TBC journalist Jerry Muro held over alleged graft

Jerry atawageuka,hawana njia,wamelikoroga na sasa itabidi walinywe.
 
Ukiwa unamiliki bastola huwa unatakiwa kutembea na copy za vibali kuthibitisha kuwa huyo sila ni yako kihalali mtu yeyeote anayetembea na bastola muda wote hivyo vitu huwa anakuwa navyo kwenye gari lake na hata wakati wa kununua hiyo bastola wanakwmbia kabisa toa copy halafu wanaithibitisha maana huwezi tembea na document orignal muda wote kuna kupoteza ama zikachaa

Mkuu una uhakika na ulichokisema kwamba ukiwa unamiliki bastola lazima pia utembee na copy za document? Kuna sababu gani za msingi kutembea na docs? Unafikiri askari makini akikukamata na bastola atakubali umuonyeshe copy za kibali kuimiliki hiyo silaha halafu akuachie? Hebu fikiria mara mbili!!!!!

Tiba
 
Swali langu ni kuwa pingu alikuwa anazitumia kwa ajili gani?

Ingawa hata kamba ni pingu..hizo ni pingu za chuma tu na sidhani kama kuna kosa kumiliki pingu. Ila alikuwa nazo za nini?

say kwa ajili ya mambo ya mapenzi na mwandani wake akirudi nyumbani; kwani ni kosa hilo? Hata miye ninazo za rangirangi..
 
Mimi nina mashaka sana na Muro. Lazima kuna issue. Tusubiri na tutaongea hapa hapa JF

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limesema lilimshikilia na kumhoji mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Jerry Muro, baada ya kupata taarifa kutoka kwa mwananchi aliyelalamika kwamba kuna matapeli wamekuwa wakimtisha wakimdai rushwa.

Aidha, limesema halina tatizo lolote na mwandishi huyo kama taarifa zilivyovuma na badala yake linafanya kazi kulingana na sheria na taratibu zake.

Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Suleiman Kova alisema hayo jana wakati akizungumza na wanahabari na kumtaja mwananchi huyo kuwa ni Michael Wage, ambaye alikuwa Mweka Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, kabla ya kuvuliwa wadhifa huo na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutokana na ubadhirifu wa fedha.

Alisema Wage alifika katika kituo Kikuu cha Polisi juzi saa 5 asubuhi na kulitaarifu Jeshi hilo, kwamba kuna watu watatu ambao wanajifanya maofisa wa Polisi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), waandishi wa habari na wanajeshi huku wakitoa vitisho wakitaka wapewe Sh milioni kumi.

Alisema mwananchi huyo alilalamika kwamba watu hao wamekuwa wakimwandama na kumsumbua tangu Januari 28 mwaka huu, wakidai kwamba yeye ni fisadi na ana majumba mengi ya kifahari Morogoro, hivyo walitaka wapewe hongo hiyo ili wasimkamate.

Aidha, Kova alisema mwananchi huyo alidai kwamba watu hao ambao walikuwa na pingu, wamekuwa wakimwambia kwamba asipotoa fedha hizo watamchukulia hatua na kumtangaza katika jamii kwa ufisadi.

“Wage alipokuja kwetu, alisema hatoi fedha na anataka watuhumiwa hao wakamatwe na wakawekeana miadi ya kukutana saa 6 mchana katika hoteli ya City Garden katikati ya Jiji kwa makubaliano kwamba watapeana fedha hizo katika eneo hilo ... polisi walifikiri ni matapeli na tukaenda muda huo,” alisema.

Alisema baada ya kufika katika eneo hilo, lengo likiwa ni kuwakamata matapeli hao, gari namba T 545 BEH aina ya Toyota Cresta, liliingia lakini mwenyewe alikataa kushuka na kumtaka Wage alifuate gari hilo.

“Polisi wangu walipoona gari limekuja na watuhumiwa kukataa kushuka, walilifuata na walipofika walishangaa kumwona Jerry Muro na baada ya Wage kusema huyu ndiye ambaye amekuwa akimsumbua sana, polisi ilibidi wamchukue mpaka kituoni ili kupata maelezo mazuri,” alisema.

