Tanzia

Pole Mkuu, hayo ndiyo majaribu ambayo Mungu anampitisha mja wake. Lakini pia yeye ni ni mwingi wa fadhila na naamini atakujalia moyo wa uvumilivu. namuombea mtoto apumzishwe mahali pema, amina
 
Mpendwa, nami naomba niungane na wenzangu kukupa pole nyingi kwa kumpoteza mtoto wako kipenzi. Ninamuomba Mungu akupe nguvu na matumaini wewe pamoja na mkeo katika kipindi kigumu mnachopitia. Bila shaka atawafuta machozi na kuwajalia watoto wengine. POLENI SANA.
 
Pole sana, naomba Mungu wetu mwenye nguvu asiyeshindwa awe pamoja na familia yako, awape nguvu na uvumilivu katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti aliye hai nazifunga nguvu zote za mwovu shetani zisipate nafasi katika familia hii, Amen.
 
Mtu mmoja, sina maneno ya kutosha kwa msiba huo, ila jipe moyo mkuu, Mungu awape faraja na kuwakumbatia kwa pendo la neema yake. Amin!
 
Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe,........, MAPENZI YAKO YATIMIZWE HAPA DUNIANI....... Tunasikitika pamoja nawe ndugu yetu, tunaomboleza kuondokewa na mpendwa mwanetu. maneno yangu ya utanguli hasa ya herufi kubwa yanafaa kwa faraja kwa wote wanaoamini. AMEN
 
Mtu Mmoja,

Pole sana kwa msiba huu mzito uliokupata. Kwa kweli ni huzuni kubwa sana kumpoteza mtoto ila tunaamini kuwa yote hayo ni mipango ya Mungu, na tuko pamoja nawe kuwaombea kwa Mungu awape nguvu wewe na mke wako katika kipindi hiki kigumu sana, na pia amuweke mtoto wako mahali pema peponi.



Ndugu zangu,

january mwaka huu nilikuja hapa na habari za furaha kuu za kupata mtoto wa kiume (angalia link hiyo hapo chini)

https://www.jamiiforums.com/mahusia...a-kiume-mama-na-mtoto-wanaendelea-vizuri.html



leo hii nina huzuni kuu pia, Mwenyezi Mungu muweza wa yote kamuita mtoto huyo kurejea kwake na kutuacha na majonzi makubwa nisiyoweza kuyaeleza vyema. machozi mengi sana yamenitoka, ila sina la kufanya zaidi.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe

RIP mwanangu mpendwa
 
Pole kamanda utapata mwingine kwa uweza wa Mungu...ulindwe kipindi hiki kigumu cha kufungia mwaka
 
Yaani nywele hadi zimenisimama ghafla jamani, pole sana ndg yangu, Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Biblia inasema shukuruni kwa kila jambo. Mungu atakupa wengine tu
 
Raha ya milele umpe ee bwana na mwanga wa milele umwangazie, apumzike kwa amani amina.


Pole sana ndugu yetu. Shukuru Mungu kwa kila jambo.
 
Dha! nimekosa cha kusema kwa kweli! Poleni sana Mwenyezi Mungu awatie faraja na kuwapa nguvu katika kipindi hiki kigumu sana kwenu. Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe.
 
pole sana mkuu. Mungu aendelee kuwatia nguvu ndugu na jamaa, na Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Mia
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom