Tatizo la Ajira kwa Watoto: Serikali Ichukue hatua kuchangia Elimu Bora na kulinda haki za Watoto

Shining Light

JF-Expert Member
Jan 8, 2024
214
288
Watoto wa umri kati ya miaka 5-17 wengi wao wanakumbwa na hali ya kulazimika kufanya kazi badala ya kwenda shuleni. Baadhi yao hulazimishwa kufanya kazi ili kusaidia familia zao na wengine hupata changamoto ya kushindwa kusoma kwa sababu ya majukumu ya kazi wanayopewa. Hii kusababisha wanafunzi kufeli shuleni kwa kukosa muda wa kujisomea.

Tumekutana na idadi kubwa ya watoto wanaofanya kazi mitaani, wakijishughulisha na uuzaji wa bidhaa au kusafisha magari. Mara nyingine, tunajiuliza kama wanapata fursa ya kutosha ya kusoma na kujifunza.

Huwa kuna tetesi nyingi za shule za umma mara nyingi zinaweka lawama kwa walimu, lakini ni muhimu kujiuliza ikiwa watoto hao wana nafasi ya kusoma vizuri wanaporudi nyumbani kwao. Wazazi wengine wanaweza kuwakatiri watoto wao na kuwalazimisha kuomba barabarani, hali inayochangia kuongezeka kwa idadi ya watoto wa mitaani.

Mbali na watoto wa mitaani, wengine kulazimishwa kufanya kazi mbalimbali, kuna pia watoto wanaolazimishwa kushiriki katika shughuli za kilimo na ufugaji wakati ambapo wangestahili kusoma. Wazazi wanaweza kutumia mamlaka yao kuwalazimisha watoto kufanya kazi, bila kujali umuhimu wa elimu.

Watoto wa kike mara nyingine wanaweza kulazimishwa kufanya kazi za ndani badala ya kusoma. Hivyo, tunakutana na wasichana wengi wa kazi za ndani ambao wanashughulika na majukumu ya nyumbani na hivyo kushindwa kupata elimu inayostahili.

Serikali inapaswa kutafuta njia za kuwasaidia watoto hawa kwa kuhakikisha wanapata haki yao ya msingi ya elimu.pia kushirikiana na jamii, mashirika ya kiraia, na sekta binafsi ili kuhakikisha kwamba watoto wanapata fursa ya kupata elimu bora na kuwa na mustakabali wenye matumaini

Wazazi wanaolazimisha watoto kufanya kazi wanapaswa kuchukuliwa hatua stahiki. Watoto wako katika kundi dhaifu na wanaweza kushindwa kutetea haki zao kwa sababu ya hofu ya adhabu au kufukuzwa njyumbani na wazazi wao.
 
Back
Top Bottom