Video: Kova azungumzia sakata la Jerry Muro

Video: Kova azungumzia sakata la Jerry Muro

Huyu bwana Wage tayari alishamwaga unga wake kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa fedha masiku kadhaa yaliyopita, na issue yake ilisharipotiwa kwenye vyombo vya dola.

Swali ni kwa nini Muro aombe rushwa ili asitoe habari ya mtu ambaye tayari habari zake za ubadhirifu wa fedha ulishatoka kwenye vyombo vya habari na tayari alikuwa hana kazi? Haiingii akilini.

Swali la nyongeza, je swala la ubadhirifu wa fedha wilayai Bagamoyo ni Muro aliliibua na ndipo Mizengo akachukua hatua za kuwawajibsha watendaji husika huko Bagamoyo?
 
You freak..

I ain't no freak.. I spicy it up baby! Hao polisi ningeombea waniulize pingu ya nini? I would have asked for a female volunteer to demonstrate infront of TV audience! You never.. konow.. tunaanzisha soko la pingu hivi hivi!! shoot.
 
Huyu bwana Wage tayari alishamwaga unga wake kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa fedha masiku kadhaa yaliyopita, na issue yake ilisharipotiwa kwenye vyombo vya dola.

Swali ni kwa nini Muro aombe rushwa ili asitoe habari ya mtu ambaye tayari habari zake za ubadhirifu wa fedha ulishatoka kwenye vyombo vya habari na tayari alikuwa hana kazi? Haiingii akilini.

Swali la nyongeza, je swala la ubadhirifu wa fedha wilayai Bagamoyo ni Muro aliliibua na ndipo Mizengo akachukua hatua za kuwawajibsha watendaji husika huko Bagamoyo?

Yes. Ukifumaniwa na mke wa mtu wakati wewe ni mme wa mtu, kosa au tatizo lako litakuwa kwa mkeo, na labda na mwenye mke pamoja na heshima mtaani. Lakini huku bado ukiwa una kashfa ya hilo fumanizi, jamaa mwingine anakuja anakwambia nipe hongo (rushwa) vinginevyo nita-release picha zinazoonyesha ukiwa na minor (mtoto mdogo wa shule au underage) chumbani unamshughulikia!. Utakataa kwa kuwa tayari una kesi ya fumanizi ya mke wa mtu?

Kuwa na under-age Tanzania kwa sasa kisheria adhabu yake si chini miaka 30.
 
Kuna uthibitisho kuwa Wage ndiye aliyemtaka Jerry afike kwenye eneo alilokamatwa?
 
Na funguo za gari za Muro kupotea katika mazingira ya kutatanisha hadi akaagiza funguo nyingine nyumbani ili afungue gari ije kupekuliwa, na kabla funguo alizoagiza hazijaletwa, funguo za mwanzo zikapatikana katika mazingira ya kutatanisha. Je inawezekana kuwa hizo risasi na miwani ya jamaa vilipandikizwa?
 
me na mume wangu tunapenda sana kufatilia kipindi cha ucku wa habari, sio mara moja au mbili mume wangu amewahi kusema kuhusu speed ya Jerry, na haya yaliotokea alishayatabiri so am not suprised at all maana tulijua yatatokea tu!!
 
dont be suprised, this is tanzania bwana.........
 
Jerry mwandishi wa habari pingu na bastola vyanini, pingu haziuzwi popote bongo bastola sawa waweza sema ulinzi wake haya risiti hana na imekutwa loaded.[/QUOTE]

Hapo ndipo kwenye utata, Inawezekana jamaa wanataka kumfanya victim kwa kisasi, lakini hilo swala la mtu kumiliki pingu inakuwaje? Ni yule mzee wa Bagamoyo alisema kuwa Muro anamiliki Bastola na Pingu (kwa mujibu wa Kova), na kweli walimkuta navyo hivyo na amekubali kuwa ni vyake, sasa bunduki ni sawa ila Pingu inakuwaje? Jamaa yupo kwenye utata ingawa jamii inaona kuwa ni kisasi
 
