TBC journalist Jerry Muro held over alleged graft

TBC journalist Jerry Muro held over alleged graft

Baada ya ila kazi nzuri iliyoifanya kwa traffic, alipaswa kushauri kuwa mwangalifu zaidi maana ni target.

Kwa waandishi makini, ziko kona nyingi za kubabatiza milioni 10.
Inaelekea wewe unajua mahali rushwa inapopatikana bila kukamatwa!!!
 
Alipokea rushwa ili afanye au asifanye nini? Tuwekeni wazi kwa hili pls!

Nimesikia juu juu tu kuwa huyo aliyeombwa rushwa ni among wale maafisa waliosimamishwa na Mh. Pinda Bagamoyo. Habari zimedai kuwa eti Jerry alimuomba rushwa hiyo ili asimtoe jamaa kwenye habari sasa hapa hata sielewi siri ni nini wakati ilishajulikana kuwa wamesitishiwa ajira zao- Mimi hii habari hainipi.
 
Nimesikitika sana na nikajihisi mwili kutetetmeka kwa mzalendo wetu Jeryy Murro kufanyiwa kitu kibaya. Najua wameamua kumwadhibu kwa makusudi, lakini naomba kutoa changamotokwa waandishi wa habari kuwa tukio hili lisiwafanye wawe waoga juu ya jeshi la polisi. Sasa naomba wawe wamechokoza nyuki mzingani kwa kumharibia mwandishi mzalendo ili rushwa isiendelee kufichuka. Issue ile ya rushwa na wakubwa wa Polisi wamo ndio maana wamemlia njama ili wasiendelee kufichua taarifa hizo.
Nimeumia sana juu ya tukio hili.
 
Nguvumali hapo kwenye Blue wanadai Muro alikubaliana na huyo jamaa aliyemtaka rushwa kuwa wakutane hotel ya City garden mjini muda wa saa nne na yule jamaa aliwatip police nao wakafika na kumtia mbaroni Jerry- kinachonishangaza ni kuwa wanadai walipompekuwa wamemkuta na bastola iliyokuwa na risasi na kwenye gari lake walikuta pingu za police ambazo mdai alidai kuwa Jerry alimfunga pingu kabla hajampa hizo pesa- jamani something is fishy in this story- au Jerry amekuwa jambazi la kutembea na bastola au police mwenye bastola na pingu? Amevitoa wapi ah hawa wanataka tu kumchafulia
kuwa na bastola si kosa kisheria, ikiwa tu imepatikana kwa njia sahihi kwasababu hata mimi ninayo nanina lipia kila fee kwa kila mwaka.
ushahidi wa rushwa kama wangehusishwa TAKUKURU ungekua umekaa vizuri, hautegemei maneno ya kuambiwa, ni mabingwa wa kuweka mitego ya pesa maarufu kama pesa za moto.
bado ipo shaka ya wazi dhidi ya kisasi kwa Muro.
ila hiyo pingu inawezekana Polisi aliidondosha alipokuwa anaetenda kutegesha mawani ambayo yule mama alidai kuwa Muro aliisahau kwenye gari yake.
 
jamani mi naombeni mwenye hizi news anijuze nipate kuelewa, ni kweli Jerry Murro yule kijana shujaa wa kuripot habari za rushwa, maadili na utawala bora amekamatwa akiomba rushwa ya milion 10?
 
Nitaafurahi ya JF bila kubeza wakanisaidia majawabu ya maswali haya juu ya kukamatwa kwa J. Muro

1. je,haifanani sana na "tumkomeshe nae amezidi kutufuatilia?"

2. waliomkamata ni PCCB au walewale anao watoa magazetini (polisi)?

3. Afisa mfukuzwa kazi toka Bagamoyo aliombwa hiyo hela kwa ajili ya nini?

4. Lengo la awali na afisa mfukuzwa kazi toka bagamoyo la kuacha miwani kwenye gari ya J.muro lilikuwa ni nini?

5.Polisi hamjui ya kwamba mnachokoza vita sasa wadau tuanze kumwaga picha lukuki za mambo yenu yaleeeeee

6. Polisi hamjui ya kwamba mkimuua Katabaro atazaliwa Rutayasingwa?

haya maswali ndo najiuliza hapa kwa umakini sana ....
hawa jamaa kama ni kweli wametega mtego kulipiza kisasi
 
jamani mi naombeni mwenye hizi news anijuze nipate kuelewa, ni kweli Jerry Murro yule kijana shujaa wa kuripot habari za rushwa, maadili na utawala bora amekamatwa akiomba rushwa ya milion 10?
Mod ziunganisheni, jamaa kaamka na kuanzisha sredi bila kupitia kilichomo kwenye maforums kwanza. Vipi Dogo Tundu, ndo unaingia ofisini?
 
I'll tell you why I'm laughing (if you didn't notice); Muro ameitwa kwenda mahali ambapo ameahidiwa kukatiwa kitu kidogo.. anatoa taarifa kwa vyombo husika (in this case, say TAKUKURU) na anaandaa watu wake wa kurekodi kitu hicho. Yule mtu mwingine anatoa taarifa kwa vyombo husika (lets assume ni Polisi); Polisi wanaandaa mtego wa kumtia matatani Muro, na mura anaandaa mtego kumtia matatani jamaa ili amrushe katika kipindi chake.

Well.. anaenda pale anakabidhiwa mzigo (polisi wanachekelea wamemnasa). Na mara moja wanaanza kujitamba kuwa jamaa anayepiga vita rushwa ndiyo huyo kakamatishwa. Habari zinaruka haraka haraka na wanamkimbiza Muro kituoni, sms zinaenea, na hadithi kolea.

Muro anafikishwa kituoni anapigishwa mkwara na maneno kibao. Anapewa nafasi ya kujitetea. Anawaambia "mna wazimu".. wanashangaaa..

should I tell you how the story end?
 
I'll tell you why I'm laughing (if you didn't notice); Muro anafikishwa kituoni anapigishwa mkwara na maneno kibao. Anapewa nafasi ya kujitetea. Anawaambia "mna wazimu".. wanashangaaa..

should I tell you how the story end?
inafikirisha, inaleta na kuchochea uwezo wakufikiri.
 
I'll tell you why I'm laughing (if you didn't notice); Muro ameitwa kwenda mahali ambapo ameahidiwa kukatiwa kitu kidogo.. anatoa taarifa kwa vyombo husika (in this case, say TAKUKURU) na anaandaa watu wake wa kurekodi kitu hicho. Yule mtu mwingine anatoa taarifa kwa vyombo husika (lets assume ni Polisi); Polisi wanaandaa mtego wa kumtia matatani Muro, na mura anaandaa mtego kumtia matatani jamaa ili amrushe katika kipindi chake.

Well.. anaenda pale anakabidhiwa mzigo (polisi wanachekelea wamemnasa). Na mara moja wanaanza kujitamba kuwa jamaa anayepiga vita rushwa ndiyo huyo kakamatishwa. Habari zinaruka haraka haraka na wanamkimbiza Muro kituoni, sms zinaenea, na hadithi kolea.

Muro anafikishwa kituoni anapigishwa mkwara na maneno kibao. Anapewa nafasi ya kujitetea. Anawaambia "mna wazimu".. wanashangaaa..

should I tell you how the story end?
Mwanakijiji mbona umekatisha hii movie? hebu malizia bana ah ilishaanza kunoga ati.

