Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,634
- 697,929
Sina sababu ya kueleza mengi sna kuhusu Elimu na investment kwa kuwa kila mahali yanazungumzwa na kurudiwa rudiwa. Lakini watu wote wanasahau element muhimu sana ya network.
Network ni namna ambavyo unajijenga ndani ya kundi muhimu la marafiki, washirika, alumnus mbalimbali na ata wale wa Masikini kabisa wa mtaani.
Network haipaswi kubagua aina fulani ya Elimu au vyeo, hii ni Sehemu ambayo wanakosea wasomi wengi wakiamini unatakiwa kuwa na marafiki wa level yako ya Elimu au fedha.
Kimsingi kundi la wasomi ata ukiwa na msiba mathalani, watatuma michango mikubwa lakini Utakutana nao kinondoni makaburini wakiwa wamechelewa ata kufika, wale masikini watalala nje siku tatu wakiimba na kuwafariji. Ni muhimu sana kuwa na network yenye mchanganyiko wa watu kwa kuwa wote ni bora kwa wakati na mahali pake.
Nachotaka kusema Leo ukiwa mzazi unawajibu wa kumsaidia Mwanao kujenga netwok ya maisha ya baadaye. Usimtenganishe na Dunia kwa kuwa unaweza kumpa kila kitu, kwa kuwa Dunia yako kama Mzazi ni robo ya Dunia atakayowahitaji wenzake:
1. Lazima acheze na watoto wa mtaani kwake ata kama hawana viatu. Viatu ni jambo la muda na kupita.
2. Unapompitia Shule hakikisha watoto anaosoma nao na wako mtaani kwako huwaachi, wabebe Wote urudi nao kwemye gari, Mafuta yanabakia yaleyale, hawa watakuwa ndugu zake wakati wewe haupo duniani.
3. uUsijisikie vibaya kumsubiri dakika 10 rafiki yake anayekaribia kutoka darasani . Wao watamsubiri miaka 10
Kwenye maisha hapo baadaye.
4. Wajue kwa Majina kadri unavyoweza Marafiki zake, wajue progress yao, wakiwa wanaumwa Mpe nafasi akawasalimie, utamjengea Bond kubwa kwenye maisha yake ya ukubwani.
5. Akiingia Darasa jipya, awaangalie watoto wenzake wasio na uwezo mkubwa, awape vitabu vyake watumie kusoma badala ya kuacha vinaharibika Ndani, kuna siku akiwa na miaka 40 kuna mwenzake Ofisini atamuonyesha kitabu Chenye jina lake alichompa. Watu wasio na uwezo wanajua kutunza vitabu.
6. Mfundishe kujali watoto wenzake na akushirikishe changamoto zao. Kuna wengine wanahitaji msaada.
7. Usiogope wala kusita kuchukua hatua anapokujuaza changamoto za mtoto mwenzake zilizo Ndani ya uwezo wako.
8. Once in a while, pita kwenye play ground yao. Waangalie ata kwa dakika 10 na kuwapongeza kwa Michezo yao. Watakukumbuka daima.
9. Wakumbushe watoto wote kuwa kila mmoja Ana nafasi ya maisha bora hapo baadaye, wawe watoto wema daima.
10. Akihama Shule, hakikisha anawaaga wenzake na kuwaambia ipo siku wataonana Tena . Asiondoke tu ghafla ata kama ni darasa la kwanza . Ina kumbukumbu sna baadaye wakiwa watu wazima.
Kumbuka mtoto mwenye networks ni tajiri wa maisha Kama tajiri mwingine. Akiwa na Shida ofisi yeyote anakuta Marafiki, akiwa na biashara anakuta kundi la wateja na akiwa mwanasiasa anakuta kundi la supporters.