TBC journalist Jerry Muro held over alleged graft

TBC journalist Jerry Muro held over alleged graft

Kova amezungumza akiwa hapa Police Central na amegoma kwnda into details kwa kuwa anasema uchunguzi bado unakamilishwa na kwamba kesho ndiyo kesho atatoa kila kitu. Kuna watu wengi sana hapa ndani na nje ya jengo wakitaka kujua kulikoni na hatma ya Muro

Sasa hii ni typical joke we toka lini mtu amekamatwa na rushwa anakuja RPC kumhoji? Walikuwa wanaongea nini huko ndani? Kama kweli ni mtuhumiwa si wafate taratibu zote kama za wengine wanaogopa nini? Uchunguzi wa nini kama wamemkuta anapokea? Am I missing something here? I think the whole issue is a crap. WELCOME TO BOMGO JERRY
 
Mkuu toka lini mtu anaweza kutoa details za kuwa kapokea kiasi fulani cha rushwa kwa ajili ya nini??mtoaji anatoa apate atakacho na mpokeaji anajua atatumiaje hiyo rushwa

Cont..........

he deserve it..unakuwa na mdomo mdomo wakati masikini analo sasa..usiku wa habari ataenda kuutangazia segerea..

Babu leo kulikoni mbona wafyatuka namna hii?
 
Asante Pasco na wengine. Mimi pia nimesikiliza TBC1 live via Radio Maria dk chache zilizopita, na wamekiri kuwa Jerry Muro alikuwa kituo cha police central leo na amehojiwa na police kwa masuala kadhaa ambayo hayajawekwa wazi( according to KOVA) na kwamba baada ya hapo AMEACHIWA NA YUKO HURU.

Taarifa imesema Kova atatoa maelezo kesho kuhusu kilichojiri. Mpambanaji dhidi ya RUSHWA, Jerry Muro yuko huru...anajipanga kupiga picha za wala rushwa mtaani.

Tulisema hapa mwanzo kuwa hizi habari ni za uhakika? Tusijekuwa tunajadili ya kusadikika? Ona sasa, wengine leo wameshinda hapa hata thread zingine hawajatemebelea. BONGO TAMBARARE
 
stand for the truth you stand alone

stand for the truth you stand alone
Government will cover up
Government will cover up.
-Lucky Dube
 
sasa ni lipi hapa?

Alikuwa Central kufutilia mwendeleozo wa vipind vyake au alikamatwa Bagamoyo akiwa na batola na pingu kama PCCB kumtishia mtumishi wa Umma ili ampe Rushwa ya Tshs 10m?....mnatuumuza matumbo nyie waandishi wa nyumba katika kufuatilia na kuripoti taarifa zenu hapa Jamvini!.


Kama yupo huru, mpaka sasa hakuna anayeweza kutupa undani wa yote kupitia mwenyewe Jerry ?
 
Ovyooooooooooooooooooooo......................

Nina wasiwasi walifikiri wanamkamata kumbe jamaa alikuwa kazini na camera zimerekodi kila kitu. Nafikiri walipofahamu hilo na kuwa hata kazini aliaga na camera man wake aliona, wakaona wataumbuka.

Ninafikiri ilikuwa hivyo. Sidhani kama watasema ukweli maana watu wazima watazidi aibika.
 
JERRY MURO MATATANI


Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linamshikilia Mtangazaji wa Shirika la Habari Tanzania (TBC) Jerry Muro (pichani juu kulia) kwa tuhuma za kudai fedha kwa njia ya vitisho.

Muro anadaiwa kumtisha aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Bagamoyo Michael Wage ambaye hivi karibuni alisimamishwa kazi na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa tuhuma za ubadhilifu pamoja na viongozi wengine wa Halmahauri ya Wilaya Bagamoyo.

Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo Suleimani Kova alikiri jeshi lake kumshikilia Muro na kuwa alimtishia Wage kuwa yeye ni Ofisa wa Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na kumtaka atoe fedha Sh milioni 10.

“Polisi inamhoji Muro dhidi ya tuhuma hizo na mahojiano yakikamilika taratibu za kisheria zitachukuliwa dhidi yake na maelezo zaidi nitayatoa kesho wakati wa mazungumzo yangu na waandishi wa habari” Kova alisema.

