Mkaguzi Kata: Mkiwapa Elimu watoto mtatengeneza Jamii isiyo na uhalifu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
76223d78-e83f-4c08-8233-fff7fc89e2bd.jpeg

Mkaguzi kata Mkiwapa Elimu watoto mtatengeneza Jamii Isiyo na uhalifu, atoa madaftari kwa Salim.

Mkaguzi Kata ya Kerege, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Suleiman Ameir amewataka wazazi wa kata hiyo iliyopo Wilaya ya Korogwe Mkoa wa Tanga Kuhakikisha watoto wanapata elimu ambayo itawakomboa kifikra na umasikini katika kata yao.

Amebainisha kuwa endapo vijana wa kata hiyo watapata elimu wataondokana na uhalifu, watakuwa vijana wema na watulivu, watakuwa vijana wasikivu kwa wazazi na jamii ambapo amewataka kila mzazi wa kata hiyo kuhakikisha vijana wanakwenda shule ili wapate elimu.

224c87c2-7763-4e36-9a05-3c2fdab2a324.jpeg

f44842f1-782a-457b-948b-0b01c74eb380.jpeg

Mbali na kuwataka wazazi hao kuhakikisha watoto wao wanakwenda shule Mkaguzi huyo ameguswa na kijana ambaye alisema anatamani kwenda shule lakini alikuwa na changamoto ya madaftari ambapo ampa madaftari hayo kwa ajili ya masomo yake.

Sambamba na hilo amewaomba wazazi kuchukia uhalifu ambao umekuwa ukirudisha nyuma maendeleo ya watu ambapo amewaomba wananchi hao kuendelea kutoa taarifa za wahalifu kwa Jeshi la Polisi ili hatua sitahiki zichukuliwe.
 
Back
Top Bottom