa Francis Ndimbo na kumpa sifa zote za ubinadamu na akaunti halafu akawa hayupo!
 
Wakuu,

Hivi hawa watu ni akina nani?

Kutoka kwenye akaunti ya binafsi ya Chenge, mamilioni ya shilingi yamelipwa kwa watu mbalimbali wakiwa ni pamoja na Janet Mashale, Mary Nchimbi, Mary Chitanda na Livingstone Ruhere.

Wengine ni Getrude Mtiga, Hawa Kiama, Leocardia Kalumuna, Athumani Sheha na David Sanga.


Hapa kuna ndoa za watu zitaota mchanga. Mtu unaweza kufikiri mama anajituma, anakuja na mlo safi, kumbe ni mafisadi yamekuingilia hata nyumbani kwako.

Jamani ambaye ana mke anayefanya kazi ofisi ya fisadi yeyote asisome hapa maana kuna hatari ya ndoa kuvunjika ndani ya muda mfupi ujao.
 
Kama habari zote hizi zinaanikwa wazi kwa effort za wat binafsi. kuna umuhumu gani wa kuwa na TAKUKURU?Wanakula mishahara bure IVUNJWE:Hawana kazi hawa.bajeti yao ikafanye kazi ingine.
 
Huyu Mary Nchimbi, si ni yule dadake waziri Nchimbi? Kama kumbukumbu zangu ziko sahihi, FMES alitueleza mengi sana kule Business Times juu ya huyu dada na chapati zake na kifo cha mtoto wa Trekta.

Sasa Fisadi Chenge hawa watoto wote walimfanyia kazi gani nzuri mpaka awalipe mamilioni?
 
Back
Top Bottom