I'll tell you why I'm laughing (if you didn't notice); Muro ameitwa kwenda mahali ambapo ameahidiwa kukatiwa kitu kidogo.. anatoa taarifa kwa vyombo husika (in this case, say TAKUKURU) na anaandaa watu wake wa kurekodi kitu hicho. Yule mtu mwingine anatoa taarifa kwa vyombo husika (lets assume ni Polisi); Polisi wanaandaa mtego wa kumtia matatani Muro, na mura anaandaa mtego kumtia matatani jamaa ili amrushe katika kipindi chake.
Well.. anaenda pale anakabidhiwa mzigo (polisi wanachekelea wamemnasa). Na mara moja wanaanza kujitamba kuwa jamaa anayepiga vita rushwa ndiyo huyo kakamatishwa. Habari zinaruka haraka haraka na wanamkimbiza Muro kituoni, sms zinaenea, na hadithi kolea.
Muro anafikishwa kituoni anapigishwa mkwara na maneno kibao. Anapewa nafasi ya kujitetea. Anawaambia "mna wazimu".. wanashangaaa..
should I tell you how the story end?