.
RUTAJUMBUKIRWA, Jerry ni product ya UDSM 1st Degree akafanya post graduate ya mambo ya media nje ya nchi, hivyo ni mwana taaluma msomi, no doubt, na ni mchapakazi hodari.
Kitaaluma alianza na TBC wakati huo TVT, ITV wakaruka dau, akahamia ITV, walipomletea zengwe, akarudi home na kupokelewa kama mwana mpotevu kwa dau kubwa.
Personal ni social, mtu wa watu mwenendo mzuri.
Ila utangazaji wowote, zaidi ya elimu na fani, ni kipaji, hivyo ili kuwa mtangazaji mzuri, sio lazima uwe umesoma sana. Watangazaji wengi wazuri wa zamani enzi zile za RTD, ni ma form four leavers ambao hawakuwa na sifa za kuendelea form five, lakini wamefanya kazi nzuri na wengi wakajiendeleza wengine mpaka chuo kikuu.
Miaka hiyo ilikuja ingia timu ya vijana wadogo wasomi mahiri na masters za journalism toka nchini za Mashariki, Urusi, Bulgaria, Cuba etc, ikatokea hawawezi kazi pamoja shule zao nzuri, wengi wameishia kwenye green pastures za PR ambazo cheti kinamater zaidi kuliko kipaji.
Utekelezaji wa maadili ya uandishi unategemea personal morals na situation husika. Mimi binafsi, japo siungi mkono rushwa wala kuendekeza njaa, naunga mkono kwa asilimia 100% those little brown envelopes ambazo waandishi hupewa, hizi sio rushwa ni facilitation tuu ili vijana wafanye kazi zao vizuri na wala sio motisha maana they are too little.
Wako waandishi wasomi wazuri na ndio wasimamizi wa maadili, wengine wanasolicit rushwa kubwa kwa blackmail, na wengine wananunuliwa na wenye fedha zao, kwa lile jukwaa la wahariri liko wapi siku hizi baada ya kilichomkuta Sakina?.
Naungana na hoja za kutohukumu wote kwa makosa ya wachache, na suala hili la Jerry, tusihukumu kwanza, tusubiri facts zaidi.