Kova alisema mlalamikaji huyo alikuwa akidai kwamba anamfahamu Jerry na amekuwa akimsumbua hata kumfuata nyumbani kwake na kukubaliana wakutane jijini Januari 29 mwaka huu na kutoa vithibitisho mbalimbali kwamba anamfahamu ikiwa ni pamoja na miwani yake aliyokuwa ameiacha ndani ya gari lake.

“Wage aliileza Polisi vithibitisho vilivyopatikana katika gari la Jerry ikiwamo miwani yake aliyoisahau, pia alieleza kwamba Jerry anatembea na bastola na pingu na vyote tulivipata katika gari lake na kumhoji ambapo alikiri kuvimiliki,” alisema.

Alisema pingu zilipatikana kwenye ‘dash board’ huku silaha ikiwa kiunoni na katika uchunguzi wa awali wa maeneo yaliyohusishwa na tukio hilo na uhusiano baina ya watu hao, polisi ilifanya upelelezi na kupata uthibitisho kupitia CCTV.

“Pia napenda mfahamu hakuna suala la Jeshi la Polisi na Muro, isipokuwa kuna mlalamikaji na Polisi na hata kama angekuwa ni askari ametenda kosa kama hilo, angechukuliwa hatua za kisheria … Jeshi la Polisi Kanda Maalum hatuna ugomvi na Muro na ni rafiki yetu sana,” alisema.

Alikiri kutambua umiliki halali wa Muro wa bastola CZ97B namba A6466 na kwa upande wa pingu, Kova alisema ni kinyume cha sheria kutokana na kwamba pingu humilikiwa na Polisi au Magereza pekee.

Pia Kamanda alisema Jeshi hilo limemtaka Muro, kuwasilisha risiti ya pingu hiyo, kutokana na kwamba hakuna sehemu yoyote inapouzwa na sheria haimruhusu mtu yeyote kumiliki labda kampuni na ni kwa kibali maalumu.

“Silaha kama hii ukimwonesha mtu ni lazima ashtuke … hivi hata kama wewe ni mwandishi wa habari za uchunguzi, pingu zinahusiana vipi na utafutaji habari? Hii pingu ukimwonesha mtu tena aliyeumwa na nyoka kama Wage lazima ashtuke,” alisema.

Hata hivyo Kova alisema kuwa kesi hiyo haitaenda mahakamani mpaka ipitie kwa wakili wa serikali na kueleza kwamba Jerry yupo nje kwa dhamana na kuwataka watuhumiwa wengine wawili wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo wajisalimishe.

Muro ameibuka kuwa mtangazaji mahiri kwa mwaka 2009 na kujinyakulia tuzo ya Mwandishi Bora wa Mwaka kupitia vipindi vyake vya Televisheni vya Usiku wa Habari vinavyorushwa katika kituo cha TBC1 na kabla ya kuhamia kituo hicho alikuwa akiendesha kipindi kama hicho katika ITV.

Miongoni mwa mambo aliyokuwa akirusha katika vipindi hivyo ni pamoja na rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na ukiukwaji wa sheria na polisi wamekuwa walengwa wakuu wa vipindi hivyo.

Wakati huo huo, Simon Nyalobi anaripoti kuwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) limelitaka Jeshi la Polisi nchini kufanya uchunguzi haraka na kumfikisha mahakamani Muro ili haki iweze kutendeka.

Akizungumzia suala la kukamatwa kwa Muro, Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga, alisema hatua iliyochukuliwa na Polisi dhidi ya Muro yawezekana zikawa ni njama za kumtisha asiendelee na uchunguzi wake wa tuhuma kubwa kubwa.

