TBC journalist Jerry Muro held over alleged graft

TBC journalist Jerry Muro held over alleged graft

Ndio kwanza nimemaliza kusoma kitabu cha mwandishi Sandelin Wundrak; The History Of Economic Thinking. Kisha nimepitia mtandaoni taarifa mbali mbali. Ndio, kwa hapa nyumbani, Jerry Muro ni habari kubwa, ni mshtuko.

Jerry Muro. Sijapata kukutana naye. Nimefuatilia kazi zake tu, kwa kazi zake anaonekana kuwa ni kijana mahiri. Katika lililomfika, nina-sympathy nae. Yuko katika kipindi kigumu sana. Kwa mwanadamu mwenzako, ni kumpa pole tu, hayo mengine ni ya baadae.

Juu hapo mnaona picha ya ukuta. Ndio, bado natafakari ziara yangu ya siku moja pale kijijini Kalenga, ni kwenye ngome ya Chifu Mkwawa wa Wahehe. Nilikwenda huko Jumamosi ya juzi hapa. Mkwawa ni yule shujaa aliyewatoa jasho Wajerumani. Katika kupitapita kwangu mitaa ya kijiji hicho nilikutana na ukuta huo.
Nikakumbuka tungo ya ndugu yangu Mrisho Mpoto; "Ni heri kujenga daraja, kuliko ukuta!" Ningependa nikutane na mwenye nyumba au mwenye ukuta huo unaokaribia kuanguka. Nilitaka tujadili juu ya ukuta wake, kifalsafa zaidi. Hakuwepo nyumbani. Alikuwa shambani akipalilia mahindi yake, anaitwa Baba Gile ( Baba Grace).

Ndugu yangu Mrisho Mpoto, labda si heri kujenga daraja wala ukuta. Labda Baba Gile wa kijijini Kalenga angeniambia kipaumbele chake na cha wenzake ni kujengwa kwa njia mbili za mawasiliano; kati ya kiongozi na mwongozwa.

Naam. Aliye gizani anamwona aliye kwenye mwanga, lakini aliye kwenye mwanga hamwoni aliye gizani. Na ajionaye yuko kwenye mwanga aweza kabisa kuwa yu gizani na asimwone kabisa aliye kwenye giza jingine. Haiyumkini aliye topeni akajaribu kumwinua mwingine aliye topeni, wote watadidimia topeni!

Unajiuliza, yanahusianaje na Jerry Muro? Hii ni tafakari endelevu, haihusiani na Jerry Muro, bali inamhusu kila mmoja wetu akiwamo Jerry Muro. Inahusu maisha.
Maisha ni mapambano, kuna kushinda na kushindwa. Ushindi una gharama. Mwanadamu jiandae na gharama ya ushindi. Ushindi waweza kuwa ghali mno. Unaweza kupambana ukashinda, lakini gharama ya ushindi yaweza kuwa jamaa na marafiki wa wote uliowashinda watageuka kuwa maadui zako, yawezekana watakuwa maadui kwako kwa muda mrefu tu. Watakukasirikia, watafanya yote nawe upate maumivu.

Hivyo, mwanadamu usifikiri tu gharama ya kushindwa, fikiri pia gharama ya ushindi. Na wakati mwingine ni gharama inayostahili kulipwa. Franklin Roosevelt alikuwa Rais wa zamani wa Marekani. Alifahamu faida na hasara za kuwa na maadui. Waliompinga katika sera zake za kiuchumi aliwaita " Watiifu wa Kiuchumi" Na akasema; wamejiunga kwa pamoja kunichukia na nakaribisha chuki zao kwangu!

Kama unapigana vita ya muhimu, kama vita hivyo vyaweza vikawa vya kushinda ( winnable). Na kwamba umejiandaa kulipa gharama ya chuki ya muda mrefu ya utakaowashinda, basi, ingia vitani, na kama la, tafuta suluhu au rudisha majeshi nyuma kimpangilio ( tactical retreat).

