Video: Kova azungumzia sakata la Jerry Muro

Hivi huwa ukikutwa na bastola unaulizwa risiti au wanatakaga kujua kama unaimiliki kihalali?? mbona mimi nazidi kuwa confused?????
 
Swali langu ni kuwa pingu alikuwa anazitumia kwa ajili gani?

Ingawa hata kamba ni pingu..hizo ni pingu za chuma tu na sidhani kama kuna kosa kumiliki pingu. Ila alikuwa nazo za nini?
 
bro jerry mtu mdogo sana kufananisha na kesi ya kombe,jerry ni mwandishi wa habari kijana tu,kwa ninavyoijua bongo mimi,sawa inaweza kuwa polisi walimbambikia lakini inaonekana hata yeye alishaingia kingi mil 10 za chapchap kijana yeyote ofisi yeyote bongo haziachi mzee,haya licha ya mambo ya rushwa vitu alivyokamatwa navyo ndio msala zaidi,na sidhani kama mtu anaweza kubambikiwa kisha kutishwa asitoe ukweli hasa kwa mwandishi wa habari,anyway story yote ni kizungumkuti tu,mi nataka na yeye atoe maelezo yake tusikie,lakini kaambiwa hatakiwi kusema chochote na kakubali,ndo mana nasema kuna mahali muro atakua kakosea na ndio maana kakaa kimya atherwise tungesikia mengine kabisa.
BK hivi kwa mtu kama JM anajijua fika yeye anawindwa kwa udi na uvumba kuhusu kuwalipuwa wala rushwa na madhambi mengineo kweli akurupuke tu akachukue rushwa ya 10 milioni kwa mtu alifukuzwa kazi na PM inakujia akilini kweli. JM anamlaka yapi ya kumrudisha mtu kazini alie fukuzwa kazi na PM. Huyo mhasibu alietimuliwa kazi kwani JM ndie alie sababisha ama ni uzembe wake kazini hadi ukafika kwa bosi wake PM akatimiliwa.
Hizi zote habari nakwambia ni ujanja wa kumnyamazisha JM asiendelee na mapambano yake ya kupinga rushwa.
JM kama upo jamvini usife moyo wala usikate tamaa mapambano bado yanaendelea wembe ni uleule
 
Hivi huwa ukikutwa na bastola unaulizwa risiti au wanatakaga kujua kama unaimiliki kihalali?? mbona mimi nazidi kuwa confused?????

Ukiwa unamiliki bastola huwa unatakiwa kutembea na copy za vibali kuthibitisha kuwa huyo sila ni yako kihalali mtu yeyeote anayetembea na bastola muda wote hivyo vitu huwa anakuwa navyo kwenye gari lake na hata wakati wa kununua hiyo bastola wanakwmbia kabisa toa copy halafu wanaithibitisha maana huwezi tembea na document orignal muda wote kuna kupoteza ama zikachaa
 
mimi namiliki bastola, kihalali....nyaraka hupaswi kutembea nazo , unless uwe unakwenda mbali na mkoa wako unaoishi.

swali ...POLICE wa TANZANIA wameanzalini kuwaachia majambazi wanaokamatwa wanamiliki silaha haramu, maana kwa tafsiri ya kamanda Muro ni jambazi ama muhalifu, mbona kapewa dhamana kabla ya upelelezi ? je kuna double standard ya implementation ya sheria hapa nnchini. tuendelee kufikiri
 
hawa police nao Jerry akutwe na pingu kwani yeye ni police ..alinunua hizo pingu za kumfungia nani??
 
hawa police nao Jerry akutwe na pingu kwani yeye ni police ..alinunua hizo pingu za kumfungia nani??

mamii in this country anything is possible!!! mi hii habari inanipa kizunguzungu, toka nimeisikia jana mpaka sasa hivi bado kuna vitu nashindwa kuunganisha, ngoja nitulie kwanza.....!!!!!!
 
mamii in this country anything is possible!!! mi hii habari inanipa kizunguzungu, toka nimeisikia jana mpaka sasa hivi bado kuna vitu nashindwa kuunganisha, ngoja nitulie kwanza.....!!!!!!
inafikirisha.
 
wajameni... Bastola anamiliki kihalali kabisa. Mimi hilo nalijua. Lakini pingu ndio litu ambacho sielewi.
 
haya sheshe ndo hilo,na jamaa kakutwa na pingu na bastola risiti hana,watu wengine unawaona kama watiifu kumbe ni majambazi na waporaji,sasa hii unaweza sema polisi walimbambikia lakini inaonekana jamaa nae kabugi mahali,naona polisi wameamua tu kumshtua kama anajisahau kama na yéye mchafu vilevile.

Ina mana hiyo bastola kaanza kuimiliki jana? kama alikuwa nayo mbona hawakumkamata nayo kabla? Mbona mpaka alipovumbua jambo no yote haya yametokea? akili kumkichwa.............
 
jamani kilichobaki kila mwanahabari kuwa makini na shughuli aifanyayo maana jamaa ndo kakutwa na pingu ambayo haiusiani na tasnia ya habari
 
Mbinu za ki Police zimetumika ku mmaliza Jerry, Hakuwa mwangalifu wa hawa watu aliokuwa akiwa umbua.
Hamna ubishi hiyo ni '' pre aranged deal'' anaye bisha na abishe.
 
JM ni kijana mwenye bidii kikazi na tumeona kazi nzuri alizozifanya kama mzalendo kufichua maovu yanayofanyika na baadhi ya askari,lakini kwa asili kila binadamu ni mhalifu kiwango cha uhalifu kinatofautiana kutokana na mazingira alipo mtu huyo,JM si msafi sana naye kuna mazingira ya shughuli zake yanamusukuma kufanya uovu polisi hawatoi hukumu tusubiri.
 
Ina mana hiyo bastola kaanza kuimiliki jana? kama alikuwa nayo mbona hawakumkamata nayo kabla? Mbona mpaka alipovumbua jambo no yote haya yametokea? akili kumkichwa.............

Kwani wao ni malaika mpaka wajue bila kupewa taarifa? Kweli hapa ni "akili kumkichwa!"
 
Hivi jamani......kweli inakujia akilini mtu amakutwa na bastola iko full hana risiti alafu akaachiwa kweli kwa dhamana ya kujizamini mwenyewe???? labda hizo stori wapelekwe watoto wa chekechea hata mtua asie enda darasani hatawaelewa?????

Yes, inakujia akilini, because it is a bailable offence! Labda kama ingekuwa ni suala la mauaji, uhaini, etc ndio hakuna dhamana! Remember Zombe et al. Kwani alipojidhamini mwenyewe ameshakimbia au kuharibu ushahidi?
 
Jerry naye atoa maelezo yake hii kitu smells fishy.

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=eUB9B2XfxVw[/ame]
 
Back
Top Bottom