“Muro ana kashfa zingine kubwa anazifuatilia zinazowahusu vigogo wa Serikali, yawezekana hii ni mbinu ya kutaka kumdhoofisha asiendelee na uchunguzi wake … lakini kama ni kweli aliomba rushwa, basi atakuwa ameidhalilisha taaluma ya habari,” alisema Mukajanga alipozungumza na waandishi wa habari jana.

Hata hivyo, alisema Muro asitumiwe kama kondoo wa kafara na kuwaasa waandishi wa habari kuwa makini katika kazi zao wakati huu hususan mwaka huu wa uchaguzi kwani lolote linaweza kuwatokea.
 
Muro siyo msafi wa kuandika habari za RUSHWA...🙁; Mara nyingi katika press conference amekuwa akipokea na kudai mshiko hili habari itoke. Kwanza hana mamlaka ya kuamua kutoa au kutokutoa habari, pili kwa kudai mshiko habari itoke anabaka taalumua ya uandishi.

Amechafua pia maana nzima ya tuzo ya uandishi wa habari na kutia aibu. Baadhi humu tunamfahamu kwa kudai mshiko na amepokea mishiko mingi sana.

Watanzania tuache ushabiki wa mambo tusiyoyafanyia utafiti.

Kwa nini wewe uliyemsafi usiende kutoa hizo habari za RUSHWA? Itasadia zaidi kuliko kulalalam hivyo. Na hiyo tuzo tutakupa wewe ili iwe na maanza zaidi. Go ahead and do it ...

Au ungeanza kwa kumrekodi ma kumtoa yeye akidai na kupokea mshiko; haki ya nani ile tuzo tutakupa wewe. Inaelekea unajifunza pole pole sana kwamba tunaamini kwa haraka zaidi picha zilizosimama na za video kuliko maneno matupu unayojaribu kutulisha hapa.
 
Jerry anajua anachokifanya refer to his statement. "Aulize nimevitoa wapi, Kova is a very minor person, siyo jeshi la polisi yule na vitu siyo vya leo nina mwaka nao wa nne"

Statement hii ina ujumbe mkubwa sana kuhusu umiliki wa Jerry wa hivi vitu. Sema tu kwamba akibwabwaja sana atajikuta anavunja miiko ya kazi yake

Kwa hiyo mkuu unataka kusema Jerry naye ni ..oka?
 
Huyu bwana Wage tayari alishamwaga unga wake kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa fedha masiku kadhaa yaliyopita, na issue yake ilisharipotiwa kwenye vyombo vya dola.

Swali ni kwa nini Muro aombe rushwa ili asitoe habari ya mtu ambaye tayari habari zake za ubadhirifu wa fedha ulishatoka kwenye vyombo vya habari na tayari alikuwa hana kazi? Haiingii akilini.

Swali la nyongeza, je swala la ubadhirifu wa fedha wilayai Bagamoyo ni Muro aliliibua na ndipo Mizengo akachukua hatua za kuwawajibsha watendaji husika huko Bagamoyo?
 
You freak..

I ain't no freak.. I spicy it up baby! Hao polisi ningeombea waniulize pingu ya nini? I would have asked for a female volunteer to demonstrate infront of TV audience! You never.. konow.. tunaanzisha soko la pingu hivi hivi!! shoot.
 
Yes. Ukifumaniwa na mke wa mtu wakati wewe ni mme wa mtu, kosa au tatizo lako litakuwa kwa mkeo, na labda na mwenye mke pamoja na heshima mtaani. Lakini huku bado ukiwa una kashfa ya hilo fumanizi, jamaa mwingine anakuja anakwambia nipe hongo (rushwa) vinginevyo nita-release picha zinazoonyesha ukiwa na minor (mtoto mdogo wa shule au underage) chumbani unamshughulikia!. Utakataa kwa kuwa tayari una kesi ya fumanizi ya mke wa mtu?

Kuwa na under-age Tanzania kwa sasa kisheria adhabu yake si chini miaka 30.
 
Kuna uthibitisho kuwa Wage ndiye aliyemtaka Jerry afike kwenye eneo alilokamatwa?
 
Back
Top Bottom