Bingwa huyo wa Tuzo za Uandishi wa Habari 2009 Tanzania alionekana akiwa sentro na mkononi ameshikilia bahasha tatu pamoja na kamera ya Video.

Alipohojiwa na wenzie juu ya kuhusika na tuhuma hizo alikana na kudai kushangazwa kuwekwa chini ya ulinzi kwa madai kuwa alipigiwa simu na mtu kupewa taarifa kuwa kuna kazi katika Hoteli ya City Garden.

“Kaka nilitaarifiwa tu kama ujuavyo kazi zetu kuwa kuna kazi City Garden niakaamua kwenda. Lakini baada ya kufika tu nilishangaa nawekwa chini ya ulinzi na askari kanzu ambao ndiyo walionifikisha kituoni hapa bila ya kunitajia kosa lanmgu. ” alilonga Muro.

Kwa upande wake Wage alidai kuwa mtuhumiwa anatumiwa na watu wengine ambapo juzi alimpandisha katika gari lake na kumfunga pingu kisha kumtaka atoe Sh milioni 10 na kwa kuthibitisha kuwa alikuwa ndani ya gari hilo alidai kuacha miwani yake yenye mikanda myeusi.

Polisi ilipomhoji Muro kama anazo pingu alikiri kumiliki pingu pamoja na bastola ambapo baada upekuzi katika gari lake lenye namba za usajili T 545 BEH polisi walikuta pingu hizo pamoja miwani iliyosemwa na mlalamikaji.

Muro alishinda tuzo ya Mwandishi bora wa mwaka kupitia vipindi vyake vya Televisheni vya "Usiku wa Habari" vinavyorushwa katika kituo cha TBC1 kila siku na kabla ya kuhamia hapo alikuwa kituo cha ITV na aliendesha kipindi cha "Ripoti Maalum".


Miongoni mwa mambo aliyokuwa akirusha katika vipindi hivyo ni pamoja na rushwa, matumizi mabaya ya madaraka pamoja na ukiukwaji wa sheria.

Polisi wamekuwa ni waathirika wakuu katika vipindi hivyo kwani mara mbili amewatoa Polisi Usalama barabarani wakiomba na kupokea rushwa hadharani kutoka kwa madereva wa malori na mabasi ya mikoani.

 
Mwanjelwa kumbe wewe bado unadhani umasikini ni tatizo?, its a fact ni tatizo wala usidhanie.

Pia ni kweli maisha ya waandishi wengi bongo ni down, ila hii isiwe sababu, kuna waandishi wengi tuu life iko poa, uandishi ni wito, wako waandishi wengi tuu life inawapiga sana, wamesoma profession nyingine zinazo lipa kama sheria, lakini bado wamengangana na uandishi pamoja na dhiki zake, what for? Its for the love of it, na ni kwa mapenzi haya, wanaishi maisha ya kimasini na furaha mioyoni mwao for doing what they love most.

Jerry is young, good and smart, ila siungani na wewe kuwa hushangai na is expected!. Sitaki kuamini na wewe uko kwenye hili kundi linalowaona vijana wadogo wakichipukia, mnakua na expectation ya kusubiri they downfall na ikitokea kama hii ya Jerry hamshangai kwa sababu mliexpect!.
Not you Mwanjelwa!.


NI kweli. Unaweza nishangaa sana. Lakini nimekupata mfano wa Koinage Jeff wa CNN. Unamkumbuka vema? Je unakumbuka nini kilimporomoa!? Na je vipi vipaji vingine vinavyokua na kuzimika ghafla? Umeweza fikiria ni kwanini? Kuna wanamusic, wanamitindo, wanasanaa, you name them. Wako wapi?!