Let me get my coke and popcorn ready.........
 
haya maswali ndo najiuliza hapa kwa umakini sana ....
hawa jamaa kama ni kweli wametega mtego kulipiza kisasi

FL1, nimepitia posts zooote, ila sijaona mahali ambapo pananipa angalau kitu cha maana. Watu wamejitahidi kuleta habari lakini ni ngumu kuunganisha dots ili walau kupata story nzima. Polisi walioaibishwa na Jerry watawezaje kuwa wa kwanza kumtia mbaroni kwa kosa ambalo lina wenyewe i.e linatakiwa kushughulikiwa na TAKUKURU? Hata kama kuna ukweli, basi polisi wamechemsha na hapo inawabidi waanze upya. Ngoja tusubiri labda polisi wataweza kufinyanga finga hiyo story yao ili ieleweke vizuri hata kwetu wenye IQ ndogo!
 
hii kitu imetengenezwa na kila siku nimekuwa ikiwaambia watu huyu kija anatakiwa kuwa makini hasa kwa maisha yake kwani ametengeneza maadui ambao ni wakali sana. ukifuatilia kwa karibu utaona ni mambo ya kijinga tena wametengeneza na wamefanikiwa sana tu, swali la kujiuliza kwa nini ufunguo wa gari lake upotee na wakati anapiga simu nymbani aletewe ufunguo wa akiba mara unapatikana huo ufunguo kwa mazingira ya kutatatnisha. la pili kwa nini huyo Wage asitowe taarifa TAKUKURU ili MURO angekamatwa na pesa za unga? Tatu ukumbuke wage alitoa ya ushashidi kuwa alikuwa na MURo kwenye gari lake na alikuta Pingu na miwani yeke iko kwenye hilo gari kweli walivikuta, hapo utaona nijinsi gani huo mpango ulitengenezwa. sasa tumkumbushe ndugu MURO kuwa ajipange vizuri si kila tukio anaenda peke yake anatafutwa hapo wamemsingizia kwa rushwa ila kuna kifo mbele yake
 
I'll tell you why I'm laughing (if you didn't notice); Muro ameitwa kwenda mahali ambapo ameahidiwa kukatiwa kitu kidogo.. anatoa taarifa kwa vyombo husika (in this case, say TAKUKURU) na anaandaa watu wake wa kurekodi kitu hicho. Yule mtu mwingine anatoa taarifa kwa vyombo husika (lets assume ni Polisi); Polisi wanaandaa mtego wa kumtia matatani Muro, na mura anaandaa mtego kumtia matatani jamaa ili amrushe katika kipindi chake.

Well.. anaenda pale anakabidhiwa mzigo (polisi wanachekelea wamemnasa). Na mara moja wanaanza kujitamba kuwa jamaa anayepiga vita rushwa ndiyo huyo kakamatishwa. Habari zinaruka haraka haraka na wanamkimbiza Muro kituoni, sms zinaenea, na hadithi kolea.

Muro anafikishwa kituoni anapigishwa mkwara na maneno kibao. Anapewa nafasi ya kujitetea. Anawaambia "mna wazimu".. wanashangaaa..

should I tell you how the story end?

Hebu endelea babu? Kwani sisi wenye akili ndogo tulikuwa tumetoka kapa. Wewe sasa unaanza kutupatia ka mwanga kwa mbaaaali!! Bado dots zipo, hebu amalizia basi kuusuka huo utando wa buibui!
 
Muro amesahau kuwa muosha huoshwa?

Yesu aliwaambia wale watu waliotaka kumpiga mawe mwanamke aliyekutwa anazini.... ambaye hana dhambi awe wa kwanza ktupa jiwe...
 
Ivumayo sana inakaribia kupasuka.......................
 
Kaanzisha vita inabidi awe makini sana.Kama wanataka kumuua kikazi basi wanaweza kumuua hata Kimwili kabisa.
Be carefull Muro,it seems nobody cares about your Hard work.Hata unaofanya nao kazi wanaweza kuwa maadui zako vilevile.
 
polisi wa Tanzania msitufanye sisi wajinga, kama jery alidai rushwa basi alipaswa kukamatwa na askari wa pccb na siyo polisi wa kova. pingu na miwani ninyi ndiyo mmevitega kwenye gari lake. huyo afisa wa bagamoyo alikuwa anatoa rushwa ili iwe nini wakati watanzania wote tunajua ni fisadi. sasa alitoa ya nini? msitufanye wajinga
 
Back
Top Bottom