Kabisa naungan na wewe, kwanza bado najiuliza kwanini gari lake lilindwe na askari likiwa kituoni??? pili ile funguo yake mbona ilipotea ktk mazingira yasio eleweka halafu baada ya kupiga cm kwao aletewe funguo nyingine ile ikaonekana ilikwenda wapi??
Kweli polisi wamechemka wajipange upya tena


Polisi hawana kesi bali wamembabika huyu kijana kama kulipiza kisasi. Ogopa polisi bongo wanaweza kabisa kukumaliza na wakaweka ushahidi fake ili wakuingize hatiani na hivyo kukuharibia maisha.
 
Watanzania lazima tuwe na mawazo pambanuzi.Kova maelezo aliyoyatoa na kifungu cha sheria alichomhusisha nacho Muro ni usanii mtupu.Polisi wanataka kulipiza kisasi tu baada ya kuumbuliwa.Polisi wa Tanzania(Trafiki) rushwa wanazochukua kuna mgawo wa wakubwa zao.Kovo anajua hili alikuwa RPC Mbeya na mambo haya anayajua vizuri sana hivyo huo usanii wake hautamfikisha mbali.Polisi wamekuwa PCCB siku hizi?
 
292.​
​
​
​
Any person who, with intent to steal any valuable thing,
demands it from any person with menaces or force, is guilty of a
​

felony, and is liable to imprisonment for five years.Haka ndiyo kakifungu alikosema Kova haya wanasheria tupeni nondo hapo.
 
Ndio kwanza nimemaliza kusoma kitabu cha mwandishi Sandelin Wundrak; The History Of Economic Thinking. Kisha nimepitia mtandaoni taarifa mbali mbali. Ndio, kwa hapa nyumbani, Jerry Muro ni habari kubwa, ni mshtuko.

Jerry Muro. Sijapata kukutana naye. Nimefuatilia kazi zake tu, kwa kazi zake anaonekana kuwa ni kijana mahiri. Katika lililomfika, nina-sympathy nae. Yuko katika kipindi kigumu sana. Kwa mwanadamu mwenzako, ni kumpa pole tu, hayo mengine ni ya baadae.

Juu hapo mnaona picha ya ukuta. Ndio, bado natafakari ziara yangu ya siku moja pale kijijini Kalenga, ni kwenye ngome ya Chifu Mkwawa wa Wahehe. Nilikwenda huko Jumamosi ya juzi hapa. Mkwawa ni yule shujaa aliyewatoa jasho Wajerumani. Katika kupitapita kwangu mitaa ya kijiji hicho nilikutana na ukuta huo.
Nikakumbuka tungo ya ndugu yangu Mrisho Mpoto; "Ni heri kujenga daraja, kuliko ukuta!" Ningependa nikutane na mwenye nyumba au mwenye ukuta huo unaokaribia kuanguka. Nilitaka tujadili juu ya ukuta wake, kifalsafa zaidi. Hakuwepo nyumbani. Alikuwa shambani akipalilia mahindi yake, anaitwa Baba Gile ( Baba Grace).

Ndugu yangu Mrisho Mpoto, labda si heri kujenga daraja wala ukuta. Labda Baba Gile wa kijijini Kalenga angeniambia kipaumbele chake na cha wenzake ni kujengwa kwa njia mbili za mawasiliano; kati ya kiongozi na mwongozwa.


Naam. Aliye gizani anamwona aliye kwenye mwanga, lakini aliye kwenye mwanga hamwoni aliye gizani. Na ajionaye yuko kwenye mwanga aweza kabisa kuwa yu gizani na asimwone kabisa aliye kwenye giza jingine. Haiyumkini aliye topeni akajaribu kumwinua mwingine aliye topeni, wote watadidimia topeni!