Swali ni hili; utafikiaje uamuzi wa ama kuingia vitani au la? Saa yangu inaniambia ni saa saba usiku hapa Iringa. Naweza kuendelea kutafakari usiku kucha, nahitaji kulala. Nawe endelea kutafakari.
Maggid
Iringa
Tembelea: http://mjengwa.blogspot.com
 
I ain't no freak.. I spicy it up baby! Hao polisi ningeombea waniulize pingu ya nini? I would have asked for a female volunteer to demonstrate infront of TV audience! You never.. konow.. tunaanzisha soko la pingu hivi hivi!! shoot.

MMM,
Thumbs up!!!!
Watanzania wengi hawajui mambo ya fetish....minyororo,pingu,mikwaju,masks etc is part of the game.
 
Jana nilikuwa namsikiliza huyo Kamanda Kova hata sijaelewa alikuwa anongea vitu gani
maneno yako yako ni mazito na ya simanzi
 
Jana nilikuwa namsikiliza huyo Kamanda Kova hata sijaelewa alikuwa anongea vitu gani
maneno yako yako ni mazito na ya simanzi
 
Haya ni maneno mazuri sana bra maggid
Pili nimpe pole bra Jerry kwa yaliyomkuta, atashinda siku si nyingi
Tatu nikuulize swali bra maggid "hii falsafa ya kushinda na kushindwa inachochewa na na nini?" Je unazungumziaje maisha ya kutafakari ushindi pasipo anguko?
 
Ujumbe mzito ndugu yangu Maggid, especially the last two paragraphs!
 
Ujumbe mzito ndugu yangu Maggid, especially the last two paragraphs!
 
http://www.youtube.com/watch?v=cl2Ow-Goxvc
haya sheshe ndo hilo,na jamaa kakutwa na pingu na bastola risiti hana,watu wengine unawaona kama watiifu kumbe ni majambazi na waporaji,sasa hii unaweza sema polisi walimbambikia lakini inaonekana jamaa nae kabugi mahali,naona polisi wameamua tu kumshtua kama anajisahau kama na yéye mchafu vilevile.

siujui nisemeje,
lakini kila kitu kinawezekana chini ya jua.
jerry Muro huenda alikutwa na pingu na bastola,
lakini je ni yeye aliyeziweka?
Polisi wana mbinu nyingi sana za kijasusi, huenda walivitupia humo kwenye gari ya muro bila ya yeye kujua, ili kumkomoa kutokana na mwandishi huyo kuwaumbua.
 
Mkuu Maggid! ujumbe ni nzito na inauzunisha na kusikitisha na kwa upande wa Jerry kweli yuko kwenye kipindi kigumu na kizito kwa upande mwingine kwa waliobaki (wanahabari) wajue wapo kwenye mapambano wasirudi nyuma hayo ni mapito ya hali ya hewa, kuna kiangazi, kipupwe, masika hivyo vyote ni vipindi vya mipito vya majira ya hali ya hewa. Daima mapambano mbele kamwe wasirudi nyuma
 
Wamekwama kumchafulia jina, sasa wamempamba na kumuinua juu washinde na walegee haooo...

Sasa na hao watu wawili waliokamatwa ambao wametuhumiwa kushirikiana na Muro katika kutaka rushwa hii ni kina nani? Jamani mie naanza kupoteza imani kwa Jerry ... au ni kwa vile siwajui vizuri polisi wa Tanzania zaidi ya rangi ya magwanda yao?
 
Tungalie hii ngoma. Ila mdundo wake mkubwa sana!
Tanzania sio kuna miujiza au vituko ila ni kichaa, nimesafiri kutoka Mwanza kwenda shinyanga kwa gari njiani kuna Check Points za Jeshi Tukufu la Polisi zaidi ya Sita na zote zina polisi wenye SMG waliovaa ki Raia(Wasio na Vazi Rasmi) Wanaonekana kama Vibaka, Je utaweza kutambua Check Point ya Polisi au Majambazi.
Tena Wanakagua kuanzia Wasafiri mpaka kazi za Traffic.
 
Back
Top Bottom