The Radar Scandal: Investigation & Progress

The Radar Scandal: Investigation & Progress

Think... tatizo la dola milioni moja kwenye akaunti yake si kwa sababu ya kiasi hicho kama account activity inaonesha savings overtime kiasi kwamba anaweza kuelezea mapato hayo kutokana na investments au interests kwenye hiyo benki over time. Kama ingekuwa hivyo SFO wala wasingehangaika naye.

Tatizo ni kuwa.

a. Kiasi hicho kilionekana kuingizwa ndani ya muda mfupi sana ni shughuli gani iliyomlipa Chenge kiasi hicho akiwa mtumishi wa serikali?

b. Kiasi hicho kinaoana na malipo ya Vithlani wakati ule ule i.e Kabla ya vithlani kulipwa, Chenge hakuwa na kiasi hicho Benki, lakini baada ya malipo hayo Chenge's account mysteriously ikajaa!

c. Ukiangalia Chenge hakani kuwa na kiasi hicho benki na hatoi maelezo kuwa kiasi hicho kimetoka wapi isipokuwa anadai fedha hizo hazihusiani na BAE Radar deal. Swali la kumuuliza ni "zilitoka wapi Shs. Bilioni moja?"

So, hili ni swali ambalo TAKUKURU na tume ya maadili ya viongozi na hata Rais Kikwete ingebidi aulizwe.
 
Hivi mtu ukishitukiwa kuwa umetoa/kupokea rushwa si unaondolewa kwenye uongozi/unasimamishwa ili uchunguzi uendelee, au nimekosea?? Sasa SFO wameshamhusisha/mtuhumu (he may still be innocent at the end of the day), so tufuate precedence tuliyoset kule uchaguzi wa CCM/NEC Arusha ambapo wale Wakulu wa2, nadhani Mollel na Lekule walisimamishwa/walizuiwa kugombea posti zile kuruhusu uchunguzi (Chama kilitoa tamko hapa) na ile ilikuwa hongo ya less than $600)..... Wale wa Chama tawala hili nalo mtasema ni uongo?? Kama wale wa $600 walisimamishwa uongozi na Chama kikatoa tamko la uchunguzi, je hili la $1M mbona linafumbiwa macho???

Well hapa nadhani Muungwana inabidi a act manake..................
 
Utajiri wa Chenge waishitua Ikulu
*Ni kuhusu kumiliki akaunti ya Sh 1 bilioni
*Yasema inasubiri taarifa rasmi sheria ichukue mkondo
*Profesa Lipumba kuuzungumzia leo

Ramadhan Semtawa, Dodoma na Muhibu Said, Dar

SIKU moja baada ya Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, kudaiwa kumiliki dola 1 milioni nje ya nchi, serikali imesema sheria itachukua mkondo wake kuona fedha hizo amezipataje.

Hatua hiyo itafanyika baada ya taarifa rasmi kuhusu utajiri wa waziri huyo kufika serikalini.

Akizungumza na gazeti hili jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba, alisema taarifa rasmi zikifika, sheria itachukua mkondo wake kwani hakuna mtu aliye juu ya sheria. Simba alisema hata yeye hayuko juu ya sheria.

Waziri Simba aliongeza kwamba, taarifa zikifika itaangaliwa katika kumbukumbu za Chenge katika ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Umma.

Alisema Chenge kama viongozi wengine, amejaza fomu za kutaja mali zake hivyo kama amedanganya, itajulikana.

Simba alipoulizwa anachukuliaje taarifa za waziri kumiliki fedha nyingi kama dola 1 milioni, alijibu: "Hata mimi nashangaa kama wewe iwapo alizipata kihalali au la."

Alisema hadi sasa taarifa hizo zinafanyiwa kazi nchini Uingereza.

"Ni vema watu wakawa na subira katika jambo hilo. Lakini kuna mtu nimemwambia, labda kauza ng'ombe wao wote ndio akapata hizo pesa, labda watu hatujui, au ana biashara nyingine," alisema Waziri Simba.

