RPC Kuzaga: Malezi Bora na Elimu ya Makuzi vinasaidia kuwajenga Watoto kujitambua na kujitathimini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,815
11,992
Wazazi, Walezi na Jamii wametakiwa kushiriki kikamilifu katika utoaji wa malezi bora na elimu ya makuzi kwa watoto ili kuwajengea uwezo wa kujitambua, kujithamini na kujiepusha na uhalifu ikiwemo ukatili wa kijinsia.

Rai hiyo imetolewa Desemba 27, 2023 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi, Benjamin Kuzaga katika Kongamano la Watoto wa Jimbo Katoliki Mbeya linalofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mwanjelwa Jijini Mbeya.
a4c46364-b679-4158-b078-ecce3c53b0ca.jpeg

603b068a-2afd-4cb2-92ae-fdf40d444f09.jpeg

Kamanda Kuzaga amewataka Wazazi na walezi kutimiza wajibu wao katika kuhakikisha wanawalinda Watoto dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji na endapo wataona viashiria vya uhalifu huo watoe taarifa kwa viongozi wa dini na Jeshi la Polisi kwa hatua zaidi za kisheria.

Aidha, Kamanda Kuzaga ameeleza kuwa, mbali na elimu ya ukatili, watoto hao walipata elimu ya matumizi sahihi ya vivuko vya watembea kwa miguu (Zebra Crossing), namna ya kutembea barabarani na matumizi sahihi ya taa za kuongozea magari (traffic lights).

Naye, Mkurugenzi wa mashirika ya Kipapa Jimbo Kuu Katoliki Mbeya, shirika linalojihusisha na utoaji wa elimu ya malezi na makuzi kwa watoto, Padri Richard Mgasa amesema kuwa, lengo la kongamano hilo ni kuwajengea uwezo watoto katika masuala ya kidini, kujua haki zao, kujitambua na kujilinda dhidi ya vitendo viovu.

"Wazazi na walezi wanapaswa kutambua kuwa watoto wanapaswa kulindwa dhidi ya uhalifu, washiriki kikamilifu kuhakikisha watoto wanapata haki zao, wanajitambua na kujilinda dhidi ya uhalifu" alisema Padri Mgasa.

Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Mbeya Mrakibu Msaidizi wa Polisi Veronica Ponela ametoa wito kwa wazazi na jamii kutofumbia macho vitendo vya ukatili wa kijinsia na badala yake watoe taarifa mapema kwa Jeshi la Polisi ili hatua zichukuliwe.
f0e03fa8-5c5d-4fc9-9e5f-73311fbf9a90.jpeg

e45b9d9d-e515-4a63-9dc8-b653e65d0bfb.jpeg
 
Back
Top Bottom