Muro wa already juu sana; kwa definition ya Tanzania. Lakini ujana wake ulikuwa hauna msaidizi. Kujiingiza kwenye mitego ilikuwa ni rahisi sana sana. That is what face many young talents in Africa. Read between lines
 
I never thought Jerry anaweza kuwa dhaifu hivyo. Na bado siamini kama sio mpango wa kumchafulia jina


Ndiyo polisi Wabongo hao ni sawa sawa na Mafia. Wanalipiza kisasi cha Muro kuwakamatisha 13 miongoni mwao waliokuwa wanachukua rushwa. Na kwa jinsi Tanzania ilivyokuwa haina sheria huyu kijana anaweza kuharibiwa maisha yake bila kuwepo ushahidi wa kutosha na wakati huo huo mafisadi wa EPA, Richmond wakiendelea kupeta!
 
Jeshi la polisi Tanzania Bana.
huyo alietoa taaeifa hajui ofisi za TAKUKURU ama, Polisi nao kama ni kweli wanapapara sana, kwanini wasiandae utaratibu maridhawa ili wamkamate kwa ufanisi ma kuondoa hofu na mashaka yote dhidi ya mpiganaji Muro.
otherwise wajiandae kuumbuka kwa kujaribu kunyamazisha wapiganaji wa vita dhidi wa wezi na waomba rushwa.......
 
Jamani hivi haiwezekani kama ni mpango wa waovu kumchafulia baada ya kuona wanafichuliwa? Sasa wanadai kwenye gari lake amekutwa na pingu na bastola -ni vyake hivi?

Ingawa nimemsikia akihojiwa na waandishi wenzie ni kama ana kigugumizi vile! Kwani anadai hakuna shutuma zozote zinazomhusu na kuwa polisi wanamchukua kwa kupata taarifa juu ya jambo flani (hakulitaja)
 
Yeye alikuwa akifichua wapokea rushwa katika mazingira fulani, lakini hakusema kwamba yeye katika mazingira fulani hapokei rushwa. sasa cha ajabu nini?
 
swala hili inabidi liangaliwe kwa umakini..kuna mchezo tu umechezwa hapo ...
jamaa wameona kwa nini wao tu kila siki .....?
sina imani kama ni kweli au si kweli
 
Jeshi la polisi Tanzania Bana.
huyo alietoa taaeifa hajui ofisi za TAKUKURU ama, Polisi nao kama ni kweli wanapapara sana, kwanini wasiandae utaratibu maridhawa ili wamkamate kwa ufanisi ma kuondoa hofu na mashaka yote dhidi ya mpiganaji Muro.
otherwise wajiandae kuumbuka kwa kujaribu kunyamazisha wapiganaji wa vita dhidi wa wezi na waomba rushwa.......
Nguvumali hapo kwenye Blue wanadai Muro alikubaliana na huyo jamaa aliyemtaka rushwa kuwa wakutane hotel ya City garden mjini muda wa saa nne na yule jamaa aliwatip police nao wakafika na kumtia mbaroni Jerry- kinachonishangaza ni kuwa wanadai walipompekuwa wamemkuta na bastola iliyokuwa na risasi na kwenye gari lake walikuta pingu za police ambazo mdai alidai kuwa Jerry alimfunga pingu kabla hajampa hizo pesa- jamani something is fishy in this story- au Jerry amekuwa jambazi la kutembea na bastola au police mwenye bastola na pingu? Amevitoa wapi ah hawa wanataka tu kumchafulia
 
taarifa nilizopata muda si mrefu mwandishi wa habari aliyejipatia umarufu kwa kufichua rushwa za trafiki naye amekamatwa kwa kuomba rushwa ya milioni 10
Nitaafurahi ya JF bila kubeza wakanisaidia majawabu ya maswali haya juu ya kukamatwa kwa J. Muro

1. je,haifanani sana na "tumkomeshe nae amezidi kutufuatilia?"

2. waliomkamata ni PCCB au walewale anao watoa magazetini (polisi)?

3. Afisa mfukuzwa kazi toka Bagamoyo aliombwa hiyo hela kwa ajili ya nini?

4. Lengo la awali na afisa mfukuzwa kazi toka bagamoyo la kuacha miwani kwenye gari ya J.muro lilikuwa ni nini?

5.Polisi hamjui ya kwamba mnachokoza vita sasa wadau tuanze kumwaga picha lukuki za mambo yenu yaleeeeee

6. Polisi hamjui ya kwamba mkimuua Katabaro atazaliwa Rutayasingwa?
 
Back
Top Bottom