Kauli hiyo ya Waziri Simba imetolewa siku moja, baada ya Gazeti la The Guardian linalochapishwa nchini Uingereza, katika toleo lake la juzi, kueleza kuanza kwa uchunguzi dhidi ya Waziri Chenge, kutokana na akaunti yake kukutwa na zaidi ya dola 1 milioni.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, taasisi ya kuchunguza makosa makubwa ya jinai nchini humo, ijulikanayo kwa jina la Serious Fraud Office (SFO), inatarajia kuanza upya kufanya uchunguzi kuhusu fedha hizo ili kuangalia iwapo zina uhusiano wowote na zile zinazoaminika kutolewa kwa njia ya rushwa, wakati Tanzania iliponunua rada ya kijeshi kutoka nchini humo kwa paundi milioni 28, ambazo ni sawa na Sh 70 bilioni, mwaka 2002.

Gazeti hilo lilieleza kuwa uchunguzi huo wa SFO unatarajia kuanza katika kipindi cha wiki sita zijazo.

Kwa mujibu wa habari hizo, uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba, moja ya mambo yanayofuatiliwa ni kujua iwapo fedha hizo zinazoaminika kuwa za Waziri Chenge, zilizowekwa katika akaunti moja iliyoko katika Kisiwa cha Jersey, zina uhusiano wowote na zile zinazoaminika kutoka katika Kampuni ya BAE System, inayotuhumiwa kuinyonya Tanzania kwa kuiuzia rada hiyo kwa bei kubwa kuliko ilivyotakiwa.

The Guardian katika habari yake hiyo iliyowekwa katika mtandao wa intaneti, liliripoti kuwa taarifa hizo zinakuja ikiwa ni miaka mitatu sasa tangu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) kwa kushirikiana na SFO na taasisi za uchunguzi za Uswisi na Jersey zilipoanza kuchunguza kuhusu kashfa nzima ya ununuzi wa rada.

Gazeti hilo lilimkariri Waziri Chenge akikiri kwamba, fedha hizo ni mali yake na akatumia fursa hiyo kukanusha kuwapo kwa uhusiano wowote kati ya fedha hizo na kashfa nzima ya ununuzi wa rada, uliofanywa wakati yeye akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) katika serikali ya awamu ya tatu.

Septemba 15, mwaka jana, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa na Mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu, walimtaja Waziri Chenge katika orodha ya vigogo 11, wakiwamo viongozi kadhaa wa serikali nchini, wanaotuhumiwa kuhusika na ufisadi wa mabilioni ya shilingi za walipakodi.

Baadaye, Septemba 19, Waziri Chenge aliliambia gazeti hili kuwa, walioibua hoja ya ufisadi dhidi ya viongozi wa serikali kama wakipata au kama wana ushahidi, yeye binafsi anatoa ruksa waupeleke katika vyombo husika vya dola ili ufanyiwe kazi.

Hata hivyo, Chenge alithibitisha kwamba yeye ni mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya Tangold, ambayo inamilikiwa na serikali na kwamba, hakuna kifungu cha sheria kinachomzuia kuwa mkurugenzi.

"Nasubiri nipate hizo tuhuma kwa maandishi maana siwezi kuzungumza tu bila kuziona, lakini kama ni ukurugenzi Tangold, mimi siyo kwamba niliwahi kuwa mkurugenzi, ni mmoja wa wakurugenzi hadi sasa. Hii ni kampuni ya serikali, tatizo nini?" alihoji Chenge na kuongeza:

"Lakini kama mtu ana ushahidi wa tuhuma za ufisadi, jamani tunavyo vyombo vyetu, si wapeleke zikafanyiwe kazi," alisema Chenge.

Waziri huyo alisema hapendi malumbano, isipokuwa yote yaliyozungumzwa atahitaji kuyaona kwa maandishi na uonyeshwe ushahidi wa yeye kuhusika moja kwa moja na ufisadi uliotajwa.

Februari 12, mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete alitangaza Baraza jipya la Mawaziri baada ya Februari 7, kulivunja baraza la awali ambapo baadhi ya mawaziri na manaibu mawaziri waliachwa na kumteua Chenge kuendelea na wadhifa wake katika Wizara ya Miundombinu.

Hata hivyo, uteuzi wa Chenge kuendelea na wadhifa aliokuwa nao katika wizara hiyo, ulizua mjadala mkali kutoka kwa wananchi, ambao wakidai kuwa hafai kutokana na kuhusika kwake na mikataba mibovu akiwa Mwanasheria Mkuu katika serikali ya awamu ya pili na ya tatu.

Pia baadhi ya wananchi walisema tangu ashike wadhifa huo mwaka 2005, hakuna mabadiliko katika ujenzi wa barabara zaidi ya mafanikio na ufanisi vilivyoachwa na serikali ya awamu ya tatu, ambayo John Magufuli alikuwa Waziri wa Ujenzi.

Pamoja na malalamiko hayo ya wananchi, Waziri Chenge aliwaambia waandishi wa habari kuwa, hawezi kujiuzulu kutokana na maneno ya watu na kwamba, suala la yeye kuendelea kukaa katika baraza hilo aulizwe Rais Kikwete ambaye ndiye aliyemteua.

Chenge alisema hayo mara tu baada ya kuapishwa na Rais Kikwete kuendelea kuiongoza wizara hiyo katika sherehe za kuwaapisha mawaziri katika Ikulu ya Chamwino, mjini Dodoma Februari 13, mwaka huu.

Akizungumzia taarifa hizo, Dk Slaa alisema ni habari za kutisha kwani mshahara na posho zake haziwezi kumfanya kuwa na akiba kubwa kiasi hicho.

"Huyu Waziri wa Tanzania ambaye mshahara wake tunaujua, posho zake zinajulikana lazima aeleze alipata wapi fedha hizo," alisema.

Dk Slaa alisema SFO wanafanya uchunguzi wa kwao na kwamba Chenge ni shahidi tu.

"Nilishamuomba Rais Kikwete amwondoe uwaziri na uchunguzi wa kina ufanyike, yatagundulika ya ajabu," alisema.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, leo atakutana na waandishi wa habari, ambapo pamoja na mambo mengine, anatarajiwa kuzungumzia tuhuma hizo za umiliki wa fedha nyingi dhidi ya Chenge.

Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Mahusiano na Umma wa CUF Zanzibar, Salim Bimani, aliliambia gazeti hili jana kuwa, Profesa Lipumba atakutana na waandishi wa habari, kuzungumzia suala hilo katika makao makuu ya chama hicho, Buguruni, jijini Dar es Salaam wakati wa asubuhi.

"Kesho (leo) saa 5:00 Profesa (Lipumba) atakuwa na press conference (mkutano na waandishi wa habari) makao makuu Buguruni, kuzungumzia hilo suala la (Waziri) Chenge," alisema Bimani, ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi wa CUF Taifa.
 
Think... tatizo la dola milioni moja kwenye akaunti yake si kwa sababu ya kiasi hicho kama account activity inaonesha savings overtime kiasi kwamba anaweza kuelezea mapato hayo kutokana na investments au interests kwenye hiyo benki over time. Kama ingekuwa hivyo SFO wala wasingehangaika naye.

Tatizo ni kuwa.

a. Kiasi hicho kilionekana kuingizwa ndani ya muda mfupi sana ni shughuli gani iliyomlipa Chenge kiasi hicho akiwa mtumishi wa serikali?

b. Kiasi hicho kinaoana na malipo ya Vithlani wakati ule ule i.e Kabla ya vithlani kulipwa, Chenge hakuwa na kiasi hicho Benki, lakini baada ya malipo hayo Chenge's account mysteriously ikajaa!

c. Ukiangalia Chenge hakani kuwa na kiasi hicho benki na hatoi maelezo kuwa kiasi hicho kimetoka wapi isipokuwa anadai fedha hizo hazihusiani na BAE Radar deal. Swali la kumuuliza ni "zilitoka wapi Shs. Bilioni moja?"

So, hili ni swali ambalo TAKUKURU na tume ya maadili ya viongozi na hata Rais Kikwete ingebidi aulizwe.

Naamini ipo siku atakuja kichaa mmoja ambaye atakuwa amechoka ma mapambano ya KIFIKRA.... ipo siku kama hatutabadilika!

Dola millioni moja ni = 1,200,000,000 divide by 30 years of service (high income from then) =40,000,000 divide by miezi 12 =3,333,333.333 ina maana jamaa toka miaka hiyo alikuwa ana make savings ya 3 million per month!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1
 
🙂 🙂 wewe wewe FD, kiboko... kwa hiyo justification naona sasa unataka SFO waanze kuchunguza offshore account zako pia... lol
 
Bongooooooo weee Bongo darisalaammm utalialialiaaaaa Bongo darisalaaaam

Kaa chonjo weeeeeee Bongo darisalaaaammmmm utalialiliaaaaa Bongo darisalaaammmmm - Profesa Jay
 
Sasa Slave, kama ukikopa Usd 63K unapata faida ya more than Usd 1Million, kwanini uwe mbunge au waziri?

Jamani hii ni nchi yetu, tusifikirie kwa #@%$&*(^%$#$, tufikirieni kwa kichwa na tutumie MOYO pia kuwaonea huruma wananchi walalahoi.

You missed the point My friend. Hiyo article unayoisema wa kwanza kuipost hapa JF nilikuwa ni mimi. Angalia time niliyoiweka mimi ni B4 wewe hujaisoma. Nimeisoma yoote. Nilichosema ni kuwa kuna evidence kuwa ana deni la $63,000 NBC. NBC nimetolea kama mfano tu, huenda ana madeni kila sehemu na kila bank duniani. Chanzo cha hela zake kinaweza kuwa ni madeni anayodaiwa na bank tofauti duniani. Tunachojua ni kuwa amekanusha kuhusika na shutma zote dhidi yake. Kabla watu kama nyinyi hamja conclude kuwa jamaa ni fisadi, tusubiri maelezo yake au ya lawyer wake rasmi. Pia ukumbuke kuwa jamaa ana bihashara ya kusafirisha prawns nje.
 
.....ni waziri anayehimiza Saccos, kuwekeza nyumbani, ukuzaji wa uchumi Tanzania.....na maneno lukuki kwenye majukwaa ya siasa........

....bora kama hela hizo zingekuwa zinalipa interest hapa Bongo... ningeona ahueni ya kinanma...

....mimi naona wapige marufuku kwa waziri yeyote kuwa na account yenye zaidi ya $50,000 nje ya nchi.... akiwa na hela zaidi ya hizo, kiongozi huyo azihifadhi katika benki za hapa nyumbani.
 
Hivi mtu ukishitukiwa kuwa umetoa/kupokea rushwa si unaondolewa kwenye uongozi/unasimamishwa ili uchunguzi uendelee, au nimekosea?? Sasa SFO wameshamhusisha/mtuhumu (he may still be innocent at the end of the day), so tufuate precedence tuliyoset kule uchaguzi wa CCM/NEC Arusha ambapo wale Wakulu wa2, nadhani Mollel na Lekule walisimamishwa/walizuiwa kugombea posti zile kuruhusu uchunguzi (Chama kilitoa tamko hapa) na ile ilikuwa hongo ya less than $600)..... Wale wa Chama tawala hili nalo mtasema ni uongo?? Kama wale wa $600 walisimamishwa uongozi na Chama kikatoa tamko la uchunguzi, je hili la $1M mbona linafumbiwa macho???

Well hapa nadhani Muungwana inabidi a act manake..................

nadhani SFO hawamtuhumu Chenge, wao wanataka kumtumia kama shahidi tu katika uchunguzi wao dhidi ya BAE. Kwa hiyo tusitarajie kuwa uchunguzi wa SFO utakuja kumtia hatiani Chenge. Kama alivyosema Mkjj hapo juu, ni kazi ya institutions zetu hivi sasa kulichukua suala hili tangu hapa lilipo na kuanzisha uchunguzi at a local level kuhusiana na ukwasi huu wa Chenge
 
Jamani mwendo ni huu huu hakuna kuwaachia, napenda kuendelea kukumbusha ishu ta EPA na RICHMOND maana kawaida yetu ni kusahau ya nyuma mara tu kitu kikipya kinapojitokeze, sasa nadhani tunatakiwa tuwe na azimio, la kupiga makelele kila siku mpaka kieleweke, weshould not be fooled now.

Kuhusu ishu ya kuandika waraka juu ya chenge nadhani kuandika si kila mtu tu anaweza kuandika, just let us be realistic, hapa JF kuna kila aina ya mtaalam, Hebu tuache blah bla hapa tufanye kazi nywnye ujuzi huu (writing)hebu aaze....
 
Sasa tuache kulalamika, email yake hii hapa achenge@parliament.go.tz

Tuandike email ya pamoja kama kikundi na kumtaka aeleze alivyopata hiyo mihela ama sivyo ajiuzulu.

Enough with kulalamika, tumuandikie na tumueleze.Ikiwezekana tutume na fax pia.Na tuendelee na utamaduni huu.Pengine hata hajui kuwa kuna watu wa "pressure group" JF wanajua hizi habari.

Mnaonaje?

WAKUBWA DOMAIN HII YA BUNGE NI KIMEO,MARA NYINGI E-MAILS HUWA HAZIENDI,SASA SIJUI NI TATIZO MAIL SERVER YAO AU NI USANII WA WATU WA IT BUNGE? DONT BOTHER HAWAPATI HUO UJUMBE NA HAWANA TIME KABISA NA HIZO E-MAIL
 
Mapambano haya hayana budi kuendelezwa kwa kina na pia nitawapatia list mpya ya mafisadi kama ilivyoweza kuwa updated hivi majuzi na kuongeza uozo mwingine mwingi ila ntawapatia summary tuu na sio kila kitu kwani bado kazi inaendelea.

Kama waziri mkuu anaweza kukiri kuwa majambazi ya EPA ni makubwa kuliko uwezo wa serikali nani anaweza kupona kwenye taifa hili?

Kama majambazi ya EPA ni makubwa kiasi hicho kwa kweli naamini kuwa Dr slaa ana ujasiri mkubwa sana kwani kama serikali yenye vyombo vyote wanashindwa na kuanza kusema wanatisha basi yule mzee wa watu alijituma na kuweka maisha yake rehani kwa ajili ya taifa lake.

Chenge ni mwizi mkubwa sasa sana amatuibia na pia kanunua kajikisiwa kake kule Maurtius akishirikiana na mafisadi wenzake .....

NA KAMA PINDA MWENYEWE AMEKIRI KUWA MAJAMBAZI HAYA NI MAKUBWA KULIKO SERIKALI BASI, KWA MANENO MENGINE NA KUSEMA KUWA SERIKALI HAINA UWEZO KABISA WA KULIONGOZA TAIFA, NAFIKIRI SASA NI WAKATI WA WAO KULIKABIDHI JESHI HII NCHI TUU....

tHESE GAYS...OOPS GUYS ARE FU..CKZ.. WANATUMIA MATUMBO KUFIKIRI KABLA YA KUSEMA BADALA YA KUTUMIA BRAIN @$#^*(()&^*()-0....!!!!!
 
You missed the point My friend. Hiyo article unayoisema wa kwanza kuipost hapa JF nilikuwa ni mimi. Angalia time niliyoiweka mimi ni B4 wewe hujaisoma. Nimeisoma yoote. Nilichosema ni kuwa kuna evidence kuwa ana deni la $63,000 NBC. NBC nimetolea kama mfano tu, huenda ana madeni kila sehemu na kila bank duniani. Chanzo cha hela zake kinaweza kuwa ni madeni anayodaiwa na bank tofauti duniani. Tunachojua ni kuwa amekanusha kuhusika na shutma zote dhidi yake. Kabla watu kama nyinyi hamja conclude kuwa jamaa ni fisadi, tusubiri maelezo yake au ya lawyer wake rasmi. Pia ukumbuke kuwa jamaa ana bihashara ya kusafirisha prawns nje.

Duh!

Sishindani kuweka posts hapa kwanza. Kama ni hivyo angalia nilijiunga lini na nina posts ngapi. Naomba ujibu ile post yangu niliyochanganua kuwa kwa mwezi toka 1978 amekuwa na wastani wa millioni 3.3 kama saving yake.

Sikumbuki nilipo conclude kuwa Chenge ni FISADI, naomba nikumbushe.

SteveD, ndugu yangu mimi nina account Swiss ila naweza kuthibitisha nimepataje hizo hela. Karibu Mbagala kwenye Hardware yangu.
Ni Hardware kubwa kuliko zote ukanda wa Temeke🙂

Karibu sana!
 
Allah's slave,

Utamaduni uliojengeka TZ ni kuwa Watu kama hao hawajibiki kwahiyo sidhani kama atajieleza kwa wananchi.
 
Kikawaida sisi tunaamini kujiuzulu ni kitu kizuri huyu jamaa anachotakiwa kufanya, lakini yeye kama yeye na ile fikra iliyopo kichwani kwake na kwa wenzake kama yeye haioni umuhimu wa kufanya vile wengi tunataka.

Huyu anaamini kabisa kuwa hapaswi kujiuzulu, kwani hakuna mwingine mwenye akili tofauti na yeye anayeweza kukamata ofisi ya umma.

Amechaguliwa kuwa waziri na mtu anayemjua kiundani na madudu yake yote, hakuna anayeweza kumweleza hadithi za kujiuzulu kama wengine kama yeye wanaendelea kutanua katika maofisi tunayoyapendezesha kwa kodi zinazotukondesha
.

VIZIWI WAKISIKIA, WATACHAGUA NYIMBO WANAYOITAKA WAO
 
Allah's slave,

Utamaduni uliojengeka TZ ni kuwa Watu kama hao hawajibiki kwahiyo sidhani kama atajieleza kwa wananchi.

Mahesabu yako nimeyaona. Sasa Chenge akija na proof kuwa alishinda lottery mtamuomba msamaha au? Mpaka sasa hakuna anayejua hizo hela zimetoka wapi.
 
Mahesabu yako nimeyaona. Sasa Chenge akija na proof kuwa alishinda lottery mtamuomba msamaha au? Mpaka sasa hakuna anayejua hizo hela zimetoka wapi.

Walks like a duck,sounds like a duck etc. etc etc. A minister from a poverty stricken country ( wangeongezea ambayo hata vyandarua wanasaidiwa) ana more than US$one million kwenye account yake bado haujawa na wasiwasi? Mimi nadhani Mheshimiwa owes the country an explanation.
 
Utajiri wa Chenge waishitua Ikulu
*Ni kuhusu kumiliki akaunti ya Sh 1 bilioni
Mwananchi
4/14/2008

...Februari 12, mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete alitangaza Baraza jipya la Mawaziri baada ya Februari 7, kulivunja baraza la awali ambapo baadhi ya mawaziri na manaibu mawaziri waliachwa na kumteua Chenge kuendelea na wadhifa wake katika Wizara ya Miundombinu...

Historia na ionyeshe Kikwete hakuvunja baraza la Mawaziri; Ni kupotoshana kama huku kwa magazeti feki ya Bongo kutakakofanya Kikwete achaguliwe tena kwa 99% mwaka 2010!

KATIBA YA JAMHURI 57 (2) Kiti cha Waziri au Naibu Waziri kitakuwa wazi litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo:-
(e) iwapo Waziri Mkuu atajiuzulu au kiti chake kikiwa wazi Kwa sababu nyingine yoyote​
 
"...hivi tukianza siasa za kuchafuana mnadhani nani atabaki humu ndani..."

Haya ya Chenge tumeshayasikia, next!!
 
Back
Top Bottom