Unajiuliza, yanahusianaje na Jerry Muro? Hii ni tafakari endelevu, haihusiani na Jerry Muro, bali inamhusu kila mmoja wetu akiwamo Jerry Muro. Inahusu maisha.
Maisha ni mapambano, kuna kushinda na kushindwa. Ushindi una gharama. Mwanadamu jiandae na gharama ya ushindi. Ushindi waweza kuwa ghali mno. Unaweza kupambana ukashinda, lakini gharama ya ushindi yaweza kuwa jamaa na marafiki wa wote uliowashinda watageuka kuwa maadui zako, yawezekana watakuwa maadui kwako kwa muda mrefu tu. Watakukasirikia, watafanya yote nawe upate maumivu.

Hivyo, mwanadamu usifikiri tu gharama ya kushindwa, fikiri pia gharama ya ushindi. Na wakati mwingine ni gharama inayostahili kulipwa. Franklin Roosevelt alikuwa Rais wa zamani wa Marekani. Alifahamu faida na hasara za kuwa na maadui. Waliompinga katika sera zake za kiuchumi aliwaita " Watiifu wa Kiuchumi" Na akasema; wamejiunga kwa pamoja kunichukia na nakaribisha chuki zao kwangu!

Kama unapigana vita ya muhimu, kama vita hivyo vyaweza vikawa vya kushinda ( winnable). Na kwamba umejiandaa kulipa gharama ya chuki ya muda mrefu ya utakaowashinda, basi, ingia vitani, na kama la, tafuta suluhu au rudisha majeshi nyuma kimpangilio ( tactical retreat).

Swali ni hili; utafikiaje uamuzi wa ama kuingia vitani au la? Saa yangu inaniambia ni saa saba usiku hapa Iringa. Naweza kuendelea kutafakari usiku kucha, nahitaji kulala. Nawe endelea kutafakari.
Maggid
Iringa
Tembelea: http://mjengwa.blogspot.com
 
I ain't no freak.. I spicy it up baby! Hao polisi ningeombea waniulize pingu ya nini? I would have asked for a female volunteer to demonstrate infront of TV audience! You never.. konow.. tunaanzisha soko la pingu hivi hivi!! shoot.

MMM,
Thumbs up!!!!
Watanzania wengi hawajui mambo ya fetish....minyororo,pingu,mikwaju,masks etc is part of the game.
 
Jana nilikuwa namsikiliza huyo Kamanda Kova hata sijaelewa alikuwa anongea vitu gani
maneno yako yako ni mazito na ya simanzi
 
Haya ni maneno mazuri sana bra maggid
Pili nimpe pole bra Jerry kwa yaliyomkuta, atashinda siku si nyingi
Tatu nikuulize swali bra maggid "hii falsafa ya kushinda na kushindwa inachochewa na na nini?" Je unazungumziaje maisha ya kutafakari ushindi pasipo anguko?
 
Ujumbe mzito ndugu yangu Maggid, especially the last two paragraphs!
 
http://www.youtube.com/watch?v=cl2Ow-Goxvc
haya sheshe ndo hilo,na jamaa kakutwa na pingu na bastola risiti hana,watu wengine unawaona kama watiifu kumbe ni majambazi na waporaji,sasa hii unaweza sema polisi walimbambikia lakini inaonekana jamaa nae kabugi mahali,naona polisi wameamua tu kumshtua kama anajisahau kama na yéye mchafu vilevile.

siujui nisemeje,
lakini kila kitu kinawezekana chini ya jua.
jerry Muro huenda alikutwa na pingu na bastola,
lakini je ni yeye aliyeziweka?
Polisi wana mbinu nyingi sana za kijasusi, huenda walivitupia humo kwenye gari ya muro bila ya yeye kujua, ili kumkomoa kutokana na mwandishi huyo kuwaumbua.
 
Back
Top Bottom