Thanks God...............

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
11,514
11,277
...............this valentine thing is almost over!

Manake mtu unaweza jikuta roho inaacha mwili hivi hivi kwa misukosuko..
Mara huyu akupigie simu usiku wa manane eti anakutaarifu kesho umalize shughuli zako mapema eti anataka awe na wewe..
Huyu unalazimika kumdanganya kuwa upo mkoani kuna msiba, hivyo hutakuwa availabe..
Huyu unamwambia kwamba umeishiwa anakutumia pesa kwenye M-Pesa eti chukua Taksi mkutane Mlimani city..
Huyu anakulalamikia kwamba humpendi kisa hujampigia simu kwenye siku muhimu kama hii..
Huyu anakupigia simu eti ameamua kujivua pendo kisa hukumjibu sms yake ya Valentine wish..
Huyu anakutumia meseji eti amekumisi wakati juzi umemtumia meseji akauchuna..
Huyu anakupigia simu eti amekuja Dar kimya kimya alitaka aku-surprise kwenye siku ya wapendanao..
Huyu unampigia simu hapokei, anakuja kupiga baadaye eti walitoka lunch na familia yake ndo maana hakupokea simu..
.....................................
Dah..!
 
Ndo matokeo hayo lakini
Yaani siku imekaa kimapenzi mapenzi tuu tena yale ya kuvuana nguo na sio lengo la mwanzilishi wa siku yenyewe
 
Ndo matokeo hayo lakini
Yaani siku imekaa kimapenzi mapenzi tuu tena yale ya kuvuana nguo na sio lengo la mwanzilishi wa siku yenyewe

eti yale ya kuvuana nguo, Loolz...
 
Tanmo ndo hali halisi
Vyumba vyote vya guest leo vimejaa tena short time na wala sio kwamba wageni ni wengi ila ni wageni wenyeji wamejaza humo
 
Tanmo ndo hali halisi
Vyumba vyote vya guest leo vimejaa tena short time na wala sio kwamba wageni ni wengi ila ni wageni wenyeji wamejaza humo

Tatizo linakuja pale baadhi yetu tunapo-define mapenzi kama kufanya ngono tu..
 
yaani sasa hivi ukitoka nje
watu wana pembe za faru tu zimetangulia
zaweza kukuparura bila hata makubaliano lol

Pembe za faru? Kuparua? Hebu nifafanulie ili tuende sawa arifu..
 
Ndo matokeo hayo lakini
Yaani siku imekaa kimapenzi mapenzi tuu tena yale ya kuvuana nguo na sio lengo la mwanzilishi wa siku yenyewe

Ni kweli mkuu; Hata Majidd ame post uzi mzuri kuhusu Valentine day isivyokuwa na maana kwetu. Naamini maambukizi mapya ya 'kale kaugonjwa' yatukuwa makubwa leo.
 
Tatizo linakuja pale baadhi yetu tunapo-define mapenzi kama kufanya ngono tu..

That's the problem mkuuu
Yaani watu wanakosea maana kabisa ya valentine. Na kwao upendo wanaudefine kama ngono tuu
Ni mbaya sana

n
 
QUOTE=patience96;3328681]Ni kweli mkuu; Hata Majidd ame post uzi mzuri kuhusu Valentine day isivyokuwa na maana kwetu. Naamini maambukizi mapya ya 'kale kaugonjwa' yatukuwa makubwa leo.[/QUOTE]

Tena makubwa sana
Yaani watu wengi wametoswa na wapenzi wao au wameenda kwa wapenzi ambao sio wao
Wengine wataenda club na wataondoka na wapenzi ambao sio wao
Full mapenzi mapenzi tuu
 
Kuna mwingine mda sio mrefu namskia akilalama mpenzi wake kaibiwa simu jana jioni na vibaka, anaongea kwa huruma kabisa.... kua kapona kupigwa bahati walichukua simu na wallet iliokua na pesa kama Lak na nusu alitoka ATM, ila uhai kaachiwa wala hajatiwa kilema. Jioni hii mpenzi wake anapatikana... binti anauliza "pole dear umenunua simu nyingine?" then huyu mpenzi wake kamjibu "imekua bahati niliokwapuliwa jana tulikua tumebadilishana na mdogo wangu.. sina hela kabisaaa hivo nimemnyang'anya tena dogo simu ile ambayo ilikua yangu"....

Go figure... binti alihidiwa mambo mengi atafanyiwa Valentine.... kapigwa changa la macho kweupeeee....lol
 
Tena makubwa sana
Yaani watu wengi wametoswa na wapenzi wao au wameenda kwa wapenzi ambao sio wao
Wengine wataenda club na wataondoka na wapenzi ambao sio wao
Full mapenzi mapenzi tuu

mola atunusuru dhidi ya ngoma..
 
Ashadii, hicho kisa kimenifanya nicheke. Yaani uwongo wa wazi kabisa jamaa ametumia, binti angemuuliza swali rahisi tu, kama uliibiwa simu ya mdogo wako mbona kuna muda simu yako haikuwa hewani, ina maana mdogo wako aliizima 'simu yako' aliyobaki nayo?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom