Bukyanagandi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2009
- 11,626
- 18,227
Mimi nazipata zoote zinazorushwa kwa sattelite tena vizuri bila chenga. Nunua sattelite dish utapata channel mpaka utakimbia halafu asilimia kubwa kama sio zote za sattelite ni Digital. Mimi nnakauelewa ka kuyarekebisha hayo madish kwa msaada tuwasiliane kwa namba 0767-387560
Hii kitu itatufanya tuanze kuwa na ving'amuzi zaidi ya kimoja kama line za simu
Naanza kuona hasa ni akina nani "wanashinikiza" Gesi ya Mtwara iletwe Dar es Salaam, wakati gharama za kutandaza mabomba hayo ya usafirishaji wa gesi kutoka huko ingetosha kujenga vinu vya kuzalisha umeme huko huko Mtwara na kutandaza mfumo wa usambazaji umeme karibu maeneo mengi nchi nzima na kiasi kidogo cha gharama kingetumika kutandaza mabomba madogo sana ya kusafarisha kiasi kidogo cha gasi kwa matumizi mengine ya Dar es salaam!!!...............
Wengi wa Wakazi wa Dar, tunapenda zaidi starehe kuliko kuzijali familia zetu!, mimi nakunywa Sinza, kuna bar 250 na zote zinajaa, kwa nini tushindwa kulipia king'amuzi elfu 10 kwa mwezi?!.
Heri ya Mwaka Mpya.
Pasco.......
Kama hupati sauti chukua remote yako bonyeza track, nenda kwenye audio track, shift yellow to stereo, shusha chungwa left or right utapata sauti mkuu.
Mkuu Ze Marco, huu uhamaji sio kumuumiza mtazamaji bali kumsaidia na kuvisaidia vituo vya TV. Naomba nikupe mfano kupitia simu za mkononi hadi za mezani.Pasco nimesoma maelezo yako na kuona huu uhamaji wa kutoka analogy kwenda dijitali ni kumuumiza muangaliaji TV tu na siyo kuheshimu teknolojia.
Unasema TV zilikuwa zinarusha signal za analogy na sasa zitaendelea kurusha signal za analogy na kwamba tofauti iliyopo ni kwamba signal hiyo ya analogy sasa itapelekwa kwa star media ili waibadilishe na kuwa digital. Sasa kama TV zinaendelea kurusha analogy signal ambayo inaweza kukamatwa na TV bila malipo wala usumbufu, kwanini mwananchi huyo alazimishwe kununua king'amuzi?
Je, kitendo cha kuipeleka analogy signal kwa star media ili waibadilishe kuwa digital inaongeza thamani gani kwa muangaliaji wa televisheni? Je, iwapo tungeendelea na utaratibu uliokuwepo ni madhara gani yangetokea?
Mkuu Ishina, DSTV, ZUKU, Easy TV na wengine watakaokuja hawana vibali vya TCRA ku distribute local contents, the official distributer wanaitwa multiplex operators wako 3. Vituo vya TV vinabaki kuwa content provider hata sisi jf tukiamua kuwa na channel yetu, tunafungua JF TV!.
DSTV wana service licence only lakini hawaruhusiwi kupokea local contents, hata vipindi kama Wanawake live, na lots of Bingo movies kwenye DSTV Swahili, zinarushwa kutokea Afrika Kusini!. Hata hiyo TBC yenyewe kwenye DSTV, iko beamed kwa nchi za Afrika Mashariki tuu, hata ukiwa South Africa, TBC haionekani!.
Hapo ilipo hata hilo la kuonyesha 5 channels bure ni ubabe tosha!, channel ya bure ilipaswa iwe moja tuu, TBC ambayo tunailipia kwa kodi zetu, nyingine zote tulipaswa kulipia!. Kwa msio fahamu TV kama CNN, BBC, Al Jazeera na nyingine za wenzetu zilikwenda digital kitambo kidogo, ukiwa ulaya kuna ma chanell ya CNN kibao suprising, hii tunayoiona huku kwetu kule haionekani!, wakati fulani nikiwa huko ndipo nililiona Tangazo la utalii la Tanzania kwenye CCN masikini Afrika hatulioni!.
Kitendo cha kuilazimisha DSTV ionyeshe hizo chanell tano za bure, ni sawa na kuilazimisha CNN itangaze matangazo ya TBC!. Kwanza huko DSTV hakuna hata chanel moja ya bure, kule inaongea pesa tuu!, na ili kuona mechi zote, lazima kila mwezi ulipie zaidi ya laki!, kama hizi za kulipia elfu 10 kwa mwezi watu wanapiga kelele, DSTV tutaigusa?.
Pasco.
Mkuu Meni', narudia tena na tena TCRA hawakukurupuka!, kama maandalizi yameanza two years back na utekelezaji ndio juzi, wamekurupuka vipi?!.mkuu Pasco nakufahamu vizuri sana kwamba hausiki na TCRA lakini wewe ni mdau nyeti katika tasnia ya habari!nakuheshimu katika hili.
TCRA wamekurupuka kwani hata wewe umekiri kuwa hakuna station inayoweza kurusha matangazo yake kidigitali.ni upuuzi na kukurupuka kumkomalia mwananchi wa kawaida ahamie digitali huku ukijua hata taasisi za utangazaji nchini hazijaanza kufanya hivyo.
Kutoa matangazo kwa miaka miwili haimaanishi kuwa tumefanya utafiti wa madhara na mazuri ya tukio hili kwa mwananchi wa kawaida na maskini wa nchi hii!
Kuhusu kinga'amuzi cha serikali ningependa nikijue kwani nahisi kitakuwa 'perfect'
Mkuu Ze Marco, huu uhamaji sio kumuumiza mtazamaji bali kumsaidia na kuvisaidia vituo vya TV. Naomba nikupe mfano kupitia simu za mkononi hadi za mezani.
Mobile zilipoingia zilikuwa analogue kama wewe ni wazamani unaweza kukumbuka mambo yalikuwaje!.
Mimi nilinunuliwa simu yangu ya kwanza na ofisi, wakati huo niko DTV mwezi July, 1995 kwa ajili ya uchaguzi!, Ni simu ya Motorola lilikuwa kubwa kama zile radio call za polisi za zamani!. Nikipiga nalipa, nikipigiwa nalipa na ilikuwa ni Dar tuu, kulipia ilikuwa ni lazima kwenda kufoleni pale mobiteli!. Handset zilikuwa ghali sana!. Kuna wakati nilisafiri kwenda UK, kuuulizia simu dukani wananiuliza analog za nini? ni nchi chache Afrika ndio tulikuwa nyuma hivyo!. Niliuziwa used pieces 20 kwa paund 4 kila simu!, niliporudi home, nili make!. Ingekuwa sio kazi, ningekuwa ni mtu wa kusafiri kufanya biashara ya used phones!. Tri Tel ndio wa kwanza kuleta GSM nchini.
GSM zilipoingia ndipo zikaleta txt sms, kulipia ikawa ni kwa kutumia vocha ukiondoa post paid, gharama zimeshuka sana. Sasa kwenye simu unaingia internet, simu kama Nokia E-90 ina program zote za computer!, hivyo ni sawa na pc!. Sasa tuna mpaka money transfer na sms banking!, just imagine simu yako ya mkononi inasaidia mambo mangapi?. Money transfer ya sumu takes less time kuliko hata cash withraw kwenye ATM kwa sababu kwa ATM lazima uifuate ilipo, M-Pesa ni kila kona, kila mahali!.
Mapinduzi ya digital kwenye simu za mkononi sasa ndio yanakuja kwenye TV!.
Kwa kuanzia
Hizo ni sababu kwa kifupi tuu na hapo kuna maltiplier effects sijazitaja!. Tusizungumzie pros only, cons pia zipo ikiwemo kifo cha jumla cha bwana "bure", amekufa na amezikwa!, hakuna tena kitu cha bure!, kwa kuanzia TCRA amelazimisha hizo channel 5 ziwe bure, yes ni bure ila sio bure bure kabisa!, ili kuipata hiyo bure, lazima kwanza ununue king'amuzi ambacho sio bure!, ukishakinunua ile elfu 39,000/= lazima ilipie ile 10,000 ya initial actvation!, inakuwa 49,000/=!, then lazima ulipie ile antenna yao 20,000/=!, hivyo ni 69,000/=!, na labda lazima umpooze yule fundi wao kuja kukusetia nyumbani kwako!. Kwenye ulimwengu wa sasa, hakuna vitu vya bure!.
- Vituo vya TV havirushi tena matangazo, vywenyewe vinakuwa ni "content providers only" hivyo zile gharama za umeme ku run transmiters 24/7 zinakuwa cut off!.
- Eneo zilipokuwa zinakaa transmiters sasa litafanya kazi nyingine imagine mfano TBC, yale majieneo yake yote ya TX sasa yatabadilishwa use!.
- Mishahara ya wafakazi wa TX inakuwa cut off!, of course watu watapoteza kazi!, lakini its high time wengine wenye uwezo wa kubadilisha kazi, watakuwa retained kwa kupangiwa kazi nyingine lakini wengine sorry ndio hivyo oparation cost ikipuguzwa huwezi kukwepa laydown as saving costs!.
- Trasmiter moja ya digital, inaweza kurusha chaneli mpaka 100!. Hapa Tanzania mpaka sasa tuna hizo TV 5 tuu za bure, kwa hii digitali, soon tutakuwa na Channel zaidi ya 100 za kwetu kama ilivyo DSTV!, hivyo we'll have more options, mfano, kutakuwa na lets say chanel 10 za dini, Mama Rawakatare na chanel yake, Mwingira ya kwake, Kakobe ya Kwake, Mzee wa Upako ya kwake, Katoliki ya wao, Walutheri ya kwao, Anglikana ya kwao, Bakwata ya kwao, hata Uaumsho wakiamua nao wanapata chamel yao kama zilivyo kwenye DSTV!. Tukija chanel ya ELimu, UDSM wanaweka yao, Mzumbe ya kwao, Sokoine ya kwao, Udom ya kwao, Elimu ya msingi na ya kwake, Chekechea na yakwao etc, Kutakuwa na chanels za miziki, movies, hadithi, mitindo, michezo, kwaya, dramas etc, you name it hivyo well have more options, more choices!.
- Ujio wa Digitali ni ukombozi kwa sisi tunaitwa "production Houses". Kuna vitu vingi vinatokea mitaani na vistudio vingi vinatengeneza vipindi, lakini hawawezi kuvitangaza kwa sababu gharamna za kurusha vipindi ziko juu!, Mfano kurusha kipindi cha 30 minutes ITV ni TZS 3,000,000+ vat, kwa TBC-1 ni TZS 2.500,000 plus VAT!. Huu ujuio wa digitali sasa sio lazima mimi nipeleke kipindi changu ITV or TBC, hata mimi sasa naweza kulipia tuu channel yangu dola 3,000 kwa saa kwa mwezi!, hivyo sasa inaitwa PPR-TV!, natangaza mwenyewe direct, natumia prime time kurusha vipindi vyangu, wakati hali ilivyo sasa wenye TV wanaweka vipindi vyao "prime Time" vyetu vinarushwa saa 5:00 usiku au mchana!.
- Quality ya picha itaboreka sana!. Hakuna chenga!, hakuna kugeuza geuza antenna!. Mpaka sasa Transmites zote za TV zetu zilikuwa analogy soon watabadili kuwa digital, ITV wameshatangaza kuanza matangazo kwa HD hivyo picha zitakuwa clear kama DSTV. Kwa sasa kinarushwa kwenye Digital bado ni analogy signal wanaitransmit digital, wakishaingiza digital signal you can see the diference!.
- Kuna uwezekana kupata 3D signals!, kwa msio elewa 3D hebu na nyinyi siku moja lipieni kiingilia muingie kwenye lile jumba la senema pale Mlimani City!, picha inaonekana kama real!. Kwe DSTV kuna baadhi ya Chanel ni HD na kuna baadhi ni 3 D ikiwemo National Geographical, na tukifika huko kwenye 3D, TV za mogongo ni sorry!.
- Sasa TV zitapatikana kwenye simu za mkononi crystal clear bila antenna!. Huu ndio mwisho wa hivi visimu vya mchina vyenye TV vilikuwa Analogia!. Kwa simu za ukweli zenye Digital TV, hapa sasa ndio mahali pake!. Wenye simu za HTC au Samsung ndio nyingi zina Digital TV ambao walikuwa wanapata DSTV only!, sasa tutaweza kupata TV nyingi zaidi na wale wenye TV kwenye magari yao ya kijapani, sasa wataweza kuona digital TV ambazo ni free to air, yaani zile za bure!.
- Internet ni kwenye TV!. Ujio huu wa digitali, sasa unafungua milango ya kupata inrenet kwenye TV screen kupitia digitali. Kwa mliofuatilia Vodacom waliwahi kutoa kibox chao cha internet, sasa sio kusubiri tena kibox cha kampuni ya simu, hiyo hiyo decoder yako ndio itakuwa internet receiver yako, kazi itabaki ni ku set controll kudhibiti watoto wastembelee zile site za ajabu ajabu ao za mambo ambayo sio kwa umri wao!.
- Mwisho huu ndio usasa wenyewe, tuko kwenye digital era, Tanzania hatuwezi kubaki nyuma!. Uamuzi wa jumla wa kuhamia digital sio choice its a must by 2015 nchi zote duniani lazima ziwe zimehamia digitali kama ilivyo kwa utandawazi its not us, ni wenye dunia yao ndio wameamua, sisi kazi yetu ni kufuata tuu ili tuendelee kuwepo au tu perish.
Pasco!.
Naanza kuona hasa ni akina nani "wanashinikiza" Gesi ya Mtwara iletwe Dar es Salaam, wakati gharama za kutandaza mabomba hayo ya usafirishaji wa gesi kutoka huko ingetosha kujenga vinu vya kuzalisha umeme huko huko Mtwara na kutandaza mfumo wa usambazaji umeme karibu maeneo mengi nchi nzima na kiasi kidogo cha gharama kingetumika kutandaza mabomba madogo sana ya kusafarisha kiasi kidogo cha gasi kwa matumizi mengine ya Dar es salaam!!!.
Nikirudi kwenye mada
Hili nalo neno!, vituo vya TV kama yalivyo makampuni ya simu , mabenki au miradi yoyote, inapelekwa kule kwenye faida!. Ndio maana kuna baadhi ya maeneo reli imepita kungine hata kichochoro hakuna!. Kuna baadhi ya maenneo kumepita mabarabara ya lami mpaka vijijini, wakati kungine hakufikiki kabisaa! hakuna hata hiyo barabara ya uchochoro!, kisa hakuna shughuli yoyote ya maana ya kiuchumi, hivyo hakuna biashara, hakuna pesa, nani aende?!.Kuna watanzania wako Nyaminywili-Rufiji, Omukihisi- Bukoba, Muhukuru-Songea vijijini, Mwazye-Sumbawanga vijijini, Oldonyo-Sambu, na kadhalika na kadhalika; hawa nao wanahitaji kupata matangazo ya Televisheni kwa unafuu kulingana na kipato chao. Pasco kwa utaratibu huu unaoupigia 'chapuo', ni wazi unataka kuwanyima fursa watanzania wenzako haki ya kupata habari kwa njia bora kabisa, kwani kwa taaluma yako ya masuala ya habari unajua kabisa wananchi wa maeneo nliyoyataja na mengine yanayofanana nayo hawaweze kumudu gharama za ving'amuzi/visimbuzi ulivyovitaja.
Nilitarajia kwa kalamu yako upaze sauti zao za kuona namna serikali kupitia TCRA na Wizara husika kushusha gharama za kupata vifaa hivi na kuhakikisha wanasimamia suala la kuhakikisha televisheni zote za 'bure' zinapatikana kwenye ving'amuzi hivi ili watanzania wote tufaidike.
Ahsubuhi njema.
--MpigaKelele
huu ni unyanyapaa!shule za kata bhana zinakela jf
Mkuu Pasco, point no. 1 unaposema TV havitarusha tena matangazo vitakuwa "content providers only" una maana gani?. Kama ni matangazo ya biashara mbona bado yanarushwa? Pamoja na ku-cut costs hizi TV zinapata vipi faida?
--MpigaKeleleee...ee!,
Kwanza nianze kwa msisitizo kuwa jemeni, mimi sio mtu wa TCRA!, naona maswali yanazidi kuelekezwa kwangu!.
Lile la gesi ya Mtwara, mimi ni mmoja wa masupporter wakubwa ile gesi ije Dar kwenye viwanda na magari na majumba ya watumiaji!. "You can never miss what you never had!". Kuna kampuni moja ya Waholanzi, waliamua kugharimia solar panels na biogas kwenye shule, zahanati, na nyumba za ibada za kujiji cha Itonjanda, huko Tabora Vijijini ili kuwahamasisha wanakijiji wengine kuchangia kidogo tuu wawekewe highly subsdized solar pannels! na mitambo ya biogas ili kukoa mazingira!. Amini usiamini, wananchi wale hawakuchangia!. Nikiwa JET,(Chama cha waandishi wa habari wa Mazingira) tukapewa tenda ya kufanya research kwa nini?!. Tulipozungumza na wanakijiji, wao wakasema shida yao kubwa sio nishati, kuni zipo za kumwaga, wala sio umeme, wameziea chemli, bali shida yao kubwa ni barabara na maji!. Mradi ended up to be a "white elephant!".
Mimi binafsi nimepeleka solar na jiko la gesi ule mtungi mkubwa kwa mama yangu kule kijijini!, huu ni mwaka wa pili sasa, mtungi mmoja haujaisha na kila nikifika, tv ina vumbi tuu kuonyeshwa haiwashwi!. Nikimuuliza mother kwa nini hupikii gesi?, sikuzoea!, chakula cha gesi sio kitamu kama cha kuni!, halafu nimeambiwa siko moja italipuka!, hivyo gesi inatumika tuu wakija wageni!. Na TV jee, hatukuzoea kuangalia! eti pia inakula umeme mwingi hivyo tunakosa mapatio ya kuchajisha simu za watu mchana!. Ile tv ni pambo tuu!. Hivyo ndivyo ilivyo gesi ya Mtwara!, hawajazoea!, na viwanda si mpaka vijengwe?!. Kazi ya kuestablish "petrochemical industry" hiyo Environmenta Impact Asssessment yake tuu yenyewe!, inachukua mpaka 5 years!, sasa wakati tunasubiri hivyo viwanja vijengwe huko, gesi iliyopo iletwe Dar ambapo viwanda tayari vipo na wa`tumiaji tupo!.
Hili nalo neno!, vituo vya TV kama yalivyo makampuni ya simu , mabenki au miradi yoyote, inapelekwa kule kwenye faida!. Ndio maana kuna baadhi ya maeneo reli imepita kungine hata kichochoro hakuna!. Kuna baadhi ya maenneo kumepita mabarabara ya lami mpaka vijijini, wakati kungine hakufikiki kabisaa! hakuna hata hiyo barabara ya uchochoro!, kisa hakuna shughuli yoyote ya maana ya kiuchumi, hivyo hakuna biashara, hakuna pesa, nani aende?!.
Wakati nikiwa mtangazaji mchanga pale RTD, nilitupa jicho langu mahali kwa kabinti fulani, kumbe cha "wenyewe" ma bisi, hivyo dawa yangu ni kutupwa kituo cha Nachingwea kama adhabu!. Kule nikashangaa kukuta hakuna hata hoteli moja ya maana! hivyo nikafikia guest!. Chakula nikaagiza kuku, nikaambia hapa hakuna kuku!, nikauliza hakuna hata hoteli yoyote yenye kuku?, nikaambiwa hakuna kwa sababu hata ukuchinja kuku, hakuna wateja!, wakasema ukitaka kuku, unaagiza asubuhi ndipo tunakununulia, kukuchinjia na kukupikia ila lazima utamla wote maana watu wa kule hawana purchasing power ya kula kuku!. Ukiuliza hiyo bei yenyewe ya kuku!, nilikula kuku mpaka!, ukijumlisha na kale kajiukarimu ka watu wa "ntwara!" almanusura ningelowea, ila kiukweli kimaendeleo hakufai kabisa!. Watu wenye pesa walikuwa ni wajeda pekee kwenye kambi yao ya Fort Koma" nao kila kitu ni barracks!.
Vivyo hivyo kwa makampuni ya simu, hayawezi kupelekja huduma zake mahali amba hapalipi, so do banks na vituo vya TV are no exception!. Kwa taarifa yako, mpaka leo kwa Tanzania nzima, hiyo coverage area ya TV Ωote zilizopo ukizijumlisha pamoja na cable na wanaotumia ma dish yao, hawafiki 30% ya Watanzia wote!, hivyo hapa unawazungumzia hao Watanzania 70% ambao are still living in the dark!. Kumbuka "you can never miss what you've never had!". Kwao life is as usual!.
Kati ya hawa asilimia 30% wanaopata TV signal, only 15 % ndio wanatumia antenna waliobaki wanatumia either cabla au dish, hivyo hao wa cable na dish huu uhamaji hauwahusu, bali wale 15% waliotegemea antenna kama za Chadema etc ndio wanahusika!.
Kwa vile kupata habari ni miongoni mwa haki za msingi za binaadamu, serikali haiwezi kuziachia tuu hizi kampuni za simu na mawasiliano kuwekeza kwa wenye pesa tuu!, hivyo imeanzisha mfuko wa Universal Communications Access Fund (UCAF) na unagharimiwa kwa kiasi kikubwa na TCRA kupitia wizara ya Mawasiliano ambao utatoa fungu la ruzuku kuwafidia makampuni ya simu na vituo vya TV kufika hata yale maeneo ya pembezoni ambako ni hasara tupu! so that hatimaye, kila mahali patafikiwa japo sii leo wala kesho ila one day kote kutafikiwa!. Hivyo soon the problem will be solved!.
Nawaombeni msiniulize maswali zaidi, mimi sio mtu wa TCRA!
Pasco.